HESHIMU MAHUSIANO YAKO. - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, February 6, 2020

HESHIMU MAHUSIANO YAKO.




Habari za jioni wakubwa kwa wadogo?

Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu.

Ni kwamba napenda kuwashauri dada zangu kwamba jifunzeni kuheshimu mahusiano yenu.

karne hii ukipata mmwanaume makini na ambaye anaonesha nia jaribu kumheshimu sana.

kuwa mbali sana na wale matapeli waliokuchezea wakakukimbia na baada ya kuona umempata mwanaume wa kweli, anayejitambua, anayetambua thamani yako unakuta wanaaza kujirudisha tena kwako ili wakuharibie tena.

Jana tukiwa tunapata chakula cha mchana katika Hotel fulani hapa jijini Dar es salaam.

Tulikuwa watatu, mimi, rafiki pamoja na mchumba wake ambaye walitarajia kufunga ndoa mwezi 5 mwaka huu.

Tukiwa tunaendelea kupata msosi, ghafla aliingia jamaa fulani hivi ambaye alipelekea uchumba wa watu kuvunjika.

Baada ya kuingia shemeji yangu aliomba akamsalimie akidai kwamba ni rafiki yake sana.

Rafiki yangu akampa ruhusa bila hiana. Ila cha kusikitisha na kushangza ni lile kumbatio alilopewa yule jamaa.

Hilo kumbatio likadumu kama sekunde 30 hivi bila kujali maumivu ambayo rafiki yangu alikuwa nayo kwa muda huo.

Baada ya hapo, shemeji alirejea mezani. Swali la kwanzalilikuwa ni yule ni nani?

Shemeji akaanza kujikanyaga. Kama utani vile jamaa akamuomba shemeji avue pete yake akitoa sababu kwamba shemeji kamuonesha dharau.

Shemeji akajua utani kumbe rafiki yangu yupo serious na lile jambo. Jamaa ikabidi amvue kwa nguvu. Jambo ambalo lilisababisha taharuki kubwa sana.

Baada ya kuchuku pete yake ilibidi tuondoke kurudi sehemu tuliyokuwa.

Hata hapa nilipo tupo kwenye kikao cha dharura kuweka mambo sawa lakini jamaa kagoma hamtaki tena mchumba wake.

Jifunze kuheshimu mahusiano yako wewe dada unayesoma hili bandiko.

Nimefupisha kwa sababu nimechoka kuandika kila kitu kilichotokea pale Hotelini.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa