Jinsi Ya Kuishi Katika Mahusiano Marefu Na Mpenzi Wako - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, February 3, 2020

Jinsi Ya Kuishi Katika Mahusiano Marefu Na Mpenzi Wako




Kuwa katika relationship ni ngumu na pia ni rahisi. Kuna watu ambao hujaribu kuingia katika relationship lakini baada ya siku mbili tatu unaona wamekosana na mwisho kuachana. Pia utapata wengine wanakuwa katika relationship miaka mitano hata kumi na zaidi.

Hapo unaachwa na maswali yasiyokuwa na majibu ukijiuliza ni mbinu gani inayowafanya wapenzi hao wawili kudumu katika mahusiano marefu kama hayo.

Well, kama wewe umeingia katika mahusiano na unataka yawe marefu basi kuna sheria na masharti ambayo unapaswa kufuata ili kuhakikisha mahusiono yako yatakuwa marefu. Baadhi ya mambo ya kufuata na kuzingatia ni kama yafuatayo:

1. Kuwa na nafasi binafsi. Katika mahusiano, yawe mapya ama ambayo yameshamiri, lazima uwe na nafasi yako binafsi. Hii inatumika kwa yeyote ambaye hayuko single. Kama mnaishi pamoja basi unahitaji kuwa na nafasi ya kuwa kivyako. Hakikisha kuwa unameet na marafiki zako, nenda kafanye mazoezi, soma vitabu ili mradi tu unakuwa na uhuru wa kufanya mambo kivyako.

2. Chagua vitu vya kupigania. Kama mmekuwa mkiishi pamoja na mpenzi wako, kufikia sasa najua kuna mambo mengi ambayo unayajua kumhusu mpenzi wako unayoweza kuyatumia dhidi yake, jambo ambalo si zuri.

So badala ya kugombana kila wakati kuhusu mambo madogo madogo, ni bora kurudi nyuma na kufikiria ni mambo gani muhimu ambayo yanahitaji kupiganiwa.

3. Mazungumzo yaendelee kunawiri. Wengi katika mahusiano huchukulia kuwa wamekuwa katika mahusiano muda mrefu na wapenzi wao hivyo hawaoni umuhimu wowote wa kuwasiliana na wapenzi wao. Unachohitajika nikuendeleza kiwango cha mawasiliano na mpenzi wako muda wote. Usibahatishe hata mara moja.

4. Tokeni deti. Kutoka deti kuna umuhimu kwa kuwa mnapata kukumbana na mambo mapya. Mpenzi wako atafurahia kwa kuwa unaleta misisimiko mipya katika maisha yenu. Hivyo kumtoa mpenzi wako deti kuangalia sinema, mkahawa ama kwenda katika sehemu za kujipumbaza kunafungua maisha mapya kati yenu.
5. Usitarajie chochote. Ukimsapraize mpenzi wako na ua ama zawadi yoyote hupaswi kutarajia chochote kutoka kwake.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa