Dalili 9 zinazoashiria kuwa uko kwenye mahusiano hatarishi - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

Sunday, March 24, 2019

Dalili 9 zinazoashiria kuwa uko kwenye mahusiano hatarishi

20190326_124716

FAHAMU MAHUSIANO YAKO KAMA YANA BENDERA NYEKUNDU
images+%252847%2529
Mahusiano yeyote yanaweza kuwa hatari kwa wakati wowote, mahusiano mabaya sio tu yale ambayo yamefika mwisho na kutengana kwa wapenzi au wanandoa, mahusiano yanaweza kuwa hatari hata wakati wa mwanzo tu wa kuanzisha uhusiano na hata wakati mahusiano yakiendelea, muonekano wa dalili mbaya,kwa wapenzi, wachumba, marafiki na familia, mahusiano yeyote yenye kuonyesha dalili mbaya zilizoorodheshwa hapo chini ni hatari sana katika afya yako ya kimwili, kiakili au kihisia na ni chanzo cha kushindwa kufanya kazi kama za kiuchumi vilivyo na ni sababunya watu wengi kurudi nyuma kimaendeleo.
Lakini kuna sababu nyingi kwa nini watu bado wanaishi katika mahusiano ya HATARI
sana,wengine hawafahamu, wengine hawataki kuamini kama mahusiano yao ni hatari kwa kujua wapendwa wao watabadilika baadae, wengine wakihofia kupoteza vitu vichache walivyonavyo kama zawadi, Mali, maisha mazuri n.k, wengine wamezoeshwa hiyo hali ya kuishi kibabe tangu waingie kwenye mahusiano, hivyo sio tatizo tena kwao bali ndo maisha yao, badala yake wameendelea kuishi maisha hayo kwa ujasiri was woga na hofu na makovu ya maumivu ya mwili na akili ambayo ni vigumu sana kupona.
⏩DALILI HATALI ZAIDI ZA KUANGALIA
. Kwa baadhi ni rahisi kuona na kutafsiri dalili mbaya katika mahusiano ambazo huwafanya wakose amani na furaha maishani mwao kwa mda wote watakaao kuwa na wenza, ndugu, au jamaa zao na hata marafiki pia, kwa mfano; unadhani dalili hatari za mahusiano ni mpendwa wako kutumia madawa ya kulevya, ulevi ulokithiri wa pombe, kuchepuka n.k. Lakini pamoja na hayo yote ukweli ni kuwa kuishi katika mahusiano ya aina hiyo ni kupeperusha bendela nyekundu, Ebu tuangalie dalili hizi mbaya hapa chini
⏩Fujo za mara kwa mara (Aggressiveness)
Tabia yeyote inayohusisha fujo na uchokozi ni hatari katika mahusiano yeyote ile, inaweza kuwa fujo ya maneno yaliyojaa kulenga kumuumiza mwingine kifikra, lakini pia mbaya zaidi ni fujo za kimwil (actual physical aggressive behavior). Tabia yeyote ya kulazimisha, kupiga kusukuma na kushinikiza ni dalili za ukatiri, na kama MTU ana kupenda hawezi kufanyia mambo kama hayo. Kuwa makini sana uonapo mpenzi wako anamalizia hasira zake kwa mfano: kupiga vitu ndani kwa hasira au kujipiga kifua na kujiraumu dhidi yako ipo siku hiyo mikono itakufika wewe, maana bendela nyekundu inapepea inasubili tukio, hivyo kuwa makini.
⏩Udhibiti usio wa kawaida (control)
Kutokuwepo mgawanyo unaokaribiana wa maamuzi ni tabia na dalili mbaya na hatari katika mahusiano, tabia hiyo huanza pale mtu anapomuona mwenzie hana thamani au duni, watu wengi was tabia hii hutaka kudhibiti mahuasiano na kuyaendesha watakavyo kwa kutegemea unawafata, hupenda kuhararisha amri zao na tabia zao hizo kuwa msaada, au kwa kusema kuwa wanajuwa kilicho bora kwako, wengine huenda mbali zaidi had I kuingilia matumizi ya simu za wenza wao kama SMS, calls, au emails na kutaka kujua kila kitu kitokacho na kiingiacho, hii ni bendela nyekundu ndani ya mahusiano
⏩Kujimilikisha (Possessiveness)
Tabia ya mtu kujifanya anakupenda sana na kukumiliki visivyo kawaida huwa wanaificha na kujifanya ni watu wenye WIVU SANA, atakwambia kuwa ni kwa sababu anakupenda ndo maana anafanya hivo, mfano; kukuzuia kwenda sehemu furani, kujisingizia wao ni wagonjwa hasa wanawake au kwa kutengeneza ugomvi, kumbuka hali hiyo sio upendo kabisa bali no kukosa uaminifu, na hii hutokana na hasa yeye mhusika kuwa na tabia mbaya na kudhani kuwa wew pia utafanya, wengi wao wamedhoofika kifkra na kugeuza huu umilikiwaji kama upendo kutoka kwa wenza wao lakini mpendwa huu sip upendo bali ni kunyemelea, mwenendo wako na siku akikubahatisha bahati mbaya utashuhudia tukio baya,maana tayari unapeperusha benders nyekundu kwenye mahusiano.
⏩Kujipendelea na ubinafsi(Self-centeredness)
Wote kwa pamoja tuna ubinafsi hili halipingiki,na ni mhimu sana kuwa na roho ya ubinafsi kipimo cha kutoathiri wengine, Inakuwa mbaya na hatari sana pale ubinafsi unapoingia katika mahusiano ya watu wawili na zaidi, inakuwa mbaya zaidi hasa mmoja anapofaidika na mahusiano na mwingine hafaidi, mfano; hawana mda wa kuhesabu na kusoma hisia za mwingine na anachopendelea, no wagumu kutoa support ya hali na mali, wanajitahidi sana kuwajumuisha wenza wao katika mambo yao binafsi lakini inapokuja kwa upande wa pili ni wagumu na hutoa Sababu zinazolenga kukosoa,sasa inapotokea mmoja hajaridhika hapo huweza tokea kutokuelewana, hali hii no wazi kuwa bendera nyekundu inapepea ndani ya mahusiano yako.
⏩Udanganyifu, (Manipulation)
Mtu muongo atatumia msukumo wa kukupa pressure au kukutia katika hatia ili ufanye au ukubaliane na mambo anayotaka yeye yawe,hii ni mbinu inayofanywa na wapenzi wengi dhi ya wenza wao, na mara nyingi mtu kufanya kitu asichiridhia ni haki yake lakini nguvu ya kunyanyaswa huwabana wengi na kukubaliana na uongo wa wapenzi wao, atatumia hasira na vitisho ili kukushawishi ukubaliane nae, oky huenda inakutokea hiyo katika mahusiano basi tambua ni bendera nyekundu inapepea kwenye mahusiano yao.
⏩Ukosoaji endelevu,(Frequent criticism)
Wote tunaweza kuwa wakosoaji wa mawazo na tabia za watu wengine Mara kadhaa lakini inapotokea mfululizo hasa kwenye mahusiano unabadilika na kuwa ukatiri mbaya sana maana huweza kutokea anakukosoa hata mbele ya watu na kukuaibisha anakuwa ni mtu wa kurudiarudia kusema tabia zako, mawazo na na maneno yako uliyokwisha kosea ili aonekane yuko sahihi, jiulize huu ni upendo au uigizaji, ni nani ampendae mpenzi wake na antaka kumdharirisha kwa namna yeyote ile? Aibu!! Mahusiano kama haya kuna bendera ndani yake yenye rangi nyekundu inapepea, jiulize mwenyewe!
⏩Hali tete,(volatility)
```
Kama uko kwenye mahusiano ambayo mood yako haina afya na unawaza hata kupata sehemu nyingine ya kupata furaha,wewe juwa una hali tete katika mahusiano, angalia sana kuwa kwenye mahusiano na MTU ambae hakuulizi maumivu yako hata raha yako, mtu anakuwa hajari kabisa, unapoona kuna mambo kama hayo na ukataka upate furaha kwingine pasina yeye kujuwa au ukaanza kuwaza kuchepuka ili ukidhi haja zako za mwili na moyo basi unatafunwa na hali tete na tambuwa benders nyekundu inapepea kwenye mahusiano yako.
⏩Kutokuwa mwaminifu,(dishonesty) 
Hakuna nafasi yeyote katika mahusiano ambayo inaruhusu mtu kutokuwa mwaminifu, sio tu kwamba ni vibaya bali pia ni utenganifu wa wa uaminifu na mapenzi ya dhati na upendo kati ya wawili,katika uongho hakuna uongo mdogo wala mkubwa, sababu za uongo huh huenda ikawa ni kujiongezea thamani, kutaka kuficha madhambi yao, kuumiza wengine au kufanya utani ambao unaumiza, mapenzi na mahusiano yasiyokuwa na uaminifu hatari yake sio ya wapenzi tu bali hata watu wengine wanaweza husika ikiwemo na familia kwa ujumla, anaekupenda atakuwa mwaminifu sana na kama hulioni hili basi kuna bendera nyekundu.
⏩Kutowajibika, (irresponsibility)
Kutokuwajibika katika mahusiano kunaweza kuwa ni vigumu sana kugundua tabia hii kawa mwenza maana wengi wao hutumia vigezo vya kimaisha kama hali ngumu ya maisha n.k kukwepa majukumu yao ya lazimakwa wapenzi wao, kwa mfano: hakuna maisha yanayoendeshwa kwa mabeno tu balki pesa na dhana nyingine za kukidhi haja za kimwili na kiroho, sasa unakuta mtu yuko kwenye mahusiano hataki kutoa au kuwajibika kwa visingizio kibao, sio mwanamke wala mwanaume anaepaswa kuwajibika bali wote ni majukumu yao ikiwa mke hana basi mme atoe na ikiwa mme hana mke atoe na sio kuwa tegemezi kwa kila kitu jua kuna siku utachokwa na hapo mahusiano yenu tauyari yataanza kupeperusha bendera nyekundu, ni lazima mke acheze nafasi yake na mme pia hivo hivo, maisha kusaidiana.
⏩MUHIMU
Mahusiano yenye afya na yaliyo bora ni kitu kimoja na kikubwa sana katika maisha lakini inapokuja togauti mahusiano huingia hatarini ,mahusiano bora ni yale yaliyo na uaminifu, wema, heshima, maelewano, ukarimu ambazo hutoa support na kuhimiza hamu ya mapenzi na upendo thabiti, lakini mapenzi hatari ni yale yaliyobeba dhana ya yote niliyoyataja hapo juu, kuwa makini na BENDERA NYEKUNDU zisome nyakati na matukio na ondoa haraka sana dalili hizo kwa kujiweka wazi kwa uaminifu sana na kusema na wako mpenzi au mtu unaedhani anakufanyia hayo yote
Pole Uzi ni mrefu kiasi lakini hujatoka bure!!

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad