Iwapo wewe ni mwanamke na umetimiza umri wa zaidi ya miaka 50, basi una uwezekano wa kupatwa na joto jingi na kutokwa na jasho mwilini, mabadiliko ya kila mara ya mhemko na kudhoofika kwa mifupa yako, unapoingia katika umri wa kumaliza kupata watoto au menopause.
Mwanagainakolojia John Ong’ech hata hivyo anasema dalili hizi huwa tofauti kwa kila mwanamke na zinaweza kuthibitiwa.
Wanawake walio na umri wa miaka 50 na zaidi wana uwezekano wa kuwa na mifupo iliyodhoofika kutokana na kupungua kwa homoni ya estrogen. Kulingana na Ong’etch, ingawaje kuna dawa za kuongeza homoni hio, zinaweza kuwaweka katika hatari ya kupatwa na saratani ya matiti na hivyo anawashauri kula vyakula vyenyeprotini ya soya.
Mbali na hayo, watoto 42 wa kurandaranda mitaani, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo kwa makosa tofauti. Vijana hao walikamatwa jana usiku baada ya kumvamia afisa wa polisi na mbwa wao katika soko la Muthurwa. Polisi wanasema walinasa vijipakiti 49 vya mihadarati na visu saba kutoka kwao.
Hayo yakijiri, hazina ya NHIF imekiri kua haina hela, na kulalamikia viwango vikubwa vya pesa zinazolipwa hospitali za kibinafsi. Naibu mwenyekiti wa bodi ya hazina hio Roba Duba anasema wanapambana kusuluhisha suala hilo na kuondoa malipo hayo kwa hospitali za kibinafsi.
Kwingineko, mwili wa mvuvi aliyezama maji katika bwawa la Masinga siku ya Jumamosi baada ya dau lake kuzama, haujapatikana. Naibu kamishna John Ayienda anasema wanashuku mwili huo ulisombwa na maji na kutokea mahali maji ya bwawa humwagika
No comments:
Post a Comment