KOVU LA MOYO 10 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, February 6, 2020

KOVU LA MOYO 10




Unasemaje wewe Mwanamke? .. Angelo alistuka na kumuuliza Poshie .. "Nina mimba ya miezi mitatu Angelo, sijui itakuaje na nyumbani wanajua kila kitu" .... Poshie aliongea kwa umakini akimwambia Angelo huku akitazama watu wasije kumsikia
Kutokana na eneo ambalo walikuwepo Angelo aliona watu wanaweza kuwasikia na hizo habari zikaenea kila kona.
Alimchukua Poshie na kwenda naye kule kwenye chumba cha rafiki yake, ambaye ni Robby, ili wakaongee vizuri ikiwezekana wapate muafaka wa jambo hilo
"Kiukweli mimi sina mpango wa kuwa na Mtoto kwa sasa Poshie, sijui tunafanyaje mpenzi wangu" ... Angelo alimwambia Poshie huku akiwa amechanganyikiwa na hasijue la kufanya ... "Mimi pia nilikuwa sikutaka kuzaa katika umri huu na ndoto zangu zilikuwa nije kupata Mtoto nikiwa katika ndoa, lakini yote haya umeyasababisha wewe Angelo bila ya wewe mimi nisingeshika huu ujauzito"
Iliwachukua daika kadhaa wakibishana juu ya hilo swala huku kila mmoja akimtupia lawama mwenzie kuwa ndio amehusika kwa uzembe huo.
"Hata kama tukilaumiana Poshie, ndio hivyo tena tatizo limeshatokea na mimi na wewe bado wadogo na hatuwezi kuwa na Mtoto kwa sasa kwa sababu bado hatujayapanga maisha yetu vizuri, hivyo tutafute njia mbadala" ... "Bado sijakuelewa Angelo ulikuwa unamaanisha nini?' ... 'Nilikuwa namaanisha kwamba tufanye haraka iwezekanavyo ili tuitoe hiyo mimba kabla haijawa kubwa" ... Kauli ya Angelo ilimchefua sana Poshie na kujikuta akimpiga kibao na kumwambia ... "Sijawahi kuona kama Angelo una moyo wa kishetani kiasi hicho? Yani unataka nimuue mwanangu aliye tumboni? Siwezi kufanya hivyo hata siku moja" ... Poshie aliongea kwa uchungu huku akilia ... "Samahani sana Mpenzi wangu kama nitakuwa nimekukosea lakini nilikuwa sina maana mbaya Poshie. Hebu tazama maisha yangu mpenzi wangu, sina kazi, sina pa kuishi hivi unavyofikiri wewe tutakilea vipi hiki kiumbe kinachokuja?" ... "Vyovyote itakavyokuwa Angelo lakini mimi na wewe hakuna hata mmoja wetu mwenye haki ya kumtoa roho binadamu mwenzake zaidi ya mungu na endapo mimi na wewe tutajipa majukumu hayo, ni sawa tutakuwa tumemuingilia Mungu katika majukumu yake" ... Poshie aliendelea kushikiria msimamo wake na Angelo alikuwa bado akimshawishi waitoe hiyo mimba.
*****
Poshie na Angelo walikuwa wakipendana sana na baada ya kubishana kwa siku kadhaa Angelo aikubaliana na Poshie wailee mimba yao kivyovyote itakavyokuwa katika maisha yao na Mungu akiwajalia watakapokuja kupata Mtoto basi pia watamlea kwa kile ambacho watakuwa nacho kwa wakati huo.
Angelo aliamua kwenda kujitambulisha nyumbani kwa kina Poshie hili afaamike kuwa yeye ndiye mwanaume ambaye alikuwa amemtia mimba Poshie .... "Karibu sana kijana na kama umejileta wewe mwenyewe ni jambo zuri sana ila kama ungesubiri mimi nikutafute ungepeta tabu sana kijana. Sasa Kijana huyu mwenzako mimi nilikuwa nina mpango wa kumuendeleza kimasomo, lakini kwakuwa wewe umeona muanzishe familia na mwenzako basi ni jambo zuri sana. Naomba umbebe mwenzako na uwende ukaishi naye huo nyumbani kwako" .. Mzee Makasi aliongea kwa umakini huku aichezesha mguu akimtazama Angelo ... "Sawa Mzee wangu nimekuelewa, ila nilikuwa nakuomba univumilie kwa sasa kwa sababu mimi sina kazi na sina pa kuishi pia nalala kwa Rarafiki yangu yeye ndio ananisaidia Mzee" ... "Mpumbavu mkubwa wee hivi wewe una akili kweli? Kama ulijijua ulikuwa na matatizo hayo kwanini mliamua kutiana mimba?" .... Mzee Makasi alimfokea sana Angelo na kumlazimisha amchukue Poshie ili aondoke naye.
Poshie aliyajua fika maisha ya mpenzi wake na aliamua kuja kumuombea kwa Mjomba wake ili amvumilie kwa sasa ili ajipange kwanza ... Mzee Makasi alimsikiliza Poshie na kumpa masharti makali sana Angelo ikiwemo na kumsaidia mwenzake kwa kila jambo likiwemo chakula ... Angelo alimwambia Mzee makasi kuwa atajitaidi kadri ya uwezo wake na atakuawa akileta uduma kila siku hapo nyumbani kwa Mzee Makasi
*****
Maisha yalizidi kuwa magumu kwa upande wa Angelo na kila sehemu alipokuwa akitafuta kazi alikuwa anakosa labda kutokana na kiwango cha elimu alichokuwa nacho
Siku za mwanzo alijitaidi na alikuwa akipeleka baadhi ya vitu kwa mzee Makasi, lakini ilifika wakati Angelo alikuwa hashiki hata sh 10. Angelo alikuwa akimvizia Mzee Makasi pindi anapokuwa hayupo na yeye alikuwa anaenda nyumbani kwake na kula chakula.
Baada ya miezi mitatu kupita Angelo alikuwa amezidi kupigika na alikuwa hana kitu kabisaa ... "Mbona upo hivyo mpenzi wangu? Niambie huna nini ambacho kinakusumbua?" ... Poshie alimuuliza Angelo baada ya kumuona amekuja nyumbani kwao huku akijisonya ... "Maisha yamenipiga mpenzi wangu, yani sijui itakuaje?" ... "Bado umeniacha njia panda Mume wangu ebu niambie kuna nini kinachokusibu?" ... "Mama Yake Roby amenifukuza nyumbani kwao na sijui nitaishi wapi" ... Angelo alimwambia Poshie kuwa kule alipokuwa amesaidiwa na rafiki yake na alikuwa amejishikisha kwa sasa alikuwa ametimuliwa na hakuwa na kwengine pa kwenda.
Poshie alivuta pumzi na kuziachia taratibu, alikaa chini na kumtazama mpenzi wake na kujikuta machozi yakimtoka kisha akamwambia ... "Mungu anamakusudi yake kwa kila jambo jema mpenzi wangu. Kila penye mafanikio basi hapakosi vikwazo, na hivi mungu ameviweka kwa makusudi kama changamoto ili hakupime imani yako kwake. Jipe moyo mpenzi wangu naamini siku moja utashinda na tutakuja kuishi kama mke na mume pamoja na mtoto wetu kwa raha na starehe" ... "Nashukuru mke wangu kwa maneno yako mazuri yenye kutia moyo, mimi nasema kila siku mke wangu, sidhani kama nitakuja kupata mke kama wewe katika maisha yangu. Lakini kwanini kila siku mimi mke wangu" ... "Hapana Angelo usiseme hivyo muda mwengine Mungu anakupa matatizo ili kukustua akili yako" .... Poshie alimwambia maneno mengi sana Angelo yaliyomgusa moyoni mwake na kumuahidi atapigana kiume ili apate kazi na watapata sehemu yao ya kuishi na yote yataisha.
Poshie alitoa chakula na kumtengea mpenzi wake na Angelo akawa anakula haraka haraka ili Mzee Makasi hasimkute hapo.
"Kula haraka Angelo Mjomba akikukuta hapa itakuwa ni ugomvi mkubwa kwa sababu kila siku analalamika kuwa wewe hauleti chochote hapa tofauti na ulivyoahidi" .... "Safi sana Mwanangu kumbe hiyo ndiyo kazi yako Mjomba? Yani mimi nanunua chakula wewe kazi yako kumuonga huyu mpuuzi wako si ndiyo?" ... Mzee Makasi alitokea ghafla na kumfokea Poshie "Samahani sana Mjomba sirudii tena" ... "Ngoja nitakuonesha nini unachotakiwa ufanye maana wewe huna akili unaitaji ukajifunze ili ujue wenzako wanatafuta vipi maisha" ... Mzee Makasi aliongea kwa hasira kisha akaingia ndani na kutoa mizigo ya Poshie na kuwatimue waondoke nyumbani kwake .... "mjomba nisamehee Sirudiii tena, Angelo hana pa kuishi wala hana kazi naomba unihurumie mjomba nitateseka Mjomba" ... Poshie alijaribu kumlilia Mjomba wake ili amsamehe lakini wapi Mzee Makasi alionekana alikuwa amedhamilia na aliingia ndani na kutoka na panga ... Angelo alijaribu na yeye kumlialia Mzee makasi lakini wapi Mzee makasi alimpiga na panga na kumkata huku akiongea maneno makali kuwa atamuuwa mtu yeyote ambaye atamletea ubishi mbele yake.
Poshie hakuamini kama Mjomba wake anaweza kumbadilika kiasi kile na kumtimua nyumbani kwake kama mbwa mwizi.
Poshie na Angelo hawakuwa na jinsi, waliamua kushikana na kuondoka wasipopajua huku kila mtu akiwa analia kama mtoto mdogo
Waliondoka na kuelekea nyumbani kwa kina Robby kwenda kujaribu kumshawishi Robby kama anaweza kumuombea kwa Mama yake walau Poshie alale hapo .... "Karibuni mbona hivyo, kuna msiba huko mlipotoka?" ... Robby alimuuliza Angelo na akamuelezea kila kitu ambacho Mzee Makasi amewafanyia na kumpigia magoti ili Robby awasaidie ... Robby alishusha pumzi na kuchoka kabisa ... "Yani sijui nikusaidieje Angelo, kiukweli mimi napenda kukusaidia zaidi ya msaada wa kawaida lakini ndio hivyo mshikaji wangu Mimi bado nipo numbani na Mama yangu hakutaki wewe ukae hapa sasa sijui kama ataweza kumsaidia Mchumba wako tena kwa hali yake jinsi alivyo ........


NINI KITAENDELEA? ...



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa