KIJANA MWENYE SIFA HIZI HAWEZI TULIA AKIOA - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, May 27, 2019

KIJANA MWENYE SIFA HIZI HAWEZI TULIA AKIOA







1.Anaigiza maisha,,,anataka kuonekana amefanikiwa kimaisha,,hajui kama anajidanganya mwenyewe.
2.Hana mipango inayoeleweka,,,,,,anajua kuongea lakini mipango ni sifuri,,,hajui kwamba kuanza mahusiano ni kubeba majukumu.
3.Anataka ngono kabla ya ndoa,,,akipewa anasema binti hana hofu ya Mungu,,asipopewa anatishia kuvunja mahusiano au kuwa na msichana mwingine.
4.Ana wivu unaowaka kama moto wa nyika,,,,anaweza kumkataza mchumba wake asiongee na mwanaume mwingine au asifanye kazi kwasababu boss wake atamtaka au anahisi kazi ile kapewa na mwanaume.
5.Ana hasira mithiri ya mbogo aliyechokozwa,,,,,anaweza kumpiga mpenzi wake au kumtukana,,ni katili,mdhalilishaji na anapenda kusikilzwa kila amri atoayo.
6.Hajui lolote kuhusu Mungu,,,na hana muda wa kutafakari habari za Mungu.
7.Ni tegemezi,,,,anategemea wazazi au kupiga mizinga kwa ndugu au marafiki ili kumudu mahitaji yake ya kila siku.
8.Si mtoaji kwasababu hana kitu cha kutoa,,,,ukimweleza shida zako hashindwi kukwambia unapenda pesa au anaweza kusema mimi sio baba yako.
9.Anapowaza kuhusu ndoa anawaza ngono tu,,,,,hafikilii kuhusu majukumu ya kula familia na mipango ya maendeleo ya familia.
10.Hajui kusifia anachojua ni kukosoa tu,,,,,anataka kupewa sifa zote hata ambazo hastahili.
11.Hujiona bora kuliko wengine na mara nyingi anapenda kushindana na watu bila sababu.
12.anapenda maisha ya maonesho(show off),,,,,Anaweza akapiga picha kwenye gari ya rafiki yake akaandika status"my new ride"anaweza kutamani hata kuombea mkopo,,,akipanda ndege hawezi kuwa na stori nyningine zaidi ya safari ya angani,,akipata nafasi ya kupiga picha na mtu maarufu basi hudhani na yeye ni maarufu na hudhani mafanikio ya mtu yule yamehamia kwake.
13.Mvivu,,,,hawazi juu ya kesho yake ,,,anaanza mradi na kuishia mwanzoni(sio njiani)kwasababu lengo ni kuwanasa wanawake wapumbavu.
14.Anashinda online anachat,,,,na anajua wazi hana biashara anayofanya mtandaoni,,,,mitandao ya kijamii imeteka maisha yake,,,haongezi tija wala maarifa ya msingi katika maisha yake.
15.Anazijua sifa zote za wife material lakini yeye hana hata sifa moja ya husband material.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa