Unahabari kuwa mapenzi ni kama upofu, Unaweza kweli ukaishi kwa mfumo huo na mwisho wa siku ukajikuta umekuwa kipofu hata katika kuongea au kuuliza na ukamkosa hata yule ambaye alitaka kuwa na wewe. Mapenzi sio upofu bali ni akili tu ya namna ya kwenda nayo. Haya hapa mambo 20 ambayo hautakiwi kuuliza pale unapo kuwa na mwanamke au kufanya haswa kwa mara ya kwanza mkikutana au kutoka.
Haya hapa.
- Mwanaume hutakiwi kuwa busy na simu yako kuliko kuwa busy na mwanamke wako.
- Kuongelea juu ya account yako ya bank au uwezo wa baba yako; hili linamkimbiza mwanamke.
- Kuwa na harufu mbaya (Mdomo, Kikwapa, Boxer nk).
- Usiulize "Wewe ni Bikira?".
- Usiuliza wavulana wangapi ambao tayari amesha anguka nao kitandani.
- Kama atalipia kutazama movie au chakula mkiwa out usijifanya kusema umesahau wallet nyumbani au ATM imegoma kutoa pesa.
- Usimwambie mwanamke aje kweko pale mnapotaka kukutana kwa mara ya kwanza 'first date' au kwa mshkaji wako.
- Usimuache msichana wako akazungumza juu ya msichana mwingine mambo yake hata kwa dakika mbili.
- Usimnunulie zawadi nyingi, Anaweza dhani kuwa unataka kumnunua 'Kumfanya mtumwa wa mapenzi kwa zawadi'.
- Kwa sababu yoyote ile ikitokea mtu mwingine anataka kupanda gari lako, Usimuweke mpenzi wako akakaa siti ya nyuma.
- Usimlinganishe na Ex wako.
- Usimuongelee juu ya kunenepa kwake au hata nywelezake labda kwa uzuri tu. Kwamfano kuzungumza kuwa ameumuka sana, nywele zake haziko poa siku hizi nk.
- Baada ya kufanya naye s3x kwa mara ya kwanza onyesha kufurahi, Hata kama huku enjoy onyesha ume enjoy.
- Table manners (Kuwa mstaarabu kwenye kula, Kula huku unatoa sauti ya namna unavyo tafuna mdomoni kwa fujo, kula huku unaongea, kumwaga mwaga chakula, kutumia kisu au sufuria kwa kula nk hayo yanakufanya mpenzi wako asifurahi kuwa na wewe).
- Focus macho yako kwenye macho yake na wala sio kwenye matiti yake au makalio yake.
- Kujifanya wewe upo level flani wakati haupo (Wanawake wanaweza kumgundua mtu anaye jidai kwa haraka sana). Usiombe gari la rafiki yako nakusema nilako, Usidanganye kuwa geto la msela wako ndio lako au kudanganya unafanya kazi flani ambapo haufanyi kazi hapo.
- Usionyeshe hisa zako za kimahaba kwenye first date.
- Usiwe mkorofi kwa muhudumu au wahudumu wa baa au hotelini ili kumuonyesha mpenzi wako kuwa unaweza.
- Usimuombe pesa.
- Usiombe hata picha, labda kama ameamua kukupa.
No comments:
Post a Comment