SMULIZI: HOUSEGIRL WA KITANGA
MTUNZI : KIZARO MWAKOBA
SEHEMU YA NNE (5)
ILIPOISHIA
“Si uonje uone kama hayana kitu!” nilizungumza huku nikimsogelea na kufungua vishikizo vya gauni langu vilivyokuwa kifuani. Nilimshuhudia Fadhili macho yakimtoka utafikiri alikuwa ameona kitu fulani cha ajabu sana hapa ulimwenguni. Sikuweza kufahamu ni kwa namna gani niliweza kupata ujasiri wa namna ile mbele ya mwanaume Yule. Akiwa bado ameshangaa tayari sidiria yangu nyeupe iliyokuwa na kitambaa cha resi ilikamatwa vyema na mikono yangu tayari kwa kumtolea kile ambacho nilikuwa nimekikusudia. Ndio nilikuwa namtamani sana Fadhili kiasi cha kusisimkwa mwili kila nilipokuwa namuona.
ENDELEA….
“No! Tumu….usi…usi….ahsante” Fadhili alizunguza kwa kigugumizi na kuondoka pasipo hata kuaga.
Nilibakia jikoni pale nimesimama huku mikono yangu ikiwa imekamata gauni langu lililokuwa wazi maeneo ya kifuani. Nilign’ata meno yangu ya chini kwa hasira na kuelekea chumbani kwangu. Sikutamani hata kwenda kumfungulia geti. Nikaona mwanaume gani yule ambaye ukimtega kwa urimbo anajinasua kwa fimbo na ukimtega kwa mambo anajinasua kwa jambo. Nikajitupa kitandani kwa hasira. “Hivi ni kwanini Fadhili ananidharau mimi, au ananiona katoto kadogo kama alivyozungumza usiku? Mbona kaka Imrani alikuwa akionekana wazi kuvutiwa na mimi pamoja na kwamba sikuwahi kumuonesha kumtaka? Au Fadhili ni mgonjwa?” nikajiuliza maneno mengi nikiwa pale kitandani.
****
Nikiwa kitandani nikajikuta usingizi ukinichukua na kulala fofofo masikini mtoto wa watu mie. Basi nilipiga mbonji hadi kwenye mida ya saa nane hivi ndipo nilipokurupuka na kutoka chumbani kwangu mbio kama mwizi. Haraka sana macho yangu yalitua kwenye saa ya ukutani ambapo ndipo nilipobaini kuwa ilikuwa ni saa nane za mchana.
“Mtume simama!” nilishituka na kuweka mkono wangu kifuani kama vile nilikuwa najipima mapigo ya moyo. Niliingia jikoni haraka sana na kuanza kufungua makabati ya vyakula ili niweze kupika. Akilini mwangu nilikuwa namuwaza sana Fadhili kwani ni yeye pekeyake ambaye alikuwa na kawaida ya kurudi nyumbani mchana kwaajili ya chakula.
“Hodiii” sauti ya mtu kutiokea nje ya geti ilisikika ikiambatana na sauti ya kugongwa kwa geti hilo. Moyo wangu ukashituka kidogo nikiamini kuwa mgongaji alikuwa ni Fadhili.
“Mungu wangu! Haya yote yanatokea wapi, mbona nimekuwa mzembe kiasi hiki leo?” Nilitoka nje na kuchungulia kwenye tundu dogo la pale getini. Moyo wangu ulipata ahuweni baada ya kumuona mgongaji alikuwa ni dada Bupe yule mama muuza mgahawa wa jirani. Nilifungua geti na kuchungulia nje kumkaribisha Bupe.
“Karibu dada” nikamkaribisha.
“Ahsante mwaya, weye wa lala weye?” mama yule alizungumza huku akijitahidi kuiga lafudhi yangu ya kitanga ingawa hakuwa anaimudu.
“Hapana sikuwa nimelala”
“Kumbe wafanyaje weye?”
“Nilikuwa napika” nikajibu kwa ufupi kwasababu sikuwa nimefurahishwa na viswali vyake vilivyokuwa vikinigusa.
“He! Saa hizi wapika! chakula cha jioni?”
“Hapana napika chakula cha mchana” nikamwambia.
“Kwanini sasa umechelewa hivyo?”
“Nilikuwa nimepitiwa na usingizi”
“Kwahiyo ndo waamka hivyo?” alihoji nami nikaitikia kwa kichwa.
“Sasa unapika nini”
“Nataka kupika nyama na ugali”
“Unataka kupika ama ndio unapika?”
“Nataka kupika”
“He! Makubwa mwaya, kwahiyo ndo mambo ya kitanga hayo?” mama yule akahoji swali la kishambenga ambalo lilinikera ile mbaya. Hata hivyo nikajikaza kuto kumuonesha kuwa nilikuwa nimekasirika.
“Karibu dada Bupe” nikamkaribisha kwa msisitizo baada ya kuona anaingilia mambo ambayo hayakuwa yakimhusu. Halafu nilikuwa naona akizidi kunipotezea muda zaidi ambao pengine ningeutumia kumuandalia Fadhili chakula.
“Sikiliza mdogo wangu, mie kule nimekwisha pika. Twende ukachukue chakula umuekee kakaako” mama yule alizungumza. Moyo wangu ulisita kwa kuhofia kuleta chakula cha hotelini nyumbani wakati ndani kulikuwa na kila kitu.
“Usiogope mdogowangu, we unahifadhi vizuri kwenye poti hata yeye akija hawezi kuelewa kama umechukua mgahawani” alisema mama yule maneno ambayo kwa kiasi fulani nilihisi yakiniingia akilini.
“Kweli dada?”
“Nenda ukalete hotipoti”
“lakini dada wewe….”
“Hakuna cha lakini bwana weye, nenda ukalete poti hukoo” dada Bupe alizungumza huku akinisukuma kwa mkono wake wa kushoto kuelekea ndani. Sikubisha hata kidogo, niliondoka haraka kuelekea ndani.
“Lete na dumu langu la juisi” alinambia dada Bupe kwa sauti wakati naingia ndani.
“Sawa” Nilijibu na kuzama ndani.
Nilipotoka na hotipoti zangu mbili mkononi sikumkuta dada Bupe pale getini. Sikupata shida sana ya kumtafuta wala kushangaa kwa kile kilichotokea. Nilitoka haraka getini na kwenda hadi mgahawani kwake. Nilimkuta akigeuza wali jikoni.
‘Hodiii” nilibisha hodi nilipokuwa naingia mgahwani mle.
“Karibuuu” dada Bupe akaniitikia kwa bashasha.
Nilipitiliza moja kwa moja hadi jikoni na kuketi kwenye kiti kidogo kilichokuwa pembeni ya jiko alilokuwa anapikia. Alipokea Hotipoti moja na kujaza ugali.
“Haa dada Bupe punguza huwo mwingi sana” nikasema
“Wacha machachari wewe kwani tumbo ni lako” akanambia huku akifunika hotipoti lile na kupokea hotipoti la mboga na kunikabidhi lile la ugali. Alifunua chungu cha nyama na kuniwekea kisha akafunika na kunikabidhi.
“Haya peleka haraka”
“Asante dada Bupe” nilijibu huku nikijiinua kutoka pale kwenye kiti.
“Nenda urudi ninashida na wewe” dada Bupe alipaza sauti wakati nilipkuwa natoka.
Nilitembea kwa haraka sana na kuingia getini pasipo kuonekana na mtu yeyote kama nilikuwa nimebeba chakula kutoka mgahawani kwa dada Bupe. Jamani kuna watu wana roho nzuri nyie, sikuweza kuamini kama mwanamke yule niliyekuwa namchukia ndiye aliyeweza kunisaidia kutoka kwenye majaribu ya siku hiyo.
Niliandaa chakula kile mezani haraka kisha nikakumbuka wito wa dada Bupe, nilitoka na kuelekea mgahawani.
****
Nilipofika mgahawani pale dada Bupe alikuwa ameniwekea chakula kwenye sahani na kunikabidhi mara tu nilipofika.
“Haya nawewe ule” Akazungumza mwanamke yule alipokuwa akinikabidhi sahani ya chakula.
“Mnh dada wewe mkarimu” nikazungumza huku nikipokea.
“Wacha maneno mengi hebu kula huko” akanambia huku akisuuza sahani haraka haraka.
Mwenzangu nikaanza kula taratibu kama vile sikuwa mimi. Nilete utani kwenye maswala ya msosi, nani kasema? Nikapiga msosi ule hadi nikamaliza.
Dada Bupe alikuwa ameketi kwenye kistuli alichokuwa amekilaza kwa pembeni akiosha vyombo. Mimi nilikuwa nimeketi kwenye kiti cha plastiki kilichokuwa pembeni yake nikichambua njegere za biashara. Nikakumbuka kitu na kuona si vibaya kumuyomba ushauri.
“Dada” niliita
“Mdogo wangu” aliitika pasipo kunitazama huku akisugua birauli.
“Mwenzio nina jambo”
“Haya lijambe” dada alisema na kunifanya niangue kicheko kutokana na vile ambavyo alinijibu.
“Sasa unacheka nini?”
“Una maneno wewe!”
“Mimi tena”
“Sasa mimi nakwambia nina jambo we unanambia nilijambe”
“Eeh, kama una jambo we jamba tu” alisema dada Bupe huku akisuuza jagi la kuhifadhia juisi.
“Hivi mimi nina utoto gani ukiniangalia?” nikahoji.
“Kivipi labda?”
“Kivyovyote vile”
“Mi nakuona mkubwa mwenzangu, huna utoto wowote”
“Sasa basi nikuchekeshe”
“Haya nivunje mbavu mwanamke mwenzio”
“Siku moja kaka Imran alikwenda hukoo kazunguuka akarudi na zawadi”
“Zawadi za nani?”
“Kaniletea mimi”
“Enhee”
“Basi nilipozifungua ndani nilicheka!” nikazungumza huku nikijichekesha kwa lazima na mwisho nikajikuta nikicheka ukweli kiasi cha kunifanya nipaliwe na mate.
“Sasa mbona unakufa mbavu mwenyewe mimi sijapewa ucheshi huo?” dada alizungumza huku akitabasamu. Nilijitahidi kuacha kucheka na kuendelea kuzungumza.
“Basi bwana”
“Haya nipe basi mwenzio nina hamu”
“Unajua vinguo vya wa toto? Yaani havinienei kabisaaa” nikazungumza na kucheka huku dada naye akiangua kicheko.
“Sasa imekuwaje Imran naye akakuletea vinguo vya watoto?”
“Yaani dada we acha tu”
“Kwahiyo umevifanyaje?”
“Nivifanye nini? Vipo ndani, nasubiri nikienda kwetu niwapelekee watoto wa ndugu zangu”
“Kwani vipoje si uniuzie mimi nina mtoto wa dada yangu ni mdogo”
“Yaani kale kamoja ni kasketi, nikikavaa kanaishia huku kwenye mapaja, na kale kengine ni kablauzi lakini na kenyewe huku mgongoni kapo wazi yaani vimkanda viwili tu ndio vimepita humu kwenye mabega” nikazungumza kwa kusisitiza na vitendo.
“Mnh! Una uhakika hizo nguo ni za kitoto?” dada Bupe aliacha kusugua yombo na kunihoji kwa makini.
“Kweli dada Bupe, yaani ukiziona mwenyewe utabroo”
“Hebu kazilete, si umesema zipo ndani?”
“Ngoja nikakuletee” nilizungumza na kuinuka pale kwenye kiti na kuelekea nyumbani mbio.
Niliona kulikuwa na ulazima wa kituko kile kushea na mtu ili nipate wa kushangaa na kucheka nye. Hata wewe ndugu msomaji ungeshangazwa na vituko vile, nakwambia ungeviona hivyo viwalo utafikiri alikuwa amenunuliwa mwanasesere.
Baada ya dakika kama mbili hivi nilirejea nikiwa nimekamatia zile nguo nilizokuwa nimenunuliwa na kaka Imran. Dada alizipokea kwa hamu kubwa na kuzifunua moja baada ya nyingine akianza na ile sketi. Aliitazama kwa makini na kuipindua pindua nyuma na mbele.
“Mnh! Nguo zenyewe ndio hizi?” dada alihoji kwa mshangao.
“Si nimekwambia mimi, yaani ni vituko”
“Hebu na hiyo” dada alisema huku akiitupia begani ile sketi na kunyoosha mkono kupokea ile blauzi niliyokuwa nimeishika.
“Yaani hiki ndio kichekesho kabisaaa” nikazungumza huku nikicheka cheka.
Dada Bupe aliitazama kwa makini blauzi ile na kuigeuza geuza. Aliinua macho yake na kunitazama usoni kwa kama vile kunakitu alikuwa anakishangaa.
“Basi mwenzangu hivyo ndivyo viroja nilivyoletewa na huyo kakaangu mimi” nilizungumza huku nikiketi na kuchukua ungo wa njegere kuendelea kuchambua. Dada alikuwa bado akinikodolea macho kwa mshangao utafikiri nilikuwa nimefanya kitu gani sijui cha ajabu.
“Mdogo wangu una masihara wewe!” dada Bupe alizungumza kwa upole.
“Sio masihara dada, we mwenyewe si unaona vituko hivyo”
“Eh! Mbona haya tena makubwa!” dada alizungumza kwa kuonekana kuchoka.
“Makubwa tena sio kidogo bali ni maburungutu” nikaongezea nikiamini alikuwa ananisapoti maneno yangu.
“Mdogo wangu, kaka yako sio mjinga” dada Bupe alizungumza kwa upole.
“Kumbe ni chizi, hata mimi nilijua tu?” nikazungumza.
“Yaani mambo haya yanaendana kabisa na hilo umbo lako”
“Eboo! Dada nawewe”
“Kweli mdogo wangu yaani kwa taarifa yako hapa mjini hatuvai magunia kama unavyojifunika wewe muda wote” alisema dada Bupe huku akionekana kumaanisha kwa alichokuwa anakizungumza.
“Yaani mimi navaa magunia?” nikahoji kwa kuhamaki
“We mwenyewe huoni? Kwa taarifa yako warembo huwa hatufichi vile tulivyobarikiwa na mwenyezi mungu” alisema dada Bupe.
“Mnh” nikaguna kwa mshangao
“Sasa unaficha unamfichia nani? Tena kama wewe vile ulivyo, nakwambia ukitupia vitu hivi mwenyewe utajikubali. Hapa mjini mama” dada Bupe alizungumza na kunirushia vile vinguo na kuelekea kwenye vyombo vyake kuendelea kuviosha.
Nilizinyaka zile nguo kisha kwa mshangao wa hali ya juu nikawa namtazama dada Bupe. Nilivuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu, nilidhani dada Bupe angeniunga mokono kumbe naye akili zake zilikuwa hazimtoshi kama kaka Imran.
“Lakini dada umeona nikivaa ninavyo chekesha?” nilizungumza kwa upole na umakini baada ya kukosa wa kuniunga mkono.
“Acha ubwege we mtoto wa kitanga”
“Dada kumbe we hujaniona ngoja nivae unione jinsi ninavyokuwa mwanasesere” nikazungumza huku nikiinuka na kuelekea jikoni. Nilivaa vinguo vile vya ajabuajabu na kujitazama mara mbilimbili. Nilipobaini kuwa sikuwa nimependeza nilichukua kanga yangu na kujifunga kiunoni kisha nikatoka nje.
Dada Bupe aligeuza shingo kunitazama. Nilipeleka mikono yangu usoni huku nikicheka cheka kwa aibu.
“Sasa hilo likanga la nini? Hebu fungua huko” alisema dada Bupe.
“Haa dada wewe!” nilizungumza kwa mshangao.
Dada Bupe alinifuata haraka sana na kuivuta ile kanga niliyokuwa nimejifunga kiunoni.
“Aaaah dada” nilipiga kelele lakini hazikusaidia kwani dada alikuwa tayari amekwisha nivua kanga ile. Mtoto wa watu nikabakia nimeziba macho kwa aibu.
“Unaona sasa wacha wehu wewe mtoto umependeza”
“Dada mwenzako siwezi kukaa hivi”
“Hebu ondoa ujinga wako hapa, we unadhani mimi ningebahatika kuwa na umbo kama lako ningelifichaficha kama unavyofanya” dada alizungumza huku akielekea jikoni kupeleka ile khanga yangu aliyokuwa amenivua.
“Dada bwana nipe kanga yangu mwenzio nivae” nilizungumza kwa sauti ya kudeka huku nipigapiga miguu chini.
Tulipokuwa tukiendelea kubishana mimi na dada nilisikia muungurumo wa gari ukielekea getini kwetu. Niliamini alikuwa ni Fadhili amerudi kwaajili ya kupata chakula cha mchana. Niliingia jikoni mbio kwa lengo la kwenda kubadilisha zile nguo nilizokuwa nimezivaa lakini nilipofika jikoni sikuweza kuamini. Dada Bupe alikuwa amezihamisha nguo zangu na kuzificha.
“Dada nguo zangu ziko wapi nivae?” nikahoji huku nikitafuta hapa na pale mle jikoni mwake.
“Uvae kwani hapo ulipo upo uchi?” dada alihoji huku akiendelea na kazi zake akiwa hana hata chembe ya wasiwasi. Kule nyumbani gari ilikuwa ikiendelea kupiga honi. Kwa kiasi Fulani nikahisi kukasirika na kutamani kulia.
“Dada usinifanyie hivyo mwenzio nataka kwenda kufungua geti” nilizungumza kwa sauti ya kubembeleza masikini ya mungu lakini dada Yule hakuonesha kunijali hata kidogo.
“Nenda bwana mwenzio anataka kufunguliwa geti huko” Dada alizungumza huku akianika kitambaa kidogo cha kufutia meza.
Kutokana na kelele za honi kuzidi ilinilazimu mtoto wa watu kutimua mbio kuelekea nyumbani kufungua geti.
Nilipofika getini sikuweza kuamini macho yangu, kumbe hakuwa Fadhili kama ambavyo nilifikiria. Alikuwa ni kaka Imran. Nikazidi kupatwa na mshituko hasa kutokana na zile nguo ambazo nilikuwa nimezivaa.
Kaka Imrana aliniona nikitokea kwa Bupe, hakuweza kuamini macho yake. Nilimuona akivuta pumzi ndefu na kuzitoa. Macho yake hayakubanduka kwangu hadi nilipofika geniti na kasheshe ikaja pale nilipokuwa natakiwa kufungua komeo la juu. Nilipoinua mkono wangu juu ile blauzi yangu ilipanda na kupelekea sehemu za tumbo langu kuonekana.
Kaka Imran alinikazia macho sehemu za kati hasa huanzi kwenye kiuno na kushuka chini. Kale kamzigo kangu ka madafu ya uwani kalifanya kasketi nilikokuwa nimekavaa kabinuke juu mithili ya breki ya trekta. Alipoteremsha macho yake chini kidogo alikutana na guu la nguvu lililokuwa limenona na kuvutia zaidi hasa kutokana na rangi ya ngozi yangu laini. Nilipofungua geti kaka Imran akawa bado ameduwaa akinikodolea macho. Nilimpa ishara ya kuingia lakini utafikiri alikuwa hanioni kumbe macho yake yalikuwa kwangu.
Itaendelea
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment