Majukumu ya Mwanaume kwenye ndoa - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, February 4, 2020

Majukumu ya Mwanaume kwenye ndoa

Brother uliyeoa,nisikilize mie Didas Tumaini nikujuze:
Acha nikupe dawa ya akili, labda itakujaza maarifa sahihi ya kutunza ndoa yako.
=> Mwanaume anayejitambua lazima anajua majukumu yake, na kamwe hawezi kuyakwepa.
Bro, unapooa basi jua majukumu yako sio tu kuacha hela ya kula asubuhi, na kufanya tendo la ndoa na mkeo usiku.
Hiyo ni sehemu ya majukumu yako, lakini kumbuka pia kumfurahisha mkeo, kumfariji, kumwelimisha, kumsaidia kwenye kila jambo, kumsifu kwa jinsi alivyo, kumsifu kwa mema yake, uzuri wake, kumlinda, kumjali, kumtunza na kumpendezesha ni majukumu yako pia.
=> Najua wengi wetu tumelelewa kwenye familia ambazo ni ngumu kuona baba na mama wameshikana mikono, wamebebana, wanalishana, kukombatiana, kufurahi pamoja, kusifiana na hata kuambiana jinsi gani wanavyopendana na kuthamini mchango wa kila mmoja kwa mwenzie.
Na hii ndio imefanya wanaume wengi kutokuwa romantic na kuendekeza kuishi kiubabe na wake zao.
Bro, tabia hiyo isiendelee ndani ya ndoa yako, usiishi na mkeo kama unaishi na dada yako.
Hebu muonyeshe upendo, mdekeze, kuwa romantic, muonyeshe kiasi gani ana thamani ndani ya maisha yako, mtamkie maneno matamu, mlishe, cheza nae, mfanye kuwa rafiki yako, furahi nae.
Sio faida tu kwa mkeo, bali faida kwa watoto wako pia.
Sababu watoto hawahitaji tu baba na mama wanaoishi pamoja, bali wanahitaji wale wanaoishi pamoja na wanapendana kwa dhati.
=> Wapendanao wengi kabla ya ndoa huwa wana ukaribu mkubwa sana, urafiki, utani, ushirikiano mkubwa, na kujikuta wakipanga mengi kwa pamoja ambayo huwa na faida kwenye mahusiano yao.
Lakini baada ya ndoa, mambo haya yote hupotea.
Wanandoa hupoteza ukaribu wao, ushirikiano wao, urafiki wao, utani wao.
Mume hugeuka MP, mwanamke huwa kuruti.
Unajua kwanini? Sababu kabla ya ndoa walijitahidi kudumisha mawasiliano kati yao.
Walichat sana, walipigiana simu sana, na hata kukutana mara kwa mara, na mambo haya yalidumisha mahusiano yao na ukaribu wao.
Bro, ukioa usiue mawasiliano na mkeo kwa kisingizio kuwa utamkuta nyumbani ukirudi.
Baada ya kazi unpitia bar au kijiwe cha kahawa, na ukirudi home, huwa unajifanya umechoka sana na chochote atakachozungumza unachukulia kama anakupigia kelele.
Bro, wanawake wanachukia upweke, na upweke ni chanzo cha mawazo mabaya yanayoweza tia dosari ndoa yenu.
Ukioa, hata kama upo busy, tenga muda wa kumtext mkeo, kumpigia simu na kumjulia hali.
Ukirudi home, tenga muda wa kukaa na mkeo, zungumza nae, cheka nae, panga nae mipango, zungumza nae maneno yenye hisia na kutia hamu ya mapenzi, akiwa na huzuni mfariji, na kama ana la rohoni mwache atoe dukuduku lake.
Kila unapopata nafasi, eg: Weekend. Basi toka na mkeo, sio lazima muende sehemu nzuri, hata kuzunguka zunguka nae tu inatosha kumfanya ajisikie vizuri. 
Mkeo usimwache ajihisi mpweke, mpe raha ya ndoa kwa kuspend muda wako na yeye.
"Usioe ilimradi tu nawe uitwe mume mtu, bali oa sababu upo tayari kumuonyesha upendo umpendae na kumpa raha milele".




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa