Ni ndoto ya kila mtu anapoingia kwenye ndoa au mahusiano kuwa na furaha. Sijawahi kukutana na mtu ambaye anasema lengo lake la kuolewa au kuoa ni kuteseka. Lakini ni watu wachache sana ambao wapo kwenye ndoa au mahusiano ambao wanafuraha. Wengi huishi kwa huzuni katika wakati flani wa maisha yao ya mahusiano.
Kuna sababu nyingi kwanini wewe kwenye mahusiano yako huna furaha na mtu pekee wakubadilisha hali hiyo ni wewe mwenyewe. Kwa kutambua wingi wa watu ambao hawana furaha katika mahusiano yao basi leo mpenzwa wangu katika mahusiano nimekuandalia tabia 16 za watu ambao wana furaha katika mahusiano yao. Lakini kabla ya kuendelea nikukumbushe kitu kimoja;
“Furaha katika mahusiano inatokana na mambo mazuri mnayofanyiana na mnayofanya pamoja. Kwa maana kuwa huwezi kuwa na furaha katka mahusiano yako kama unamfanyia mwenza wako mambo mabaya, hata kama yeye anakufanyia mambo mazuri bado nafsi itakusuta na itakuondolea furaha. Lakini pia kama mwili mmoja mnapaswa kufanya mambo mazuri kwa pamoja, mambo ambayo yatawapa furaha kwa pamoja”.
(1) Hawapeleki Matatizo Yao Kwa Ndugu Au Marafiki; Wakati mwingine unaweza kudhani kuwa watu hawa hawana matatizo, lakini ukweli nikuwa wakikutana na changamoto yoyote huongea wao kwanza kabla ya kuanza kulalamika kwa ndugu au marafiki. Kulalamika lalamika kwa ndugu kunafanya kutengeneza picha mbaya, ndugu kumchukia mwenza wako na hivyo kuingilia mahusiano yenu kwa ushauri mbaya au hata kwa kumdharau na kumdhalilisha.
(2) Hawalinganioshi Maisha Yao Na Wengine; Wanajua kua kujilinganisha na wengine watapunguzia kujiamini na hata wakati mwingine kuwafanya kujidharau wenyewe. Wanaridhika na walicho nacho na huyaona mahusiano yao kama ni ya kipekee. Kujilinganisha na mwingine ambaye hujui undani wake kunakufanya kushindana na mtu ambaye hata humfahamu, wanandoa wenye furaha huheshimu ndoa yao na hawailinganishi na yeyote.
(3) Hawalaumu Wenza Wao Kwa Mapungufu Yao; Kila mmoja anajua wajibu wake na anapokosea basi hukuabli makosa kuliko kubakia kulaumu mwingine. Wanajipima wao na kuangalia usafi wao kuliko kufanya mambo kwa kuangalia makosa ya wengine. Kwa mfano, mke au mume anapopitiwa na kuchepuka badala ya kumlaumu mwenzake kuwa alikuwa hamridhishi, hujua amekosa yake akaomba msamaha, akajirudi na kuangalia ni kwa namna gani atamfanya mwenza wake kumridhisha.
(4) Wanajua Maisha Ni Burudani, Hawachukulii Kila Kitu Siriasi; Kwao ni kama walikutana jana, hata kama washazeeka kwenye ndoa, bado wanataniana, bado wanatoka pamoja, wanacheza pamoja na kufanya mambo yote ambayo huko awali walikuwa wakiyafanya. Hawasingizii majukumu na kukasirika kasirika, wanaamua kuwa na furaha kila wakati, huchukulia changamoto kama shemu ya maisha.
(5) Hawakosoani Wanarekebishana;Wanajua namna ya kuongea, mwenza akikosea badala ya kumkosoa kwa dharau huzungumza na kueleweshana. Wanajua kuwa mtu huelewa zaidi pale unapoonge anaye taratibu, hawajifanyi kama wanajua kila kitu na kila wakati wapo tayari kujifunza. Hakuna maneno ya ukali wala kisirani, ukosoaji huwa ni wa kurekebisha na kufundishana.
(6) Wanaongea Kuhusu Pesa; Wanajua kua matatizo mengi ya ndoa husababishwa na pesa, hivyo huweka mipango mizuri kuhusu matumizi ya pesa zao. Ni wawazi katika vipato vyao na wanapanga namna ya kutumia pamoja. Hakuna mwenye nguvu zaidi katika kupanga matumizi ya vipato vyao hata kama havilingani au mmoja hachangii kipato kabisa.
(7) Hawawazii Mabaya Wenza Wao; Watu wenye furaha ni wale ambao huwaza mazuri kwa wenza wao, hawana mawazo hasi kuhusu wenza wao. Kwa mfano mwenza wao anapochelewa kurudi huwaza labda kazi zimemzidi au kuna kitu cha maana anakifanya kuliko kuanza kuwaza labda anachepuka. Kumuwazia mabaya mwenza wako hata kama hajalifanya utaumia kama vile amefanya na itaondoa amani ndani ya nyumba.
(8) Wanawasiliana; Wanajua wenza wao si malaika kwamba watajua wanachowaza, mmoja akitaka kitu kwa mwenza wake hasubiri mwenzake kubuni au kufikiria sana, humuambia na kama hakiwezekani basi anaridhika. Mwenza wako si mnajimu kwamba kila wakati atajua unawaza nini au unataka nini, muambie unachohitaji ili akufurahishe.
(9) Hawajipangii Majukumu ya Kudumu;Kwenye ndoa kila kitu nikusaidiana, kwamba watu wenye furaha hawapangiana kazi kama ofisini kwamba mke ni lazima apike, afue au afanye usafi. Mume nilazima kutoa hela ya chakula, ada na vitu vingine. Wao hufanya chochote, mke anaweza lipa ada akanunua chakula bila kinyongo, mume akaamua kupika au kuosha vyombo. Kwakifupi hufanya mambo kama wenza na si kwa kutegeana eti kusema hii ni kazi ya flani?
(10) Wanasaidiana; Yaani badala ya kulaumu tu na kulalamikia kuwa mbona wewe hujafanya hiki na yule hajafanya kile wao husaidiana katika majukumu. Mmoja akiona kitu hakiko sawa, akiona mwenzake hajamaliza au hayuko vizuri kufanya kitu flani basi hukifanya bila kinyongo kwa furaha ya kumsaidia mwenza.
(11) Wanashukuru; Kila mmoja anatambua majukumu ya mwenzake na namna anavyojitahidi kumfurahisha mwanzake. Wanashukuru kwa kila kitu, hawashukuru tu kwa maneno bali pia kwa vitendo na kutoa tabasamu, hata kama ni kwa kitu kidogo tu ambacho mmoja wao atamfanyia mwingine lakini watashukuru pamoja.
(12) Wanafanya Mambo Mengi Kwa Pamoja; Wanajua kuwa ndoa ni pamoja na kushirikiana kufanya mambo pamoja. Si katika majukumu ya kifamilia tu bali hata katika mambo mengine kama michezo na burudani. Hutembea pamoja, kufanya mazoezi pamoja, kula pamoja, kuangalia mpira pamoja na kufanya angalau kitu kimoja kwa pamoja kamka wanandoa.
(13) Wanaungana Mkono; Iwe ni katika kazi au hobi, watu wenye furaha huungana mkono hata kama hawafurahii kile ambacho wenza wao wanakifanya lakini kwakuwa wanajua kuwa kinawapa furaha basi huungana mkono. Mwanamke ambaye hapendi mpira atamsindikiza mumewe uwanjani kama ambavyo mwanaume ambaye hata hajui urembo ni nini atampeleka mkewe kwenye mashindano ya urembo.
(14) Wanasameheana Na Kusahau:Hawakumbushani mambo yaliyopita, wakishasamehe basi husahau na hata mmoja wao akirudia kosa lile lile basi hawatasme hii ndiyo tabia yako bali watarekebishana na kusonga mbele. Hawaweki kumbukumbu ya makosa ya wenza wao na hawana vinyongo, hutoa madukuduku yao kwa kuongea na si kwa kulalamika pembeni na wakishaonge abasi husahau.
(15) Kila mmoja anatambua udhaifu wa mwenzake; Kila mmoja anamjua mwenzake vizuri anatambua udhaifu wake na amekubaliana nao, kuishi nao na pia kumsaidia mwenza wake kutokana na udhaifu huo. Hamsengenyi wala kumnyanyapaa mwenzake kutokana na ushaifu huo. Atamsaidia mwenza wake kuficha ushaifu huo na kuonyesha mbele za watu kuwa mwenza wake ni mkamilifu.
(16) Wanasali Pamoja; Labda hii ilipaswa kuwa ndiyo sifa ya kwanza lakini nimeiweka mwisho ili kuonyesha kuwa yote hayo hayawezi kuwezekana bila Mungu. Watu wenye furaha wanamjua Mungu na mioyo yao inaamani kwanni wanajua kua kuna nguvu ya ziada ambayo inawalinda.
WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment