Mwanamke! Utakua na sifa zote za kukufanya uonekane mzuri na bora kuanzia nje, ndani ya moyo na hata akili lakini ukishindwa kutulia kwenye mahusiano na kila unayekua nae anakuacha basi thamani yako inaweza potea kwa kiasi kikubwa.
Utaanza kujichukia, imani yako itashuka na ukishabebwa na ile kauli ya "WANAUME WOTE NI SAWA" ndo basi tena.
Usimringie mwanaume mwenye upendo wa dhati ukaenda kwa yule mwenye kipato kizuri kwa madai eti ndio anaendana na hadhi yako.
Unaangalia hadhi wakati hamna upendo baina yenu? Unadhani mtakua mnazungumza lugha moja? Hebu jitafakari sana na tambua utu wako ni muhimu na usiuuze kirahisi ukaja jutia baadae.
No comments:
Post a Comment