KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA KWANZA - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, February 5, 2020

KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA KWANZA






Ilikuwa ni majira ya saa sita za mchana, joto likiwa kali kama ilivyo kawaida katika jiji la Dar Es Salaam. MAGOSHO kijana wa marehemu Mzee Machaku alikuwa jikoni akitayarisha chakula cha mchana kwenye nyumba ya mhindi NAKESHWAR alipokuwa akifanya kibarua cha kazi za ndani.
Bi. Fahreen ambaye alikuwa ni mke wa Nakeshiwar alifungua mlango wa jikoni taratiibu na kumkuta kijana akishughulika kazi zake za kila siku.
Bi. Fahreen alisimama mlangoni pale na kumtazama Magosho kwa jicho la tathmini na udadisi mkubwa. Aliweza kuona mgongo wa kijana yule uliokuwa umetuna kidogo pengine ni kutokana na mazoezi ya viungo ukiwa ndani ya fulana ya mikono mifupi iliyoacha misuli ya mikono yake iliyokuwa imejazia kiasi kuonekana na mwanamke yule. Bi Fahreen aliendelea kumchambua kijana yule kwa kumteremsha hadi miguuni na kuona misuli ya miguu ile ilivyosimama ipasavyo utafikiri mafungu ya magimbi.
Magosho alikuwa bize na kazi yake pasipo kufahamu kama nyuma yake kulikuwa na mtu akimchunguza.
Bi. Fahreen alimsogelea taratibu Magosho na kusimama nyuma yake. Alimeza funda kubwa la mate na kutoa pumzi ndefu. Umbile la kijana yule lilikuwa limevutia na kumkosha ndani ya mtima wake. Alitamani kupata japo nafasi ya kumkumbatia tu pengine nafsi yake ingeridhika.
Akanyanyua mkono wake wa kushoto na kuupeleka sehemu za kiunoni kwa Magosho taratibu huku akisita sita. Alihofia sana endapo kijana yule asingemuelewa angeiweka wapi sura yake. Hata hivyo alijipa moyo na peleka mkono wake kwenye kiuno kile. Alipomgusa tu Magosho alishituka kwa nguvu na kugeuka nyuma huku akitoa sauti ya mshituko.
“Hee! Kumbe veve iko oga sana?” alihoji Bi. Fahreen kwa rafudhi yake ya kihindi huku akijichekesha chekesha kinafki mbele ya kijana yule.
“Ah! Mama kumbe ni wewe!” alisema Magosho huku akishindwa kutafakari kitendo kile alichafanyiwa na bosi wake wa kike.
“Mimi iko toa dudu veve kwenye nguo yako. kwani Iko baya?” alihoji Bi. Fahreen akijibaraguza.
“Ahaa! Nashukuru mama hakuna ubaya” alijibu Magosho na kugeuka kuendelea na upishi.
Kitendo cha Magosho kuruka kama vile alikuwa amepigwa na shoti kilileta msisimko zaidi kwenye mwili wa Bi. Fahreen. Yani mwanamke yule alikuwa kama vile amepandwa na pepo gani sijui katika ubongo wake. Alikuwa hajielewi wala hajitambui kwa kila ambacho alikuwa anakifanya kwa wakati ule. Aliinua mkono wake na kuuweka kwenye bega la Magosho.
“Vipi Chakula bado iva?” akajifanya kuhoji huku mkono wake ukiwa bado kwenye bega la Magosho akimtekenya tekenya kwa vidole vyake.
“Namalizia mama” Magosho alijibu huku akihisi msisimko ndani ya mishipa yake ya damu. Alitamani kumwambia mke wa bosi wake atoe mkono kwasababu alikokuwa akielekea kulikuwa siko.
Mama yule wa kihindi aliendelea kuuchezesha mkono wake pale kwenye bega la watu bila huruma. Akapeleka mkono wake wa kulia kwenye kiuno cha kijana yule na kuendelea kufanya utundu wake.
Magosho ambaye alikuwa akikoroga jikoni alijikuta akishindwa kuendelea na kazi. Akainua macho juu kusikilizia hali fulani iliyosababishwa na vidole vya Bi.Fahreen kwenye kiuno chake. Alimgeukia mama yule na kumkuta amelegeza macho kama vile alikuwa amekunywa supu ya bamia.
Bi.Fahreen akatumia mikono yake kuvuta kichwa cha Magosho hadi usawa wa kifua chake. Ufupi wa Magosho ulipelekea nywele zake ndefu za kibantu kumchoma choma mama yule kwenye madafu yake mawili ya kifuani na kupelekea msisimko mkubwa.
Magosho alianza kupoteza uvumilivu na kuuma memo yake kwa nguvu huku amefumba macho na akisikilizia mapigo ya moyo wake yalivyokuwa yakienda mbio.
Baada ya mwanamke yule wa kihindi kuzidisha vituko, kijana Magosho akajikuta akizunguusha mikono yake na kuanza kuchezea furushi la mama wa wawatu ambalo lilikuwa likimfanya kuonekana tofauti na wahindi wengine. Kiukweli Bi. Fahreen alikuwa ameumbwa na kuumbika utafikiri mwanamke wa kibantu. Kuanzia juu alikuwa na umbo la kawaida lakini kuanzia chini ya kiuno chake chembamba kulikuwa na hipsi zilizotanuka kiasi cha kuwa na uwezo wa kutosha kubeba furushi kubwa lililokuwa nyuma.
Umbo lile adimu lilifanya mama yule kuonekana mnene kama ungemtazama kuanzia chini. Lakini pia ungemuona ni mwanamke mwembamba kama ungemtazama kuanzia juu na kuishia kitovuni. Jamani! Wacheni Mungu aitwe Mungu. Kuna watu wameumbwa nyie, Mnh!
*****
Magosho alikuwa ni mtoto wa mama Ashura ambaye alikuwa hohe hahe asiye na mbele wala nyuma. Mama huyo alikuwa akiwapenda sana watoto wake waliokuwa wawili tu kama mboni za macho yake. Halkadhalika Magosho na dada yake Ashura walikuwa wakimpenda sana mama yao kuliko kitu kingine chochote.
Asubuhi Magosho akiwa amelala juu ya kitanda cha teremka tukaze kilichokuwa kimepambwa kwa ukili chakavu ulioashiria kutengenezwa muda mrefu uliopita. Macho yake yalikuwa juu ya paaa lililo kuwa na tundu kubwa lililopitisha mwanga wa jua la asubuhi kwa kiasi fulani uliopelekea nuru kiasi ndani ya chumba kile kidogo kilichokuwa na kiza kutokana na na udogo wa madirisha yake.
Harufu mbaya iliyokuwa ikizalishwa na mfereji wa maji machafu uliopita usawa wa dirisha lake ilipenya ipasavyo kwenye tundu za pua yake na kusafiri hadi kwenye vifuko vya kuzalishia mate na kusababisha funda kubwa la mate kujaa mdomoni. Aliyatema chini na kuyafukia kwa mguu wake wa kushoto kwa urahisi kutokana na vumbi lililokuwa mle ndani ya chumba chake kilichokosa sakafu.
Sauti ya nzi mkubwa aliyekuwa na rangi ya kijani ambaye aliingilia kwa kupitia kwenye tundu la paa ilimgutusha. Nzi yule aliruka hapa na kutua pale mle chumbani. Magosho alijiinua kwa hasira na kuanza kumputa kwa kipande cha mti wa ufagio alichokitoa uvunguni.
Purukushani zile ziliendelea kwasababu kila alipojaribu kumpiga nzi yule aliruka na kwenda kutua sehemu nyingine. Alipotua juu ya mfuniko wa ndoo ya plastiki alimnyatia na kuinyanyua fimbo juu na kuitua kwanguvu juu ya ndoo ile iliyotoa sauti kubwa ‘Paaa’. Hata hivyo nzi aliruka na kutoka nje kupitia dirishani. Akamtazama kwa hasira na kutoa msonyo mrefu.
Sauti ya kicheko ilimgutusha na kumfanya kutupa macho mlangoni. Kumbe muda wote alipokuwa akifukuzana na nzi yule mdogowake Ashura alikuwa amesimama mlangoni akimtazama huku akicheka kwa kuziba mdomo kwa mikono. Tukio la kupiga kwenye ndoo kwa nguvu halafu akamkosa adui yake ndilo lilimfanya binti yule kuangua kicheko cha sauti. Ayubu alijikuta akifadhaika kwa kile alichokuwa akikifanya kuonekana na mtu mwingine.
"Unacheka nini?" Magosho alihoji.
"Hujui?" alihoji Ashura huku akiendelea kucheka.
"Dogo usinichanganye" Magosho alijifanya kukasirika.
"Dah! ila we mkali Broo. Yaani umempiga…..kahepa, ukampa tena…. kahepa, Ukavuta tena kwanguvu akakwepa, uka...." Ashura alikatishwa kauli yake na Magosho.
"Ashura ondoka" alisema Magosho kwa hasira.
"Dah! utadhania mchina vile jinsi ulivyokuwa ukipambana. Huuu haaa!...huuu!...haaa!" alisema Ashura huku akimuiga kaka yake alivyokuwa anampiga nzi.
"Ashura ntakutwanga ukaseme kwa mama yako" alisema Magosho huku akimsogelea mdogo wake Ashura taratibu.
"Thubutuuu! umemshindwa nzi utaniweza mie?" Ashura alizungumza kwa uchokozi huku akitabasamu kwa furaha. Alikunja ngumi na kumnyooshea kaka yake.
"Haya njoo sasa....njoo" alisema huku akirudi nyuma. Magosho akainua mti ule wa fagio na kutaka kumpiga nao. Ashura akatimua mbio kutoka nje huku akimcheka kaka yake.
Magosho alikuwa akipendana sana na dada yake Ashura ambaye alikuwa ni wa pekee. Ingawa walikuwa wamepishana sana kiumri lakini walikuwa wamezoea kutaniana na kufurahi kwa pamoja. Kutokana na sababu hiyo ndiyo maana Ashura hakuhofia kumtania kaka yake kwa kile kilichotokea. Pale Magosho alipochukua ufagio hakuwa na lengo la kumpiga mdogo wake bali alimtishia tu na alifahamu kuwa angekimbia.
Baada ya dakika kadhaa Magosho alitoka chumbani kwake na kumkuta mama yake pamoja na Ashura wakikaanga mihogo ya biashara.
"Wakuonja basi jamani" alisema Magosho kwa utani
"Lete hela hakuna cha bure hapa" alijibu Ashura huku akikata muhogo mbichi na kuumenya.
"Nawewe nini? Hebu kwenda huko" alisema Magosho huku akiinama na kuokota kipande cha muhogo kilichokwisha kaangwa.
"Chukua chai kabisa unywe" alisema mama Ashura huku akigeuza mihogo kwenye karai lililokuwa limeinjikwa jikoni.
"hapana mama nikinywa chai nitachelewa. Huu muhogo unatosha" alisema Magosho.
"Kwahiyo leo unakwenda kuhangaikia wapi?" Mama Ashura alihoji.
"Nakwenda mjini labda leo naweza kubahatika"
"Sawa ila uwe makini mwanangu" alisema mama Ashura kwa msisitizo.
"Sawa mama usijali" alijibu Magosho huku akivuta hatua kuondoka.
"Nzi huyo nyuma yako…" Ashura alipaza sauti kumtania kaka yake akimkumbushia tukio la kumpiga nzi chumbani kwake.
"We subiri nikirudi ndo utanitambua" alisema Magosho pasipo kugeuka nyuma na kutoweka machoni mwa Ashura na mama yake.
***
         Safari ya Magosho ilikuwa ni ya mjini Kariakoo ingawa hakufahamu ni sehemu gani ambapo alilenga kufika. Lengo lake lilikuwa ni kwenda kutafuta ajira ili aweze kulea familia yake iliyokuwa na maisha magumu hasa baada ya kufariki kwa baba yao mpendwa mzee Machaku kwa ugonjwa wa malaria. Ingawa hawakuwa na maisha mazuri kipindi cha uhai wa baba yao huyo lakini kwa kiasi fulani maisha hayakuwa ya taabu kama wakati ule waliokuwa nao.
Magosho Alipofika mjini alianza kuzunguuka kwenye mitaa ya kariakoo. Alipinda kushoto na kukamata barabara ya vumbi. Alitembea kwa mwendo mrefu huku akisoma vibao vya mashirika mbalimbali barabarani. Mungu hamtupi mja wake, macho yake yalitua kwenye bango moja kubwa lililoandikwa kuwa walikuwa wanahitajika wafanyakazi hata kwa wale wasio kuwa na elimu kubwa yaani walioishia darasa la saba. Magosho akavuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu akiwa haamini macho yake. Ajira zile zilikuwa zikitolewa kwenye kiwanda cha kusindika maplastiki.
Alifuata njia ambayo mshale uliokuwa umechorwa kwenye bango lile ulimuelekeza na kwenda kutokea nje ya jengo kubwa la ghorofa. Alipofika getini alimkuta mlinzi kama ilivyo mila na desturi ya makampuni mbalimbali.
“Habari yako afande” Magosho alianza na kumsalimia.
“Jambo ndugu” afande yule akasalimia badala ya kujibu salamu.
“Sijambo, nimeona tangazo la ajira. Sijui utaratibu upoje?” alihoji Magosho.
“Ahaa! Ni kweli. Sasa unatakiwa kusaini kwanza hapa. Gharama yake buku mbili” alisema afande yule huku akimfunulia daftari.
Magosho akakumbuka kuwa mfukoni mwake kulikuwa kumesalia shilingi elfu mbili tu. Inamaana kama angetoa buku mbili ile basi angerudi kwa miguu kwasababu angekosa hata nauli.
“Yaani broo hapa unaponiona nina buku tu mfukoni” Alisema Magosho kwa sauti ya kubembeleza.
“Sasa unadhani tutafanyaje?”
“Naomba nisaidie ndugu yangu”
“Siwezi, kama huna pesa we ondoka tu” alisema afande huku akifunga daftari lake.
ITAENDELEA



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa