NAMNA MVULANA ANAVYOWEZA KUTAMBUA DALILI ZA MSICHANA ANAYETAKA KUISHI PAMOJA - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

Monday, May 13, 2019

NAMNA MVULANA ANAVYOWEZA KUTAMBUA DALILI ZA MSICHANA ANAYETAKA KUISHI PAMOJA

20190326_124716



FB_IMG_1552928218281


Wavulana wengi nao wameishia kuoa wanawake ambao kwa hakika hawawapendi lakini walichopendewa huenda umaarufu, kazi nzuri, fedha zake, au anataka katika familia ya kitajiri ama msichana amekosa aliyemtaka kwa hiyo anaolewa na huyo ili kumkomesha mvulana aliyemkataa. Ukweli wa mambo ndoa hiyo haitakuwa na mibaraka na furaha ya kweli bali huzuni kwa wakati mwingi maana hakuna upendo wa dhati. Sasa Mvulana utatambuaje kuwa msichana huyo anakupenda kwa dhati.
Zipo dalili za muhimu sana mvulana ataziona kutoka kwa msichana wa kweli.
  1. Ni binti ambaye anajiheshimu na pia akutanapo na wewe uso wake unaonyesha tabasamu la dhati.
  2. Macho ni dalili kubwa kupita zote. Maana anapokutazama anajisikia haya. Mtaalamu mmoja alisema “Macho ni dirisha la roho (nafsi).” Wapo wengine ambao macho yao kila wakati ataelekeza kwako kuonyesha umakini wa kukusikiliza wewe kuliko mtu yeyote. Mara nyingi atakuwa anakukodelea macho yako sio mahali popote. Kisha anakuwa na aibu nyingi kwako. Wavulana huwa wanaangalia wapi? Unajua!
  3. Mazungumzo yake kwako yanaonyesha heshima na tahadhari kubwa sana maana anakitu anataka ukione chema kutoka kwake. Anapenda kuzungumza mambo unayovutiwa nayo.
  4. Msichana anapenda kuwepo mahali ulipo kila wakati. Kama ni kanisa atataka benchi unalokaa liwe sambamba ama kikundi chako awepo. Ama safari zozote unazopanga kwenda naye hata kama hakutaka kwenda anakwenda. Tena anasema kama unaenda nami nitaenda. Hiyo ni dalili nzuri kabisa. Chuoni mwalimu anapowapa zoezi la kikundi atatafuta kukuangalia kwa sekunde chache ili kuonyesha muwe pamoja kwa zoezi hilo.
  5. Anakuwa ni msichana anayesikiliza mambo yako kwa makini na kutaka kujua mambo unayopendelea katika maisha. Huwa anapenda kuuliza maswali mengi yanayohusu maisha yako ya baadaye. Anakuwa na kumbukumbu za mambo yako mengi kuliko wewe. Anatamani kukuuliza kuwa unapendelea au vipi kuhusu jambo hili? Ujue ni ishara
  6. Lugha ya mwili:
i.                     Kuelekeza macho upande wako kila wakati,
ii.                  kutaka kushikana mikono kwa salamu ama anapocheka atataka kugongeana mkono na wewe ama kukushika mahali popote aidha kichwani au mabegani.
iii.                 Tabasamu kila mara akuonapo na kidevu chake kinang’aa kwa furaha.
iv.                kukutetea mara kwa mara unaposhutumiwa,
v.                  na anapogundua unapenda aina gani ya rangi za nguo au nywele atafanya kama upendavyo.
vi.                Anapokaa anapenda kuweka miguu yake kama x na kisha kubadilisha mara kwa mara. Ule mguu wa juu utakuwa umeelekea kwako nayo ni dalili kwako.
vii.              Msichana anayekupenda atakuwa anapenda kugusa midomo yake (lips) ama kuuma uma au kuchezea glass ya maji au kitu chochote mkononi kuvuta usikivu wako. Pia kuchezea nywele zake au wanaovaa hereni au bangili watazichezea.
viii.            Labda hapa utahitaji X-ray kuangalia hili: anapokuona tu utaona mboni za macho yake zitacheza cheza kuonyesha shauku aliyonayo kwako. Mboni za macho yake zitaisaliti tamaa au shauku yake kwako. Mboni (dilated) zake zinapanuka sana.
ix.                Anapokuona kwa mara ya kwanza ananyanyua Nyusi zake kwa haraka sana kwako. Hata wanaume linatokea ila kwa wasichana ni tendo la haraka zaidi. Amini usiamini ni jambo la hakika kwa mtu unayevutiwa naye siku zote nyusi zako zitainuka na kuanguka kama ishara ya msisimko. Inachukua kiasi cha robo sekunde kucheza kwa kila mtu duniani kote. Kwanini? Kupandisha nyusi kunafungua zaidi macho kupata Mwanga zaidi ili kuona kwa usahihi unachotaka.
x.                  Kukuonyesha kiganja chake cha ndani (wrist) ni aina nyingine kuwa anakupenda.
xi.                Msichana mwenye aibu: kichwa atainamisha chini kisha atakuangalia kupitia kope (eyelashes) zake kwa juu zikiwa zinatazama chini. Halafu anaogopa ama kuwa na wasiwasi zaidi (increasingly Nervous).
xii.               
  1. Msichana anatamani kujua habari za wakati wako ujao utakuwa wapi. Mnapoagana anaweza kukuuliza utasali wapi wiki ijayo? Je utakuja maombi? Wikiendi utaitumia wapi
  2. Zingatia kwamba Msichana anayekimbilia mfanye naye mapenzi anataka kujihakikishia usalama wake kimwili kwako lakini sio kwamba anakupenda kama mtu kamili mwenye heshima zake. Hivyo ikiwa kweli anakupenda hata kubali kulala nawe kwa kuzini.
  3. Msichana anayekupenda ataepuka mara nyingi kula mbele yako. Anatamani sana kukuvutia wewe. Kumbuka wasichana wengi hawajisikii amani dhidi ya mkao wa kula.
  4. Msichana atakuwa ni mtu wa kujihami sana dhidi ya watu wanaotaka kufanya udadisi juu ya mahusiano yako na yeye. Hataki watu wajue hilo haraka.
  5. Msichana atakuwa mgumu kukubalia na jambo lolote unalozungumza vizuri juu ya msichana mwingine.
  6. Msichana atakuwa ni mtu anakueleza mafanikio yake mengi anapohitaji kupata pongezi au sifa kutoka kwako.
  7. Msichana anajenga uadui ama kutopendezwa na wanawake wowote wanaonekana kuwa karibu na wewe. Atakuwa anatumia lugha ya ukali au kujitenga nao.
  8. Msichana atatamani kukutambulisha kwa marafiki zake na pia kukutana na wa kwako.
  9. Msichana atakuwa wazi kukueleza siri zake ambazo hajamwambia mtu yeyote kisha atataka ushauri kutoka kwako. Hiyo ni dalili tosha kuwa anataka urafiki kwako.
  10. Msichana atakuwa anapenda kukualika kwenye sherehe Fulani Fulani ama matukio Fulani ama matembezi maalumu. Usimuhukumu haraka kuwa ana mwenendo mbaya bali msikilize atajifunua kwako. Anaweza hata kutuma marafiki zake ambao aliowatambulisha kwako lakini anaowaamini kukueleza kusudi lake wazi wazi.
  11. Msichana atakuwa anakutazama kwa kuibia mara nyingi unapofanya mambo yake huku akitabasamu ama mnapoachana atakuwa anakuangalia sana na mara unapogeuka bila yeye kutazamia atatabasamu kwa fumanizi hilo.
  12. Wakati msichana anapokuwa na marafiki zake kisha mara unapoingia mahali walipo unakuta wote wananyamaza kimya ama vicheko vya kipumbavu vinakoma na kutaka kuondoka ni dalili kuwa tayari amekiri mbele yao penzi lake kwako.
  13. Msichana anakosa raha na uchangamfu mara anapogundua una jambo linakusibu ama unapougua. Hata na yeye anaugua kwa kukuhurumia wewe. Atatoa taarifa kila mahali juu ya kuumwa kwako. Atahitaji kukusaidia katika tatizo lako.

Kipimo ambacho Mwanaume unaweza kuthibitisha kuwa msichana anakupenda:
  1. Ikiwa unapenda mzaha msichana atapenda kuleta mizaha itakayokufanya ucheke naye lakini akiwa na tahadhari nyingi asije akakukwaza ama kumuona mhuni. Mvulana ili kuthibitisha hili zungumza kitu cha kichekesho mkiwa kikundi cha watu hata kama hakichekeshi sana msichana yule atacheka sana kwa ajili yako. Lakini akitabasamu tu atakuwa anakuhurumia tu.
  2. Msichana anapokuwa amependeza msifie kuwa leo umependeza kweli: ikiwa anakupenda atacheka na hata kukusogelea zaidi kwa kugonga ama kukusukuma kidogo.
  3. Msichana unapojaribu kuongea naye anajisikia aibu sana kuliko wavulana wengine anaowachukulia kama marafiki tu.
  4. Unapowaona marafiki zake wanakusogelea wewe zaidi na yeye anakuwa mbali nawe, tambua ni dalili kuwa huenda amewatuma. Watakuwa wanakuzungumzia habari zake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad