Tafsiri Hii Isiyo Sahihi Inavyogharimu Mahusiano, Jifunze Kitu Hapa - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, March 2, 2020

Tafsiri Hii Isiyo Sahihi Inavyogharimu Mahusiano, Jifunze Kitu Hapa





Wakutanapo watu wapenzi haina maana kuwa ndoto na misimamo yao ya msingi kwa maisha inakufa. Haimaanishi kuwa hawana matarajio kuhusu wapenzi wao, hivyo ule msemo kuwa "Kama unanipenda unikubali kama nilivyo usitake kunibadili" wakati mwingine unagharimu mahusiano mengi kwani si kweli kuwa mtu ataendelea kuvumilia au kukubaliana na tabia au maamuziyako ambayo yanaendana na kinyume na ndoto zake na matarajio mengine kuhusu mpenzi anayemuhitaji.

Mahusiano yanahitaji kutoa kafara kwa mambo ambayo mwenza wako ameyatambua kuwa ni madhaifu yako na anakuhitaji uyarekebishe. Using'ang'anie kusema wewe ndio hivyo hivyo ulivyo, na asitake kukubadili.
Kabla haujaanza kuwa mbishi na kujitetea kuwa usitake kubadilishwa jiulize mambo haya mawili
1. Je unafaidika nini na kuendelea kuwa hivyo ambavyo mpenzi wako hapendi na anakutaka ubadilike. 

2. Je, umejiweka kwenye nafasi ya mpenzi wako na kujiuliza kama ni wewe ungekuwa unapokea hiyo hali ungekubali ?

3. Je si unasema unampenda huyo mpenzi wako, na maana yako ya kumpenda ni ipi haswa ? Je si kwamba upendo ni kutaka kumuona mwingine akiwa na furaha, ni kumfanyia yatakayompendeza na zaidi sana sio tuu kumfanyia unayoona wewe yanafaa bali upatapo nafasi kufanya ambayo kweli mpenzi wako anahitaji. Na hayo anayokuambia hapendi pengine kujirekebisha kwako ndio jambo kubwa sana litakalomfanya ajisikie kupendwa.

N:B Ni kweli kuna mambo ya msingi ambayo mpenzi wako hawezi kubadili na inabidi mjadiliane mapema kabla hata ya kuanza mahusiano kama vile maswala ya kiimani yaani dini, maswala ya wapi mtaishi, aina ya kazi, mahusiano na ndugu n.k.
Katika vyote mjijengee uwezo wa kuzungumza na kupeana sababu za kwanini mna misimamo tofauti na jinsi gani mnaweza kukubaliana kutofautiana ikibidi.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa