Mpenzi msomaji leo tutazungumzia tabia ya baadhi ya wenzetu kuwatega waume wa wenzao ili kuwanasa.
Tabia hiyo imeshamiri sana huko majumbani tunakoishi hasa kwa wanaume ambao mambo yao kiuchumi yapo vizuri.
Shoga, kumtega mume wa mwenzako kwa sababu ana fedha, gari, nyumba na vitu vingine vya thamani ni kukosea na kumdhalilisha mumeo.
Hata kama mumeo bado mambo hayajamnyokea usimsaliti kwa kutoka na mume wa jirani yako, kumbuka maisha ni sawa na kuzichanga karata leo kwa yule na kesho kwa huyu.
Utakuta mwanamke aliyeolewa akibaini mume wa mwenzake anakaribia kurudi au kakaa sehemu atavaa nguo za kimtego na kujipitisha ili atokewe tu!
Kwa kawaida wanaume wengi wanashindwa kujizuia wanapoona maungo tata ya wanawake, atakapobaini unafanya hivyo ili akutokee hatakuacha.
Shoga, hebu jiulize ukifanyiwa hivyo utafurahi? Bila shaka hautapenda basi usimtege mume wa mwenzio ili utoke naye kimapenzi kwani maumivu utakayopata wewe mumeo akiibiwa naye atayapata pia !

No comments:
Post a Comment