ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA NNE : alijibu Edgar akiwa na uakika kuwa, amjuwi mama yake Malaika “au mama ananichezea akili, ila kama anakufahamu lazima atajuwa namna yakututafuta” aliongea Malaika huku anajilaza kifuani kwa Edgar, “hivi anaweza kuja na polisi?”aliuliza Edgar “Hapana, kwa jinsi alivyo kusifia, pia alikuwa apendi niolewe na Martin, sema baba na shangazi ndio walio kuwa wanashupalia” wakati wakiendelea na maongezi mala mlango ukagongwa mioyo yao iklipuka waka tazamana Edgar akamwonyesha hishara Malaika akimbilie chumbani wakati Malaika akiinuka mlango ukagongwa mala ya pili safari hii, iliambatana na sauti, endelea.............
“hoya Edgar umelala kaka” Ilikuwa sauti ya Jastin, wote waka shusha pumzi Edgar akaenda kufungua mlango huku Malaika akikaa vizuri kwenye kochI “kaka nasikia leo umecheza kama komandoo Rambo” Ilikuwa ni baada ya kusalimiana na kupeana taharifa za ofisini “kaka yule mpuuzi alitaka kuninyang’anya mke” alisema Edgar kwa utani woe wakacheka, “kaka ila mlipanga kimya kimya sana, ilitukio la kanisani, siku nyingine tuambizane mnaweza kuitaji msaada wa haraka” Waliongea mengi sana kisha Jastin akaondoka zake, na wao walimsindikiza kisha wakarudi zao, na kuingia kulala, akika usiku wao ulikuwa mzuri sana, kiasi kwamba Malaika alisema ataki kurudi kwao, kwani atazikosa raha alizo zipata usiku ule ***** Usiku saa tano nyumbani kwakina Martin, licha ya kuwa na wageni wachache wakinywa pombe, pia alionekana kijana moja akiwa amesimama na mzee Komba, nje ya nyumba pembeni kidogo kwenye giza, alionekana mwenye ndevu nyingi sana zilizo zunguka mdomo, na kujaa chini ya kidevu, juu kabisa yakichwa cha jule jamaa akukua na nywele ata moja alivalia suluali ya jinsi nyeusi na jaket jeusi, chini buti jeusi “tume jitahidi kusaka watu wenye pikipiki kama hile, lakini atuja fanikiwa, ila kuna dogo mmoja uwa anauza viatu pale sokoni, uwa anapikipiki kama ile, tuna taka tupajuwe kwao ili tufanye uchunguzi, kama atakuwa anausika, japo tuna mshuku kwa asilimia nyingi sana, inasemekana siku moja alionekana akipanda gari la Malaika pale mitaa ya zimanimoto, pengine ndo alikuwa anapanganae njama hiyo” aliongea Para “Inawezekana akawanae kimapenzi?”aliuliza mzee Komba kwa sauti ya kilevi “hawezi kuwa na bahati hiyo, mtu mwenyewe ni fala tu! yani kesho tunamtia mkononi, tena tuna mleta na huyo binti” aliongea Para kwa majisifu “Mtakuwa mmefanya jambo la msingi sana, yani nataka yule binti afanyiwe kitu kibaya sana mpaka familia yake ihame mji, kwa ahibu ” aliongea mzee Komba kwa sauti iliyojaa hasira ya kilevi, “limekwisha hilo nipo na vijana wangu wakazi, hiyo kwao nikama chai tu” Para aliongea kwa majigambo ya hali ya juu sana, kiasi kwamba mzee Komba alikubali kwamba, yule jamaa anaweza kazi, basi akatoa bunda la fedha kisha akampatia Para ambae alizipokea huku akimhakikishia mzee Komba, kuwa kazi yake kesho inakamilika “hiyo ni yabia tu! nitakupatia nyingine kesho ukimaliza kazi” *** ASubuhi siku yapili mama Malaika aliamka mapema, huku idadi kubwa ya watu mle ndani wakiwa bado wamelala, kutokana na pombe walizo kuwa wamekunywa jana yake, baada ya kuoga na kujiweka safi, alianza kukagua kitabu cha kampuni ya simu Tanzania, akiangalia namba za simu na anuani zake akutumia mda mrefu kuipata ile namba, ya kina Edgar, kisha akasoma kwa umakini anuani iliyo amalizia na mtaa anaopatikana mmiliki wa namba ile aliyotumia kuongea na Malaika jana usiku, alipolizika akaingia chumbani kwa Malaika aka chukuwa begi dogo kisha akakusanya bahadhi ya nguo, zikiwepo zandani na viatu pea chache kisha akachukua vipodozi na mafuta, yani na vifaa ambavyo aliamiani ni muhimu kwa mwanae, akavitanguliza kwenye gari kisha akarudi chumbani, akamwambia mume wake ambae bado alikuwa amejilaza kitandani, kwamba anaenda kukagua miradi yao, maana leo ilipangwa maduka ya funguliwe baada ya jana kufungwa sababu ya sherehe, kabla ya kuondoka alichukua fedha kiasi cha laki mbili. Moja kwa moja alielekea mjini ambako alizungukia maduka yote na kuakikisha yamesha funguliwa, baada ya hapo akamalizia ofisini akashugulikia viporo vya siku mbili alafu akaanza safari ya kwenda seed farm, kama anuwani ya simu ilivyo onyesha ***** Jastin akiwa pale kijiweni, alikuja dada mmoja na kumwulizia, Edgar akidai alimwagiza viatu vya watoto vya shule, na fedha alisha mpatia, Jastin akamwambia kuwa Edgar leo atokuja, kama vipi aje kesho ata kuwepo, yule dada akamwambia bora amwelekeze alipo, sababu kesho ni jumatatu mtoto anategemea viatu hivyo kuendea shule, Jastin pasipo kujuwa lengo na zumuni la yule dada, akamwelekeza seed farm kwa kina Edgar, yule dada aliondoka haraka haraka, bila ata kuaga wala kushukuru, Moja kwa moja yule dada alielekea kwenye uchochoro mmoja, ambao kulikuwa na gari la kukodishwa Taxi, limeegeshwa, ndani yake kulikuwa na vijana watatu walio shiba vyema, kwa maumbo yao, mmoja wao akiwa yule mwenye ndevu nyingi na kipara, yule dada akaingia ndani ya gari na kukaa kiti cha mbele, akaonyesha ishara gari liondoke “seed Farm” **** Ilikuwa saa nne kasolo, Edgar na Malaika walikuwa wamesha amka toka saa moja na nusu, walikuwa mamevalia track suit na matishert waka jiunga wote kwa shuguli ndogo ndogo za pale nyumbani, wakianza na mazoezi kidogo lakini ya leo yalitawaliwa na utani mwingi na michezo ya kimapenzi, pia waka fanya usafi maeneo yote wanayo kaa, waka fungulia kuku pia kulisha sungura, waka washa moto kwa maandalizi ya kifungua kinywa, waka anza kupasha samaki ambao waliwavua pamoja siku ambayo Malaika alifungiwa ndani, waka wabanika pamoja na nyama ya kuku iliyo bakia jana jioni, pia waliandaa ndizi za kukaanga na mayai ya kuku ya kukaanga, chai ikichemka bila kusaahu kachumbari, lakini walipo kaa mezani tayari kuanza kula, wakagundua kuwa, sukari akuna, hivyo ikabidi kidume Edgar kikimbie dukani kununua sukari, ***** Mama Malaika alikuwa amesha iacha barabara ya kwenda tunduru na kuingia mtaa wa seed farm, mwanzo wa mtaa aliona nyumba nyingi zikiwa karibu karibu, akaona kuna shemu inamaduka mengi mengi, aka simama akitaka kuulizia kwakina Edgar, wakati akiingia hapo kwa mwendo wataratibu, mala akapigiwa honi kwa fujo na gari nyingine nyuma yake, ilikuwa ni taxi, akasogeza gari lake pembeni ya barabara, akiruhusu lile taxi lipite, ambapo lile taxi lilipita na kwenda kusimama mbele yake kidogo, akuwajari wamiliki wa lile taxi, japo lilimkela kwa honi walizo mpigia kwa fujo, wakati wanaenda kusimama karibu, mama Malaika akatulia ndani ya gari akijaribu kuangalia mtu wakumwuliza nyumbani kwakina Edgar, akutaka kujulikana kuwa yeye ni mama Malaika, kutokana na tukio la jana, ambalo habari yake imetapakaa mji mzima, wakati anaendelea kuangalia, akamwona Edgar mwenyewe akija mbio mbio, pale madukani, akaingia kwenye duka moja, ambapo alitumia kama dakika mbili kuhudumiwa, kisha akatoka akiwa amebeba mfuko wa brue, hapo mama Malaika akashuka toka kwenye gari na kumwita,“we! kijana, we! kijana mwenye mfuko” Edgar aligeuka huku akizidi kupiga hatua adi alipo mwona yule mama, ndio akasimama, na kumfwata yule mama alie mwita, pasipo kujuwa kuwa nimama mkwe “pole mwanangu naona hupo mbio mbio” aliongea mama Malaika, akiachia tabasamu la mama kwa matoto “haa! mama unafikaga adi huku?” aliongea Edgar huku akijichekesha chekesha, “ndiyo mwanangu, uwa napenda kutembea tembe siku kama hii ya jumaapili, naona na kuchelewesha ingia kwenye gari, nika kuache hapo mbele” mama Malaika alijuwa akijitamburisha mapema pengine huyu kijana angeingiwa na uoga, na kukataa kuelezea uwepo wa Malaika nyumbani kwake, na Edgar naye Pasipo kujuwa kuwa huyu ndie mama mkwe wake, na leo ni mgeni wake, aliingia kwenye gari, waka lipita lile taxi wakielekea nyumbani kwake, njiani waliendelea na story za kawaida, pasipo kujuwa lile taxi lina wafwata kwa nyuma, liliwaachia umbari kidogo ili isiwe lahisi kuwastuki, Malaika alikuwa akimalizia kuandaa chai mezani, kwa vitu vilivyo pungua, mala kwa mbari akasikia mlio wa gari ukija nyumbani kwao, aka chungulia dirishani, akaliona gari likisimama, lile gari analifahamu akajiuliza “kapajuwaje hapa, au nikweli wanafahamiana na Edgar muda mrefu, wanafahamiana kivipi?” alijiuliza Malaika, Mala anamwona Edgar akishuka, na mama yake pia akashuka upande mwingine wa dereva “mh! kumbe kweli wanafahamiana, mbona Edgar alikataa kwamba hamfahamu mama, ngoja waje wanieleze ukweli” alisema Malaika huku akiufwata mlango mkubwa na kutoka nje, et! Kawivu kalimshika “kumbe kweli mna fahamiana, sasa mbona Edgarulikataa” Edgar alishangaa kumwona mama Malaika akinyoosha mikono yake mbele, ikiwa ishara ya kumtaka mwanae amkubatie, malaika akamkumbatia yule mama “waoooo mwanangu umenifurahisha sana! ebu! shusha begi lako kwenye buti, tuongee mwanangu” aliongea mama Malaika akionyesha furaha ya kweli kukutana na mwanae “inamaana Malaika huyu ndie mama yako?” aliuliza Edgar akiwa bado ameshangaa “ndiyo ni mama yangu, kumbe ulikuwa unamfahamu?” Malaika alitoa begi kwenye gari, na Edgar akalibeba wakaingia ndani wote kwa pamoja wakakaa mezani, nakuanza kunywa chai, huku Edgar akisimulia Malaika siku ile ya kwanza kukutana na mama Malaika, jinsi alivyo kuwa siku ile alivyo kuwa amevurugwa akili, pia akamsimulia kisa cha Martin na Sophia na kumwagiwa na mama Malaika maji na kukutana na mama Malaika, pia kunusulika kugongwa na gari la Martin na kukutana na Malaika “kumbe mama yule kijana ulie nisimulia ni huyu Edgar” aliuliza Malaika kwa mshangao mkubwa, “tena jina lake nimelijuwa jana ulipo litaja kwenye simu jana usiku, unajuwa ilifikia kipindi niliomba kuwa ndio angekuwa mchumba wako” Waliongea huku wakinywa chai, chai ambayo mama Malaika aliita ni chai nzito, tena akuitaji kabisa chai yenyewe yeye alikula na kushushia maji kutokana na pombe alizokunywa jana, walifanya yote kwa shangwe, pasipo kujuwa kuwa nje kuna mtu na wachungulia na kuwasikiliza wanacho ongea, itaendelea ...... kwa story zaidi, like page yetu ya Hadithi ZA MBOGO EDGAR
No comments:
Post a Comment