MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 03
TULIPOISHIA: Baba alitushika Mimi na mdogo wangu akatulaza mabegani kwake ili kutufariji kisha akasema: nikiwaona nafarijika Sana.
Baada ya muda tulitoka magereza, tukiwa tupo mlangoni kwa mbali nilishtuka kuona gari ya Derick aliokuja nayo Muda Si mrefu shuleni nikajuwa atakuwa Yeye kichwani nikaanza kuwaza Huyu mtu kufuata nini huku?
Kabla...........
SONGA NAYO!
Kabla gari lile halijatufikia nilimshika mkono Latina na kukimbia nae Mpaka kwenye mfereji mmoja uliokuwa pembeni ya barabara ya kutoka magereza kuelekea mjini, Latina akiwa haelewi elewi alipandisha kichwa juu akaona gari inapakiwa mbele ya mlango ndipo nikamshusha kwa haraka na kusema: unataka nionekane?
Latina: Mbona kama vile gari la Derick.
Nilimnyamanzisha: shiiiii!!!
Latina alitabasamu kisha akapandisha kichwa taratibu akamwona Derick anatoka kwenye gari na Rafiki yake wakaingia magereza ndipo akasema: wameingia hivi wamekuja kufuata nini?
Nikamuuliza: wameingia ndani?
Latina: ndio.
Nikamjibu: twende nyumbani.
Tulitoka hapo tukikimbia Ila Latina alikuwa bado hajajuwa chanzo cha Mimi kukimbia, tulipofika mjini tulijipumzisha ndipo Latina akaniambia huku akiwa ameyashika magoti yake: hakikisha utoe sababu za msingi za kumkimbia Derick.
Nikamjibu: ni sawa ila kabla ya kwenda nyumbani twende kumwona kwanza mama.
Latina: sio mbaya Ila dada haya yote ya nini?
Muda mdogo simu yangu iliita nikapokea na kuuliza Nani mwenzangu maana namba Ilikuwa ngeni, ajabu sauti ya Derick iliskika akiniambia: Najma Kwanini unanifanyia hivo?
Nilichomoa macho na kumuuliza: kukufanyia nini?
Derick: sielewi Kwanini unanifanyia haya yote basi please Nipe muda tuongee.
Nikamuuliza: namba zangu kakupa Nani?
Derick: kwasasa natoka magereza nilienda kumuona baba yako Kanipa namba yako embu niambie upo wapi nije tulizungumzie swala la baba yako?
Nikamjibu: swala la baba yangu liache hivo na usinipigie tena.
Nilikata simu kisha nikazima kabisa ili asinipate tena ndipo Latina akaniambia: wewe ni mjinga wa kiasi gani ila sorry kwa kukuita hivo ila unayataka wewe.
Nikamjibu: acha iwe hivi.
Latina: ila ungekubali Labda angetusaidia!
Nikamjibu: Sina imani hivi Latina Mbona unaongea Sana unajuwa kilichotokea Baadae?
Latina: Kwani kilitokea kitu gani?
Nikamjibu: baada ya pale.......
Nilianza kumsimulia* Derick hakuweza kuonana Nami mpaka nikamsahau kabisa nilipokuwa nasoma secondary hapo nilikuwa na miaka 18 Derick alikuja shule Kama hivi alivyotangazwa chuo aliponiona tu akaanza kuniomba msamaha Oohh amenimiss Ooohhhh siku nyingi kweli ukweli Na Mimi nilikuwa nimemmiss alinichukuwa kama siku ile utotoni nilivyo zeze nikaanza kumtembeza eneo mbali mbali nikajikuta nimevutika nae Mpaka nikasahau nyumbani, Derick alinipeleka supermarket akaniomba nichague vitu vinavyoendana na milioni kumi ile hela alioniahidi ila kwa kuwa Mimi nilimsaidiaga kipindi kile kiroho Safi sikutaka anilipe nilikataa ila akazidi kunilazimishia Ila sikuwa tayari, alinipeleka kwenye hoteli kubwa akaagiza chakula cha thamani tukala wote kwa furaha hakika nikazidi kuzama kwake, Baada Ya hapo alinipeleka kwenye movie kama vile vile siku Zile tupo wadogo ila tuliangalia movie inayohusu watu wawili wanaopendana kwa dhati movie ya Romeo na Juliet Baada ya kuona movie ile Ilikuwa tayari ni saa moja usiku Tulitoka nikidai kurudi nyumbani mapema Kama siku Zile tulirudi nyumbani mdogo mdogo kwa mguu huku akinisindikiza Hakuna Aliekuwa akiongea na mwenzie sikujuwa ni Nini ndipo aliniomba nisimame nikasimama akazunguka nyuma yangu Akachomoa kitu mfukoni Kumbe kilikuwa ni kidani chenye thamani ya milioni tano akanivalisha, nilifurahi Nikamuuliza: chanini hichi?
Alisogeza mdomo wake karibu na skio langu la kulia Akanijibu kwa sauti ya Chini saana huku akiwa bado yupo nyuma yangu: Naomba kama hautojali niweze kuwa kama Romeo mbele yako.
Sikuamini kwanza nilisisimka mno kwa pupa nikageuka kumtazama tukagonganisha Vichwa Tulianza kucheka hovyo ndipo akaniambia: I'm serious about this! Nipe nafasi ukweli nilikupenda toka siku ile bado tupo wadogo unajuwa nilitamani Sana hii zawadi nikuvishe maana niliachiwa na marehemu bibi yangu aliniambia cheni hii alivalishwa na Babu siku ya kwanza anamuomba uchumba akaihifadhi miaka hamsini ndo akanipa Mimi ili ikafikia hatua nikampata nimpendae basi nimpe zawadi hii please Najma Nipe nafasi hio.
Ukweli sikutaka kumficha maana hata mimi nilitokea Kumpenda nikamkubalia Akachomoa milioni kumi akanipa akimaanisha siku ile tuliahidiana atanipa Ila hakunipa Ila Leo hii ameniletea ahadi yangu ukweli sikuzichukuwa pesa zile maana Mimi sizowei kula vya watu vingi.
Alinipeleka Mpaka nyumbani hakutaka kufika Tuliagana akarudi, ukweli siku hio sikuweza kupata Usingizi ukija kumwangalia Derick nikijana na kila Sifa ya kuitwa mwanaume hata ya bila pesa, kila Mara nilimtumia ujumbe hata Yeye pia Alinitumia ujumbe, Uliza sasa Baada ya Yeye kurudi kwao kama Ndo wingereza.*
Latina akaniuliza: Kwani ilikuwaje?
Nikamjibu: hata salamu, hata simu, basi hata barua ya bure mwenzio niligeuka kichaa chakula kilikuwa hakipiti kinywani ukweli mdogo wangu wanasema Hisia mtu pekee ndie anaziendesha Ukitaka Kumpenda mtu Sana ni wewe Ukitaka kumchukulia Poa ni wewe ila kwangu hio haikuwepo Nilishindwa kabisa kuzizuia Hisia zangu kwake kila siku nilikuwa mwenye majonzi nikiamini Ipo siku ntapata ujumbe kutoka kwake ila Mpaka sasa Leo hii ndo anarudi anakuja na ukichaa wake ohh tuonane au anataka anifanye kama siku zote akija huku niwe wa kumliwaza, Mimi sio mwanamke wa Aina hio mdogo wangu.
Latina alishusha pumzi na kuniuliza: kwahio ile cheni unayokuwaga nayo siku zote ndo hio aliokupa?
Nikamjibu: ndio.
Latina: inathamani ya milioni tano?
Nikamjibu: ndio.
Latina: heee! Mbona tunapata pesa ya kumtunzisha mama.
Nikamjibu: kwahio tuuze?
Latina: Eee.
Tulikubaliana hivo tukaalisha safari ya kuelekea kwenye hospital ya Vichaa tukaelekea nyumbani ili tukauze ile cheni, tulitafuta mteja siku hio kila tuliekuwa tukimpa anadai atupe Elfu hamsini wengine Mpaka Elfu ishirini tukajikuta tunakata tamaa.
Baada ya siku mbili kupita nikiwa nipo darasani huku somo likiliendelea professor aliendelea kutoa somo mwishowe akaanza kugusia ugonjwa wa Ebola: ugonjwa wa Ebola umekuwa sugu kwasasa Mpaka nchi jilani Kenya watu asilimia 2 wamengundulika wana ugonjwa Huo Na kwasasa ambao wameshapoteza maisha ni watu stini hii Hali imeitia Hofu nchi yetu sana Kikubwa mjilinde msipokee Wageni kwasasa Mpaka ugonjwa huu utulie.
Tulipotoka wanafunzi walianza kulijadiri swala lile ndipo Rafiki yangu Joyce akanifuata na kuniambia: unajuwa Najma Mpaka sasa mambo yako siyaelewi.
Nikamjibu: Rafiki yangu Matatizo ya familia.
Joyce: pole Ila huu ugonjwa wa Ebola umekuja kwa kasi kubwa Sana tofauti na siku zingine.
Nikamjibu: kwanza nimeshangaa kuskia.
Joyce: aisee siku hizi zote ndo habari ya mjini ila ni kwasababu wewe Upo kwenye wakati mgumu ndo maana hujali chochote.
Nilitabasamu kisha tukaendelea kuelekea nyumbani.
Baada ya siku tatu ugonjwa Huo wa Ebola Ulianza kusadikika kuwa tayari vijiji jilani na Kenya baadhi ya watu wamepimwa ikagundulika virus hio imewapata, Raisi wetu Pamoja na viongozi wengine wakiwemo wanasayansi wakubwa wa nje walichanganyikiwa mno kila siku kwenye vyombo vya habari waliwatuliza wana nchi wasijali ni ugonjwa mdogo utaisha Ila wajilinde Sana Kama atatokea mtu yeyote mwenye dalili zifuatazo kama kuchemka sana (homa Kali) hivo usimguse yakupasa ukatoe taarifa kwenye vituo maalumu walivyoviteua.
Chuoni kwetu maprofesa walianza kuchakachua vitabu mbali mbali vinavyohusu ugonjwa wa Ebola hivo kila somo tuliokuwa tukipewa ni kuhusu Ebola ni namna gani tunaweza kujiepuka na ugonjwa Huo ikiwezekana kuuteketeza mazima.
Siku hio mimi na Latina tulikuwa chumbani huku tukijadiri kuhusu ugonjwa Huo.
Latina: mbona kila mwaka ugonjwa Ukitaka kuamka huwa Unaanza Kongo?
Nikamjibu: ndio inasadikika watu wanaoishi mapolini wanakula nyamafu sana bila kujuwa wanyama Hao wameuwawa na Nini hivo wanajikuta wanaambukia na wanaanza kuambukiza wengine.
Latina: hapo sasa ndo nataka kujuwa, hao minyama wanapatapataje Huo ugonjwa?
Nikamjibu: mara nyingi Nyani ndo wanaleta ugonjwa Huo.
Latina: kwahio Nyani akishakufa wao wanamla bila kujuwa nikipi kimemuua si eti?
Muda Huo simu yangu iliita nikapokea na kuuliza: huwezi kupiga Muda mwingine tofauti na huu?
Alikuwa ni Joyce Akanijibu: nakupigia muda wowote ninaojiskia Upo!
Nilitabasamu na kumwambia: Umekosa Usingizi mi nakujuwa.
Joyce kwa sauti ya Chini akaninong'oneza: oyo niskilize kwa umakini wanasayansi wakubwa nahisi kuna Jambo ambalo wameligundua kuhusu Ebola ila bado Ni Siri sijaelezewa vizuri.
Tuliangalia na Latina maana nilikuwa nimeweka kwenye sauti ya Juu sana ndipo Nikamuuliza: Nani kakwambia?
Joyce: si Unajuwa kuwa professor Rodrigo ni mpenzi Wangu.
Nikamjibu: fuatilia vizuri Utanipa habari nzima sawa.
Joyce: Poa.
Asubuhi ilipowadia chuoni walitutangazia turudi nyumbani tutaanza kusoma hili swala likishatulia hivo walituomba tukakae majumbani kwetu kwa usalama zaidi maana tayari ndani ya jiji la dar es salam imebainika kuna mtoto amengundulika anaugonjwa Huo hivo Nihatari sana kwetu kukaa sehemu moja, tulipotoka tu majadiriano Kati yetu wana chuo yalianza hakika swala hilo liliyayusha Ubongo wa watu wengi, nikiwa narudi nyumbani Pamoja na Latina Joyce alikuja na kuniomba tuongee nilimwambia Latina aende kumwangalia baba jela ikiwezekana akamwambie kuhusu Hali halisi ya nchi aweze kujilinda huko, Mimi na Joyce tukarudi nyuma, tulielekea moja kwa moja kwenye Ofisi ya professor mkuu wa chuo hicho tukamkuta professor Rodrigo mpenzi wake Joyce amekaa ndipo tukamsalimia na kukaa, Rodrigo kwa sauti ya Chini kama vile anajiogopa akasema: Najma nikizani unanijuwa Mimi Nani?
Nikamjibu: ndio wewe ni professor Rodrigo mtoto wa professor mkuu wa hapa.
Rodrigo: sawa kwahio baba yako unajuwa anadaiwa shiingapi hapa?
Nikamjibu: ndio Najuwa ila pesa hio kwasasa Hawezi kuilipa maana yupo jela.
Rodrigo: sawa kwasasa hapa wewe na mdogo wako mnadaiwa milioni kumi bado baba yako yupo jela inatakiwa mmtowe kwa milioni tano ili asipige miaka mi 5 huko na bado mama yako ni mgonjwa anatakiwa afanyiwe matibabu nikihisi ili apone inaweza kughalimu milioni moja na nusu au milioni mbili, Najma unawapenda wazazi wako pia hata wewe unajipenda, vipi hio hela utaitoa wapi?
Nilijiinamia nikashindwa nimjibu nini ndipo akaendelea kusema: ndo maana Nimekuita hapa uje tulijadi swala lako ikiwezekana lipatikane utatuzi.
Machozi yalikuwa tayari yameanza kuelelea machoni kwangu ndipo Rodrigo akasema: usijali hapa kuna inshu ya Chini Chini inaendelea Ila bado ni Siri na inahitajika iwe Siri ndo maana nimewaiteni hapa kwenye Ofisi ya baba yangu nilijuwa kuna usalama Tosha kwanza kwa hili ninalotaka kukwambia ulimeze usisubutu kumueleza mtu yeyote.
Nikamjibu: siwezi kufanya ujinga Huo.
Rodrigo: huu ugonjwa wa Ebola umekuwa tishio kubwa hapa nchini na sio hii nchi tu Mpaka Kenya burundi sasa hivi Hali ni mbaya sana haswaa kongo ndo usiseme kabisa, hapa tumefanya uchunguzi tumegundua chanzo cha ugonjwa huu wa Ebola.
Mimi na Joyce tulishtuka na kumuuliza: unasemaje?
Rodrigo: semeni taratibu.
Joyce: kwahio mmejuwa chanzo?
Rodrigo: ndio huo ugonjwa wanyama wanautoa kwenye mti flani uliopo ndani ya msitu wa Equatorial mti Huo ukitoa matunda wanyama Kama Nyani wanayapenda sana matunda Yale wanayala mwishowe yanawaletea maradhi wanakufa na watu wakiona Mnyama amekufa wanamchukuwa wanamchoma hawahakikishi wanamchoma vizuri ili mavairasi yaweze kufa wanamla hata hajawiva vizuri madhara yake ugonjwa unatoka hapo.
Jasho Ilikuwa imeanza kutufumuka Mimi na Joyce ndipo Nikamuuliza: kwahio Sisi tunafanyeje?
Rodrigo: hapa kuna kikosi kinaandaliwa watu Kama kumi na tano hivi ila ni kimya kimya licha selekali inajuwa ila laia hawatakiwi kujuwa chochote wameona wachague wanasayansi ambao maswala haya wanayaelewa vizuri waende kutalii huko ikiwezekana wajuwe chanzo cha ugonjwa huu ili swala Hili liweze kuchukuliwa hatua bado mapema hata Mimi hapa Nipo miongoni mwahao waliotuliwa, sasa nimewaita ili kuwashilikisha ikiwezekana nanyi muungane nasi.
Moyo wangu ulisita Ila Joyce alikubali ndipo Rodrigo akaniuliza: Najma haupo tayari?
Nikamjibu: nahisi sipo tayari.
Rodrigo: vipi kuhusu wazazi wako? Na vipi kuhusu madeni ya baba yako?
Joyce akadakia: Najma kubali Baada ya zowezi hili tutapata mabilioni ya pesa acha kuwa mzembe.
Nikamuuliza: sasa Rodrigo itakuwaje mbona Mimi sielewi.
Rodrigo: tunaelekea huko Kongo ndipo kuna msitu Huo wa Equatorial sema Ndio au Hapana maana hapa hatuna muda je Upo tayari?
Unahisi nini kitatokea!
Usikose mkasa huu!
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment