HATA KAMA MNASHIRIKIANA KWA KILA KITU HAKIKISHA UNA KITU CHA ZIADA - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, May 24, 2019

HATA KAMA MNASHIRIKIANA KWA KILA KITU HAKIKISHA UNA KITU CHA ZIADA



Ni jambo zuri kwa mwanamke na mwanaume kuweka vipato vyao mezani na kupangia matumizi,,hata kama mwanamke hana kazi lakini mwanaume unapaswa kumshirikisha katika mambo yako muhimu hasa katika kupanga matumizi ya familia,,lakini mwanaume unatakiwa kujua kuwa wewe ndo kichwa cha familia,,,,
Kichwa cha familia nikimaanisha kuwa katika kila kitu kinachotokea ndani utaulizwa wewe,,kuna wanaume wana tabia moja,akipata mshahara anampa mke wake apangie matumizi,ni jambo zuri pia,lakini ni vizuri kama una kipato kingine cha ziada ambacho mke wako hakijui,,kama mwanaume unatakiwa kujua mambo mawili makubwa ambayo yatakusaidia kujua namna ya kutumia pesa zako,,
Jambo la kwanza ni kwamba wanawake wanajua kwamba mwanaume muda wote ana pesa hata kama anajua mshahara wako,,hata kama umpe mshahara wote yeye apange lakini katika kichwa chake anaamini kuna sehemu unapata pesa na hata kama ulimpa anaamini kuna zingine unazo,,kwa maana hiyo acha kumpa narudia tena acha kumpa pesa zote na hakikisha unakuwa nazo kukiwa na tatizo kubwa,,
Jambo la pili ni kuwa mwisho inarudi kwako mwanaume mambo yanapokuwa magumu,,hapa namaanisha kuwa,kama umempa mke wako pesa zote na akajua kuwa huna,,makini likitokea tatizo na yeye kashazimaliza usidhani ataenda kwa baba yake kuomba hapana,,mtoto akiumwa kalazwa hospitali basi atakuja kwako hata kama alikuacha mtupu,,
Hivyo utakuwa mwanaume wa ajabu sana tena ambae hajielewi kama mtoto ataumwa na mke akakugeukia halafu useme pesa zote ulimpa,,hivyo kama mwanaume unapaswa kuwa na akina NA sio tatizo linalotokea mnaanza kuangaliana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa