KOVU LA MOYO 40. - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, February 8, 2020

KOVU LA MOYO 40.






Chozi la uchungu lilitoka katika mboni za macho ya Robby ... Hakutegemea kama siku moja angekuja kukutana na binadamu aliotokea kuwapenda na kuvutiwa na mwenendo wa Maisha yao kama Poshie na Angelo
Nini kimewasibu? ... Ndilo swali ambalo Robby lilikuwa likimchanganya .. wote walikuwa wamepata majeraha makubwa lakini Angelo alikuwa akionekana ni mtu aliyetoka kuumia muda si mrefu ... pingu aliyokuwa amefungwa Angelo ilizidi kumchanganya na kuanza kuhisi labda Angelo na Poshie wote wamefanya tukio la Ujambazi au Angelo atakuwa amemfanyia kitu kibaya mwenzake na Wananchi wamemshambulia yeye.
Yalikuwa ni maswali ambayo Robby alikuwa akijiuliza kichwani mwake bila ya kupata jibu kamili lakini ukweli ulibaki kwa Poshie na Angelo nini kiliwatokea nafikiri msomaji wewe unajua.
Robby hakuwahi kukutana na hali ya udhuni katika maisha yake, kama jinsi alivyokutana nayo siku hiyo. Alibaki ameduwaa na hasijue la kufanya, huku akiwa amepoteza kabisa kumbukumbu ya nini ilichompeleka hapo hospitali.
Alimpenda sana Poshie alimpenda kama Shemeji yake, ndoto zake zilikuwa ni kuwakuta wakiwa katika furaha ili awapatanishe na mapenzi yao yaendelee lakini wapi amekuja na kuwakuta wote hawajitambui na hajui nini kilichowasibu .... Akiwa bado ameduwaa ghafla akaja ndugu yake na kumwambia kitu kiichostua na kumfanya aondoke haraka eneo lile huku akiwa amechanganyiiwa
Kama ulikuwa na Roho ndogo usingeweza kumtazama Poshie mala mbili kwa jinsi alivyokuwa amevimba usoni ... Hali yake ilikuwa mbaya na bado hakuweza kurejesha fahamu zake, Madaktari walijitaidi kwa uwezo wao wote ili kuakikisha wananusuru maisha ya poshie
********
Baada ya kuwekwa mapumziko Dr Ally taratibu aliweza kupata nafuu na kufanikiwa kurejesha fahamu zake ... Alijishangaaa sehemu alipo na vipi amefika .... Baadae alinyanyuka na kutazama dirishani ili kutambua sehemu alipo na akagundua kuwa alikuwa maeneo ya Polisi na hapo ndipo akakumbuka kuwa aliambiwa Poshie amefariki ... Alikaa chini na kulia kwa uchungu. Dr Ally aliumia sana kumpoteza Poshie, alijitolea kila kitu katika maisha yake ili kuokoa maisha ya yule binti, lakini wapi Yeye ndiyo anabaki kuwa chanzo cha kupoteza maisha ya Poshie ... "Nakuchukia sana Aisha ... Aisha nakuchukia wewe Mwanamke, urembo wako ulinifanya nijue kuwa utakuwa mwalimu wa tabia na mfano bora kwa wasichana wanaochipukia kumbe wapi Aisha unakuwa na moyo wa kikatiri kama Shetani? ... Heti wivu? wivu gani wa kipuuzi mpaka unafikia hatua ya kupoteza maisha ya mtu kwa sababu yangu?" ... Masikini Dr Ally aliongea peke yake kama mtu aliyekuwa amechanganyikiwa kiasi fulani .... "Pole sana Dr Ally unaonesha ni jinsi gani ulivyoumia" ... Dada mmoja ambaye alikuwa ni Muuguzi katika kale kaospital kalichokuwa maeneo yale kulipokuwa na kituo cha Polisi ..... "Aisha umefuata nini hapa? ... Aisha wewe muuaji ... Aisha unataka kuniua!! Aisha ananiua jamani njoeni muumtoe" ..... Dr Ally alipiga kelele na kuzidi kumuogopa yule Dada akimuona kuwa ni Aisha ...
Dr Ally alikuwa amepatwa na msongo wa mawazo na kumfanya achanganyikiwe. Haraka walimkamata na kumfunga kamba kisha wakamkimbiza Hospital kubwa kwa matibabu zaidi
*******
Baada ya kufika kule ambapo alipokuwa amelazwa Mama yake, Roby hakuamini baada ya kumkuta Mama yake akifunikwa shuka tayari kupelekwa katika chumba cha kuifadhia Maiti.
Masikini Robby alikuwa amechelewa kidogo kuagana na mama yake kwa sababu ya Angelo na Poshie .... Robby aliganda kama mtu aliyepigwa na shot ya umeme aliona kama anaota vile, alijaribu kufikicha macho yake ili kuakikisha ukweli wa tukio husika .... "M-A-M-A" ... Ndiyo neno pekee ambalo alifanikiwa kulitoa tena kwa tabu katika kinywa chake na baada ya hapo ni machozi ambayo yalitililika kwa wingi huku macho yake yakiwa yanayasindikiza kile kitanda ambacho kilikuwa kimebeba mwili wa marehemu Mama yake.
Kidonda juu ya kidonda, Robby aliumia sana kumpoteza Mama yake kipenzi na ukizingatia yeye alikuwa na Mzazi mmoja tu aliyebakia naye ni mama yake huku Baba yake akiwa amefariki siu nyingi.
Aliyakumbuka Mateso waliyokuwa wameyapata Angelo na Poshie pindi walipolazimishwa kuingia katika majukumu ambayo hawakuyategemea katika maisha yao .... Yote ilitokana na kukosa Wazazi waliowazaa ... Wazazi Wa Poshie wangekuwepo kamwe wasingekubali kumtoa mtoto wao kwa mtu ambaye alikuwa hana kazi, hana kibarua wala sehemu ya kulala ... Angelo angekuwa na wazazi kamwe hasingedanganyika kuja Dar akiwa mdogo kuja kutafuta maisha na hata kama angekuja basi baada ya kupata matatizo ya Poshie basi Wazazi wake wangemsaidia kwa hali na mali hili kumnusuru mama na mtoto aliye tumboni
Kitu cha pili kilichowafanya Poshie na Angelo wapate tabu ni Elimu. wote walikuwa hawajasoma tena afadhali ya Poshie aliweza kufika angalau darasa la saba na kufuta ujinga, lakini Angelo yeye hakusoma hata darasa moja ndiyo mana hata maisha yake yalikuwa ni ya mtu ambaye alikuwa amekosa kitu muhimu katika maisha yake ..... Robby alikuwa anasoma na anayemsomesha alkuwa ni Mama yake, leo Mama kafa nani atakayemsomesha hicho ndicho kitu ambacho kilikuwa kinamliza sana Robby
*********
Dr Ally alipatiwa tiba ya haraka sana na kuambiwa ukweli kuwa Poshie hajafa, amepatikana na anaendelea vizuri .... Hakuamini masikio yake mpaka alipoenda kuthibitisha mwenyewe na kugundua kuwa Poshie hakufa na alikuwa bado yupo hai .... Baada ya kupata nafuu Dr Ally alimuhamisha Poshie Hospital aliyokuwepo na kupempeleka katika Hospital yao. Huko aliungana na madokta wenzake na kuanza kumpatia tiba ya nguvu Poshie .... Kadri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga ndivyo na hali ya Poshie ilivyokuwa ikizidi kuimalika na kurudi katika hali yake taratibu
******
Baada ya kumzika Mama yake Robby alijaribu kurudi pale Hospital kama anaweza kuwapata marafiki zake lakini kwa bahati mbaya alifanikiwa kumpata Angelo na Poshie alikuwa ndiyo hivyo tena amehamishwa na Dr Ally ....
Robby hakusita kumuhudumia ndugu yake kwa kipindi chote ambacho alikuwa anaumwa hapo Hospital ... hakuweza kuongea nae kwa sababu alikuwa chini ya ulinzi, lakini alitamani sana kuona ndugu yake anapona na amwambie kila kitu kuhusiana yeye na Poshie.
Baada ya kupata nafuu Angelo alipanda mahakamani, lakini upande wa mashtaka hakuwepo hivyo kesi yake ikapigwa tarehe na dhamana yake ikawekwa wazi ..... Robby akajitaidi na kumchukulia dhamana rafiki yake na kwenda naye nyumbani
Angelo alihisi haibu kubwa sana kutokana na Matusi aliyoyafanya pale mtaani lakini ndio hivyo tena atafanyaje wakati maisha yamemshinda .... "Karibu sana nyumbani hapa ndipo ulipoanzia Angelo wala usiogope, sema ndiyo hivyo tena Bi mkubwa hatunaye lakini muda huu alikuwa kashaanzisha zogo" ... Robby alimwambia Angelo na kumfanya Angelo aangushe chozi kama mtoto mdogo .... Hakutegemea kama siku moja anaweza kurudi nyuma na kuanza moja lakini leo yamemkuta
Robby alikuwa na shauku ya kutaka kujua kilichotokea baina ya Angelo na mwenzake hivyo usiku huo Angelo aliutumia kumueleza kila kitu Robby na hakumficha hata kitu kimoja na aliweza kumwambia kwa sababu moja tu, Angelo alikuwa mtu muhimu sana katika maisha yake ..... Robby alilia sana baada ya kusikia unyama ambao Angelo amemfanyia Poshie mwishowe wote wakajikuta wakilia kama watoto wadogo.
Robby alimlaumu sana Rafiki yake lakini mwishoni wakakubaliana wamtafute Poshie ili Angelo akamuombe msamaha na ikiwezekana Warudiane ili wamlee mtoto wao hasije kupata tabu ...
Walipanga mipango mingi mipya ya maisha yao baina ya Robby, Angelo pamoja na Poshie ambaye hapo hakuwepo ... Kubwa zaidi ilikuwa ni kufungua biashara ya genge na mkaa kwa sababu Robby hakuwa na pesa ya kumrudisha chuoni uganda
********
Poshie alifanikiwa kupona salama usalimini japokuwa alikuwa na kilema cha jino ila baadae alitafutiwa la bandia na kuziba pengo .... Aisha na watu wake walipandishwa kizimbani na kupatikana na hatia na wote kwa pamoja wakahukumiwa miaka mitano jela pamoja na faini .... Aisha alilia sana kwa sababu wivu ulikuwa umemponza na kilichokuwa kikimuumiza zaidi ni kwamba aliyekuwa akimpenda na kulilia wivu ndiye aliyemchoma na kukamatwa .... "Nimemfanyia mabaya sana Poshie naomba umuoe kama zawadi ya mateso aliyoyapata juu yako, hakuna kitu chochote ambacho unaweza kumlipa na moyo wake ukakunjuka zaidi ya mapenzi ya dhati" .... Aisha alimnong'oneza Dr Ally sikioni wakati anaenda kupanda gari la polisi tayari kwa kwenda jela huku akiwa analia kwa uchungu .... Dr Ally alistuka na kuduwaa na kuishia kushangaa
********
BAADA YA MIEZI 6
Poshie aliendelea kuishi na Dr Ally kama kaka na Dada huku wakiziendeleza biashara zao kama zamani na kuziboresha zaidi ... Poshie alizidi kunawili na kupendeza kiukweli usingeweza kumjua kama nini yeye kwa jinsi alivyokuwa amependeza .... Urembo wake wa siku nyingi ulmrudia na kumfanya amvutie kila mwanaume aliyekutana naye na kwa jinsi alivyokuwa na mwili mzuri mpaka aamue tu kukwambia kama amezaa ila kama akiamua kukudanganya ni lazima uingie katika mkenge ..... Siku moja akiwa anatoka kumchukua Henry Shuleni na gari yake aina ya Noha njiani akakutana na Robby ..... Mwanzo Poshie alimpita lakini baadae akarudisha gari nyuma na kuisimamisha kisha akashuka na kumuita ..... Robby akageuka na kustuka wakakimbiliana na kukumbatiana.
Poshie alimchukua Robby mpaka nyumbani .... "Karibu sana nyumbani jisikie huru" ... Poshie aliongea na kumkaribisha na kumfanya Angelo aduwae kwa maisha ambayo poshie alikuwa akiishi
Robby alimuadisia kila kitu jinsi alivyompoteza Mama yake na kushindwa kuendelea na masomo ... Poshie alilia sana na kumuhaidi kuwa yeye anajitolea kumsomesha .... "Nashukuru sana Shemeji Mungu atakubariki sana" ... Waliongea mengi yakiwemo ya Angelo, Baadae walipanga Kesho yake Robby aje ili ampatie pesa na aanze kufuatilia mambo muhimu
Robby alipotoka pale alienda kumwambia kila kitu Angelo na wakapanga kesho yake waende wote ili naye akamuombe msamaha .... "Kaka Poshie amekuwa mrembo sana yani hauwezi hamini utafikiri siiyo yeye" ... "Yani natamani hata kuche haraka ili niende kumuona mke wangu, lazima atanisamehe"
******
Siku iliyofuata walipendeza na kufunga safari kwenda kwa Poshie ... walifika nyumbani kwa Poshie na kukaribishwa na mlinzi kisha wakapita mpaka ndani.
Poshie alikuwa akijiandaa akitaka kutoka, ndipo msichana wake wa kazi alipomuita na kumwambia kama kuna wageni .... Poshie alitoka na kukutana uso kwa uso na Angelo alistuka paaaaaaaa!!! .... "Robby umefanya nini? Huyu kafuata nini nyumbani kwangu?" .... "Hapana Poshie usifanye hivyo" ... "Angelo toka nyumbani kwangu" .... Poshie alichukia na kuanza kumtimua Angelo. Angelo akapiga magoti huku akilia na kumuomba msamaha ..... "Nisamehe Mke wangu Dunia imeniadaa" .... "Nani mkeo Mimi Siyo mkeo tena ukome kuniita hivyo nimesema toka nyumbani kwangu" .... Poshie alipaza sauti kwa nguvu na kuongea kwa uchungu ..... "Jamani imekuaje tena mbona kelele?" .... Dr Ally aliingia na kuuliza ... "Huyu ndiyo Angelo aliyejifanya Prince na kuniaribia Maisha yangu ... Nakuchukia Angelo sitaki nikuone" .... Poshie aliongea kwa uchungu huku akilia ..... Dr Allly alimbembeleza na kumtuliza .... "Usipende kutoa hukumu kwa mwanadamu ambaye amekukosea! kitendo cha kulipa kisasi ni ishara ya kumhukumu binadamu mwenzako na hiyo ni kazi ya mwenyezi mungu. Hebu mtazame Baba mtoto wako, Yule tayari ameshahukumiwa na Mungu siyo yule kabisa ambaye umenisimulia .. Jifunze kusamehe 7x70 hata vitabu vinatuambia" .... "Dr Ally aliongea kwa upole kisha akamgeukia Angelo na kumwambia ... "Umemuumiza sana mwenzako ndiyo mana yupo katika hali kama hii na tukisema tukumbushe yaliyopita, tunaweza kusababisha matatizo makubwa sana ... Kuwa huru na mwambie Mama mtoto wako ulichotaka kumwambia"
Angelo alimeza mate huku machozi yakimtoka akamtazama Poshie na kumwambia ... "Nakupenda sana Mke wangu, naomba unisamehe kwa yote niliyokufanyia .... Nilikuwa naomba twende tukaishi kama zamani yani mke na Mume" ....
Poshie alilia sana kisha akamjibu ..... "Nilikupenda sana Angelo na wewe unajua ilo, kosa langu kubwa lilikuwa ni kukuonesha kama mimi nakupenda ... Sikutegemea kama siku moja ungekuja kunitia kidonda cha moyo kilichotaka kuondoa uhai wangu ... Namshukuru sana Dr Ally kwani yeye ndiye mwanaume pekee aliyeweza kutibu kidonda cha moyo wangu na likabaki KOVU LA MOYO nimekusamehe ila stokusahau ... Kwa swala la mapenzi mimi siwezi kurudiana na wewe kwa sababu naweza kulichubua KOVU langu na kikawa tena kidonda ... Kwa sasa nina mpenzi wangu huyu hapa anaitwa Dr Ally nafikiri unamuona ndiyo Mume wangu mtarajiwa" .... Poshie aliongea na kumstua kila mtu akiwemo mwenyewe Dr Ally Kwa sababu hawakuwahi kuliongelea hilo .... "Mimi siamini kama huyo anaweza kuwa mpenzi wako hebu naomba unithibitishie" .... Angelo alimwambia Poshie kwa sababu aliamini kwakuwa yeye ndiye aliyemtoa bikra Poshie basi hawezi kuwa na mtu mwengine zaidi ya Yeye ... Poshie alimgeukia Dr Ally na kumpelekea Mdomo na kilichofuata ni juice ya mahaba huku Angelo na Robby wakishuudia kisha Poshie akamwambia Dr Allly ... "Nakupenda sana Ally, naomba nikukabidhi maisha yangu" ... Dr Ally hakuwa na la kujibu zaidi ya kuduwaa
Angelo aliondoka bila ya kuaga Robby alijaribu kumuita lakini wapi .... Robby aliaga na kuhaidi kuwa atarejea kesho yake
Dr Ally kumbe alitokea kumpenda sana Poshie lakini alikuwa anaogopa kumwambia kutokana na Poshie alipata matatizo kwa kila mwanaume aliyemsaidia hivyo na yeye angemwambia basi angemuona tapeli ..... Tokea siku hiyo Poshie na Dr Ally walikuwa wapenzi na wakafanikiwa kufunga pingu za maisha .... Poshie hakusitisha haadi yake na kuendelea kumsomesha Robby
Nyumba ya kina Robby iliuzwa na familia na Angelo akarudi mtaani kuendelea kuomba kama ilivyokuwa zamani
MWISHO
JE UMEJIFUNZA NINI KUPITIA STORY HII??? ... TOA MAONI YAKO NIJUE KAMA UJUMBE WANGU UMEFIKA



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa