Vitu vyote vya kuongeza nguvu za kiume ninavyo mwilini mwangu- Snura - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, February 19, 2020

Vitu vyote vya kuongeza nguvu za kiume ninavyo mwilini mwangu- Snura

Msanii wa filamu na muziki Snura Mushi, amesema vitu vya kuongeza nguvu za kiume kama Alkasusu, tende na mihogo mibichi vinapatikana mwilini mwake ila huwa anampatia mpenzi wake Minu Calypto pale anapohitaji.
“Mambo hayo ya Alkasusu, Urojo, juisi ya tende na mihogo mibichi vyote vipo mwilini mwangu akinigusa tu anavipata,  kila siku  kwetu ni Valentine Day penzi letu lipo juu kama dirisha la chooni, halafu kuhusu umri nimemzidi miaka kidogo sio mingi kihivyo kama watu wanavyofikiria” amesema Snura Mushi.
Pia wapenzi hao wamekiri kuwa waliachana kipindi cha nyuma na wamesema sababu ya kuachana kwao ni mambo ya nje kuwa mengi kuliko mapenzi yao.
“Tuliachana kweli kuna vitu tulipishana kidogo ila kuachana sio kufa,nafikiri mambo yanakuwa mengi kwetu sisi, watu wanaongea vitu vingi sana, hakuna kitu chochote kibaya alichonifanyia hakunisaliti wala sijakuta message yoyote mbaya, maana hayo ndiyo makosa makubwa ya watu kuachana” Snura Mushi na Minu Calypto.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa