Nikasema "Omary nilikuheshimu sana kama mwanaume tena nikakupenda ila nimefika mwisho" yule dada akasema "Omary huyu ni mwanamke wako?" Nikamjibu "Ulidhania uko peke yako au? Anyways nimekuachia hangaika nae" Omary akasema "Tina nyamaza mbona unazidi kuharibu?" Nikasema "kuharibu? Ooh yeah ndo anayekuweka mjini siyo samahani" yule dada akawaniwasha tena kofi akasema "Mwanamke una mdomo mchafu sana huna akili za kufkiria unakurupuka hufai kuwa na mdogo wangu Omary nikimuona tena huyu binti utanitambua" Omary akasema "Dada siyo hivyo makosa ni yangu sikuwakutanisha mapema naomba dada upunguze hasira kidogo" akasema "Nimemaliza na weekend hii uje nyumbani baba anakusubiri"
Yeleeewiiii kumbe ni ndugu..Kumbe ni dada yake Omary!! Mungu wangu ndo nimefanya nini Tina mimi.. akachukua mkoba akaondoka Omary akanikata jicho nikaangalia pembeni "Akasema Tina kwani kichwa yako imebeba maji au?" Nikanyamaza yaani naona aibu balaa nikasema "Samahani Omary" akasema "Samahani mana ake nini? Kila nikikwambia nyamaza husikii watu wanatakiwa watengeneze mahusiano mazuri na mawifi wewe umeharibu kila kitu" Nikamwambia "Sasa kwani mimi ni malaika?ningejuaje kama yule ni dada yako wewe ulitakiwa kuongea mapema kabla mambo hayajawa hivi saivi unanilaumu" akasema "Kwaiyo unanilaumu mimi kwa ujinga wako? Kama mtu humjui usikurupuke jaman ona sasa ulicho kifanya" nikamwambia "Samahani sasa tufanyeje?" Akasema "Toa kwanza chakula jikoni tule.."
Wifi aliacha chakula jikoni nikazima jiko nikampakulia mimi nilikua nimetoka nyumbani nimekula hivyo sina njaa.. Tumemaliza kula mambo mengine yakaendelea mtoto kujituma ili hasira zipungue ajue jinsi ha kuonge na dada mkubwa..
Mpwipwiii ukapigwa wa maaaana baada ya mpwipwi namuliza "Baby bado umenuna?" Akasema "Nna hata uwezo wa kukununia? Jumamosi twende nyumbani kwetu inabidi tu tuweke maswala wazi kisha twende kwenu nataka tufunge ndoa Tina" Nilishtuka macho yakanitoka "unataka tufunge ndoa?" Akasema "Ndio au wewe hutaki tina?" Nikamwambia "Proposal gani iyo ya kitandani jaman watu wana propose na pete" Akanisogeza karibu akanikumbatia akasema "Sijali watu wanafanya nini as long as Tina yuko na furaha chochote anachotaka mimi nitafanya" Na mimi nikampa dendaaaa tukaanza tena kuutafta mpwipwi ulipo..Piga mpwipwi wa maana kama hatutopiga tena..
Akasema "nikishapewa ruhusa kwenu naomba tuishi pamoja" nikamwambia "hilo ndo ulilo bakiza..
No comments:
Post a Comment