Fimbo unayo, Unahangaika wa kukuchapa - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, March 3, 2020

Fimbo unayo, Unahangaika wa kukuchapa


WAUNGWANA  Jumatano nyingine nakuja Shangingi wenu mstaarabu kabisa uongo uongo? Halooo, kama nawaona wengine hapo mlivyokunja sura utafi kiri mjusi kabanywa na mlango; watu wengine sijui mpoje! Unanichukia wakati hata hunijui inahusu? Sikulishi, sikuvishi, kwa nini ujipe presha bure kuniwaza? Bibi pita huko, fanya yanayokuhusu nami nifanye yangu.
Ukiona nakukwaza pita kule. Maisha yenyewe mafupi haya kwa nini tupeane stress zisizokuwa na kichwa wala miguu? Nakuchamba halafu vimba mpaka upasuke. Leo nataka niwape darasa kidogo sio kutwa kulaumiana; Oooh sijui mwenzangu hanipi kitu roho inapenda, umewahi kumwambia au unakufa na tai yako shingoni? Watu wengine sijui mkoje, wewe unaona mtu wako hakupi raha duniani wewe unaanza kutangaza kwa majirani; bibi yanawahusu? Unamtangazia nani wakati maisha ya kwenu, unataka watu wakuoneshe kwa vitendo halafu uanze kuwalaumu wakati mambo umeyakosea mwenyewe? Bibi ukiona mambo hayawi matamu, mueleze mwenzio.
Macho yawe makavu kabisa, umpashe apashike kwamba mwenzako sifurahii…eeh bibi usipomwambia yeye utamwambia nani? Kuteseka hivyo vipi wakati mtu yupo nyumbani? Fimbo unayo mkononi halafu uanze kuhangaikia mtu wa kukuchapa? We wa wapi? Bibi sema usikike, mambo ya kwenda kuzungumza pembeni na wambeya wakati mtu yupo nyumbani kwako yanasaidia nini? Unamuogopa nani wakati huyo mtu wako.
Mboga unayo, viungo kama vyote; unahangaika nini kwenda kutafuta mpishi? Haya mambo yanafaa mkipeana elimu. Wewe unajua hiki na mwenzako anajua kingine mnafundishana. Hakuna anayejua kila kitu bibi. Usijishaue ukajifanya wewe hodari kumbe hujui lolote.
Nyinyi wenyewe mjue namna ya kuzungumza lunga moja mnapokuwa kule mahala. Ukishamueleza wapi panakupandisha mzuka, naye akishajua anakuwa anapiga honi tu muda wote; uongo jamani? Sio wewe unataka afunge breki yeye amekanyaga mafuta; inahusu? Raha ya mechi ni magoli kila mtu anajua sasa mnayafungaje? Sio kila mtu anafungafunga hovyo tu, mfunge kwa pamoja. Mnafunga kwa pamoja mkiwa kwenye dunia ya raha kila mtu anabaki pambee.
Anakuwa hana hamu, kafi ka Kigoma mwisho wa reli. Hayo ndio maisha, jamani mmenisoma? Huu mwaka mpya, badilikeni. Yale ya mwaka 2019 tuyaache yaende mwana kwenda. Huu uwe mwaka wa kuboresha uchumba na ndoa zetu bibie. Watu tuishi kwenye dunia ya raha isiyokuwa na karaha. Mapenzi ni burudani kama mtaimba wimbo mmoja! Jamani mimi nawapenda bure, na niwatakie siku njema inshallah Mungu akipenda tukutane tena hapahapa wiki ijayo!



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa