MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 02
TULIPOISHIA: Nilichana ile karatasi iliokuwa imeandikiwa namba kisha nikaichana Chana vipande vidogo vidogo kwa hasira na kutupa Chini, Latina na Joyce walibaki wameachama kwa mshangao ndipo nikawapita na kuondoka zangu.
Nikiwa nipo njiani naelekea magereza machozi yalianza kunitiririka ndipo nikasema:........!!!!!
SONGA NAYO!
Ndipo nikasema: Kwanini Mimi!!
Latina alinifikia na kusema: sorry dada kama ntakuwa nimekukosea.
Nikamjibu: ni sawa tu.
Latina: Ila dada mi sintachoka kukuuliza embu niambie jamani Mimi mdogo wako ujuwe.
Nikamjibu: kuhusu?
Latina: kuhusu Derick.
Nikamjibu: Yule ni mpuuzi sana staki hata kukumbuka habari zake.
Latina: ila ulimjua Kabla?
Nikamjibu: ndio.
Latina: alikuwa Nani kwako?
Nikamjibu: mpenzi wangu.
Latina alishtuka na kuniuliza: kiaje sasa?
Nikamjibu huku nikiendelea kusonga mbele taratibu: unajua Latina wanaume ni wa baya Sana.....
Ndipo nilianza kumwadithia ilivyokuwa Mpaka nikajuwana na Derick * miaka kumi iliopita nikiwa na miaka kumi na mbili nilikuwa napita pita zangu mtaani huku nikielekea Sokoni kwa bahati mbaya tukagongana na kijana mmoja na kijana huyo alikuwa ni Derick nae alikuwa bado mdogo na alionekana kumkimbia mtu flani au kitu flani maana alikuwa anapumua kwa kasi ndipo Nilinyanyuka na kusema: samahani kwa hili.
Alinyanyuka na kuniambia: Mimi ndo wakukuomba msamaha Jina langu naitwa Derick.
Alinipa mkono bila wasi wasi nikampa wangu na kusema: Mimi Najma.
Derick: sorry unaweza kunizungusha mtaani ntakulipa.
Niliposkia Malipo Nilikubali nikaamua kuairisha safari yangu ya kuelekea Sokoni na hapo yalikuwa ni Majira ya saa nne asubuhi nikachukuwa jukumu la kumtembeza maeneo mbali mbali, kwa kuwa tulitembea kwa mguu aisee nilichoka Sana siku hio mpaka kujutia kukubali jukumu hilo Ila Derick hakuonekana kuchoka maana alionekana kuvutiwa Sana na Mazingira yale, nilipoona kama vile ananipotezea Muda nilimwambia aende kwao Nami niende zangu Sokoni ila aliniambia atanilipa milioni tano, aisee Niliposkia hivo nguvu ziliniingia nikaanza kumpeleka sehemu mbali mbali ila kila nimtazamapo kuongea kwake aisee hakufanana kabisa na Watoto choka mbaya ndipo Nikamuuliza: kwenu wapi?
Derick: sipajui Kwani kwetu wapi?
Nilitabasamu na kumjibu: Acha Utani.
Derick: twende sehemu Inaitwa Kariako.
Nikamjibu: sawa ila nawahi.
Tulienda kariako yalikuwa tayari ni Majira ya Mchana saa nane, tulipofika Derick alianza kushangaa watu walivyo wengi na mambo yanayouzwa kwenye soko hio tulizunguka nikijaribu kumwambia kuhusu kurudi nyumbani akaniambia anaongeza pesa mpaka ikafikia milioni kumi Nami pesa ilivyokuwa inapanda ndivyo nilizidi kupata moyo wa kumzungusha.
Kwa kuwa tulitembea Sana Tuliamua tupumzike ndipo Nikamuuliza: kwenu wapi?
Derick: maeneo ya Kuleeeeeee.
Nikamuuliza: sasa wewe Mbona unataka nikuzungushe mtaani Kwani toka uzaliwe hujawahi kuzunguka?
Derick: naskia njaa unaweza kunikopa hela Tukienda kwetu ntakurudishia na Zile milioni kumi!
Nikamjibu: pesa ni ya baba amenituma nikahemee.
Derick: si ndo hivo unikope kwanza.
Nilichomoa Elfu tano tukanunua chakula tukaanza kula Ila Mimi niliamini Sana pesa ile Kama ntapewa, Baada ya kumaliza Tulianza upya kuzunguka kwenye soko ile Mpaka saa kumi jioni, Nami kutokana nilipenda pesa kuliko haikuwa mbaya kwangu maana nilihesabu akinipa milioni kumi ntamkabidhi baba na atafurahi, tukiwa tupo njiani Derick aliniambia: twende kuona movie.
Nilishangaa na kumuuliza: movie?
Derick: eeehh.
Nikamjibu: kwanza wewe ni tapeli Mimi na wewe viishie hapa maana naona nimegeuzwa mdoli na pesa yako baki nayo usinijuwe nisikujuwe.
Derick: Ila wewe ndo mwenyeji wangu nisaidie tukitoka kuangalia movie nakuahidi tunaenda nyumbani na pesa yako Ntakupa.
Nilimtazama machoni Nikaona Labda yupo sahihi kwa kile anachokiongea ndipo Tulienda wanakoonesha movie tulipofika tulimkuta muhudumu mwanamke akatwambia tuchaguwe movie, nilipoona cover ya Movie inayohusu wapendanao niliichagua na kusema: Tutaangalia hii.
Mdada Yule Akaniambia: Nyinyi ni wapenzi?
Tulishtuka na kuangaliana ndipo nikamjibu: Hapana Sisi ndugu.
Mdada Yule akasema: hii inahusu mtu na mpenzi wake na watu wakubwa sio Watoto kama unahitaji movie ya Watoto chaguweni hii.
Tulipoangalia cover Ilikuwa ni Movie ya vita vita kiukweli Mimi sikupendi Ila Derick alionekana kuipenda sana ndipo mdada Yule akasema: watu wawili Elfu ishirini.
Nilishtuka na kusema: heee!! Turudi bwana.
Derick akasema: Hapana tuone ntakurudishia na ile hela yako Baada ya movie please.
Nilikuwa mjinga sana pesa ya mahemezi Elfu ishirini na tano yote niliitoa kwa mambo ya ujinga, tuliingia tukaanza kuona movie Ila Mimi movie za kivita vita sikuzipenda hivo kutokana na uchovu Wa kutembea siku nzima nilijikuta nameegamia begani la Derick na Usingizi ukanivuta, Derick aliendelea kuangalia Mpaka usiku saa mbili Nami Usingizi nilizidi kuvuta taratibu, Baada ya movie kuisha aliniamshaa nikaamka na kusema: bado tupo hapa?
Derick: eeeehhh!
Nilinyanyuka kwa hasira kisha nikatoka nje, Derick Baada ya kuona nimetoka nje nae alinifuata aliponifikia aliniuliza: kwahio unaondoka?
Nilimkata kibao kwa hasira na kusema: umenigeuza mjinga sana.
Derick Baada ya kupigwa kibao alijishika shavuni Nami Muda Huo nilikuwa nimeondoka.
Nikiwa nipo njiani naelekea nyumbani njia nzima nilikuwa nalaani maana baba yangu licha alikuwa sio mkali sana Ila kwa hili sizani kama angenisamehe, ghafla niliskia sauti ya Derick akiniita Ila sikutaka kusimama bali Niliongeza mwenda, Derick alipoona Kama vile nampotezea alinifuata akikimbia aliponifikia alinishika mkono na kusema: sorry please niskilize kwanza.
Nilimkazia jicho na kusema: unahitaji nikupige?
Derick: Hapana.
Nikamjibu: pesa baki nayo niachie uzima.
Derick: Ila Mimi ukweli ukiniacha hapa I'll die maana I don't know home ukweli Mimi ni mgeni nasomea wingereza hapa Nimekuja holiday Nikaona nitoroke ili niuangalie mji vizuri please nisaidie kwetu sipajuwi vizuri.
Nilimtazama kwa umakini kisha nikampushi na kuondoka zangu na kumuacha akinisindikiza kwa macho ukweli aliponiambia Ooh anasomea wingereza kwanza nilimuona tapeli flani.
Nikiwa nazidi kusonga nilisimama nikamkumbuka alivyokuwa anayashangaa Mazingira na alivyokuwa anaongea kingereza Kidogo nikamwamini ndipo niliona nirudi nyuma kumtazama nilipofika eneo lile nilipomuacha nilianza kumuangaza angaza Ila sikumwona nikiwa naendelea kumwangaza nilimuona akiwa amekaa pembeni ya nyumba flani ukweli nilimuonea huruma kwa sauti ya Chini Nikamuuliza: utalala hapo?
Aliponiona alinifuata aliponifikia aliniuliza: umerudi?
Nikamjibu: usijali tupo Pamoja ntakusaidia.
Derick: nipeleke kituoni watanitangaza.
Nikamjibu: usilete mambo ya kimama mama! hapa sio ulaya twende nyumbani kwetu ni wakalimu sana ikifika asubuhi baba atakupeleka kwenu maana anajuwana na matajiri wengi.
Tulianza safari ya kuelekea nyumbani tulipofika niliogopa kubisha hodi Ila Nikaona potelea Kote Kama nikupigwa acha iwe hivo maana nilikosea sana, niliingia ndani moja kwa moja na Derick akanifuata nyuma, sebuleni niliwakuta wazazi wangu wawili wakiwa kama vile wanajadiri kitu flani nikajuwa hapo nazungumziwa Mimi, waliponiona walinikimbilia na kuanza kuniuliza hali yangu ndipo nikawajibu: mi mzima Ila baba I'm sorry.
Baba: Kikubwa ni wewe Upo Salama Huyu nae Nani?
Sikutaka kuwaficha niliwaeleza kila kitu ndipo baba akamwambie Derick: pole Sana kijana hapa umefika jiskie huru ntatoa taarifa kituoni kuhusu wewe nikizani wazazi wako watakupata kirahisi sasa Najma mpelekee maji mwenzio bafuni aoge.*
Kabla sijamaliza kumwadithia Latina aliniuliza: siku hio nilikuwa wapi Mbona sikumwona?
Nikamjibu: wewe si ulikuwa Unasoma bodingi!
Latina: sawa Nimekumbuka Enhe ikawaje?
Nikaendelea kumpa story * Baada ya pale tulilala asubuhi ilipowadia tuliamshwa na minghurumo ya gari tulipotoka nje tulishangaa kuona gari tatu nzuri za kifahari kweli zimepaki karibu na mlango wetu Na watu Kama Sita akiwemo mama flani alieonekana kupaniki kuliko wote, baba kwa sauti ya Kawaida aliwasalimia na kuwauliza: sijui tuwasaidie nini?
Yule mama akasema: tumepigiwa simu kituoni maana tulikuwa tumelipotia kuhusu mwanetu aliepokea toka Jana asubuhi sasa police walitutaarifu kuwa mlitoa taarifa kuwa kijana wetu yupo hapa.
Baba: ndio yupo hapa.
Yule mama alishusha pumzi kwa furaha ndipo baba Akaniambia: kamwamshe mwenzio.
Nilirudi ndani nikamkuta bado amelala ndipo nikamwamsha akaamka tukatoka nae nje, mama Yule alieonekana kama mama yake alipomwona alimkimbilia na kumkumbatia kisha akaanza kumuuliza kuhusu Hali yake Derick akamwambie yupo sawa, ndipo mama yake alimshika mkono akaondoka nae Baada ya kuwashukuru sana wazazi wangu ila Derick kuondoka kwake jicho lilikuwa kwangu hata walipopanda gari aliendelea kunitazama Mpaka mama akanitania kuwa mtoto wa watu watanifunga* hivo ndo ilivyokuwa.
Nilimaliza kumsimulia tukawa tayari tumefika magereza kabla hatujaingia ndani latina alinishika mkono na kuniuliza: Baada ya hapo ilikuwaje?
Nikamjibu: sikumwonaga tena Mpaka miaka Sita ikapita bila salamu wala kumwona.
Latina: sasa mbona wewe uliniambia mlikuwa wapenzi embu niambie vizuri.
Nikamjibu: Ntakwambia tukitoka kumwona baba.
Tuliingia ndani, Baada ya muda baba aliletwa tukakumbatiana kwa furaha maana siku zilikuwa nyingi bila kumwona tukiwa tumekaa baba aliniuliza: maisha huko yanasemaje mbona siku nyingi mama yenu haji kuniona hata Nyinyi pia nilikuwa na wasi wasi mkubwa.
Tulitazamana machoni Mimi na Latina ndipo nikamjibu: baba sorry kwa hilo?
Baba: Ila Nyinyi wawili Mnasoma vizuri kweli? Maana msiwe mmevunjika moyo kisa mimi mpaka mkaacha shule.
Nikamjibu: tunasoma baba ila I'm sorry tumeshindwa kumfanya mama aweze kulichukulia swala lako kikawaida.
Baba: una maana gani?
Nikamjibu: ukweli mama kwasasa amepatwa na ukichaa toka uhukumiwe.
Baba alishusha pumzi na kuniuliza: kivipi sasa?
Nilianza kulia ndipo nikamjibu: kwasasa yupo kwenye hospito ya vijaa Ila sorry.
Baba: usiseme hivo Namjua mke wangu ananipenda sana ndo maana yote yametokea.
Nikamjibu: Ila usijali tutakutoa jela.
Baba: miaka mitano ni mingi sana mnisamehe Watoto wangu siwezi kuwapa vile mnavyovihitaji kama baba.
Nikamjibu: usiseme hivo baba Sisi tunajitosheleza Kikubwa wewe mzima kuhusu Sisi isikupe tabu kwasasa tupo watu wazima na kuhusu mama atapona Allah yupo.
Baba alitushika Mimi na mdogo wangu akatulaza mabegani kwake ili kutufariji kisha akasema: nikiwaona nafarijika Sana.
Baada ya muda tulitoka magereza, tukiwa tupo mlangoni kwa mbali nilishtuka kuona gari ya Derick aliokuja nayo Muda Si mrefu shuleni nikajuwa atakuwa Yeye kichwani nikaanza kuwaza Huyu mtu kufuata nini huku?
Kabla...........
Unahisi nini kitatokea!
Usikose mkasa huu!
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment