UTANIKUMBUKA TU SEHEMU YA NNE-04 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, March 23, 2020

UTANIKUMBUKA TU SEHEMU YA NNE-04






Kayumba akiwa katika hali ya huzuni na majonzi aliondoka huku akimuacha Edga amesimama akimsindikiza kwa macho,lakini moyo Edga hakuwa tayari kumuacha Kayumba aondoke, alijua fika kijana huyo hana mahali pakuishi mjini na hivyo kwa mara nyingine tena alikimbilia na kisha kusema naye akimuomba waungane kuwa kitu kimoja ili waendeshe maisha mbali na kundi lile lililo chini ya Boko.
"Kayumba braza, ukweli sipo tayari kukuruhusu uondoke. Wewe ni kama ndugu sasa, kwa maana hiyo nataka tuwe kitu kimoja. Mjini maeneo ni mengi sana, vile vile kazi ni nyingi pia", aliongea Edga mara baada kumfikia Kayumba.
"Tufanye hivyo Kayumba, kwa kile ulicho nieleza kamwe sipo tayari kurudi kambini. Wale ni watu wabaya", aliongeza kusema Edga,ikwa wakati huo Kayumba akimtazama tu pasipo kuongea neno lolote. Baadaye Kayumba alishusha pumzi kidogo kisha akajibu "Mimi sijasoma, itawezekana vipi kupata kazi?.."
"Kayumba..", aliita Edga kisha akasema "Kila mtu na riziki aliyoandikiwa, sio kila aliyefanikiwa amesoma lahasha. Unaweza usiwe na elimu yoyote lakini ukapata mafanikio makubwa kuliko yule mwenye elimu. Wangapi hawana elimu ila wanawaajiri wanye elimu zao? Utakuta mtu kasoma mpaka macho yamepovuka ila pesa hana! Na vile vile utakuta mtu elimu ziro lakini utajiri alio nao moto wa kuotea mbali. Amini nakwambia braza, kusoma sio kupata kazi. Kwa maana hiyo basi, mimi na wewe ni wasaka tonge, tupambane tutumie nguvu zetu kusaka tonge...",alisema maneno hayo Adga akimuasa Kayumba ilihali muda huo Kayumba alionekana kuinamisha uso wake chini kana kwamba kuna jambo alikuwa akilitafakari. Punde aliinua uso kisha akajibu " Sawa kaka nimekubali ", hakika lilikuwa ni jibu ambalo lilimpelekea Edga kuonyesha tabasamu, alimpokea Kayumba begi kisha akasema "Hakuna kukata tamaa, kwani wao wana nini na sisi tuna nini mpaka tushindwe".  Edga alipokwisha kusema hivyo alishikana mkono na Kayumba wakagongeana mabega kisha wakaondoka.  Sasa walau furaha inamrejea kijana Kayumba, jambo la kupata rafiki ndani ya jiji la Dar es salaam inampelekea kuwa na amani kidogo ndani ya moyo wake tofauti na hapo awali alivyokuwa akifikiria namna ya kuishi baada Catherine kumkana. Ni saula ambalo lilimfanya kumshukuru Mungu, na sasa aliweka mikakati ya kusaka pesa ili apate nauli ya kumrudisha kijijini kwao akaendelee na maisha ingawaje ilimuwea ngumu kumsahau Catherine gaidi wa moyo wake. Kila leo Kayumba alikumbuka Catherine, ni maumivu makali sana ambayo alihisi huku akitamani siku yoyote amsahau ili moyoni awe na amani.
  "Hii maskani ni nzuri sana, vile vile kuna utulivu wa kutosha. Hapa panatufaa sana kwa kuanza maisha mapya ingawa jambo la kuzingatia ni kuwahi kuamka ili tusiwe kero kwa mwenye duka", alisikika akisema Edga,maneno hayo alikuwa akimuasa Kayumba baada kufurahishwa maskani mpya walionzisha kwenye moja ya duka Kinondoni.
  "Ni kweli Edga, na sitochoka kukushukuru kwa wema wako",alisema Kayumba kwa sauti ya chini huku mkono ukiwa shavuni.
"Ahahahaha.. Hahahahah", Edga aliangua kicheko kisha akasema "Hilo ni jambo la kawaida Kayumba, vile vile hata mimi nastahiri kukushukuru kwa sababu mpaka sasa nadhani nisingekuwa duniani. Kifo kilikuwa karibu yangu,na laiti usingeniambia basi ningezidi kuwaamini wale watu, kitendo ambacho kingenipelekea kifo. Aah! Kayumba. Tuachane na hayo, kitu ambacho mimi sijafurahishwa nacho kutoka kwako "
" Kitu gani Edga?.. ", alihoji Kayumba wakati huo akitoa mkono shavuni. Edga akajibu." Muonekano wako, tangu siku ya kwanza tuonane uso wako hujawahi kuonyesha tabasamu kwa muda mrefu. Kwa maana hiyo unaonyesha moyo wako unasiri kubwa mno, vipi unaweza kunieleza kinacho kusibu?.."
"Aah, Edga. Ni kweli upo sahihi, ni story ndefu sana lakini kwa sasa hebu tuzungumze kuhusu maisha. Hasa hasa kazi ya kufanya"
"Vizuri, acha hilo suala tuliweke kiporo kwanza. Siku tukiwa na nafasi basi utanijuza.."
"Shaka ondoa", aliunga mkono Kayumba. Ndipo Edga alipoanza kuzungumza uwezekano wa kupata kazi. Aliwaza hili na lile, mwishowe alishusha pumzi ndefu akamtazama Kayumba kisha akamuuliza "Hivi kubeba zege unaweza?.."
"Bila shaka, mimi ni mwanaume Edga inanibidi nipambane ili mkono uende kinywani", alijibu Kayumba. Maneno hayo yalimfurahisha sana Edga ambapo alimpigia piga Kayumba kunako bega huku akisema "Hayo ndio maono ya mwanaume,mwanaume hasifiwi kula bali anasifiwa kazi. Basi kesho twende sehemu moja hivi, najua pale hauwezi kukosa kazi",
"Ni kazi ngumu ila nina imani utaiweza", aliongeza kusema Edga kisha wote kwa pamoja wakafurahi wakagongeana tano, na mara moja safari ya kusaka lepe la usingizi ilianza ambapo wawili hao walilalia mabox huku pasipo na shuka.
  Usiku ulikuwa wa tabu sana kwa kijana Kayumba hasa pale anapoyatuliza mawazo yake, sura ya Catherine ilimjia mara kadhaa pindi alipoyafumba macho yake. Jambo hilo lilimpa shida ingawaje alitamani sana siku moja aweze kumsahau, akiamini kuwa endapo ikMitokea siku hiyo atafurahia maisha daima. Lakini baadae alipitiwa na usingizi, aliamka alfajiri mapema baada Edga kumuamsha.
  "Kumekucha kaka", aliongea Edga huku akiliweka pema box lake la kulalia.
"Mmh, ni siku nyingine sasa", alijibu Kayumba wakati huo akizinyoosha mbavu zake kwa kujipinda kulia na kushoto mbele na nyuma. Zoezi hilo lilipo kamirika, naye alilihifadhi mahali pema box lake kisha akasema "Nipo sawa, tuondoke zetu"
"Ahahahah...hahahaha..", aliangua kicheko Edga, maneno ya Kayumba yalimfanya afurahi. Alipoakatisha kicheko chake akasema "Nakukubali sana braza", Edga alipokwisha kusema hivyo safari ya kwenda kusaka tonge ikaanza.   Wawili hao walitembea kutoka Kinondoni mpaka Kawe, huko walipata kibarua cha kubeba zege kwenye moja ya mradi wa kujenga gholofa uliokuwa ukifanyika. Vijana wengi walionekana wakichakarika, wapo waliokuwa wakichanganya zege na wengine wakibeba vile vile wengineo wakijenga. Ni kazi ambayo ilionekana kuwa ngumu sana, kiasi kwamba ilimfanya Kayumba kushusha pumzi huku akijishauri mara mbili mbili uwezekano wa kuweza kuifanya kazi hiyo.
"Nitapambana hakuna namna", aliapa Kayumba ndani ya nafsi yake wakati huo huo ilisikika sauti ikisema "Edy naona kwa sasa umeokoka, au mambo yamekua magumu?.."
"Ahahahaha.. Acha zako bwana", alijibu Edga akianza kwa kuanguka kicheko.
"Hujui tu, ila kitambo nilikuwa najua kazi yako na wenzako, ila ukweli ni kwamba yale sio maisha. Kifo kilikuwa karibu yako, jasho la mtu haliliwi Braza", aliongeza kusema mtu huyo, akimwambia Edga. Dhahiri shahili alifahamu fika Edga na ndio maana alikuwa akimueleza masuala hayo ambayo yalimpelekea Edga kuishia kucheka. Punde si punde sauti nyingine ilisikika ikitoa amri. Ilisema "Huu muda wa kazi, maongezi baadaye"
"Sawa kiongozi", mtu huyo aliyekuwa akisema na Edga alitii amri kisha akaendelea kuchakarika kama ilivyo kwa Kayumba na Edga ambao nao walianza kazi kwa kasi na nguvu ya hali ya juu.
   Jioni ilipowadia kila mmoja alipata ujira wake, shilingi Elfu tatu. Na sasa walirejea maskani ingawaje kila mmoja alikuwa hoi bin'taabani hasa hasa Kayumba. Alilalama maumivu kila sehemu ya mwili wake, ilichoka sana siku hiyo jambo ambalo lilimpelekea kutokurudi kazini siku iliyofuata na wala Edga hakuweza kumuwekea kinyongo kwani alitambua fika kijana mwenzake hana uzoefu wa kazi hizo.   Siku iliyofuata Kayumba alijihisi kuwa shwari, nguvu na uchovu walau ulipungua na hivyo aliona ni vema akiendelea kusaka tonge huku kichwani akiwa na malengo ya kurudi nyumbani kwao baada kuona alichofuata mjini kimekwenda kombo.
"Mwili wangu sasa upo safi kabisa. Ukweli ile kazi ni ngumu sana asikwambie mtu", alisikika akisema Kayumba,wasaa huo ilikuwa yapata saa nne usiku.
"Hahahaha..", Edga alicheka kisha akasema "Kabisa, yani hapa mwili wangu umechoka mithiri ya samaki aliyechina. Ila nimepata wazo"
"Wazo gani?.", alihoji Kayumba wakati huo akionekana kuwa makini kumsikiliza swahiba wake. Edga akajibu "Ngoja kwanza nikanunua chakula kwa mama Zamoyoni halafu nije nikukwambie". Edga alinyanyuka kisha akazipiga hatua kuelekea mgahawani kunua chakula, alinunua na maji kisha akarejea maskani. Wawili hao waliketi na kuanza kula, huku zogo mbali mbali nalo likitawala.
"Enhee nipe maneno sasa", aliongea Kayumba.
"Wazo langu ni kwamba tubadirishe upepo, nikiwa na maana kwamba ile kazi ya kubeba zege tuachane nayo. Tutafute kazi nyingine, hata ya kuosha magari nayo pia sio mbaya aidha kazi ya ukuli"
"Kweli hilo wazo nzuri sana, unaaakili mno ", aliunga mkono Kayumba.  Kicheko kilizuka baina yao kisha wakagongeana tano, na sasa walilala wote wakiwa na dhamila moja tu.
  Kesho yake palipokucha, Edga alimuamsha Kayumba wakaanza safari ya kusaka kazi. Mabibo sokoni walifika, ujanja ujanja wa kijana Edga ulipelekea kukubaliwa kuungana na wabeba mizigo wa ndani ya soko hilo. Na ndipo walipoanza kufanya kazi,istoshe siku hiyo ilikuwa siku njema upande wao, sokoni yalifurika maroli kibao yaliyo sheheni mizigo ambayo ilitakiwa kushushwa. Kayumba alichakarika kwa nguvu zote, mwili wake ulioonyesha kuwa wa mazoezi aliutumia ipasavyo mpaka pale alipojihisi kuchoka ilihali jua tayari lilikuwa likitoweka kwa maana hiyo jioni iliwadia. Walipokea ujira wao wasaka tonge hao kisha safari ya kurejea maskani ikaanza. Lakini wakati wapo njiani, mara ghafla Kayumba alipigwa na butwaa baada kumuona mrembo akizipiga hatua kuelekea kwenye moja ya duka huku nyuma akiwa ameacha gari lake hatua kadhaa. Kayumba alimkodolea macho mrembo yule huku macho yake yakitia shaka kuwa huwenda amemfananisha na sasa alingojea ageuke ili amtazame. Punde si punde mrembo yule alirejea, na hapo ndipo Kayumba alipogundua kuwa macho yake yapo sahihi. Kwenye kiza totoro alipata kumuona Catherine akilisogelea gari wakati huo huo kabla hajalikaribia gari hilo, ndani alitoka mwanaume ambapo walikumbatiana huku kwa macho yake Kayumba akishuhudia. Roho ilimuuma sana, machozi hayakuwa mbali kumtoka ilihali muda huo huo Edga alipasa sauti kumuita.
  "Kayumba.. Kayumba..hebu tuondoke bwana", aliita Edga huku akisogea mahali aliposimama Kayumba.
"Kayumba..", alipomkaribia alimuita kwa mara nyingine tena, na hapo ndipo Kayumba alipoyaondoa macho yake yaliyokuwa yakiisindikiza gari la Catherine, na sasa alimgeukia rafiki yake huku akiyafuta machozi. Edga alitaharuki kumuona Kayumba akilia machozi, lakini wakati akiwa kwenye hali hiyo ya taharuki,kwa sauti ya majonzi Kayumba alisema "Hivi nimemkosea nini mimi Catherine?..Kosa langu ni mimi?.."
  "Catherine?..", alizidi kutaharuki Edga juu ya maneno hayo aliyoyaongea Kayumba.

       
Itaendelea.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa