BIBI HARUSI MTARAJIWA MALAIKA SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Tuesday, January 28, 2020

BIBI HARUSI MTARAJIWA MALAIKA SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI







ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA MOJA : ghafla mama Martin aliona mwili ukimlegea, na macho yake ya kijawa na giza, kisha akapoteza fahamu, huku akianguka chini, mama Malaika alitabasamu kidogo, ni tabasamu la matumaini mapya, huku mume wake akishangaa kwa kitendo kile cha mwanae kukataa ndoa kanisani, kisha akamshuhudia mwanae kiinama chini, akavua viatu vyake vilefu akavishika mkononi, kisha akakunja gauni lake na kulishika kwa mkono mwingine, alafu akaanza kutembea akipita katikati ya watu, kuufwata mlango mkubwa wa kuingilia, macho yote usoni kwa Edgar akijaribu kumpa ishara fulani, , endelea........
Edgar alipoona vile akawa ameshajuwa kinacho endelea, akaijuwa nia ya Malaika, ambae leo alikuwa amependeza maladufu, kuliko siku zote, akiwa mwenye wasi wasi Edgar akarudi nyuma haraka na kutokea malango alioingilia, wakati Malaika baada ya kuona kuwa mlango mkubwa ulikuwa mbari, alipinda kushoto na kuufwata mlango mdogo wa ubavuni mwakanisa, nao ni utumika kuingilia, ndani ya kanisa waumini karibu wote walikuwa wamesimama, wakimtazama Malaika, huku sauti za minong’ono ya chini chini ikiendelea, baada ya kumshuhudia Malaika akitoka je kabisa ya kanisa, nao wakatoka kwenye viti vyao na kumfwata bibi harusi, waone anaelekea wapi, lakini awakufanikiwa, kwani walisikia muungurumo wa pikipiki ile ile ambayo waliisikia dakika chache zilizo pita ikiingia pale Kanisani, “inmaana Edgar ame mtorosha bibi harusi” aliwaza  baba yake Edgar ambae alikuwepo mmoja kati ya waumini mle kanisani, sasa ulisikika muungurumo wa pikipiki, ukisogea upande ulipo mlango anaotokea Edgar na kuzungukia upande alio tokea Malaika bibi harusi, “mkamateni huyo” Ilisikika sauti ya mtu toka ndani, ni sauti ya mzee Haule, lakini akuna aliewai, maana walimshuhudia Malaika akipanda kwenye pikipiki, na kujishikilia vizuri akizungusha mikono yake kwenye kiuno cha Edgar, “Edgar tuondoke”, maneno ya Malaika yaliambatana na pikipiki kuondoka kwa kasi ya hajabu, na kupotea zake, huku nyuma bahadhi ya watu pamoja na mzee Haule, wakashauri wajaribu kuwafwatilia kwa magari, ili wajuwe wanako elekea ikiwezekana wamkamate Malaika, lakini walishindwa kufahamu walielekea wapi,
Watu waliokuwa wamekaa sehemu ya nyuma ya kinisa, ndio walio fanikiwa kuiona sura ya kijana aliekuja na piki piki, maana ndie alietoroka na bibi harusi, lakini wengi kati yao awakuwa wakimfahamu kijana yule, kundi kubwa la waumini lilikuwa nje ya kanisa, kila mmoja akiongea la kwake, na watu wachache walibaki ndani wakimpepea mama yake Martin aliekuwa amelala chini kapoteza fahamu, wakatihuo Martin naye alihisi kizunguzungu kilichofwatia na giza kutanda usoni kwake kabla ajajibwaga chini, watu wachache waliobakia mle ndani ya kanisa pamoja na waumini wachache, alikuwepo padre na wasaidizi wake, pia wasimamizi wapambe wa maharusi (best man) na mzee Komba mabasi, waligawana na kuanza kumpa huduma ya kwanza Martin, na mama yake, huku waki pambana na arufu mbaya ya pombe, iliyosikika wazi toka mdomoni kwa Martin, watu walio kuwa wamemzunguka Martin ni padre na wasaidizi wake, pia baba Martin na waumini wachache , dakika chache baadae ya kachukuliwa magari mawili, na kuwakimbiza hospital, ***** mama Malaika alikuwa amesimama pale nje ya kanisa pamoja na waumini wengine, akiwaza mawili matatu, jambo la kwanza, ni kwamba mwanae amefanikisha kuikwepa ndoa, sasa je baada ya hapo ataishi wapi, au amerudi nyumbani, Jambo la pili, je? ni kweli Malaika alikuwa na mwanamume toka za mani?. “kwakweli yule mwanamke atakuwa anajuwa tabia za huyu mwanaume, ndio maana amekimbia” mama Malaika alisikia maneno hayo toka kwa mshana mmoja aliekuwa atuwa chache toka alipo simama yeye pale nje ya kanisa, akatega masikio vizuri, “haaaaa wewe ayaishi tu!, kama ni vibaya kwanini ulimkubari” aliongea mwenzie na Veronica, na veronica akadakia, “weeee yani usiku wa harusi una lala guest na kimada” maneno hayo yalimfikia mama Malaika, akajikuta akitabasamu, wakati huo Mzee Haule alikuwa amesimama kwenye kundi la waumini, kila mmoja akiongea la kwake lakini kauli iliyo mfikia moja kwamoja ni ya binti mmoja akiwaambia wenzake “nilitaka nishangae, kwa mwanamke mwenye kujieshimu kama huyu dada, akubari kuolewa namshenzi yule, bora alivyo kimbia” mwingine akadakia “tena leo sijuwi alilala wapi yani amekuja nyumbani kwao asubuhi ana nuka pombe” mzee Haule aliendelea kusikiliza, akiwatazama wale wanawake watatu, mmoja wapo akiwepo vero nica, alie lala na bwana harusi sku moja kabla ya harusi,  “si nilikuwa nae pale hotelini nilipo fikia, si kujuwa kama ndie bwana harusi mwenyewe ndio huyu,” aliongea Veronica, akimweleza mmoja wao, hukiachilia yule aliekuwa amekaanae ndani ya kanisa, “weeeee, usiniambie Vero” alistuka yule mmoja wao, huku mzee Haule akitega sikio kusikiliza maongezi hayo ambayo ndio kwanza yalikuwa yana mzibua masikio, “yani ni melala naye mpaka asubuhi, na kama nisinge mwamsha, angekuwa ana amka saa hivi” Veronica aliongea kwa sauti ya chini, huku mwenzake akiziba mdomo kwa mshangao, “weee! Ndio huyuuuu! ulietusimulia kuwa umepata bwana umemchuna  laki tano?” aliuliza mwenzie, “mi mwenzio alipo nionyesha ndani ya kanisa nika juwa amemfananisha” aliongea yule aliekuwa na Vero nica toka ndani ya kanisa, “ndiyo wala sikujuwa kama ndie bwana harusi mtarajiwa, nime lala naye siku mbili” hapo mzee Haule alipata kitu kipya, “ndio maana Malaika alikuwa apendi kuolewa na huyu mshenzi, sasa yule kijana ninani?, na mbona kama sura yake siyo ngeni machoni mwangu” **** Mzee Mbogo akiwa amesimama pamoja na mwanae na mkewe, walishindwa kuamini kilicho tokea, walisimama kwa muda akijadiriana kwa sauti za chini, “siku zote panya uw anakimbilia kwenye shimo la karibu, pasipo kuangalia kama kuna nyoka ndani yake” aliongea mzee Mbogo yani baba yake Edgar, kwa sauti ya chini kabisa, “una maanisha Edgar atakuwa amekimbilia seed farm?” aliuliza mama Edgar, ambae sasa alisha anza kuvuta picha ya sauti aliyo wai kuisikia ndani ya nyumba ile siku aliyo mkuta Edgar akiwa na mwanamke, “aswaaa, tena ndio sehemu pekee ambayo wanaweza wakakimbilia,” aliongea baba Edgar, wakati huo Prosper mdogo wake Edgar alikuwa akiwasikiliza, kwa umakini, mwisho akatia neno, “ina maana, yule mwanamke ni rafiki yake kaka?” aliuliza Prosper na kuwa fanya wazazi wake wamtazame, “hilo ndio jibu ambalo mama yako alisema tuta lipata siku chache zijaazo” alisema baba Edgar kisha wote wakacheka, wakiwa wamejikausha kama awafahamu lolote juu ya tukio lile, waliingia kwenye land rover 109, wakaondoka zao, wakatimua vumbi kuelekea seed farm, kwa kawaida siyo mbali sana, ni mitaa iliyofuatana, njiani walionekana kujadiriana mambo mengi sana yanayo usu tukio hilo, la mtoto wao kutoroka na bibi harusi, “hivi ametumwa au ....” aliuliza baba Edgar, akionyesha kuto elewa elewa, jinsi mambo yanavyo kwenda, muda fupi baadae, walikuwa wamesha fika nyumbani kwa mtoto wao, lakini hakuwepo, walikuta milango imefungwa, “ukisikia mtu anafungwa, ndio hivi, eti mama Edgar, huyu akuona pakwenda kutafuta mchumba, akaja kuiba kanisani?” aliongea mzee Mbogo akimtazama mke wake, huku amejishika kiuno “huyu mtoto ametufyekea chini, yani ataki atakutuona tukiwa na amani,” aliongea mama Edgar kwa kulalamika, “tena kabisaaaa! ameenda kujitwisha yule binti wawatu, atampanini yule zaidi ya kufubaisha tu!” aliongea mama Edgar, safari hii akuwa ameweka mikono kichwani “alafu yule binti nae na mshangaa kweli, na yeye anakubari vipi kupanda lipikipiki libovu kama lile, anaacha magari mazuri ya kwao” wazee hawa walilalamika kwa zamu, mwisho wakaingia kwenye gari, nakarudi kanisani, kujuwa kinacho endelea, wakiwa pale kanisani maamuzi ya litolewa, watu wote walio alikwa waende chabruma hotel na kadi zao, wakaendelee na vinywaji na chakula, mpaka watapo julishwa kinacho endelea, **** Mzee Mbogo aliamua kuwa, waende wakauzurie hiyo hafla, uku wakifwatilia kila kitacho zungumzwa ili wajuwe atima ya kijana wao, pia wajuwe cha kufanya, kabla awaja anza kusumbuliwa kwa kosa la mtoto wao, kuiba bibi harusi kanisani, **** baba na mama Malaika waliingia kwenye gari na kuwafwata hospital wakina Martin, walipo fika walimkuta Martin akiwa amepata fahamu, lakini mama yake amezimia tena, kwa mala ya pili, sasa ata mzee Haule aliweza kusikia harufu ya pombe toka kwa Martin, akaamini maneno ya wale wanawake, toka walipo fika pale hospital mzee Komba alionyesha kuto kuwajari, wazazi wa Malaika, muda wote alikuwa amewanunia, mwishoe akatoa kauri moja ya hasira “kama swala lilikuwa ni ela ya mahali bwana Haule, si ungeniambia nikupe kuliko kujifanya unakubari watoto waowane alafu unaniaibisha mbele za watu” maneno hayo ya kushangaza yalimstua sana mzee Haule, “Husiseme hivyo mzee mwenzangu, hii aibu niyetu wote” mzee Haule alitumia busara, japo alishaanza kupata majibu ya swali lake “Hapana Haule mke wangu alipozinduka, akasema kuwa, mkeo alikuwa anajuwa mpango wa Malaika kukimbia kanisani” aliongea mzee Komba, akimkazia macho mama Malaika, na Kauli hiyo ilimstua sana mama Malaika, mzee Haule akamtazama mke wake kwa mshangao, itaendelea .................... kwastory zaidi like page yetu Hadithi ZA MBOGO EDGAR



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa