CHOMBEZO: MPANGAJI Episode: 21 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, February 15, 2020

CHOMBEZO: MPANGAJI Episode: 21



“Okey.Nitafanya hivyo”.Nilimjibu na kuingia ndani na kumwacha yeye amesimama pale gizani.

Usiku huohuo nikiwa napanga nguo zangu ili kesho asubuhi na mapema niondoke,ndipo simu yangu ikaita.Nilipoangalia,alikuwa ni Gasper.
“Niambie Master P.Mtoto wa Vitoto”.Alianza Gasper kwa furaha.
“Dah! Huku mambo mwamala kaka”.Nilimjibu nikimaanisha mambo yameharibika.

“Kivipi kaka”.Naye aliniuliza.
Huku nikiwa naongea kwa sauti ya chini,nikamjibu.
“Eee bwana Shei ana mimba, kaka”
“Acha bwana,ya nani?”.Naye aliniuliza.
“Yangu kaka”.Nikamjibu.
“Hapo sasa kaka.Halafu nina taarifa mbaya zaidi kwako kuhusu kazi ya baba yake”.Naye akazidi kunipa mshawasha.
“Eheee,embu niambie”.
“Baba yake FBI”.Aliniambia.
“Una maana gani?”.Niliuliza.
“Baba ya Jasusi kaka.Jitu la CIA lile”.Alizidi kunipa hamasa Gasper ya kutaka kujua maana ya maneno yake.

FBI ni shirika la kipelelezi la Marekani huku CIA ni shirika la Kijasusi la Marekani pia.

Mashirika haya yanafanya kazi aina moja lakini katika majukumu tofauti.Kazi zikiwashinda FBI zinaenda kwa CIA,na kazi zikishindwa na CIA,zinapelekwa FBI.Sasa naambiwa kuwa baba wa Shei ni Jasus sijui FBI,halafu nimempa mimba mtoto wake.

“Bado sijakuelewa Gasper.FBI si huko Marekani kaka?”.Bado nilitaka kupata ufafanuzi halisi wa maneno yale.

“Kazi ya FBI si waijua?Au CIA si wajua kazi zao hawa?”.Aliniuliza Gasper.

“Ndio kaka.Hao ni wapelelezi”.Nikamjibu huku nikiwa na bonge la mtetemo.

“Basi na huyo dingi ni mpelelezi.Yupo usalama wa taifa huyo mzee wa hapa Tanzania.Hapo kanisani ni kujivalisha ngozi ya kondoo tu! Ili tusishtukie ishu.Ila ukweli dingi ni FBI”.Aliongea Gasper na nilijihisi mkojo kutoka baada ya kujua baba wa Sheila yupo usalama wa taifa.

“Kaka…..Kaka……Kaka mbona kimya?”.Sauti ya Gasper ilisikika lakini nilishindwa kuipa jibu na niliamua kukata simu tu!.

Baada ya kuikata ,nikaanza kupanga nguo zangu haraka haraka na kuweka vyeti na vitu vyangu muhimu mahala pake. Kisha nikakaa kitandani na kuvuta pumzi ndefu huku nikiomba kesho ifike haraka niondoke bila familia ile kuniona.

Baada ya mawazo na kusali sana,sala ambazo sijui zilikuwa zinaenda kwa nani,lakini nilikuwa naomba hadi mizimu ya mabibi inisaidie.Nilipitiwa na usingizi mzito ambao mwisho wake ulikuwa ni kesho yake saa kumi na moja asubuhi.

Ni kaka ndiye aliyekuja kuniamsha na kunitaka nijiandae haraka kwani gari linaondoka saa kumi na mbili,saa moja kuanzia pale nilipoamka.

Nilinyanyuka na kwenda bafuni ambapo sikutumia muda mwingi sana.Na hadi dakika kumi na tano zinaisha tayari nilikuwa mezani napata kifungua kinywa kwa mwendo wa haraka.

Baadae nilisikia kaka akigonga mlango wa baba mwenye nyumba. Dakika kama moja,tayari mlango ule ulifunguliwa na mzee yule alikuwa uso kwa uso na kaka.

Baada ya salamu,niliitwa na mimi ili niage kabla sijaondoka.

Mwili ulikuwa tayari ushaanza kulowa kwa jasho licha ya baridi kali iliyokuwa inapiga asubuhi ile.Macho ya mzee yule yalivyokuwa yananiangalia,waweza sema huyu mzee anataka kukurukia ili akutafune mzima mzima. Nilikuwa nimekaa kwenye kochi moja kumwelekea yeye,hivyo uso wake niliuona moja kwa moja.

“Kwa hiyo kijana unaondoka?”.Aliniuliza swali hilo mzee yule baada ya kuniona nimekaa sawia kwenye kochi mojawapo la mle ndani.

“Ndiyo mzee,nadhani MUNGU akipenda tutaonana”.Nilimjibu kiuhakika huku nikiwaza itakuwaje kama tayari kishajua kuwa mimi ndiye mtuhumiwa anayenitafuta kwa muda sasa.

“Okey.Basi vizuri.Nashukuru sana kwa yote tangu ulipokuja hapa.Na kama una cha kuongezea,huu ndio muda wake.Usiogope”.Mzee aliniambia maneno ambayo yalinifanya nikae njia panda nikijiuliza yana maana gani?.Ina maana mzee anajua ila anategea mimi nimwambie kuwa nimempa bend Shei?Au anataka kunitega ili nijitaje kuwa nimempa kitu mwanae.
Maswali hayo nilijiuliza haraka sana kichwani mwangu,na jibu nililolipata ni kwamba huyu mzee ananitega tu! Ili nijitaje.Sasa kaumia,sijitaji wala nini.

“Hapana mzee,sina chochote zaidi ya kukuomba uniagie kwa wengine”.Nilimwambia hivyo na kumfanya atabasamu kwa tabasamu la upande mmoja.Kisha akafungua kinywa chake.

“Mimi siwezi kukuagia bwana.Ngoja niwaite uagane nao”.Alisema mzee yule na kutaka kuwaita wanawe ili waniage.Lakini kwa kuwa kaka alikuwepo na anaenda na muda,alisimamisha zoezi hilo na kumwambia mzee yule kuwa tunachelewa.

“Okey.Kama mnawahi,sawa.Ila ningependa huyu awaage hawa watoto”.Mzee yule bado alikuwa anasisitiza ombi lake.Lakini hadi muda ule tunaongea,tayari zilibaki dakika ishirini za mimi kuripoti kituoni kwa ajili ya kurudi zangu Morogoro.

Hatimaye nikabeba mizigo yangu kwa ajili ya kwenda kituo kikubwa cha mabasi pale Arusha.Kaka akiwa kwenye usukani na asiye na wasiwasi juu yangu,alikuwa anacheka sana jinsi mzee yule alivyokuwa anang’ang’ania niwaage watoto wake.

“Tuambiane dogo.Ndiyo baba mkwe nini?Maaana alivyokung’ang’ania,dah!Kama ruba vile”.Kaka alikuwa anaongea huku akifuta machozi kwa sababu ya kucheka.

Mimi nilikuwa na mashaka sana,na hata cheko yangu niliyoitoa ilikuwa na woga mwingi ndani yake.

“Hamna.Si wajua hawa wazee walivyowaswahili”.Nilimjibu kaka ila moyoni nilitamani sana nimwambie nini kinachoendelea.Sema sasa nilihisi ataniona wa ajabu na atakasirika sana kwa kitendo nilichokifanya kwa Sheila.Mtoto ambaye Mzee Donyo alimuona kama mkombozi wa familia ile hapo baadaye kwani dada mtu,tayari alishakubuhu kwa wanaume.

“Dogo sema bwana.Sisi ni kaka zako”.Kaka alizidi kunisisitiza lakini kwa utani mwingi hadi nikaona ni bora nifunguke tu!.Liwalo na liwe.

“Bro,pale bwana kuna matatizo makubwa tu!Ndo maana unaona mzee kanikazia niwaage wale watoto”.Nilianza hivyo kumwambia kaka huku bado macho yake yakiwa barabarani kuelekea kituo cha mabasi.

“Matatizo gani dogo tena”.Kaka aliniuliza.

“Ni Sheila”.Nikamjibu kifupi tu!.

“Sheila kafanyaje sasa,mbona hauwi spesific?”

“Sheila ana mimba yangu bro”.Nikamjibu na kugeukia dirishani ili nisione sura yake itakavyobadilika.

Kinyume na mategemeo,alionekana hata hajashtuka na zaidi alicheka sana.

“Nilijua tu!Utakuwa wewe.Ila nikawa nakusubiri nione na mimi kama utanificha,ha ha ha haaa.Dogo una kazi sana”.Alicheka kaka na kuniambia maneno hayo ambayo kwangu yalizaa mawazo mengine.

“Sasa na kazi gani Bro?”.Ilibidi nimuulize.

“Wewe unadhani unaweza kula vya watu na kuondoka mjini hivi hivi?”.Kaka aliniambia kwa mafumbo.

“Sijakuelewa kaka una maana gani”.

“Ukiondoka hapa Arusha bila tatizo,kweli mizimu yako itakuwa mikali sana.Niamini nachokwambia”.Kaka alinijibu na kuzidi kusababisha mimi tumbo la kinyesi kunibana hasa nikifikiria kazi ya mzee yule.

Nilipumua pumzi ndefu na kukaa kimya kwa mawazo ambayo sidhani kama alikuwepo wa kuyawazua muda ule.

“Tatizo lako wewe dogo hujali kitu hata kidogo.Hukuona shida kuwachanganya wale mabinti wote na mbaya zaidi kwako dhana ikawa shida kuitumia kwa huyu mtoto tegemezi wa Mzee Donyo.Sasa mimi sitaingilia masuala yenu,na ni bora palepale ungejitaja tu ili yaishe”.Kaka alizidi kunipa mawazo na kunifanya sasa kile kinyesi kugonga hodi kwenye boxer langu.

“Halafu wewe isitoshe ni mjinga sana tena sana.Mimi pale naheshimiana sana na yule mzee,ila kwa kuwa kwako ujana na maji ya moto,basi ukaamua kuwamwagia wengine.Sasa uaminifu kati ya mimi na mzee yule,hamna tena.Unadhani mimi kwa sasa nitahamia wapi?

Sijapanga kabisa kuhama muda huu.Embu fikiria dogo,kwa nini umenifanyia hivyo?”.Kaka sasa alibadilika na kuonesha wazi kuwa naye kachukia sana kitendo changu.Hakuishia hapo,akaendelea.

“Nyumba yangu ukaifanya nyumba ya ngono.Kitoto kidogo,miaka kumi na tisa.Kisheila,kinaingia ndani na kufanya unyambilisi na wewe.Eti mnajidai mmeoana wenyewe.Sasa kazi ni kwako.Mimi siingilii nakwambia”.Hadi kaka anamaliza kuongea hayo,mimi nilishalowa jasho kama nimtoka mazoezini.

“Na ninavyomjua mzee yule.Nadhani ukitoka hapo utakuwa umejifunza na umebadilika”.Kaka aliniambia hayo wakati gari linaingia pale kituoni.

Baada ya kuhakikisha nimepanda kwenye gari la wasafiri wa kwenda Morogoro,aliniaaga na kuniambia nisali sana.

***********

Baada ya dakika tano,gari lile lilianza kupiga honi likiashiria kuwa muda wake wa kuondoka umewadia.Mimi nilifumba macho na kumshukuru MUNGU kwani safari ilikuwa imeshaanza.

Tukatoka getini,na kuingia kwenye barabara tayari kwa safari ya kwenda Morogoro.

Amani ikanitawala kiasi chake baada kuona saa zima tunasafiri bila misukosuko.Usingizi ukanipitia kamanda na kuona kuwa tayari nimemaliza kazi.
************

Nilikuja kushtuka ghafla baada ya gari kupiga breki kali zilizofanya hata watu wengine mle kwenye basi kupiga kelele za hofu na hamaniko.

“Huyu dereva mshenzi nini.Anataka atuue wengine hapa?”.Aliongea mama mmoja mwenye mimba baada ya breki ile.

****Usikose Episode ya 22...



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa