ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI : “ mamdogo yule” alisema Eva, huku anaonyesha kidole kwenye upande wakushoto wa safu ya maduka, mimi nakaka tuka tazama kule aliko onyesha Eva, kweli tulimwona mamdogo Irene, anatoka kwenye moja ya duka,(siyo la mpemba) akiwa ameshika boxi la balbu, (taa) hhapo wote tuka mtazama kaka usoni, tukamwona anatabasabamu, kisha tuka mtazama Madogo, ambae akuwaametuona, sababu yeye alishika njia ya kuelekea nyumbani, “asalamu aleikumkum” tulishtuliwa na sauti yakike toka nyuma yetu,wote tuka geuka, na kukutana na Fatma aliekuwa ametazama kaka, huku usowake ukiwa umetawaliwa na tabasamu languvu. …….. endelea………
Ukweli Fatma ni mzuri sana, ata nguo zake alizo vaa usiku huu, licha ya kuwa gauni refu la mauwa mauwa, na kichwa chake kikiwa wazi zikionekana nywele nyeusiii, alafu ndefu, pia nikama alikuwa amejilemba vizuri usoni, akipaka wanja, narangi ya mdomo, huku macho yake makubwa ya duara nikama yalikuwa yanatazzama nusu, yani kama vile anasinzia, na ata macho yake yalipokutana na kaka, tukamwona yule Fatma ana tazama chini kwa aibu, “safi habari yako” alijibu kaka, ambae ukatoriki ulikuwa umemjaa sana, akihisi kuwa akiitikia aleikum salaam, atakuwa ameingia dini ya watu wengine, “nilizania utokuja, nimekaa weee, mpaka nikachoka” alisema Fatma, kwasauti iliyojaa aibu, “kwanini nisije sema Popa alisahau kunipa ujumbe, ndio kanipa jioni hii” alijibu kaka ambae macho yake nikamayalikuwa yanaukagua mwili wa Fatma.
Naam Tukiwa tunasubiri kwa hamu kusikia alicho itiwa kaka, mala tuka mwona Fatma anatazama upande wa madukani, na kushtuka kwanguvu, “mtumeee, kaka huyoooo!” alisema Fatma na sisi tuka tazama upande ule alikokuwa ametazama yeye, hapo wote tuka mwona Mpemba, akiwa anaongozana na vijana wawili, ni wale ambao nilimwona nao mchana, walikuwa wanatembea kwa kasi, kuelekea upande wa nyumbani ambako mamdogo alikuwa ameelekea muda mfupi uliopita, ni wazi kaka alimtambua Mpemba na kushtuka sana, akamtazama Fatma, “yule ni kaka yako?” aliuliza kaka kwa mshangao, “ndiyo ni kaka yangu, asije nikuta ikawa balaa, basi naomba nikuage, nimefurahi kukuona, asante kwa kuitikia wito, ukiniitaji mtume Popa aje niambie” alisema Fatma kisha akaondoka kuelekea kule alikotokea, sizani kama kaka aliweza kusikia maneno ya mwisho ya Fatma, maana tayari alisha geuka na kutazama kule walikokuwa wanaelekea wakina Mpemba, “Popa, jitaidi kuharakisha, tuwai kumwokoa mamdogo” alisema kaka kisha akaanza kuondoka na sisi tukamfwata.
Naam wakina mpemba walikuwa mbele yetu, mita kama hamasini hivi, ma mdogo atukuweza kumwona, na mbaya zaidi manyunyu ya mvua yalianza kuongeza kasi, na kushuka kwa wingi, ambapo dakika kama mbili mbele tuka ona mvua inaanza kushuka kabisa, tena ni mvua nyingi, kaka Denis aliongeza mwendo, na sisi tukaongeza, tena kwa kukimbia.
Tulitembea huku mvua inatunyeshea, mbele yetu wakina Mpemba nao walikuwa wanatembea, kuelekea kule tulikokuwa tuna elekea sisi, nazani wao awakutuona, zaidi waliongeza mwendo, bila shaka walikuwa wana muwai mamamdogo, sababu wakati tuna karibia kufika nyumbani kwa kina Eva, tuliwaona wanaanza kukimbia, wakimkimbilia mama mdogo ambae sasa tulianza kumwona, ni baada ya kuufikia mwanga wa taa za nje, uliokuwa una mulika eneo lote la uwanja wa kina Eva, kasoro kwenye kibaraza ndio kulikuwa na giza, nazani ndiyo ile taa aliyoenda kununua mamamdogo Irene, hapo tulimwona kaka Denis nae akitoka mbio kuwawai wakina Mpemba, na kutuacha sisi tuna mfwata kwambali huku mvua inaendelea kutuchamanda.
Naam niliweza kuona wakina Mpemba wakimfikia mama mdogo, alie kuwa amelowa chapa chapa, kabla ajafikia kibaraza, na kumzunguka, “aya niambie sasa, unanipa unipi?” aliuliza Mpemba, huku mmoja wawale vijana wawili waliokuwa na mpemba akimshika mama mdogo Irene, hapo tulimwona mamdogo akiwa ameduwaha kwa mshtuko, maana akutegemea kutokewa na tukio kama lile, akabakia anaanatetemeka, huku ana anamtazama Mpemba kwa macho ya huruma, “nauliza utanipa mwenyewe, au nikufanyie unyama?” aliuliza Mpemba, ambae yeye pamoja na wenzake awakumwona kaka alie kuwa anawajia mbio mbio, “naomba niache nitakulrudishia vitu vyako vyote” alisema mama mdogo kwa sauti ya uoga, “sina aja ya vitu, mi nataka unipe” alisema mpemba, kisha aka mshika mkono, “twende ufungue mlango, tumalizane” alisema mpemba akimsogeza mama mdogo kwenye kibaraza, kisaidiwa na mmoja wawale vijana, “kwa usalama wenu, mwacheni mala moja” alisema kaka huku anawasogelea mbio mbio, na hapo ndipo wote walipo geuka na kumtazama kaka, nikama walishtuka kasoro, mamdogo ambae nikama aliachia tabasamu la mshangao, “henheee, umejileta mwenyewe, tena wewe ndio ninakuchukia kama nini” alisema mpemba alie kuwa bado amemshika mamdogo, huku yule mwingine akimwachia mamdogo na kusogea kule anakotokea kaka, ambae alikuwa amesimama mbele ya kijana yule mwingine, “dogo kwa usalama wako wewe, bola ujikate (ondoka zako) zako, kabla atuja kuharibu sura yako ya kishtobe (mschana)” alisema mmoja wawale vijana, “naposema kwa usalama wenu namaanisha kwausalama wenu kweli, naomba muondoke” alisema tena kaka, hapo tukawasikia wale vijana wawili pamoja na mpemba wakiangua kicheko cha dharau, “inaonekana dogo, uijuwi habari yetu sasa ngoja tukuonyeshe” alisema yule alie kuwa karibu na kaka, huku ananyoosha mkono wake wakushoto, na kujaribu kumshika ukosi wa shati la kaka Denis, eneo la kifuani.
Hapo sisi ambao tulikuwa tumesha karibia eneo lile, tulimwona kaka, akiudaka mkono wa yule kijana, na kuunyonga, kwa kuuzungusha, kisha akamsukuma kwanguvu, tukamwona yule jamaa akirudi hatua kadhaa nyuma na kujikosa kosa kuteleza kwenye tope, huku anajishika mkono akiugulia maumivu, lakini hilo alikuwa onyo kwa yule mwingine, ambae alihamaki, “unajifanya mbabe siyo?” alisema huku anna mvamia kaka kwa lengo la kutandika ngumi ya mkono wakulia, lakini kwa wepesi ambao kaka amejaliwa, nilimwona akikwepea upande wakushoto kwake, yani kulia kwa yule jamaa, huku akiudaka mkono wa kulia wa yule kijana wa Mpemba, hapo nilitaka kufumba macho sababu, nilisha juwa kinachofwata, maana uwa namwonaga kwenye mazoezi yake pale anapokwepea upande wowote, uwa kina fwata nini, lakini nilisha chelewa kufumba macho, niliweza kumwona kaka akiachia ngumu moja nzito kwenye ubavu wa kulia wa yule kijana, huku akiwa bado ameushika mkono, kisha aka uzungusha ule kono wa kijana, na na kuuleta mgongoni kwake, alafu aka mfyetua miguu yote miwili yule kijana akajibwaga chini, huku ikisikika sauti ya “kha!” ungesema kuna kijiti kikavu kimevunjika, “mama mkono wangu” alilia yule kijana, kwa sauti ambayo iliashilia kuwa alikuwa katika maumivu makali, wakati huo yule wakwanza nae alikuwa anamvamia kaka, hapo nilijikuta nikipiga kelele, “usiende weweeeeee!” maana nilijuwa kinachoenda kumpata, lakini aikusaidia kitu, maana tayari alisha rusha ngumi kuelekea kwa kaka, ambae akujiangaisha kuipangua, kama anavyo fanyaga kwenye mazoezi, nato aliipisha kidogo huku anamwachia yule alie kuwa analia pale chini, yule jamaa akajaa na kupitiliza, hapo kaka ali mtwanga ngumi moja ya shavuni, nusu tumwagikiwe na damu zilizo ruka mdomoni kwa yule jamaa, ambae alipotaka kupiga kelele, tuliweza kuona jino likianguka, toka mdomoni mwake, ile anageuka kwa ghadhab, aka kutana na ngumi nyingi za kifua, kiasi cha kumfanya akate pumzi kwa sekunde kadhaa, kitendo cha kujibwaga chini, ndicho kilicho kuwa msaada kwa yule jamaa, hapo ndipo mvua zanguo zilipo koma
Hapo kaka akamtazama mpemba, ambae bado alikuwa amemsika mkono, ma mdogo Irene, huku akiwa kama smeshikwa na bumbuwazi, “nazani mmesha elewa niliposema kwa usalama wenu” alisema kaka Denis, kwasauti ambayo ilionyesha wazi kujawa na ghazab, “umeambiwa niache wemshenzi” alisema mamdogo, huku ana inua goti la mguu wake, na kugonga sehemu za siri za mpemba, ambae aliachia mkono wa mamdogo Irine na kujishika sehemu zake za siri, na kisha akapandisha tumboni, huku mimi na Eva tunacheka kweli kweli.
Wakati Mpemba ana jishika tumbo, akiugulia maumivu ya kupigwa kengere zake, mamdogo akamwongezea, kofi la usoni, “unang’ang’amia nikupe nikupe nini, unazania mimi ni duka la ushirika?” alisema mama mdogo, huku mpemba akichomoka mbio, kuingia kwenye kichaka ha upande wa kulia, wa nyumba ya kina Eva, ambako ni upande wa madukani, ikionyesha kuwa aliona kazi kuifwata barabara, huku akifuatiwa na wale wenzie walio jizoa zoa chini na kuanza kukimbilia kule alikokimbilia Mpemba, mpaka walipo toweka, tuka waona kaka na mamdogo wanatazamana, kisha wakatabasamuliana, huku ma mdogo anatazama chini kwa aibu, “asante, walitaka kunifanyia vitu vibaya” alisema ma’mdogo kwa sauti iliyo tawaliwa na aibu, huku akitazama chini, kaka Denis, akujibu kitu, zaidi alibakia anacheka cheka, walionyesha wazi kuitaji kupatana upya, ukweli kitendo kile kilini furahisha, sijuwi kwanini, lakini waliniuzi walipo geuka mabubu, walibakia kama mabwege, na wala awakukumbuka kuwa tulikuwa tumelowa chapa chapa.
“Mamdogo nasikia baridi” alisema Eva, na hapo nikama mamdogo na kaka walishtuka na kugundua kuwa tulikuwa tumelowa, hapo mamdogo akatoa funguo na kufungua mlango, nikamwona kaka anajiandaa kuondoka, “Eva mkaribishe mchumba wako akavue nguo zime lowa” alisema mamdogo, huku anacheka cheka, “kwani Pross utaenda kuvaa nguo zakike?” aliuliza kaka, huku mimi nazama ndani, sikusubiri upuuzi wake, “kwani vibaya mtu kuvaa kanga au kitenge cha mpenzi wake?” …….. endelea……… kufwatilia mkasa huu hapa hapa kwa
No comments:
Post a Comment