Leo tunaanza masomo na maombi juu ya mahusiano. Kila kijana au msichana anataka mwenza anayemcha Mungu, mwaminifu, mkweli, mkarimu, anayejali na mwenye upendo wa kweli. Na kwakweli hayo ni mambo muhimu ya kuyatafuta kwa mwenza wa maisha. Sasa cha kujiuliza kwanza ni je wewe unazo hizo sifa zote? Je mtu akitafuta mwenye sifa hizo unaweza kuwa mmoja wapo? Kumbuka Mungu anakupa wa kufanana naye, adamu alipomwangalia hawa aliona wanafanana ndipo hapohapo akapata kibali kwake.
Kabla hujaanza kuzunguka huku na huko kutafuta mchumba mcha Mungu, anza leo kumcha Mungu. Haiwezekani binti au kijana unakesha baa, club na mambo kama hayo halafu Mungu akupe mwenza mchamungu, la Mungu hawezi kumpa mtoto wake anayemcha mtu kama wewe ambaye huendi kanisani, huna maombi binafsi, haufuati neno la Mungu na hauna uhusiano binafsi na Mungu. Kuna mtu alisema binti ukae ndani ya Yesu ili kijana akitaka kukuoa ampate kwanza Yesu ndipo akupate wewe.
Unataka kijana mkarimu, mpole, mwenye upendo wa kweli. Hakikisha hizo sifa unazo kwanza wewe. Jambo la kwanza la kuwa na mahusiano imara ni ku invest kwako kujenga kiroho chako, character na muonekano. Hivyo kabla hujaangalia kushoto na kulia jiangalie kwanza wewe.
No comments:
Post a Comment