JE HAYA NI MAPENZI!! 101: - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, February 21, 2020

JE HAYA NI MAPENZI!! 101:





Sam alienda maliwatoni kupunguza maji ya bia
alizokunywa kwa usiku huo, na kurudi zake kwa
lengo la kulala sasa.
Akashangaa kumuona Ritha akiwa kajilaza
kitandani huku akiwa mtupu kabisa kwani nguo
zote alitoa na alikuwa akitabasamu.
Sam akamuangalia kwa kutikisa kichwa na kumuuliza,
"Unafanya nini Ritha?"
Ritha aliendelea kutabasamu na kumfanya Sam aongee tena,
"Ritha tafadhari, usitake nifanye makosa niliyoyafanya zamani sana na yanayonitesa hadi leo"
Huku Ritha akitabasamu pale kitandani akamuuliza Sam kwa sauti ya kimahaba,
"Makosa gani hayo?"
Ila kabla Sam hajajibu, tayari Ritha alishainuka na kumfata Sam alipo kisha kuanza kumpapasa katika mwili wake na kumnong'oneza kwa sauti laini kabisa hata Sam nae akalainika,
"Usiwe na tatizo mpenzi, mi ndio tiba yako"
Maneno ya Ritha yalimuingia vizuri Sam na kujikuta akikubali,
"Ila Ritha kama hii ni tiba kwangu basi ngoja nifanye"
Ritha akataka kumvua Sam nguo ila Sam akapinga na kumwambia Ritha,
"Tafadhari tuzime taa kwanza"
"Hilo si tatizo"
Ritha alihisi kuwa huenda Sam anaona aibu, na kwenda mwenyewe kuzima taa na kuhakikisha mlango kuwa umefungwa vyema, kisha akarudi alipo Sam na kuendelea na zoezi lake.

Muda kidogo Ritha alitoa kelele ya juu na kufanya watu karibu wote kwenye hoteli ile kushtuka na gafla ile kelele haikusikika kabisa.
Moja kwa moja Ritha alikuwa amezimia na Sam kumalizia shughuli yake.
Sam alipomaliza alijilaumu sana kwa kitendo kile alichomfanyia Ritha kwani alijua wazi kuwa na huyo lazima atafata nyayo za wakina Neema.
Alijikuta akijipiga piga mwenyewe kwani hata msiba wa Neema haujapita huku wa mwingine ukinukia.
"Hivi hawa wasichana wana majini au ni nini jamani? Mbona kunipa dhambi nisiyotaka kuitenda kila siku? Mbona wakinifanyia hivi? Mbona Sabrina hajawahi kuyatenda haya ingawa nimeishi nae, tuseme ni mshamba wa mapenzi au ni kitu gani? Nakumbuka nilipokuwa nikimwambia tusubiri alikuwa akichukia tu na kununa. Inakuwaje kwa hawa? Na kipi kinanivuta hivi hadi natenda mambo yasiyo stahiki?"
Sam alijiuliza maswali bila majibu huku akimtazama Ritha pale alipozimia na kupanga jinsi ya kutoka naye pale hotelini.

Sam akapata wazo la kusema kuwa amezidiwa ili aweze kumkimbiza hospitali na iwe njia moja wapo ya kuondoka naye pale hospitali.
Cha kwanza kabisa alifuta damu iliyokuwepo pale chini kisha kumvalisha nguo Ritha na kumbeba begani kisha kutoka naye.
Mlinzi wa ile hoteli aliwaona ila akajua ndio mahaba ya kileo na pia hakuweza kufatilia zaidi kwani alimtambua kuwa ni Sam na anatambua ni jinsi gani anavyopatana na mabosi wao.
Sam alimpakiza Ritha kwenye gari kisha kuondoa gari eneo lile huku akifikiria pa kwenda naye, hapakuwa na mahari pengine pa kwenda zaidi ya nyumbani kwake ili amsikilizie Ritha atakapozinduka.
Alifika na kuingia nae vizuri ndani kisha akamlaza kwenye kiti pale sebleni na hakutaka hata ashtuke muda huo kwani alijua wazi kuwa lazima angefanya fujo.

Usiku ule Jeff akiwa ametulia chumbani kwake, akaamua kwenda  sebleni kama kupoteza muda tu akamsikia mama yake akiongea na simu.
Akajikuta akipata hisia kuwa huenda mama yake alikuwa akizungumza na Dorry kisha akapata mashaka kuwa huenda mama yake anahusika pia katika kumtuma Dorry aongee maneno yale kuhusu Sabrina.
"Mmh kama mama kamtuma basi inamaana kuwa kuna vitu ametambua kuhusu mimi na Sabrina. Hata kama ametambua si atuache wenyewe tu, ila kama mama anahusika sijui kwakweli maana atakuwa ameniudhi sana"
Alikuwa akiyawaza hayo, akasikia kuwa mama yake amemaliza kuongea na simu kisha muda huo huo akasikia simu yake ikiita.
Akainuka na kwenda chumbani kuiangalia, akaona namba ya Dorry akatikisa kichwa na kuamini zaidi kuwa mama yake ndio kamtuma Dorry kusema yale aliyoyasema jana yake.
Jeff akaipokea ile simu na moja kwa moja sauti ya Dorry ikasikika,
"Nimekukumbuka sana Jeff jamani"
Jeff akacheka na kumwambia Dorry,
"Mwambie mama atafute binti mwingine wa  kunishawishi mimi ila sio wewe ambaye ulimaliza waswahili na kuwaanza wachina"
"Mbona sikuelewi Jeff"
"Ndio unielewe tu, najua unafanya kazi ya kunipeleleza basi ujue umeshindwa. Na vilevile hata kama nikiamua kuwa na mchepuko basi huwezi kuwa wewe. Kwaheri"
Jeff akaikata ile simu kisha kukaa kitandani kwake akijiwazia ila mawazo yake yote yalikuwa juu ya Sabrina na juu ya ile barua ya Neema, huku akiyafikiria maneno ya Sam.
"Lazima nisimame kiume sasa, lazima nimwambie ukweli Sam. Sijui tutasikilizana ila Mungu anisimamie kwa hili"
Kisha akalala.

Kulipokucha Jeff aliamka kisha akajiandaa na kumuaga mama yake kuwa anaenda kwakina Sabrina ila alimgundua mama yake kutokuwa na furaha kwa siku hiyo,
"Mama vipi unaumwa?"
"Hapana hata siumwi"
"Sasa mbona umepooza hivyo?"
"Mawazo tu mwanangu hata usijali"
Ila Jeff aliweza kuelewa kwa haraka kuwa mama yake atakuwa kaambiwa na Dorry majibu aliyopewa kwahiyo hayakumfurahisha kabisa na ndiomana ameonekana kusononeka kiasi kile.
Jeff akaondoka pale na kuelekea kwakina Sabrina.

Alimkuta Sabrina tayari alikuwa n je akifua nguo za watoto wake na kumsalimia.
Mama Sabrina naye alikuwa pembeni akiwaangalia tu na kumfanya Jeff atoe na salamu ya mbali kuweza kumfikia mama Sabrina kisha akatulia pale ili kuweza kuzungumza na Sabrina ambapo walijikuta wakitazamana kwa dakika kadhaa bila ya kusemeshana chochote ila Jeff mwenyewe akaamua kuumaliza ukimya ule kwa kumuuliza swali Sabrina,
"Umeotaje leo?"
Sabrina akamshangaa Jeff kwa lile swali na kufanya na yeye kuuliza pia,
"Kuotaje kivipi?"
"Yani siku ya leo umeota vitu gani?"
"Kwanini umeniuliza hivyo?"
"Nimekuuliza tu kwani kuna ubaya?"
"Hapana ila nimeshangaa swali lako ukizingatia leo ni kweli nimeota ndoto mbaya sana."
"Ndoto mbaya kivipi?"
"Ni ngumu kuielezea kwakweli"
Jeff akaitoa ile barua ya Neema na kumpa   Sabrina,
"Barua yako ni hii uliiangusha"
Sabrina akashtuka na kumuuliza Jeff,
"Umeisoma?"
Jeff akatikisa kichwa kuashiria kwamba ile barua ameshaisoma.
Sabrina akaichukua na kuiweka kifuani kama alivyoweka siku ya kwanza, Jeff akamwambia,
"Kuwa makini usije ukaiangusha tena"
Sabrina akaona ni vyema aipeleke chumbani kwake kwanza kwahiyo akaachilia kufua pale na kwenda ndani.
Muda wote huo mama wa Sabrina alikuwa akiwaangalia na kuona yote yaliyoendelea ingawa hakuweza kusikia kuwa wanazungumzia kitu gani.
Sabrina alipotoka nje akamkuta Jeff amesimama pale pale kisha akatabasamu baada ya kumuona tena Sabrina pale nje na kumuaga kwa kumwambia.
"Ukimaliza kuisoma niambie"
Jeff akaondoka zake.

Mama Sabrina akamsogelea mwanae na kumuuliza,
"Hivi kuna kitu gani kati yako na Jeff?"
"Kivipi mama?"
"Kwani amekuja kufanya nini asubuhi hii?"
"Kuna mzigo ameagizwa na mama yake ndio aliniletea"
"Mmmh"
"Mbona unaguna mama?"
"Hamna kitu"
Kisha mama Sabrina akaenda kuendelea na majukumu yake aliyokuwa akiyafanya, ila Sabrina akatambua tu kuna kitu mama yake amekihisi kuhusu yeye na Jeff.

Sam alikuwa ndani kwake na kumuangalia Ritha hadi pale alipozinduka na kukaa huku akijaribu kuvuta kumbukumbu zake, kisha akakumbuka tukio lililompata na kumtazama Sam huku akijikuta kushtuka na kuongea kwa nguvu,
"No, hapana wewe Sam sio binadamu wa kawaida. Nimefikaje hapa?"
Ritha akainuka na kujiangalia mara mbili mbili, akahisi maumivu kwenye sehemu za siri na kumfanya akumbuke vizuri mchezo mzima.
Hakuweza kuvumilia kwakweli na kutaka kutoka ila Sam akamzuia na kumwambia,
"Tafadhari Ritha naomba iwe siri"
Ritha akamfyonya Sam na kumwambia,
"Kafanye siri na baba yako mzazi mbwa wewe"
Sam akamuangalia tu Ritha bila ya kumwambia neno la ziada kwani swala la kutajiwa baba yake mzazi lilishamuumiza kichwa tayari na kumfanya ajisikie  vibaya kwa wakati huo.
Akakaa chini na kutafakari, akaangalia utajiri aliokuwa nao na kila kitu alichonacho.
"Hivi ni kwanini nimeshindwa kumpata baba yangu mzazi hadi leo? Huyu baba popote pale alipo na alaaniwe...."
Akasita kidogo na kujiuliza,
"Kwani amefanya kosa gani hadi alaaniwe? Aah ndio ameniacha mimi nilelewe na baba wa kambo mwenye roho mbaya na kufanya nisipate mapenzi ya mama mzazi ingawa mamdogo naye kanilea vizuri sana. Ila nadhani mamdogo kanilea vizuri kwavile hakuwa na mtoto"
Akafikiria tena, ila akaona ni muhimu amfahamu baba yake ili huyo baba yake aumizwe na mafanikio aliyonayo kwasasa.
"Atambue wazi ingawa hakunilea ila nimefanikiwa sana"
Wazo kuhusu baba yake lilimjia baada ya kuambiwa na Ritha kuwa akafanye siri na baba yake mzazi.

Ritha alipofika kwao akaamua kujitazama vizuri sasa na kujiona akiwa anatokwa na damu.
"Mungu wangu, hivi yule mwanaume ni binadamu kweli? Kwanini nilifikia hatua ya kulala nae? Kwanini sikufikiria haya kabla? Eeh Mungu naomba urudishe muda nyuma tafadhari, naomba urudishe muda kabisa niwe sikuondoka hapa nyumbani kabisa? Mambo gani haya yamenipata jamani?"
Alijisikilizia na maumivu nayo yakamzidia sehemu yake ya siri na kumfanya uzalendo kumshinda.
Akamuita dada yake wa karibu ili aweze kumuomba ushauri,
"Ritha vipi? Tatizo ni nini?"
"Yamenikuta makubwa dada huwezi amini, yani najiona kama naota vile"
"Hebu nieleweshe mdogo wangu, umekuja hueleweki. Nguo imechafuka damu, inamaana umeingia kwenye siku zako bila kujijua?"
"Ni kheri ingekuwa hivyo dada, ila kuna mwanaume mmoja kanifanyia ushenzi sana leo halafu anasema nisiseme"
"Kakufanyia nini?"
Machozi yakamtoka Ritha kwani aliweza kurudisha matukio nyuma kwa haraka sana kasoro tukio la kuzimia tu kwani hakuwa na kumbukumbu nalo.
"Dada, katika maisha yangu sijawahi kukutana na aina hii ya mwanaume ila leo kwa mara ya kwanza nimekutana na mwanaume mwenye maumbile ya tofauti na wanaume wengine"
"Unamaana ana maumbile makubwa?"
"Ingekuwa hivyo nisingelalamika"
Akatulia tena kwa kilio kwani kadri alivyoelezea ndivyo alivyoona moyo wake ukizidi kuumia na kumfanya machozi yamtoke zaidi.
"Dah pole mdogo wangu, itabidi twende hospitali jamani"
Dada wa Ritha aliyejulikana kwa jina la Mage, akainuka ili afanye kama kumuhamasisha Ritha kuwa wainuke na waende hospitali ila alimshangaa Ritha akijinyoosha pale chini na kuwa kimya gafla.
"Ritha, Ritha, wee Ritha wee"
Kimya, akadhani kuwa Ritha anamfanyia mchezo na kujaribu kumtikisa tikisa ila Ritha alikuwa kimya.
Mara Mage akashtushwa na mlio wa simu ya Ritha, akaichukua na kuipokea kwani hata yeye hakujielewa wala kujitambua pale.
Akasikia sauti ikiongea upande wa pili,
"Tafadhari Ritha usimwambie yeyote ile habari utakufa"
Mage akajikuta akiuliza kwa ukali,
 "Wee nani wee nani?"
Simu ikakatika na kumfanya Mage apatwe na uoga zaidi kuwa huenda Ritha amekufa, na ndio hapo alipoanza kupiga kelele za kuomba msaada.

Sam alijilaumu kwa kitendo chake cha kupiga simu tu na kuanza kuongea bila kuuliza anayeongea naye.
Mara gafla akapatwa na maumivu ya moyo yaliyomfanya atambue moja kwa moja kuwa kuna tukio limetokea na hakufikiria mbali zaidi ya kufikiria kuwa ameshampoteza Ritha.
"Maskini Ritha jamani, haikuwa kusudio langu jamani. Pole Ritha"
Sam aliumia na kukumbuka maisha yake ya nyuma ambapo alipoteza maisha ya wadada kadhaa na sasa lile swala lake limejirudia tena kwa staili hiyo.
Aliilaumu nafsi yake na alimlaumu mtu wa kwanza kumuharibu yeye kisaikolojia na kimaumbile.
Alijikuta akikumbuka mambo mengi sana.

Barua ya Neema ilimpa mshtuko wa hali ya juu Sabrina alipokuwa akiisoma na kumfanya akumbuke jinsi alivyokuwa anamchukia Sam kwa kukataa kufanya nae tendo la ndoa.
Akajikuta akishangaa tu mlolongo wa maisha yake na kumfanya ajifungie ndani siku nzima akifikiria yale yanayoendelea katika maisha yake.
Na kupata jibu la kwanini Jeff yupo kama sehemu ya maisha yake.

Kwenye mida ya saa moja usiku, Jeff alienda tena nyumbani kwakina Sabrina na kumkuta mama Sabrina sebleni ambaye moja kwa moja alimuuliza,
"Na saa hizi umetumwa tena?"
Jeff akaitikia kwa kichwa tu,
"Haya mfate muhusika yupo chumbani kwake"
Jeff akainuka na kuelekea chumbani kwa Sabrina.
Alifika na kufungua mlango kisha kuingia chumbani mule ambapo Sabrina alipomuona Jeff aliinuka na kumkumbatia kisha akamuachia na kuangalia chini kama mtu mwenye aibu, kisha Jeff akamshika Sabrina usoni na kuiinua sura yake halafu akambusu mdomoni.
Kitendo kile cha Jeff kumbusu Sabrina mdomoni kilionwa na mama Sabrina kwani naye alienda chumbani kwa Sabrina.
Kwahiyo akawashtua kwa mshangao na kuwafanya nao  washtuke pia.

Itaendelea

JE HAYA NI MAPENZI!! 102:

Kitendo kile cha Jeff kumbusu Sabrina mdomoni
kilionwa na mama Sabrina kwani naye alienda
chumbani kwa Sabrina.
Kwahiyo akawashtua kwa mshangao na kuwafanya
nao washtuke pia.
Kisha mama Sabrina akauliza,
"Nini kinaendelea?"
Sabrina hakujibu ila naye aliuliza,
"Kwani nini mama?"
Mama Sabrina akatikisa kichwa huku akimuangalia Jeff aliyekuwa kimya kabisa kama hausiki vile na lile swali lililoulizwa.
Kisha kikatawala kimya cha muda mfupi pale ndani kwani hakuna aliyemjibu mwenzie.
Kisha Sabrina akaingizia stori zingine kwa kujifanya kumuuliza Jeff,
"Hivi ulimwambia Sakina kama nimeupata ule mzigo?"
Jeff akaitikia kwa kichwa kumaanisha kukubali kuwa amemwambia,
"Mbona hajaja sasa?"
"Sijui mwenyewe"
Mama Sabrina akatoka na kujua wazi wanajigelesha ingawa hata yeye binafsi anashindwa kuwaelewa kuwa wanamaana gani.

Wakabaki wawili mule chumbani kama ilivyokuwa mwanzoni.
Jeff akamsogelea Sabrina na kumwambia,
"Nisamehe, tatizo langu siwezi kuzuia hisia zangu kwako. Nisamehe tafadhari"
Sabrina hakujibu kitu ila alimsogelea na kumkumbatia kisha akamruhusu kwenda nyumbani.
Jeff hakuongeza neno zaidi ya kumbusu Sabrina kwenye paji la uso kisha kuondoka zake.
Sabrina alikaa na kujiinamia kwani alijiona wazi akimpenda zaidi Jeff sasa tena zaidi ya alivyokuwa akimpenda mwanzo kwani sasa alitamani kuwa nae karibu zaidi.
Alijifikiria sana na muda mwingine kujiuliza kuwa kwanini amepatwa na mawazo ya aina hiyo kwasasa ila jibu ni kuwa ile barua aliyoipata toka kwa Neema kuhusu Sam ndio iliyomshtua.
Akawaza kuwa huenda Sam alikuwa na tatizo alilokuwa nalo yeye zamani,
"Ila mbona Jeff ameweza kulala na mimi bila matatizo? Lazima kuhusu mimi yule mtaalamu alichanganya mada. Na vipi kuhusu Sam, kama idadi ya waliokufa kwaajili yake ni kubwa hivi basi lazima kuna ukweli juu ya hili"
Akawaza na kuwaza ila alijua wazi kuwa maelezo kamili atakuwa nayo Sam tu.

Jeff naye aliporudi kwao, alimkuta mama yake aliyemuuliza
"Ushatoka kwakina Sabrina?"
"Ndio mama"
"Hivi kwanini unanificha Jeff? Kwanini unanificha mama yako?"
"Kukuficha nini mama?"
"Hivi ushawahi kufikiria kuwa mke wa mtu ni sumu?"
"Mke wa mtu ni sumu? Natambua hilo, ila mama nipe tafsiri ya mke wa mtu"
Sakina alimuangalia mwanae na kumuona kuwa anapenda sana masikhara hata kama kitu ni cha kweli ila akaamua kumjibu tu,
"Mke wa mtu ni mwanamke aliyeolewa au anayeishi na mwanaume"
"Nikuulize kitu mama ila usichukie"
"Niulize tu"
"Mtu aliyeolewa akiwa anaishi mwenyewe bila mumewe je huyo ni mke wa mtu?"
"Hivi wewe mtoto wewe una wazimu au? Kwani mtu akiishi mwenyewe ndio nini si alishaolewa tayari"
"Nimekuuliza huku nikichukulia mfano wako. Baba yuko wapi?"
"Mjinga wewe huna akili kama baba yako, nitokee hapa. Ukiongelea wanaume za watu baba yako mtoe kwanza hajielewi. Toka zako hapa umeniudhi sana"
Sakina aliinuka na kwenda chumbani kwake.
Jeff alielewa wazi kuwa amemkera mama yake kwahiyo akajipanga kumuomba msamaha kama akitoka ndani au asubuhi kwani hakuweza kumuita muda huo anaojua wazi amemuudhi.

Sam alikuwa nyumbani kwake huku akijilaumu kwa kitendo chake cha kumaliza hawa wadada,
"Lazima nimwambie ukweli Sabrina, nimwambie ukweli ili moyo wangu upate kuwa huru kwani nimechoshwa na haya matukio kwasasa. Kwanini jamani? Nilishaacha hii tabia zamani ila toka kipindi cha Neema ndio tabia hii ikajirudia kwa kasi sana. Kwakweli sijui la kufanya, nadhani cha muhimu nikae mbali na hawa wasichana"
Alijifikiria sana pia akafikiria kuhusu mazishi ya Neema ambapo hakujua kama wamezika au la na huku akigundua msiba mwingine wa Ritha, kwahiyo hicho kitu kilimuumiza sana na kumfanya akose raha kabisa.
Hata muda huo hakuweza kulala moja kwa moja ila alikunywa kwanza pombe kwa lengo la kupunguza mawazo aliyokuwa nayo.

Dorry akiwa nyumbani kwao pia, ni siku hii akapokea tena ile simu ya maajabu aliyowahi kupokea kipindi cha nyuma ambapo alipigiwa kuhusu matatizo ya Sabrina.
Akasita kidogo kupokea leo ila akaona ni vyema kwa yeye kupokea tu ile simu.
Dorry akapokea na kuanza kuongea,
"Haya leo kuna mapya gani? "
" sina mapya ila nimekupigia kukuaga Dorry, asante kwa kazi uliyonifanyia"
"Ila mbona hujaniambia kuwa wewe ni nani hadi leo? "
" Unataka kufahamu kuwa mimi ni nani? Sipendi nikutishe na wala sitaki unione. Mi niliwahi kuwepo zamani sana kwenye maisha ya ndugu wa Sabrina, nilimpenda huyo ndugu, nilimlinda kwa kila hali na sikupenda kuona akihangamia na ndicho nilichofanya kwa Sabrina huyu. Ila jua kwamba mimi si kiumbe mzuri wala si kiumbe mbaya, kwani kuna wakati nakuwa na roho ya kusaidia ila sitaki kuwa karibu sana na wewe kwa kukuhofia kunizoea sana kisha ulie kwa mazoea yako juu yangu. "
" Kwakweli nakuwa mgumu kukuelewa, kwanini ulinichagua mimi katika kumsaidia Sabrina? Na pia wewe ni nani hadi usionekane? "
" Dorry nimekuchagua wewe sababu imekuwa rahisi sana kukutumia kwa haraka na kuondoka zangu ila mfano ningemchagua Sabrina ingekuwa ni ngumu sana kwa mimi kuondoka katika mwili wake. Sababu kubwa niliwapenda hapo mwanzo ingawa hawakunitaka ila nikawasaidia "
" Na mbona sauti yako mwanzoni ilikuwa ikifanana na sauti ya Jeff? "
" Ninao uwezo wa kuiga sauti ya mtu yeyote nimtake na nilifanya hivyo ili wewe iwe rahisi kunielewa "
" Wewe ni nani lakini? "
" Mimi si kiumbe wa kawaida, usitake kunijua kwa undani zaidi Dorry."
Dorry akashtuka baada ya kusikia kuwa sio kiumbe wa kawaida, ambapo yule mtu aliendelea kuongea
"Na ninauwezo wa kufika hapo ulipo na kukaa karibu yako muda huu. "
Dorry akashtuka zaidi na kujikuta akiachilia ile simu ila muda huo huo akasikia sauti ya mtu akicheka mule chumbani kwake na kumfanya uoga uongezeke ila akasikia sauti ikimwambia,
" Usiogope Dorry siwezi kukudhuru, kwaheri"
Lile neno la kwaheri likajirudia mara kadhaa kama mwangwi kisha kupotea kabisa.
Dorry aliogopa sana na kutoka chumbani kwake, kwakweli ile hali ilimfanya ashindwe kulala mwenyewe siku hiyo.

Kulipokucha, Sam naye aliwaza kwenda kuwapa pole ndugu wa marehemu ila pia akawaza kuzungumza na Sabrina ambaye alijua wazi kuwa kuna haja ya kumwambia ukweli wa mambo yote kuhusu yeye.
"Itabidi tu nifanye hivi, siwezi kuishi na hii siri maisha yangu yote. Lazima nimwambie mtu mmoja nilivyo na mtu huyo si mwingine bali ni Sabrina tu."
Aliyawaza hayo na muda kidogo akapokea simu kutoka namba mpya na kuanza kuongea naye,
"Jana ulipompigia Ritha ni mimi uliyeongea naye, kwa kifupi Ritha amekufa ila kwakweli sikuelewa maneno yako ulisema Ritha asitoe siri kwani akitoa tu atakufa na pia nakumbuka Ritha kuna maneno alikuwa akiniambia na ndio akafa gafla. Kwani wewe ni nani?"
Sam alimsikiliza yule dada na kusikiliza mazungumzo yake ambayo yalitawaliwa na yeye mwenyewe toka mwanzo kisha Sam akamwambia,
"Kama unahitaji kunifahamu njoo unione."
"Nikuone kivipi?"
"Ili utambue kuwa mimi si mtu mbaya kama unavyonifikiria, na pia nimeudhunishwa sana na hizo habari za kifo cha Ritha. Kwani mnazika lini?"
"Tunazika leo, ila kama sio mtu mbaya kwanini ulikuwa ukimtahadharisha Ritha?"
"Nilimtahadharisha kwavile sikutaka afe, sikutaka kumpoteza. Hujui tu ila Ritha ni mtu wa muhimu sana katika maisha yangu. Yani sikutaka kumpoteza kabisa, nimeumizwa sana na kifo chake. Nipe maelekezo ya mahali pa mazishi nije"
Huyu ndugu wa Ritha alimuelekeza Sam bila ya kujua kuwa huyu Sam ndio yule yule mwanaume mbaya aliyeambiwa na nduguye Ritha kabla ya kufa kwake.
Sam alipomaliza kuongea na ile simu akajiandaa kisha kuondoka pale kwake.

Kutokana na ile simu ambayo Dorry aliongea nayo usiku, akaamua kufunga safari ili aende kwakina Sabrina kuwaeleza yote yaliyokuwa yakijitokeza kuhusu yule mtu huku akiamini kuwa huenda ikawa ni msaada kwake kutambua ni kitu gani kilikuwa kikimfatilia katika maisha yake ya kipindi hicho.
Njiani akakutana na Sam kwani huyo Sam alisimamisha gari yake na kumsalimia Dorry,
"Unaenda wapi? Vipi yale matatizo yako yaliisha?"
"Matatizo yangu yamekuwa makubwa kuliko mwanzo, ulinitupa sana na kunisahau. Umefanya nikakosa msaada wala mtu wa kunisapoti kabisa yani"
"Pole sana Dorry, na huyo ndio mwanao?"
"Ndio ni mwanangu"
Sam akacheka na kumuuliza,
"Mbona kafanana na wachina jamani?"
Dorry nae akacheka kwa kujisikitikia,
"Yani wee acha tu haya yangu"
"Haya panda kwenye gari nikupeleke kwanza halafu niendelee na safari zangu"
Dorry akaona ni afadhari kapata lifti na kupanda, Sam naye aliendelea kuzungumza na Dorry kwa kumwambia,
"Unajua unapotaka kumsingizia mwanaume kuhusu mtoto unatakiwa kuwa makini na ujue mwanaume uliyetembea naye mwanzo anafananaje, sio mwanaume mweusi ukamletee mtoto mweupe au mwanaume mweupe ukamletee mtoto mweusi ila afadhari hapo kuna cha kusema kuwa kafanana na mjomba  au shangazi sasa wa kwako kazi ipo uzae na mchina usingizie mswahili"
Sam alikuwa anaongea huku anacheka tu ila yale maneno yalimuingia vilivyo Dorry ingawa nae alitabasamu na kumfanya Sam azidi kuongea,
"Kipindi kijacho kuwa makini, msingizie mtu unayeona angalau anaendana na mwanaume ambaye ni muhusika wa ile mimba ila nyie wanawake mnanichekeshaga sana dah"
Sam leo aliongea anachojisikia hadi pale walipofika kwakina Sabrina na kumuacha Dorry ashuke kisha yeye kuendelea na safari yake.

Dorry aliingia kwakina Sabrina na kuwakuta kisha akasalimiana nao, waliitikia ila walimshangaa kuwa siku hiyo imekuwaje yule Dorry kufika eneo hilo.
"Karibu sana"
Mama wa Sabrina alimkaribisha kisha kuanza kuzungumza mawili matatu, ni hapo ambapo Dorry aliamua kumueleza mama Sabrina jinsi ilivyokuwa toka siku ya kwanza anapigiwa simu na yule mtu wa ajabu na maelezo aliyopewa na yale aliyoambiwa kwa jinsi ya kumuokoa     na kile alichokifanya katika kupigania maisha ya Sabrina.
Pia akamuelezea simu aliyopigiwa usiku na mtu huyo kuhusu yale aliyokuwa akimuelekeza.
"Eeh mbona kazi ipo? Au hicho kitu ndio kilichompata shangazi wa Sabrina kipindi kile?"
"Alipatwa na nini kwani?"
"Ni historia ndefu ila nadhani mkikutana anaweza akakuelezea ilivyokuwa ila hata mimi nitajaribu kumwambia haya. Kwakweli pole sana"
Sabrina nae akatoka na watoto wake pale nje na kumfanya Dorry awatazame na kujisemea moyoni kuwa lazima wale watoto watakuwa wa Jeff tu.
Muda kidogo Jeff naye akafika pale nyumbani kwakina Sabrina kwaajili ya mambo yake binafsi, akashangaa kumuona Dorry pale na hata Dorry naye hakuweza kuhoji zaidi.
Jeff aliwasimulia kisha akavuta kitu na kukaa pale pale nje halafu akamchukua yule mtoto mkubwa wa Sabrina na kukaa naye.
Mama Sabrina alitulia tu akiangalia matukio yote yanayotendwa na Jeff pale huku akingoja atulie na  ajaribu kumuhoji kilichompeleka kwa muda huo.
"Jeff karibu maana sikukukaribisha"
"Asante"
"Saizi huna mzigo?"
"Mzigo? Hapana, nimekuja kusalimia tu"
Jeff alikuwa akicheza cheza pale na mtoto Cherry.

Sam alifika msibani na watu walijaa sana pale kwenye msiba kwani kila mmoja ilionyesha kutokuamini kuwa Ritha amekufa.
Ilikuwa ngumu sana kwa wao kuamini jambo hilo na walionekana kuomboleza sana, na wengine kuzimia haswa wale ndugu wa karibu na Ritha.
Sam aliamua kuwasiliana na yule ndugu wa Ritha ambaye ni kweli alijitokeza kwa Sam ila macho yake yalikuwa mekundu sana na kuonyesha kuwa amelia kupita kiasi.
"Poleni sana dada, taratibu gani zinaendelea hapa?"
"Tunangoja kuaga mwili wa marehemu kisha twende kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele"
Mage aliongea huku akifuta machozi na muda kidogo ikaonekana taratibu za kuaga mwili wa marehemu zimeanza.
Leo Sam aliamua kujipa moyo kwa kwenda kuuaga mwili   wa Ritha ingawa hajawahi kufanya hivi kwa wasichana wote aliowapitia.
Sam alipita kuaga ila alipatwa na mshtuko mkubwa sana kwani maumivu aliyoyasikia moyoni mwake yalikuwa zaidi ya yale alipogundua kuwa amekufa.
Kwakweli Sam kwa maumivu yale hakuweza hata kustahimili kwenda kuzika kwani alirudi kwenye gari yake kisha kuamua kumpigia simu Dorry ili tu ampe lifti ya kumrudisha nyumbani kwao.

Dorry alikuwa akimtazama tu Jeff na yule mtoto kisha kumtazama mtoto aliyebebwa na Sabrina na kuona ufanano uliopo.
Akatamani kuuliza jambo ila akasita, muda kidogo akapigiwa simu na Sam kisha akawaaga pale na kuondoka.
Alimkuta Sam nje akimsubiri ampeleke, kisha akapanda kwenye gari na safari ikaanza,
"Umejifikiria nini kuja kunifata?"
"Aah nimeamua tu"
"Na mbona sasa hivi huna furaha, tofauti na nilivyokuona asubuhi?"
"Maisha tu mdogo wangu"
Sam hakuwa na raha kweli kwani aliona maiti ya Ritha ikijirudia rudia kwenye akili yake.
Alimfikisha Dorry nyumbani kwao na kumuaga, Dorry nae akamshukuru kisha akamwambia
"Nawe uwe makini kama watoto ulionao ni wako kweli"
Sam akatabasamu kwavile alikuwa anaelewa kila kitu na kurudi kwake.

Sam alipofika nyumbani kwake aliingia ndani ila sura ya maiti ya Ritha bado iliendelea kucheza na akili yake hadi kumfanya ajilaumu kuwa kwanini alienda kuaga.
Akakaa akijifikiria hilo, mara gafla akashangaa akinaswa kibao cha shavu na mtu asiyemuona.

Itaendelea

JE HAYA NI MAPENZI!! 103:

Sam alipofika nyumbani kwake aliingia ndani ila
sura ya maiti ya Ritha bado iliendelea kucheza na
akili yake hadi kumfanya ajilaumu kuwa kwanini
alienda kuaga.
Akakaa akijifikiria hilo, mara gafla akashangaa
akinaswa kibao cha shavu na mtu asiyemuona.
Sam alishtuka sana na kujiuliza kuwa ni kitu gani kilichomnasa kofi, wakati akijiuliza alishtuliwa tena na kofi lingine na kumfanya akimbilie nje.
Yule mlinzi wake akamshangaa na kumfata kisha akamuuliza,
"Vipi tena bosi nini tatizo? "
" Kuna maajabu humu ndani leo hata sijui kuna kitu gani jamani "
" Kwani vipi tena? "
Sam akamueleza kwa kifupi tu huyu mlinzi wake kuwa anashangaa kunaswa vibao ndani kwake tena na mtu asiyemuona.
" Mmh bosi hadi nyumba yako ina mambo hayo? "
" Kwani wewe unayajua mambo haya? "
" Hapana ila nadhani ni mambo ya kishirikina bosi maana kwa hali ya kawaida hilo haliwezekani itakuwa ni ushirikina tu. "
" Sasa nifanyeje hapo jamani "
" Samahani kwa ushauri huu bosi ila hapo ni kwenda kwa mtaalamu tu"
"Mtaalamu?? Mtaalamu wa nini sasa? "
Yule mlinzi akajaribu kumueleza kuhusu wataalamu anaosemea yeye kuwa ni wale waganga wa kienyeji na kumfanya Sam amuangalie tu kisha akapanda kwenye gari yake na kuondoka kwani kwake aliona hapafai kwa siku hiyo.

Jeff naye pale nyumbani kwakina Sabrina aliaga na kuondoka zake huku akijiuliza kuwa Dorry alienda kufanya nini kule kwakina Sabrina.
Alirudi kwao na kumuuliza mama yake kama Dorry ameenda na pale,
"Kheee kwani Dorry alikuwa mitaa hii? "
" Ndio me nilimkuta kwakina Sabrina na akaniacha pale, nikajua amekuja huku"
"Mmh huyu mtoto mbaya jamani kweli kabisa kashindwa kuja hata kunisalimia!! "
" Ndio upime hapo kuwa uzuri wa mtu si machoni pekee, moyo wa mtu ndio wenye uzuri. Unamsifiaga Dorry hapa tena bila hata ya kufikiria makosa yake. Kakudanganya kuhusu mimba na kulea yasiyokuhusu mwisho wa siku ukaletewa mtoto wa kichina ila bado ukapata moyo eti tukapime DNA ila mama yangu dah. Bado akakimbia kwa makosa aliyoyafanya ila unaendelea kumbembeleza kuwa awe na mimi. Pole sana mama yangu ila mimi kwakweli siwezi kuwa na yule Dorry namjua vilivyo na alinisimulia mwenyewe kila kitu. Kuna siku makaratasi kayatoa yeye maskini mama wa watu ukajua ni ushirikina, mganga kakulia pesa tu hakuna kitu. Pole mama yangu ila sasa ujifunze "
Sakina alijiinamia chini na kuanza kukumbuka hiyo siku ya makaratasi hadi akajua kuwa ni ushirikina kwakweli kwa swala hilo akajiona mjinga sana.
" Duh kumbe ndio nilichezewa mchezo kiasi hicho, kwakweli huyu mtoto hafai hata kunishtua kuwa ni yeye hakuna. Halafu lile liganga liongo sana limekula pesa yangu tu na Mungu alilaani miaka yote "
Jeff alikuwa akitabasamu tu na malalamiko ya mama yake pia alifurahi kwani ilikuwa ni njia nzuri ya kupatana naye.

Sam alienda baa na kunywa pombe ili akili yake ichangamke kwani aliamini kuwa akilewa itamsaidia kukwepa baadhi ya mambo,
" Wachawi dawa yao kuwamwagia pombe tu, hivi huyo mtu wa kuniroga mimi nae anaanzaje jamani. Nitawashughulikia mmoja mmoja. "
Alikuwa akizungumza mwenyewe huku akinywa pombe, muda kidogo aliwasili rafiki yake ambaye ni mmiliki wa baa ile, kisha kusalimiana pale na maongezi madogo madogo kuendelea,
" Hivi kaka mkeo yuko wapi siku hizi? "
" Yupo tu"
"Mbona siku hizi huji nae? "
Sam akajifikiria kidogo na kujiona akimkumbuka Sabrina kisha akainuka pale alipokuwa anakunywa na kumuaga yule rafiki yake kwani aliona ni vyema aende kuzungumza na Sabrina kuliko kuendelea kunywa pombe zisizo na faida kwake.

Sabrina na mama yake wakiwa wanajiandaa kulala washtushwa na sauti ya hodi, hasa mama wa Sabrina alishtuka sana ukizingatia kwa kipindi hiko pale nyumbani kwao walikuwepo wawili tu yaani baba wa Sabrina hakuwepo kwa kipindi hiko.
Mama wa Sabrina akainuka na kwenda kumgongea Sabrina chumbani kwake, Sabrina akatoka
"Umesikia kuna mtu anagonga nje?"
"Nimesikia, hivi atakuwa nani usiku huu?"
"Hata mimi nashangaa"
"Au baba?"
"Hakusema kama atarudi leo kwakweli, hata sijui atakuwa ni nani"
Wakasita kwenda kumfungulia ila mwisho wa siku mama Sabrina akaona ni vyema kwenda kumfungulia kuliko kumuacha nje.
Alifika getini na kumuulizia,
"Kwani wewe nani?"
"Mimi ni Sam mama"
"Sam usiku huu?"
"Ndio mama"
Mama Sabrina aliporidhishwa na ile sauti ya Sam ndipo alipofungua mlango kisha geti kubwa na kumfanya Sam aingize gari yake ndani, kisha akamkaribisha,
"Ila mbona ni usiku usiku jamani?"
"Matatizo tu mama, halafu  nimeikumbuka familia yangu"
"Khee familia yako umeikumbuka usiku! Sasa utaondoka saa ngapi?"
"Siondoki, nitalala hapa hapa mama"
"Khee utalala hapa hapa kwa misingi ipi?"
Mama Sabrina aliona hapa Sam akimletea mada zisizofaa na kumshangaa tu ingawa alimkaribisha ndani na kumuita Sabrina ambapo Sabrina nae alimshangaa Sam kufika pale kwao kwa muda ule kisha akamuuliza swali lile lile ambalo Sam ameulizwa na mama wa Sabrina.
"Mbona umekuja usiku Sam?"
"Jamani mbona zamani nilikuwa siulizwi hayo maswali? Vipi siku hizi mnaniuliza kama mwizi?"
"Si kwa nia mbaya Sam, kwanza kumbuka hapo zamani tulikuwa tukiishi kifamilia zaidi tofauti na sasa. Wewe fikiria tu kwa jinsi unavyokaa kimya hata wiki hakuna cha mawasiliano wala nini halafu unaibuka usiku gafla kama hivi lazima tuwe na mashaka na wewe"
"Basi msiwe na mashaka na mimi, nimeikumbuka tu familia yangu na ndiomana nimekuja"
"Sasa ndio usiku? Na utaondoka saa ngapi?"
"Sidhani kama ni vyema kunipangia muda wa kuja kuiona familia yangu, Sabrina kumbuka kwamba wewe ni mke wangu. Haijalishi ni mambo gani yametokea kati yetu bado wewe utabaki kuwa mke wangu. Na vile vile nimeamua leo nije nilale hapa, wala sina mpango wa kuondoka leo"
"Khee Sam, utalalaje kwa wakwe zako? Kuna kipindi uliniambia mwenyewe kuwa si jambo jema kwa mtoto wa kiume kulala kwa wakwe sasa vipi leo unataka kulala kwa wakwe zako?"
"Kwani wakwe ni simba au nyoka hadi waogopwe? Kutokulala kwa wakwe ni kujitunzia heshima tu kwa mtoto wa kiume ila inapotokea dharula inabidi tu mtu alale. Wewe ni mtoto wao na mimi ni mumeo kwahiyo mimi ni mtoto wao pia sasa kwanini nishindwe kulala kwa wazazi? Mi nitalala hapa hapa sebleni hata msihangaike"
Sabrina alimuangalia Sam na kumshangaa anavyoongea kiasi kile ila kwavile alimsikia akinuka pombe akajua wazi si akili yake bali ni akili ya pombe ndio inayomtuma kufanya vile.
Sabrina akaona ni vyema amuandalie chumba cha kaka zake na kumuomba akalale chumbani kuliko kulala sebleni.
Sam alikubali na kwenda chumba alichoandaliwa na Sabrina kwa usiku huo.

Sabrina alirudi chumbani kwake huku akisikitikia akili ya pombe ilivyomuendesha Sam huku akihisi kuwa akiamka asubuhi lazima ataona aibu kwa kulala kwa wakwe zake.
Kisha na yeye akalala kwa muda ule.
Usiku wa manane wakati Sabrina akiwa kwenye usingizi mzito, akajiwa na ndoto.
Alijiona yupo mahali na akamuona mtu mbele yake ila yeye na yule mtu walitenganishwa na mstari mweusi kati yake yani yeye alikuwa upande mwingine na yule mtu upande mwingine.
Kisha yule mtu alimgeukia Sabrina na kumfanya Sabrina amshangae kwavile mtu huyo alikuwa ni Neema.
Sabrina akauliza kwa uoga,
"Wewe si umekufa wewe?"
"Ndio nimekufa, kwani tatizo kuja kukusalimia Sabrina? Mimi na wewe tumetenganishwa na kitu kidogo tu, huo  mstari hapo chini"
Sabrina akautazama ule mstari, na kumtazama Neema kwa uoga.
"Basi huo mstari mdogo umetenganisha uhai na mauti, wewe ukivuka huo mstari ni mwisho wako wa kuwa hai na kisha utakuwa mfu kama mimi. Ila mimi nikivuta huo mstari siwezi kuwa hai ila nitakuwa mfu hivi hivi na hiyo ndio tofauti ya mimi na wewe"
Kisha Neema akavuka ule mstari na kumfata Sabrina alipo, na kuendelea kumwambia
"Mwambie Sam, ni mimi niliyemnasa vibao nyumbani kwake. Sijafurahishwa na kile alichokifanya kwangu, kwa wanawake wote waliokufa kipindi hiki kwaajili yake ameweza kuhudhuria mazishi yao. Kwanini kwenye mzishi yangu hakuja? Hiko ndio kimefanya nimnase vibao na hiyo hali itamtesa mpaka pale atakapokuja kuomba msamaha kwenye kaburi langu"
Sabrina alishangaa sana na kuuliza jambo ambalo halikuhusiana kabisa na alichokuwa anazungumza Neema.
"Kheee kumbe wafu wakifa wanaweza kuongea?"
"Sio wafu ila ni viumbe vilivyomo ndani yao ndio vinaweza kuyatenda hayo"
"Kwahiyo wewe ni nani?"
"Mimi ni kiumbe ninayeishi kwenye mwili wa Neema, ila nimesikitishwa na kitendo alichokifanya Sam. Kama na wewe umesikitishwa basi inuka tuvuke wote ule mstari ili uwe kama mimi halafu tumuangalie Sam kama atakuja na kwako"
Sabrina akashikwa mkono na yule mtu hadi karibia na ule mstari ila alipotaka kuvuka akasita, yule Neema akawa anamvuta na kumwambia,
"Njoo Sabrina huku ni kuzuri zaidi"
Ila bado Sabrina akasita, yule Neema akaonekana kama kutaka kumvuta Sabrina ni hapo ambapo Sabrina alishtuka kutoka usingizini huku jasho jingi likimtoka.

Jeff naye akiwa amelala, alijikuta akiongea kwa nguvu na kumshtua mama yake ambaye alienda haraka kumgongea.
Jeff naye akaamka na kwenda kumfungulia mama yake huku akihemea juu juu,
"Vipi mwanangu kwani una matatizo gani?"
"Ndoto mama"
"Ndoto gani maana nimekusikia ukisema kwa nguvu hapana Sabrina hapana usiende. Ni kitu gani Jeff?"
Naye Jeff akashangaa kusikia kwamba hayo maneno alikuwa akiyasema kwa nguvu.
"Kwahiyo mama nilikuwa nasema kwa nguvu kabisa"
"Ndio, sasa unafikiri mimi ningejuaje kwa mawazo yako? Umemuotea vibaya Sabrina au ni nini?"
"Ni kweli, nimeota ndoto mbaya sana na kujikuta nikimzuia Sabrina asiende"
"Kheee sio mamdogo tena ni Sabrina tu inamtosha mmh makubwa haya"
"Mama naona vyema tukaendelee kulala tu, tutazungumza vizuri asubuhi"
Jeff aliona mama yake akitaka kubadilisha mada, hivyo akamuomba kurudi kulala tu.
Jeff alirudi chumbani kwake huku akitafakari ndoto aliyoiota kwani alimuona kamavile Sabrina akitumbukia ziwani tena ziwa lenye kina kirefu.
"Hii ndoto inamaana gani hii? Lazima kesho asubuhi niwahi ili nikamueleze Sabrina"
Alitafakari sana ila na usingizi nao ukakatika kabisa na kumfanya ashindwe kulala tena huku akiangalia tu masaa yanavyoenda kwa kasi na kuikaribisha alfajiri.

Sabrina naye kwa ile ndoto hakuweza kulala tena na kuona kama vile ni mkosi kwa usiku wake.
Alimtazama mtoto wake,
"Anataka nife halafu wanangu niwaache na nani? Hivi inamaana ningevuka ule mstari ndio ningekufa kweli? Mbona mambo ya ajabu haya?"
Sabrina hakuweza kulala tena huku akihofia kurudiwa tena na ile ndoto.
Na kulipokucha alikuwa wa kwanza kutoka ndani ya chumba chake na alifanya hivyo ili kuangalia kama Sam ataondoka asubuhi hiyo basi aweze kufunga milango yao.

Jeff naye aliamka kwao na kujiandaa kisha akatoka, kabla hajafika mlangoni mama yake akamuuliza
"Unaenda wapi?"
"Hivi unajua kama mi ni mkubwa kwasasa mama?"
"Hata kama mkubwa ila kumbuka bado unaishi kwangu, haya asubuhi yote hii unaenda wapi?"
"Naenda kwakina Sabrina"
"Mmh hata kama kusoma sijui ila picha nimeelewa"
"Ndio maneno gani hayo mama?"
"Wee nenda tu, mi sina usemi"
Jeff akaondoka zake.
Sakina akajifikiria sana juu ya mtoto wake.
"Yani aliyemroga mtoto huyu wallahi amekufa kwamaana angekuwa hai angemuonea huruma. Jeff mwanangu ni mzuri, kila msichana anamtamani. Leo hii kweli akatembee na Sabrina? Mmh! Hivi huyu Sabrina nae haoni aibu kutembea na Jeff, mtoto aliyemlea kweli? Kweli binadamu hatuaminiki, nilimuamini sana Sabrina na wala sikufikiria kama ipo siku atatembea na mwanangu. Mmh Sabrina umenishinda jamani."
Sakina alijikuta akisononeka sana dhidi ya Sabrina ambaye alimuweka kama ndugu yake wa karibu.

Sabrina akiwa pale sebleni, muda kidogo akasikia mtu akigonga mlango na kumfanya ainuke na kwenda kumfungulia.
Alikuwa ni Jeff ambaye aliingia pale getini na kumkumbatia Sabrina ila Sabrina alitulia tu kwa kuhofia Sam kutoka ndani, na muda kidogo kweli Sam alitoka na kumuona Jeff akiwa amemkumbatia Sabrina.
Sam aliwaangalia tu, ila Sabrina alipomuona Sam akamtoa Jeff na kumfanya Jeff naye atazame kule aliposimama Sam akiwaangalia.
Jeff akapatwa na wazo la haraka kuwa aondoke ila akili yake ikamwambia kuwa kuondoka ni nidhamu ya uoga ukizingatia Sam ameshajua kila kitu.
Kwahiyo alichokifanya ni kwenda kumsogelea tu Sam na kumueleza kuwa ameota ndoto mbaya kuhusu Sabrina.
Muda huo Sabrina naye alikuwa karibu yao akiwasikiliza ndipo hapo na yeye alipopata ujasiri wa kuelezea ndoto yake mbele yao.
Na kumfanya Jeff ashangae na kuona alikuwa sawa kumuotea Sabrina kuwa yupo kwenye matatizo.
Sam naye aliikubali ndoto ya Sabrina kwani ndio mambo yaliyomtokea jana yake.
Sam akawauliza Jeff na Sabrina,
"Sasa tunafanyaje kuhusu hili?"
Sabrina akajibu,
"Hakuna jinsi, hapa ni wewe kwenda tu huko kaburini kwa Neema kuomba msamaha"
"Basi itabidi mnisindikize jamani"
Hakuna aliyepinga kwavile wote tayari wana makosa dhidi ya Sam.
Basi Sabrina akaenda kujiandaa na kumuachia mama yake watoto kisha wote  watatu kuondoka yani yeye Sabrina, Jeff pamoja na Sam.

Wakiwa kwenye gari Sam alionekana kusikitikia sana maisha yake,
"Tukitoka huko naomba twendeni mahali nikawaeleze siri iliyojificha kwenye maisha yangu. Ila kabla ya yote nakuomba Sabrina wewe ndio uende kuulizia kwakina Neema kaburi lilipo."
Sabrina hakupinga swala hili na ilikuwa rahisi kwa Sabrina kwenda kwakina Neema na kuulizia lilipo kaburi la Neema na ilikuwa rahisi kuelekezwa kwavile baadhi ya ndugu walimuona siku ile hospitali.
Kisha akarudi tena kwenye gari na kuelekea makaburini alipoelekezwa.
Walienda moja kwa moja mpaka kwenye kaburi la Neema.
Wakasimama mbele ya kaburi lile huku Sam akiwa kwenye harakati za kupiga magoti kwa kumuomba msamaha marehemu, mara gafla wakashtuka kumuona Sabrina akianguka chini.

Itaendelea

JE HAYA NI MAPENZI!!  104:

Wakasimama mbele ya kaburi lile huku Sam akiwa
kwenye harakati za kupiga magoti kwa kumuomba
msamaha marehemu, mara gafla wakashtuka
kumuona Sabrina akianguka chini.
Jeff alikuwa wa kwanza kuinama pale alipoanguka Sabrina na kumsaidia kuinuka huku akimpa pole na kumuuliza kuwa tatizo ni nini,
"Kwani vipi Sabrina? "
" Hata sielewi kwakweli, nashangaa tu na mimi"
Sam aliwatazama kwa muda wakati wanainuana kisha akamwambia Jeff kuwa amtoe Sabrina lile eneo la makaburi,
"Tafadhari Jeff, toka eneo hili na Sabrina niacheni mimi kwanza kwa dakika tano nitawafata mlipo. "
Jeff hakupinga kwani aliinuka pale na kuanza kukokotana na Sabrina kwavile alikuwa akichechemea kisha kutoka pale kwenye makaburi na kwenda kusimama mbali kidogo wakimsubiri Sam.

Sam aliamua kupiga magoti pale kwenye kaburi la Neema ili amuombe msamaha, kwavile hiko kitendo kilikuwa ni mara ya kwanza kwake kukitenda kwahiyo ilikuwa anafanya kama kulazimishwa tu kwani hakuwahi kufanya mambo kama hayo kabla.
Alianza kwa kuongea sauti ya kunong'ona ila alikuwa kamavile akizungumza na mtu kwavile alikuwa akitoa maneno ya kuomba msamaha huku akiamini kuwa Neema anamsikia,
"Tafadhari Neema nisamehe, naomba unisamehe sana. Halikuwa kusudio langu mimi kutokuja kwenye mazishi yako. Kwanza nilipatwa na mshtuko mkubwa sana kwa kifo chako kwani mwanzoni niliamini kuwa wewe ni mwanamke pekee uliyeweza kukaa na siri ya maumivu. Nilifarijika kwa wewe kukaa na siri ile huku nikiamini kuwa kuna kipindi nitapata dawa ya kuweza kukusaidia wewe na kukufanya uondokane na yale matatizo. Neema, tambua kwamba haikuwa kusudio langu wewe ufe, sikutaka kukuua Neema na ndiomana nilikuwa nakukwepa. Hata sijui ni shetani gani aliyenipata au aliyetupata hadi kutenda vile. Si kosa langu Neema, sikutaka kukuua. Tafadhari Neema.........!!"
Wakati Sam akiendelea kuongea akashangaa kuona pale mbele ya kaburi la Neema kama video imewashwa.
Kwenye ile video, akajiona yeye na Neema.
Akamuona Neema akichukua dawa na kuweka kwenye chakula ambapo yeye akala kile chakula chenye dawa. Akaona kama akili yake ikichanganyikana.
Kisha akamuona Sabrina akiwa sebleni ameshika simu, mara akamuona kama kateleza na kuanguka chini. Kisha akaona upepo mkali ukimuinua Sabrina pale chini na kisha kumbwaga kwa nguvu ni hapo alipoanza kutokwa na damu mdomoni.
Sam alikuwa akishangaa tu yale matukio aliyokuwa akiyaangalia na kuanza kuunganisha na akili yake.

Sabrina na Jeff walishangaa kuona Sam amekawia kumaliza kule makaburini na kujiuliza kuwa huenda Sam amepatwa na matatizo.
"Mmh mbona kakawia sana?"
"Huwezi jua labda ana mengi ya kuzungumza na marehemu."
"Mmh hapana, twende tukamuangalie bhana Jeff"
"Basi acha niende mie kumuangalia"
"Tunaenda wote"
"Wee Sabrina si ulianguka kule wewe? Unataka twende wote kweli jamani!"
"Ndio tunaenda wote"
Jeff akamsihi pale Sabrina ila hakusikia na kumfanya Jeff aseme kuwa wasiende kabisa,
"Basi tusiende, tuendelee kumsubiria tu."
"Kama hutaki kwenda naenda mwenyewe"
Sabrina akaanza kuongoza kuelekea makaburini na kumfanya Jeff amfate kwa nyuma tu kwani Sabrina alikuwa mbishi haswa.

Walipofika pale kaburini kwa Neema, wote watatu walishtuka kwani ile video iliyokuwa ikionyesha iligeuka kuwa tunguli mbili zilizofungwa vitambaa viwili vyenye rangi nyeusi na nyekundu.
Hiki kitu kiliwashtua sana na Sam alikuwa wa kwanza kukimbia na kuwafanya wao wamfate kwa nyuma.
Sabrina alianguka tena wakati akikimbia na kumfanya Jeff asimame kumsaidia anyanyuke kwanza na aweze kumkongoja kama mwanzo.
 Jeff alimuhurumia sana Sabrina ila alimlaumu kwa ubishi wake na kujikuta akisema,
"Watoto wetu wasirithi tu huu ubishi wako"
Sabrina alimkata jicho Jeff ila aliendelea kukongojana nae hadi wakatoka nje ya lile eneo la makaburi.

Sam alikuwa kwa mbali kabisa akiwbngalia hadi pale walipomfikia.
Sam alisikika akiongea,
"Tupandeni kwenye gari jamani tuondoke yani sijui kama nitathubutu tena kuja makaburini"
Wakaingia kwenye gari ila Sabrina aliamua kumuuliza Sam kuwa kimetokea kitu gani kwani hata wao waliunganisha tu mbio.
"Yani ni mambo ya ajabu, ajabu kabisa sijapata kuona wala kuamini mambo haya jamani. Dah makaburini ndio kuna mambo hivi? Nilikuwa nasikiaga stori tu"
Jeff naye akaongea kwa uelewa wake,
"Ila sio makaburini kote kwenye mambo ya ajabu, huwa inategemea tu marehemu kafa vipi halafu pia kwenye marehemu alikuwa akijihusisha na nini enzi za uhai wake. Mbona makaburi mengine yapo kawaida tu huwa mtu anaweza kupita hata usiku wa manane juu ya kaburi na hakuna ubaya wowote"
"Ila kwa stahili hii mimi hunipitishi tena huko makaburini"
Sabrina nae akachangia,
"Kwani kulikuwa na nini? Mbona mi sijaona chochote!"
"Sasa mbona na wewe ulikimbia?"
"Nilikimbia kwavile niliwaona nyie mkikimbia"
"Mi niliona tunguli, na vile Sam alikimbia na ndiomana na mimi nikakimbia"
"Bora yenu na bora huyo Sabrina ambaye hajaona chochote ila alifata mkumbo tu hadi kaumia. Kuliko mambo niliyoyaona mimi jamani, kwakweli nilistahili kukimbia kwa........."
Sam alijikuta akifunga breki kwa gafla kwani alikuwa akiendesha huku akiongea.
Ila kuna mtu alitokea mbele ya gari yao na kumfanya afunge breki kwa gafla sana.
Wote watatu wakamuangalia yule mtu pale mbele kisha Sam akawaomba washuke kwa pamoja ili wamuulize kuwa yule mtu alikuwa na shida gani na kwanini alisimama barabarani hadi wao kutaka kumgonga.
Wakashuka na kumfata yule mtu ambapo naye alisogea pembeni ya barabara, Sam alikuwa ni mtu wa kwanza kumuuliza kuwa alikuwa na tatizo gani,
"Mbona ulisimama barabarani kwani tatizo ni nini? Hujui kama ni khatari? Ningeweza kukugonga pale"
"Nilijua usingenigonga na hata kama ungegonga basi usingenigonga mimi"
"Wewe ni nani na kwanini ukafanya hivyo?"
"Mimi ni mganga wa kienyeji, kazi hii sijaianza jana wala juzi. Ni kazi ambayo nimeifanya kwa muda mrefu sana toka nikiwa mdogo, katika uganga wangu sijawahi kumfata mteja ila wewe nimekufata"
Sam akashangaa na kuhamaki,
"Kwani na mimi ni mteja wako?"
"Wewe ni mteja wangu ndio, nishatengeneza dawa nyingi kwaajili yako bila ya wewe kujijua."
"Kivipi? Sikuelewi ujue!"
"Nielewe tu, ni hivi kuna mtu alikuwa anakuja kwaajili ya kukutengeneza wewe ni hapo uteja wa mimi na wewe ulipoanza. Mule ndani kwako nimeshaingia mara nyingi sana, na bila kunihitaji tena mimi nakuhakikishia kuwa ile nyumba yako hautaweza kuishi vizuri kwakile ambacho kimo ndani yake."
Sam akawaangalia wakina Sabrina kama wao wanajaribu kumuelewa huyu mganga kwavile yeye alishavurugwa na habari za makaburi akaona ni ngumu kumuelewa.
Sabrina alipoona Sam akiwaangalia sana aliamua kutoa ushauri,
"Sam, twende naye nyumbani kwako basi kwani hakuna jinsi hapa ukizingatia leo tumefata wenyewe haya mambo"
Sam hakupinga kwavile Sabrina ameongea ukizingatia ndiye mwanamke pekee anayemuamini ingawa ameshamsaliti kwa mara kadhaa.
Kisha wakapanda kwenye gari pamoja na yule mganga halafu safari ya kwenda kwa Sam ikaanza, hapo kwenye gari walikuwa kimya kabisa kwani hakuna aliyeweka stori ya aina yoyote ile.

Walipofika nyumbani kwa Sam walishuka na kuingia ndani kwa pamoja huku mlinzi wa Sam akiwakaribisha na kuwaangalia tu.
Waliingia na kwenda kukaa sebleni huku wote wakimsikiliza yule mganga kuwa anataka kufanya nini, ambapo yule mganga alianza kwa kuongea nao,
"Kwanza na huyu mwanamke namfahamu vizuri sana"
Huku akimuonyeshea Sabrina na wote kuwa kimya wakimshangaa kuwa Sabrina amejulikana vipi kwa yule mganga ila Jeff akahisi kuwa huenda vile ambavyo Sabrina alikuwa akipelekwa na mama yake yani Sakina kwa waganga hao. Ila Sabrina naye aliamua kuhoji kuwa yule mganga anamfahamu vipi,
"Kheee na mimi unanifahamu! Umenifahamia wapi?"
"Sio kwamba mmewahi kuonana na mimi la hasha ila mimi nimekuwa nikiwaona katika shughuli zangu za kiganga."
Ilibidi wawe makini na waweze kumsikia kuwa anataka nini kutoka kwao na kipi kilichompeleka kwao, yule mganga aliamua kuwaeleza kwa kifupi,
"Walikuja wabinti wawili wakiwa na lengo moja tu ila mmoja huyu alimsindikiza mwenzie. Waliitwa Rose na Neema, kwenye darubini yangu nilimuona huyu Rose akimshawishi Neema kuwa waje kwangu na kwavile Neema alijawa na tamaa dhidi ya kijana aliyeitwa Sam   aliamua tu kufata ushauri wa rafiki yake kisha wakaja kwangu.
Mi kama mganga huwa hakuna kinachonishinda. Wao walihitaji Sam amsahau mkewe hilo halikuwa gumu kwangu ila tatizo huyu mke hata kama angesahaulika ingekuwa ngumu kukubaliana na hilo hata angeweza kuharibu dawa kwani katika darubini yangu niliona huyu mwanamke akiwa katika ulinzi mzito uliojificha"
Bado walitulia wakimsikiliza ila pale mwanzoni ilikuwa ngumu kumuelewa kuwa amedhamiria kitu gani.
Sabrina aliuliza kwanza,
"Neema unayemzungumzia hapa ni huyu marehemu au ni nani?"
"Ni huyo huyo marehemu hata huyo Rose ni marehemu pia"
Yule mganga akaendelea kuwaeleza kuhusu dawa ambazo aliwapatia na masharti ambayo aliwapa,
"Dawa zilikuwa za kumdhuru mke na kumvuta mume, ipo ambayo iliwekwa chini ya mti pale nje na ipo ambayo iliwekwa ndani baada ya Neema kukubalika kwa Sam kwa njia ya madawa. Ile iliyochimbwa chini ya mti nje ilikuwa na lengo kuwa huyu mke asiweze kufika hapa na kama akiweza basi adhurike. Ile dawa ilitolewa kabla ya kifo cha Neema, ya humu ndani sasa ni kulinda penzi yani mume asiweze kwenda kwa mkewe. Dawa hii itakuwa ikimuangalia kwa kila anachokifanya na inaweza kumpa adhabu iwapo akimkera muhusika ambaye ni Neema na ndicho kilichotokea kwako Sam"
"Bado sijakuelewa kabisa yani"
Sam alimwambia yule mganga kuwa hakuna anachoelewa.

Yule mganga aliamua kwanza kutoa ile dawa aliyowaambia kuwa ipo mule ndani na kufanya wote kubaki midomo wazi, kisha akawaeleza jinsi Sam alivyowekewa dawa kwenye chakula na jinsi dawa aliyomtupia Sabrina ilivyomtesa.
"Kilichonifanya nijionyeshe kwenu ni hii dawa tu ambayo ilikuwepo humu ndani kwani sikuwa na la kufanya na pia hii dawa haikutakiwa nije kuitoa kishirikina. Ilitakiwa nije kama nilivyo na ndiomana nikafanya hivi ila kwa kifupi Sam tambua kwamba haikuwa akili yako wewe kumchukia mkeo na  wala kwa mkeo haikuwa makusudi ya Mungu yeye kuumwa kiasi kile, ni mambo tu ya duniani"
Jeff alielewa ni jinsi gani mama yake anapenda kwenda kwa waganga kwani hiyo ya kutokuaminikuwa kitu fulani ni mipango ya Mungu ndio kilichomfanya awe maarufu kwa kuhudhuria kwa waganga na kudanganywa.
Akajikuta akimuuliza mganga huyu kama anamfahamu mama yake,
"Hivi mama yangu humfahamu kweli?"
"Anaitwa nani?"
"Anaitwa Sakina"
Yule mganga akafunga macho ya dakika kadhaa kisha akaadha kumuelekeza Jeff kuhusu Sakina anayehisi ndiye mama yake,
"Sakina ninayemuona mimi kuwa ndio mama yako yupo hivi, aliachwa na mumewe miaka ya nyuma iliyopita. Historia yake ni kwamba yule mwanaume alitafutiwa kwao na kuolewa nae ila hawajawahi kupendana katika maisha yao. Aliishi na yule mwanaume ila mwanzoni mwanaume huyo alimuheshimu sana mkewe na kuanza kumpenda ingawa ni mwanamke aliyechaguliwa kwao. Ila katika pita pita mwanaume  huyo akapata mwanamke ambapo yule mwanamke alimkorogea madawa ya kumvuta. Kitendo hicho hakikukubaliwa na mama yako, naye akaenda kwao na kumletea madawa mumewe. Huyu mume alikuwa njiapanda kachanganywa na madawa, kuna mdada alikuja kwangu akidai kuwa huyu kijana ni yeye ndiye aliyestahili kuolewa nae, nikamtengenezea dawa. Kwahiyo yule mume aliondoka kimoja kwa mama yenu, na nina uhakika hadi leo hamjamuona wala hamjui alipo"
Jeff alishangaa sana kwani yote yalimlenga mama yake kweli, na sasa akaelewa sababu ya baba yake kutokuonekana tena nyumbani.
"Ila wewe mganga ni mbaya kwakweli, tena ni mbaya sana. Kwanini madawa yako unafanya mtu anaisahau familia yake? Hebu ona huyo baba hata mimi mtoto wake kanisahau kweli? Sijapenda dawa zako jamani. Kwanza mapenzi gani haya ya madawa jamani?"
Akawaangalia kwa zamu Sam na Sabrina kisha akauliza tena,
"Je haya ni mapenzi? Kweli jamani, yani mtu anapenda kwa madawa? Sasa ndio mapenzi gani haya?"
Jeff alionyesha kuchukizwa sana na hii stori aliyoelezewa na huyu mganga kumuhusu mama yake kwani siku zote alijipa matumaini kuwa ipo siku baba yake atarudi ila kumbe kuna mtu kamfunga kwa madawa.
Jeff aliinuka pale na kuanza kuondoka kwani alishaumizwa tayari.

Jeff alitoka nje kabisa na hakuna aliyemzuia kwani hata alipokuwa akitoka ndani yule mganga alipotaka kumzuia, Sam alimwambia amwache tu aende kupumzika.
Jeff alitoka kabisa kwenye eneo la nyumba ya Sam huku akielekea stendi kupanda daladala.
Gafla mbele yake akatokea yule mganga na kumwambia,
"Turudi, bado hatujamalizana mi na wewe"
Jeff akashtuka kwavile alimuacha ndani huyu mganga.
Ni hapa ambapo Jeff aliamua kukimbia ila mbele kidogo alijikwaa na kuanguka.

Itaendelea

JE HAYA NI MAPENZI!! 105:

"Turudi, bado hatujamalizana mi na wewe"
Jeff akashtuka kwavile alimuacha ndani huyu
mganga.
Ni hapa ambapo Jeff aliamua kukimbia ila mbele
kidogo alijikwaa na kuanguka.
Alipoinuka alijikuta mlangoni kwa Sam na kuamua kukimbilia ndani kama ishara ya kukwepa kinachomfata.
Sam na Sabrina wakamshangaa kwa ujio wake wa kuhema wakati aliondoka kwa hasira.
Sabrina alikuwa wa kwanza kuinuka na kumshika Jeff kwani alikuwa kama mtu aliyepandwa na wenge,
"Vipi wewe Jeff, una tatizo gani?"
Jeff akaangaza kote na kuwaona wote yani Sam pamoja na yule mganga wakiwa wamekaa tu wakimuangalia na kumfanya ashangae zaidi kwani yule mganga ndiye aliyemfanya ajikwae na kuanguka.
Sabrina ilibidi amfanye Jeff akae kwenye kiti ili aweze kutulia kwavile aliona hapa swali lake likiwa halijajibiwa.
Yule mganga alikuwa kimya tu na kuwaangalia katika harakati zao za kumtuliza Jeff, kisha walipotulia ni hapo ambapo yule mganga alianza tena kuzungumza,
"Hamtakiwi kunifanyia hasira mimi, wafanyieni hasira binadamu wenzenu wasiopenda maendeleo yenu ila kunifanyia hasira mimi ni sawa na kusumbua miyoyo yenu tu. Tulieni hapa kwanza ili tumalizane kwa amani kabisa"
Sam naye akauliza,
"Kwani kipi kimempata huyu mwenzetu?"
"Akili yake ikitengemaa atawaambia yeye mwenyewe. Ngoja tumalize haya kwanza"
"Haya nakusikiliza, tuambie cha kufanya ili tumalizane nawe."
"Cha kufanya ni hivi, mnatakiwa kunipa gharama zangu za kuweka mambo ya hapa sawa"
"Hilo sio tatizo, kuna lingine?"
Huyu mganga akakaa kimya kwa muda kwanza kwani alijua kuwa hawa watahitaji msaada mwingine kutoka kwake ila hakuna walichomuomba zaidi ya kutaka amalize yale mambo yake aliyoweka kwenye nyumba ile.

Mama Sabrina alishangaa sana kwa Sabrina na hao wakina Sam kukawia kurudi kiasi kile,
"Hivi hawa watu hawa wana akili gani? Hivi hawajui kama kuna watoto wadogo wamewaacha humu ndani jamani?"
Alikuwa na kibarua kizito kwa siku hiyo cha kuwabembeleza wajukuu zake wote wawili.
Muda kidogo akafikiwa na ugeni, mgeni huyo alikuwa ni wifi yake mdogo na kumkaribisha kwani alishamaliza swala la ugomvi wake na yeye.
"Karibu sana"
"Mbona watoto wote umebaki nao mwenyewe?"
"Wee acha tu yani, wajina wako kaondoka hapa asubuhi na mapema akiwa na mumewe ila hajarudi hadi muda huu"
"Kwani ameanza tena kuishi kwa mumewe?"
"Hapana, ila alikuja tu kumsalimia"
"Afadhari maana napatwa na hisia mbaya sana dhidi ya nyumba ya mumewe"
"Hisia zipi hizo?"
Shangazi wa Sabrina hakujibu ila alimchukua yule mtoto mdogo wa Sabrina na kumshika kisha kubadili mada baada ya kumuangalia tu,
"Kheee huyu mtoto kila anavyoendelea kukua ndio anavyozidi kufanana na kale kakijana ka Sakina. Ama kweli dunia haina siri"
Mama wa Sabrina alimuangalia kwa makini na kumuuliza kuwa anamaanisha kitu gani,
"Unajua wifi yangu huwa una maneno ya mafumbo sana wewe, sijawahi kukuelewa kwa haraka kwakweli. Unamaanisha nini?"
"Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye sikio haambiwi sikia. Kusoma hujui hata picha huoni? Siongei mengi siku hizi sababu sitaki kugombana na watu hususani wajina wangu"
Mama Sabrina akatulia kidogo ili kuepusha maneno na yeye.

Sakina nae akiwa nyumbani kwake alijikuta akifikiria kuhusu Sabrina na Jeff,
"Hivi kama kweli huyu Jeff mwanangu anamahusiano kweli na huyo Sabrina hivi mi nitafanyaje jamani? Mbona kinaona kama nazidi kuchanganyikiwa? Ngoja niende leo nikazungumze na Sabrina nipate ukweli wa mambo."
Akatoka pale kwake na kuanza kuelekea kwakina Sabrina.

Yule mganga akaanza tena kuendelea na hoja zake ambapo aliwauliza wakina Sam,
"Vipi hamtahitaji msaada mwingine toka kwangu?"
Huku akimtazama Jeff na kuuliza tena,
"Hata wewe huhitaji msaada wa kuweza kumrudisha baba yako?"
Jeff alimuangalia tu yule mganga bila ya kujibu chochote na kufanya Sam aongee kwa kumsihi yule mganga kuwa amalizane nao tu,
"Mganga tumefurahi kukufahamu, iwapo   kutakuwa na tatizo lolote basi tutakuita tena kwahiyo hakuna tatizo kwa sasa. Tumalizane tu na mambo haya kwanza."
Basi yule mganga akaamua kumwambia kwanza Sam kiasi anachohitaji kwa muda huo ambapo kwa Sam haikuwa tatizo sababu pesa alikuwa nayo ila aliwaomba waondoke wote ili aweze kwenda kumtolea mganga huyo pesa toka kwenye mashine za kutolea hela.
Kwahiyo wakainuka pale na kwenda kupanda kwenye gari ya Sam kisha safari ikaanza hadi pale Sam alipofika kwenye kituo cha kuwekea mafuta na kusimamisha gari kisha yeye kwenda kwenye mashine ya kutolea pesa.
Kwenye gari alibaki yule mganga pamoja na Sabrina na Jeff ambao wao walikuwa wamekaa kiti cha nyuma cha gari lile.
Yule mganga akawaangalia na kusema,
"Halafu ninyi ni wapenzi, halafu hamtaki niwasaidie shauri yenu."
Jeff na Sabrina wakatazamana huku Sabrina akitamani huyu mganga aende zake tu maana aliona anawaharibia mambo yao tu.
Jeff aliiona hasira ya Sabrina kwa yule mganga hivyo akaamua kumshika mkono Sabrina.
Yule mganga aliwaangalia zaidi na kumfanya apate kingine cha kuongea,
"Tena mapenzi yenu ni siri, kumbuka wewe ni mke wa mtu"
Huku akimuangalia Sabrina na kumfanya Sabrina azidi kupatwa na hasira na kumjibu,
"Kama mke wa mtu je!"
Jeff akamziba Sabrina mdomo kwani alijua ataendelea kuropoka zaidi, ni muda huo Sam alirudi kwenye lile gari na kukuta Jeff kamziba mdomo Sabrina,
"Kwani vipi jamani?"
Jeff alimuachia Sabrina ila yule mganga ndiye aliyejibu tena lengo lake likiwa kuwakomesha Sabrina na Jeff,
"Kwani wewe hujui?"
"Kujua nini?"
"Hujui kama mkeo ana mahusiano na huyo kijana!"
Sam hakuongea kitu zaidi ya kuwaangalia tu Sabrina na Jeff ambapo Sabrina aliinamisha kichwa chini.
Sam akatoa pesa na kumkabidhi yule mganga kisha akamwambia,
"Niambie pa kukurudisha sasa"
Yule mganga akamuomba Sam amshushe hapo hapo kwenye kituo cha mafuta.
"Hapana, haitakuwa njema kukuacha hapa. Wee niambie tu pa kukupeleka"
Kisha akamuelekeza, na safari ikaanza huku wakiwa kimya kimya kwenye gari.

Sakina nae alifika kwakina Sabrina na kumkuta mama wa Sabrina na shangazi mtu.
Aliwasalimia na kumuulizia Sabrina,
"Huyo Sabrina hayupo, ameondoka hapa asubuhi na mapema akiwa ameambatana na Sam pamoja na Jeff. Walisema watawahi kurudi ila nashangaa kuwa hawajarudi hadi muda huu, sijui tatizo ni nini kwakweli"
Sakina aliinama kwa dakika kadhaa akimfikiria mwanae kuwa imekuwaje kaondoka na watu hao.
"Kumbe Jeff ile asubuhi alikuja huku kweli!"
"Mwanao hapa imekuwa ni sehemu ya salamu yake ya asubuhi, kila siku lazima apite hapa"
Hoja hiyo ilizidi kumpa maana Sakina na kujikuta akimuuliza mama wa Sabrina,
"Hivi mama, wewe unahisi nini kinaendelea hapo?"
"Kuendelea kivipi? Sijui chochote kwakweli"
Shangazi wa Sabrina akadakia kama kawaida yake,
"Kusoma  hamjui hata picha hamuoni loh!"
Sakina akauliza tena,
"Unamaana gani shangazi?"
"Kaa hapo na umshike huyu mtoto umbembeleze kidogo"
Sakina akakaa kisha shangazi akamkabidhi Sakina yule mtoto mdogo wa Sabrina amshike.

Sam alimfikisha yule mganga mpaka kwenye eneo alilosema kisha akashuka ili awaache waende.
Sam akageuka nyuma sasa na kusema,
"Sabrina, njoo ukae hapa mbele tafadhari"
Sabrina hakupinga, akashuka na kwenda kukaa kwenye kiti cha mbele karibu na Sam huku wakimuacha Jeff siti ya nyuma.
Sam akaondoa ile gari huku akitabasamu ila Jeff na Sabrina walikuwa kimya kabisa.
Walipokuwa njiani, Sam akamuona mtu aliyemfahamu na kumfanya asimamishe gari.
Mtu huyo alikuwa ni Aisha yani yule dada aliyekuwa akiishi na marehemu Neema kabla ya kifo chake.
Sam akaona ni vyema wampe lifti dada huyo,
Akamuuliza kwanza,
"Unaelekea wapi Aisha?"
"Naenda nyumbani"
"Tafadhari naomba panda kwenye gari tukusogeze kidogo"
Kisha Aisha akapanda na kukaa pamoja na Jeff kwenye ile siti ya nyuma.
Kabla Sam hajaondoa gari, akaona ni vyema akiwatambulisha kwanza,
"Aisha, huyu ni mke wangu anaitwa Sabrina"
Kisha akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Huyu anaitwa Aisha, ni mdada aliyekuwa akiishi na Neema kabla ya kifo chake"
"Namkumbuka huyu, nilimuona nyumbani kwa Neema siku mauti ilipomkumba"
Sam akashtuka kidogo kusikia kuwa Sabrina alikuwa nyumbani kwa Neema siku aliyokumbwa na mauti, na kwamaana hiyo Neema alimwambia siri yote Sabrina na ndiomana ikafa.
Ingawa Sam alishtuka ila hakupenda hawa wagundue mshtuko wake, kisha akamtambulisha Jeff kwa Aisha,
"Na huyo ni kijana wetu anaitwa Jeff"
"Mmh kama nimewahi kukuona mahali vile"
Sabrina akategesha sikio lake kwa umakini ili asikie kuwa ni wapi ambapo huyo Aisha alimuona Jeff ila muda huo huo Jeff nae akajibu,
"Itakuwa uliniona siku ile hospitali nilipomfata Sabrina"
Sam akaona jinsi gani mzunguko wa siri yake umezidi kuwa mpana hivyo akaamua waendelee na safari yao sasa kwani utambulisho ulishaisha.
Kisha akamfikisha Aisha eneo lake husika, wakati Aisha anashuka alimpa simu Jeff amuandikie namba yake kwa madai kuwa kuna jambo anataka kumwambia, kisha akaijaribisha pale na kuita halafu yeye akashuka.
Kwakweli kitendo cha Aisha kubadilishana namba na Jeff kilimuumiza sana Sabrina ni hapo alijua kuwa amejawa na wivu wa mapenzi, tena mapenzi ya Jeff ila hakuweza kusema ni jinsi gani ameumizwa kwa kumuhofia Sam atamuonaje.

Safari ya sasa ilikuwa ni kurudi kwakina Sabrina, ni hapa ambapo Sam akaongea kwanza,
"Jamani, niliwaambia kuwa kuna mengi nataka tuzungumze ila kwa yaliyotokea leo nimekosa hata muda wa kuyaongelea. Najua Sabrina unatakiwa kuwahi nyumbani sababu ya mtoto, ngoja tukuwaishe ila tafadhari sana ninachohitaji kuzungumza nanyi ni muhimu sana. Sasa sijui  tufanyaje!"
Jeff akachangia,
"Nadhani ni vyema kama tutazungumza kesho"
Sam akakubaliana na hili wazo kwani aliona kidogo lina mantiki kwavile muda ulikuwa umeenda kweli.
Kwahiyo safari ya kurudi ikaendelea.

Sakina alikuwa katulia kabisa huku kamshika mtoto wa Sabrina ambapo shangazi akamuuliza,
"Umeelewa nini hapo?"
Sakina akatingisha kichwa kuwa hajaelewa chochote,
"Basi ngoja nikubadilishie swali, vipi mtoto unamuonaje?"
"Namuona ni mtoto mzuri na mwenye afya"
"Kafanana na nani?"
Sakina akaguna kwanza kwani jibu ni wazi kuwa mtoto huyo kafanana na Jeff, ila hakutaka kutoa jibu la moja kwa moja kwanza kwani alimtazama mama wa Sabrina ambaye ni bibi wa mtoto na kumuuliza kwa kujishuku,
"Eti mtoto si kafanana na wewe bibi yake?"
Mama wa Sabrina akacheka tu, ni hapo ambapo shangazi akaongea tena,
"Najua wazi mnafahamu ukweli ila mnajaribu kuukwepa ukweli huo. Haya mambo hayanihusu ni juu yenu wenyewe  katika jitihada zenu za kukwepa ukweli."
Sakina na mama Sabrina wakatazamana tena.
Muda kidogo wakina Sabrina nao walikuwa wamerudi.
Wakasalimia pale kisha Sam akaaga kuwa anaondoka, ni hapo ambapo shangazi wa Sabrina nae akaaga ili aweze kupata lifti ya Sam.
Ila Sam kabla ya kuondoka akamuita kwanza Sabrina pembeni na kumwambia,
"Sabrina, ingawa kwa yote yaliyotokea tafadhari niheshimu. Nipe heshima yangu kama mumeo."
Kisha Sam akaondoka huku akiambatana na shangazi wa Sabrina.

Nyumbani walibaki wanne sasa, Sabrina, Sakina, Jeff na mama Sabrina ambapo Jeff nae alijifanya kuaga kuwa anaenda nyumbani.
Sakina nae akaona ni vyema aongozane na mtoto wake.
Kwahiyo wakaondoka.
Ni hapo hata mama Sabrina aliona ni bora atumie muda huo kupumzika kwani kazi ya kubembeleza watoto wawili kwake ilikuwa mtihani tena kwa siku hiyo ukizingatia kuwa walisumbua sana kwahiyo akaona vyema akapumzike tu.

Sam alimpeleka shangazi wa Sabrina hadi anapoishi kisha yeye kuondoka.
Ingawa alifanya mizunguko yote hiyo kwa siku moja ila bado hakuwa na amani ya kurudi nyumbani kwake na kuamua kurudi  tena kwakina Sabrina ili akapumzike huko.

Bado Sabrina aliumizwa na kile kitendo cha Jeff kubadilishana namba na Aisha.
Akaamua kuchukua simu ya mama yake na kuwasiliana na Jeff kwa kumuonya kuwa asiwasiliane na yule dada.
"Tusiongee kwenye simu Sabrina, acha nije huko kwanza"
Muda kidogo Jeff alifika kwakina Sabrina na kumkuta Sabrina pale sebleni.
"Tena naomba uifute hiyo namba sasa hivi"
"Hata jina sijaiandika, usinifikirie vibaya Sabrina tafadhari"
Sabrina akajisikia aibu kidogo kwa wivu aliokuwa nao dhidi ya Jeff ukizingatia kuwa Jeff ni kijana mdogo sana kwake.
Sabrina akasimama na kuangalia pembeni kwa aibu yake.
Jeff naye akasimama na kwenda nyuma ya Sabrina na kumkumbatia na kusahau kuwa wapo sebleni.
Jeff alimkumbatia kwa nguvu sana Sabrina na kufanya roho yake isuuzike.
Wakiwa kwenye staili ile, mlango wa kuingilia sebleni ulifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Sam. Na mbele yao alitokea mama yake Sabrina kutoka chumbani kwake, kwahiyo macho ya mama Sabrina na macho ya Sam yalikutana katika kumshangaa Jeff na Sabrina.

Itaendelea



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa