Tunajua hakuna binadamu mkamilifu na wengi hujaribu kukabiliana na mapungufu yao bila mafanikio yoyote, lengo ni kuhakikisha kutowakera wenza wao kutokana na madhaifi yao.
Ukishajua mwenza wako kakupenda jinsi ulivyo na mapungufu yako basi usifanye makusudi ukazidisha kumkera, jitahidi kupambana na kupigana ili kupunguza udhaifu wako.
Usichoke! Yawezekana mwenza wako ashakwambia ukweli kwamba hiyo tabia uliyonayo inamkera lakini wewe huelewi chochote, basi ujue unamuumiza sana.
Yawezekana unakunywa pombe kupita kiasi, yawezekana una wivu uliozidi vipimo, yawezekana una hasira za karibu yaani unakasirika hata bila sababu muhimu, au pia umekuwa sio mzuri kwenye kubembeleza au mawasiliano na mwenza wako, yawezekana umekuwa mtu wa kusahau mambo ya muhimu hadi mwenza wako anaona humthamini, yawezekana unaongea sana kiasi cha kushindwa kufikiria unachosema au kumjibu mwenza wako, nk. Jitahidi sasa upunguze au uache kabisa ili mwenza wako awe na amani nawe.
No comments:
Post a Comment