Nilikuja kushtuka ghafla baada ya gari kupiga breki kali zilizofanya hata watu wengine mle kwenye basi kupiga kelele za hofu na hamaniko.
“Huyu dereva mshenzi nini.Anataka atuue wengine hapa?”.Aliongea mama mmoja mwenye mimba baada ya breki ile.
“Hamna mama.Kuna gari limekuja mbele ya basi letu na kumwomba dereva asimamishe na ndo maana imekuwa ghafla hivi”.Aliongea jamaa mmoja ambaye alikuwa amekaa dirishani.
Hadi hapo mimi nilihisi kama nataka kufa,lakini haikuwa hivyo.Nikatamani labda niwe ndotoni hivi,kisha nikafumba macho ili nione kama itakuwa ndoto.
Lakini nilipofumbua,nilisikia yule jamaa anasema kuna majamaa watatu pamoja na Mchungaji wameshuka na wanaongea na dereva.
Hapo sasa ndipo nilitaka hata kujitupa nje kupitia dirishani kisha nikimbie kwa nguvu zangu zote hadi sehemu ilipo salama.Lakini nilipoangalia nje,dah! Sijui hata tulikuwa wapi maana kulikuwa ni pori tupu.
Dakika kadhaa baadaye,niliona hao majamaa watatu wameingia mle ndani huku wamekamata picha mkononi.
Walipotua macho yao kwangu tu! Wala walikuwa hawana haja ya kuendelea hadi siti ya mwisho. Wakaja kwangu na kuniamuru ninyanyuke,nami nikatii. Wakataka nitoe na mizigo yangu yote.
Bila zengwe nikatii huku sasa lile tumbo la haja kubwa,likirudi katika hali ile ya mwanzo..
Baada ya kushusha mizigo yangu,waliniongoza moja kwa moja hadi kwenye Pajero waliyokuja nayo.Mizigo wakaitupia kwa nyuma,ma mimi wakaniweka kati huku Baba Sheila akiwa upande ule mwingine usawa wa dereva.
Safari ya kwenda nisipo-pajua ikaanza.
**********
ENJOY.
Hakuna aliyemsemesha mwenzake hadi pale tulipofika.
Kulikuwa kama ni kambi hivi ya jeshi au tuseme labda ya wakimbizi,au sijui niseme vipi.Kwani wapo waliokuwa wamekaa na wapo ambao walikuwa wanalinda usalama.
Baada ya kuingia pale ndani.Nikatolewa nje ya gari na moja kwa moja nikaanza kupelekwa kwenye jengo moja ambalo sifahamu hadi leo lipo wapi na ni la nani.
Baba Sheila akiwa mbele,mimi na wale jamaa watatu tukiwa nyuma,tuliingia ndani ya jengo lile ambalo lilikuwa kama meli ya kivita hivi au nyambizi,zile meli za kivita zinazozamia kwenye bahari.
“Kijana umeingia sehemu mbaya sana.Heri ungeendelea na yule mwingine.Yule hata ungempa UKIMWI,kwangu si kitu.Alishanitoka moyoni.Ila huyu,aisee sikuachi”.Aliongea Baba Sheila baada ya kuingia chumba kimoja kilichokuwa na mitambo mingi-mingi,sijui hata ya nini.
Baada ya kuongea hayo,nilishtukia nguo zangu hasa tisheti ikivutwa kwa hasira na kuchanwa na wale jamaa.Kisha wakaja kwenye jinzi langu nalo wakalivua kwa hasira.Nikabaki na kikaptula cha maua maua na singlend,ambavyo navyo vikanyofolewa pamoja na boxer langu la Man United.
Mzee aliwaoneshea ishara wale jamaa kwa kidole.Na wao wakatii kwa kunipeleka sehemu moja ambayo ilikuwa kama ina senyenge.Wakanifunga pingu hapo kwa kunining’iniza huku mgongo wangu ukigusa zile senyenge.Baada ya hapo,wakaamuriwa waondoke wale jamaa.
Vya watu shida nyie.Mateso niliyopokea pale,nilisema nikitoka mzima,MUNGU atakuwa ngome yangu daima.Niliapa kuwa nitamrudia MUNGU na kuwa mfuasi wake.
Ile senyenge iliungwa kwenye umeme.Yaani pale wale jamaa walivyotoka,Baba Sheila alikuwa anabofya sehemu moja na kufungua kidude flani hivi kimeandikwa namba.Nadhani ni mita ya kupimia umeme.
Alipofungua kile kidude alisababisha zile senyenge kunipiga shoti mgongoni. Pale nilipolia,yeye alisema hata mwanangu atalia vivyo hivyo wakati anajifungua toto lako. Hapo alizidisha nguvu ya umeme na kuwa juu zaidi ya mara ya kwanza.
Kama haja kubwa na ndogo,zote zilitoka pale.Kilichofuata ni mimi kufumba macho nikigugumia kwa maumivu jambo lililiosababisha nipoteze fahamu.
************
Naweza kusema, kupoteza fahamu ilikuwa pona yangu kwenye ule umeme.Lakini haikuwa pona ya mateso yangu.
Baridi isiyo kifani,ilikuwa imenishika hadi nikazinduka.Nilipoangalia,nilikuwa nipo sehemu moja kama swimming pool,lakini ndani yake kulikuwa na maji ya baridi hadi yanatoa mvuke.
Na kila baada ya dakika kumi,wanaweka barafu karibu ndoo sita za rita ishirini.Niliambiwa nitakesha humo kwenye baridi kama Sheila atakavyokesha na mimba yangu mtaani usiku na mchana akitafuta pa kujihifadhi.
Maswali mengi mengi nikajiuliza juu ya maneno yale.Kwanza nilijiuliza kwa nini Mzee yule alisema nitakesha kama Sheila atakavyokesha na mimba yangu mtaani.Ina maana Sheila katoroka kwao au huyu mzee kamfukuza aende huko mtaani.
Nilibaki na maswali hayo ambayo sikupata jibu lolote hadi leo.
Kama kupiga kelele za kuomba wanisamehe,nilizipiga sana.Na kama kulia nililia sana ili wanitoe mle kwenye swimming pool la mateso ya baridi.
Mwisho wa siku pumzi ilinikwisha baada ya muda mrefu wa mimi kukaa mle kwenye mibarafu.Miguu ikashindwa hata kusogea.Midomo ikabaki wazi na mikono nayo,ikakakamaa. Hapo napo niliona kama kuzimu kunaniita.
Wakanitoa kabla sijapoteza fahamu.Wakati huo ilikuwa mida ya saa mbili za usiku.
Nikapelekwa kwenye chumba kimoja ambacho mwanzoni nilihisi faraja kuingia mle.Kilikuwa kina joto balaa,lakini kwa kuwa nilikuwa nimeshikwa na baridi,niliona afadhari kuwemo mle.
Nusu saa mbele,nilianza kuona kero la joto lile.Na nilizidi kuona kero baada ya ubaridi ule kunitoka mwilini kabisa.Sasa jasho likavaa ngozi yangu,na kama kuwiva,sasa nilikuwa na wiva haswaa. Hapo spika za chumba kile nilisikia zikisema,eti navyojisikia joto lile, ndivyo na Sheila atakavyojisikia wakati jua litakapokuwa linamuishia mwilini kutafuta chakula.
Mateso yalizidi kiwango,na kama kunyooka,nilinyooka sana kwa muda ule mchache.Nikazimia tena kamanda.
**********
Nilipozinduka ilikuwa ni asubuhi katika chumba kimoja kidogo sana.Ilikuwa ni faraja kwani hakikuwa na mateso kama ya jana yake.
Lakini baadae,walikuja jamaa wengine wawili na kuanza kunibana mbavu na zaidi waliporidhika na zoezi lile,wakachukua virungu fulani vya chuma na kuanza kunigonga kwenye ugoko na kwenye vile vinundu ambavyo ndivyo viungio vya miguu yangu .Hapo nilikuwa si mtu tena,bali mfu.Yale maumivu,kamwe siwezi kuyasahau na siyafananishi na maumivu yeyote katika maisha haya.
**********
Wiki nzima nilikaa nateswa pale,mateso ya kila aina,hadi kugalagazwa kwenye siafu. Na saa nyingine baada ya mateso wanakuletea mwanamke wanakwambia mpe mimba huyo,ukishindwa hata kusimamisha kichapo kinaendelea.Sikuweza zoezi lao hata moja,hivyo mateso kwangu yakawa ni kama chakula tu!.
Mwisho kabisa Mzee yule alisema anataka nisikie maumivu kama ambayo atayasikia mwanaye wakati anajifungua.Hapo alisema anataka amkate P wangu.
Daah! Kama kuomba msamaha ingekuwa ajira,mimi ningekuwa nalipwa mshahara mkubwa sana.
Niliomba msamaha hadi ulimi ukakosa mate nikabaki kukaa na kusubiri wafanye watakacho kwani nilikuwa sina uwezo wakukurupuka na kupambana nao.
“Sasa chagua moja.Tuchome haya mavyeti yako ya elimu uliyotafuta miaka sijui kumi na mbili au tukate huyo anayekupa kiburi”.Baba Shei aliniuliza.
Kwa wakati ule,vyeti vilikuwa si kitu.Ila hii kitu bwana muhimu.Niliwaomba wachome tu!Na bila kusita mbele ya macho yangu,nilishuhudia vyeti vikichomwa moto.
Mwisho kabisa,waliniminya sehemu ya shingoni ambayo ina mshipa mkubwa wa damu.Hapo nikapoteza fahamu.
*********
Nilipozinduka nilikuwa Morogoro tena nyumbani huku kaka yangu yule wa Arusha ikisemekana ndiye aliyenileta lakini aliondoka na kuacha ujumbe ulionipa pole lakini ukinitaka nisiwasiliane naye tena,yaani alikuwa kachukia.
Ni wiki moja lakini kwangu ilikuwa kama miaka.Sikuamini kama nimetoka salama.Nilimshukuru MUNGU japo ndugu yangu aliamua kunitenga.Najua ilikuwa ni hasira tu! Na mimi nimemsamehe kama alivyonisamehe.
Pale nyumbani,Stela na shangazi yake walikuwepo lakini Maimuna hakuwepo. Nilipomuulizia,walisema aliondoka baada ya kujigundua ana mimba,na mhusika nilikuwa ni mimi.Hawakusita kusema kuwa natafutwa sana baba yake.Hapo nikazidi pia kupagawa.
Mwezi ukakata na hali yangu ikatengamaa tayari kwa pirikapirika za maisha.
Hakuna aliyenijali kama hapo mwanzo.Kitendo nilichokionesha kwa kaka yangu kule Arusha,wengi kiliwagadhabisha hasa baada ya Mzee yule kumfukuza kaka nyumbani. Nashukuru kuwa mzee yule hakumdhuru kaka.Hiyo ni sababu kaka naye alikuwa ni mtu wa usalama kama mzee yule,fununu hizo nilizipata kwa baba yetu.
Huyo Stela alikuwa kabadilika sana.Tabia za umalaya ndo zikawa zake.Shangazi yake alisema kamshindwa. Mbaya zaidi akawa ananitaka kimapenzi na wakati mwenzake sina hamu tena na hiyo kitu.
**********
Nilitoka pale Morogoro na moja kwa moja nikaenda Kondoa kwa Maimuna kwa kutumia ramani niliyopewa na Shangazi wa Stella.
Nilipofika nilipiga magoti na kuomba msamaha kwa wazazi wa Maimuna huku nikiahidi matunzo na kumchukua Maimuna baada ya mambo yangu kukaa vizuri.
Mimba yake ilikuwa tayari kubwa na kwa kuwa baba nilikuwa mimi,hawakuwa na kipingamizi.Msamaha ukapita.
Baadae niliamua kusomea udereva.Nilipomaliza nikatafuta reseni ambayo ilinifanya niajiriwe kwenye kampuni moja ya usafirishaji ambayo hadi leo nipo huko.
Mambo yalipokaa vizuri,nilimchukua Maimuna na kuanza kuishi naye tukiwa na mtoto wetu mmoja.Lakini baadaye tuliongezewa mwingine na Sheila ambaye alimbwaga mtoto yule siku moja asubuhi sana.Aliacha ujumbe tu! Wa karatasi kuwa yeye ndiye kamleta mtoto yule.
********
Maisha yakawa hivyo. Miaka sasa imepita tangu mkasa huu utokee. Sasa hivi nina watoto watatu,lakini ile tabia,imenitokea puani.
Sasa nimeokoka,na maisha yangu nimemkabidhi MUNGU.Namshukuru Mai,japo alikuwa Muislam lakini alikubali kufunga ndoa ya bomani ambayo ndio hadi sasa inadumu.
Naamini mmejifunza mengi katika kuridhishana kimapenzi,kujikinga na magonjwa,kuwaheshimu wale wanaojiuza na kuwaona kama hawakupenda kuwa vile.Pia nadhani umejifunza kuwa cha mtu mavi na siku za mwizi ni 40.Mateso niliyoyapata,siwezi kuyasahau.
Chungeni sana vijana.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment