Ushawahi kusikia kuhusu ndoa iliyodumu muda mfupi zaidi ? kama hujawahi kufikiria kuhusu ufupi wa ndoa basi masaibu yaliomkumba Ben na mpenzi wake Bernice yatakushangaza na kukuacha kinywa wazi .
Baada ya Uchumba uliodumu miezi sita ,wawili hao waliamua kwamba itakuwa dhambi kushiriki mapenzi bila kwanza kufunga ndoa . Ben na Bernice walikutana kanisani na uhusiano wao ulianza kama urafiki kabla ya kuboreka na kuwa wapenzi . Hakuna aliyeweza kuwatenganisha wawili hao na wenzao kanisani waliwatazama kama kielelezo cha jinsi wapendanao wanavyofaa kuishi . Harusi kubwa ilipangwa na wapenzi hawakuwa na shaka kwamba ndoa yao itakuwa bora na itadumu lakini mipango ya binadamu ,Mola keshaijua .Siku ya siku ilipofika walifunga pingu za maisha . Kila kitu kilionekana kwenda kwa njia safi na hata mipango ya jinsi watakavyoishi baada ya fungate au honeymoon ilikuwa ishafanywa . Urembo wa Bernice uliwavutia wengi na Ben alijiona kama mtu mwenye bahati kubwa sana kuweza kupendwa na kipusa huyo ambaye kulikuwa na stori nyingi za jinsi alivyowakataa wanaume wengi waliotaka kumuuoa . Bernice alikuwa mtu wa kipekee ,hakuwa na rafiki hata mmoja wa kike na Ben alijiambia kwamba hilo sio jambo la kumpa wasi wasi kwa sababu huenda ni maumbile yake kutaka kujifanyia mambo yake kivyake .
Kwa sababu ya msaada mkubwa waliopewa na kanisa katika kufanikisha ndoa yao,Ben na Bernice waliambiwa na viongozi wa kanisa lao kwamba hawatatoa hata shilingi moja kwa harusi yao ila watayarishe tu hela za kwenda honeymoon ! wapenzi walifurahi na hata wakaamua eneo ambako watasafiri kwenda fungate yao .Ikaamuliwa kwamba baada ya harusi basi wangesafiri kwenda Singapore kwa muda wa wiki tatu kabla ya kurejea na kuanza maisha rasmi kama mke na mume . Ben alijawa furaha akijua kwamba wakati wa honeymoon ndipo atapokuwa akifanya tendo la ndoa na mke wake kwa mara ya kwanza ,na pia Bernice alikuwa amemweleza kwamba yeye alikuwa bikra . Bahati iliyoje kwa mwanamke wa umri kama wa Bernice kuwa bikra ,kweli nimebahatika mimi! alijiambia kimoyomoyo .
Walipofika Singapore katika hoteli ambayo wangeiita makao yao kwa wiki tatu Ben na Bernice walifahamu kwamba kuna jambo ambalo lazima lingeziteka ndimi zao –kushiriki mapenzi ila Ben aligundua kwamba mke wake hakuwa na kasi ya kuzungumzia suala hilo wala hata kuonyesha daalili kwamba wangeshiri mapenzi . Kwa muda mfupi waliokuwa katika chumba cha hoteli yao alijihisi ni kana kwamba yupo mle ndani na dadake! Usiku ulipowadia , Ben keshajivua nguo zote huku damu ikimpa msukumo na kuufanya moyo wake kupiga kwa kasi .Kungoja kwake kwa zaidi ya miezi saba sasa kulikuwa kumefika tamati! Hatimaye anaifanya ndoa yake kuwa rasmi kwa kumpa penzi moto moto mkewe! Dunia ina ukatili,na hakuna anayekutayarish a kwa ukatili huo . Bernice alipoingia kitandani ,alionekana kutetemeka na kuzongwa na wasiwasi .
‘Kuna tatizo? Mbona unaonekana kuwa na wasi wasi ?’ Ben alimuuliza .
‘Niko sawa ,lakini tunafaa tuzungumze.Kuna jambo ambalo unafaa ujue’ Bernice alijibu .
Ben alipomuangalia mkewe kwa karibu na kumuona akitokwa machozi alijua hapa kuna habari mbaya .Lakini alishangaa mbona habari hiyo mbaya ilikuwa ilkija wakati huu na sio muda wote ambao walikuwa na Bernice .
‘ Ben , kwanza nataka ujue kwamba nakupenda sana na wewe ndiye mwanamme wa kwanza ambaye nimekubali kumfungulia moyo wangu’. Bernice Alianza
‘ Najua usiku wa leo ni wetu wa kwanza kushiriki tendo la ndoa .Na umeingoja sana siku hii .Ila ningependa ujue kwamba mimi ni huntha.Nina sehemu mbili za siri ,ya mwanamke na ya mwanamme’. Bernice alifichua . Ben alipatwa na mshutuko na pale pale kumbukumbu zote za jinsi hawajawahi kuoga pamoja kama wapenzi na hata hajawahi kumwona Bernice uchi zilimjia . Akakumbuka jinsi mkewe alivyokuwa akikwepa Ben asimuone akiwa uchi .hapo ndipo alipojua kweli sababu ya mkewe kukataa sionekane naye uchi .Alikuwa na haya ya kusema kwamba ana sehemu mbili tofauti za siri !
‘Bernice,Lakini mbona unaniambia hayo sasa .baada ya kufunga ndoa na kufika honeymoon?’ Hilo ndilo swali pekee ambalo Ben aliweza kujikakamua kumuuliza mkewe. Uchungu mkali ulimpitia mwili mzima asikose kujua mbona Bernice alingoja hadi wakati huu ili kumfichulia jambo kubwa kama hilo . Ben alichukulia kisa hicho kizima kama usaliti mkubwa wa penzi .Alionekana kana kwamba alitumiwa vibaya lakini hakuwa tayari kukubali kwamba mke wake ni huntha. Juhudi za Bernice kujaribu kumweleza kwamba aliogopa angemuacha iwapo angesema ukweli mapema ziliambulia patupu .Ben alifunga virago vyake na kumuambia Bernice anarejea nyumbani Kenya . Ndoa yao ilikuwa imekwisha!
No comments:
Post a Comment