SMULIZI MPYA: HOUSEGIRL WA KITANGA 01 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, December 23, 2019

SMULIZI MPYA: HOUSEGIRL WA KITANGA 01



SMULIZI MPYA: HOUSEGIRL WA KITANGA
MTUNZI : KIZARO MWAKOBA

SEHEMU YA KWANZA

Mimi ni msichana niliyekulia kwenye maadili ya dini ya kiislamu. Naweza kusema kuwa nawashukuru sana wazazi wangu kwa kunilea vizuri na kunifanya niwe mtoto mwema katika kijiji chetu cha Tanganyika kule mkoani Tanga wilaya ya Muheza. Wazazi wengi walikuwa wakitamani sana vijana wao wawe na tabia kama niliyokuwa nayo mimi.
MWANTUMU ndilo jina ambalo nilikuwa nimepewa na wazazi wangu siku ya saba baada ya kuzaliwa. Wakati mwingine nilikuwa nikiwasikia watu wakiniita TUMU. Hivyo nikakuzwa na majina hayo yaani Tumu ama Mwantumu. 
Mzee Mohamedi ama wengi walizoea kumuita mzee Mudi pamoja na mke wake Bi.Zamda ndio walikuwaMAPEMi wangu walionileta hapa ulimwenguni pamoja na kunilea katika maadili mema.
 Kawaida yangu huwa sipendi kujisifia hata kidogo, lakini kusema ukweli mimi nilikuwa ni msichana ambaye nilikuwa nimeumbwa na kuumbika vilivyo. Hapa sifa na utukufu tumpe muumba. Umbo langu lina urefu wa wastani yaani sio mrefu sana na wala sio mfupi wa kuchukiza. Uso wangu wa duara uliokuwa na rangi nyeupe mara nyingi ulikuwa ukipendezeshwa na mtindo wa nywele zangu niliokuwa nimezoea kusuka ambao wengi huuita twende kilioni. Macho yangu ya kusinzia niliyokuwa nikiyafumbua kwa taabu yalizidi kuvutia hasa pale nilipokuwa nikiachia tabasamu mara kwa mara na kuacha meno yangu madogo meupe yaliyokuwa na mwanya mdogo katikati kuonekana. 
Umbo langu lilitaka kufanana na umbo la chupa ya bia. Juu nilikuwa mwembamba wa kawaida na kifuani nilikuwa na madafu mawili ambayo hayakuwa na ukubwa wa kuchukiza lakini pia hayakuwa madogo ya kujificha. Kuanzia kiunoni kushuka chini nilikuwa nimejazia vilivyo na kunifanya nivutie. Nyonga yangu ambayo ilikuwa ikitofautisha umbo langu la juu na la chini ilikuwa imetanuka mno kiasi cha kunifanya hata mimi mwenyewe kujitazama mara kwa mara hasa nilipokuwa pekeyangu chumbani.
Maadili niliyokuwa nimepata kutoka kwa wazazi wangu yaliniwezesha kuhitimu masomo yangu ya shule ya msingi katika shule ya msingi iliyokuwa ikifahamika kwa jina la Mkumbi nikiwa salama pasipo kuharibikiwa na tabia za makundi rika ambazo vijana wengi hukumbana nazo. Wasichana wengi wa kijijini kwetu hawakufanikiwa kumaliza shule kutokana na sababu mbali mbali kama vile kubeba mimba na wengine kufukuzwa shule kutokana na tabia zao ajabu ajabu.
Ingawa nilifanikiwa kuhitimu masomo yangu salama lakini naweza kusema sikuwa na bahati ya kuweza kuendelea na masomo ya shule ya sekondari. Siwezi kusema kuwa nilikuwa nimefeli mtihani, Laa hasha! bali kipindi kile shule za sekondari zilikuwa ni chache mno, hivyo wanafunzi wengi tuliishia elimu ya msingi na waliochaguliwa kuendelea walikuwa ni wachache.
****
Maisha ya kijijini hayakuwa na ujanja zaidi ya kilimo hasa kwa wale wenzangu na mimi ambao hatukupata bahati ya kuendelea na masomo. Zaidi ya kilimo kwa sisi wasichana tulikuwa tukisubiri siku ziende ili tuolewe basi.
Kusema ukweli mwenzenu mimi pamoja na kwamba nilikuwa nimekulia kijijini lakini jembe lilikuwa likinipiga teke kabisaaa. Nilikuwa nikienda tu shambani kwa lengo la kuwaridhisha wazazi wangu lakini nilikuwa nachukia sana kulima
Nakumbuka Jumapili moja nilikuwa njiani nikitokea shambani, nilikuwa nimepumzika chini ya mti mti mmoja mkubwa sana ambao kule Tanga tumezoea kuuita mvule ambao ulikuwa ukitoa kivuli kizuri. Nikiwa pale chini ya mvule alifika mwanamke mmoja ambaye nilikuwa nikimfahamu kwa jina moja tu la Mama Kibo. Mama yule ambaye naye alikuwa akitokea shambani alifika pale nilipokuwa nimeketi na kutupa jembe lake chini kwa kishindo.
“Ophhhh” Mama Kibo alipumua kwa nguvu, alikuwa na kila dalili ya kuchoka kutokana na kazi ya kulima pamoja na kutembea umbali mrefu.
“Pole sana mama” nilimpa pole mama yule huku nikitoa tabasamu la kumkaribisha kwenye kivuli kile cha kubembeleza usingizi.
“Ah! Ahsante mwanangu hujambo?”
“Sijambo mama Kibo, Shikamoo”
“Marahaba. Naona wapumzika mama” alisema mama yule kwa lafudhi ya kitanga.
“Jua kali mamaangu, ukishindana nalo hili laweza kukuua” nilizungumza ili kuonesha umuhimu wa mapumziko yale.
“Nikweli kabisa. Vipi leo mbona uko peke yako?” mama kibo alihoji huku akijiweka kwenye shina la mti ule wa mvule nakuegemea.
“Baba amekwenda Pongwe kuchukua maji, na mama amekwenda Muheza kuna vitu amekwenda kununua?” nilimjibu mama yule ambaye alionekana kutaka kufahamu walipo wazazi wangu ambao mara zote nilikuwa nikiongozana nao kwenda na kurudi shambani.
“Ahaa” mama Kibo alinijibu kisha akachukua kidumu cha maji kutoka kwenye kikapu chake na kukipeleka mdomoni. Nilimtazama mama yule jinsi alivyokuwa akiyabugia maji yale kwa pupa. Ilionekana alikuwa na kiu kwa muda mrefu ila alikuwa akitafuta pozi la kukituliza. 
Alipomaliza kunywa maji yale alikiweka chini kidumu kile kisha akabehua kuashiria kuwa alikuwa ametosheka. Alipeleka mkono kinywani kujifuta majimaji amabayo yalikuwa yamemmwagikia mdomoni wakati anakunywa. Baada ya zoezi lile fupi aliinua macho na kunitazama usoni.
“Hivi mwanangu unampango gani?” alihoji mama Kibo kwa sauti ya chini.
“Mpango wa vipi mama Kibo?”
“Hapa kijijini”
“Mnh! bado sijakuelewa”
“Wategemea utaishi hivyo hadi lini?” alihoji mama Kibo kwa ile lafudhi yake ya kitanga.
“Kwani naishije jamani mama kibo, mbona kawaida tu?” nilihoji huku nikionekana nilikuwa bado sikuelewa swali lake.
“Kwanini wataka jizeesha na jembe mwana mdogo!”
“Mnh! mama Kibo bwana, jembe si ndo kila kitu hapa kijijini kwetu?”
“Si kweli!”
“Kumbe nifanyeje sasa?”
“Waonaje ukenda mjini?” Mama Kibo alihoji swali ambalo kwangu nililiona ni kama vile fumbo. Heti niende mjini! Sasa mimi binti niliyezaliwa kijijini Tanganyika na kukulia kijijini Tanganyika, huko mjini ningeenda kwa nani? na ningeenda kufanya nini?
“Sasa mjini nikafanye nini mama Kibo?” ilinibidi nimuulize vizuri mama yule ambaye nilimuona akizungumza maneno ya kusadikika na yaliyokuwa yamejaa pumba.
“Mwanangu mjini ndiko kwenye maisha” alizungumza mama Kibu huku akiokota kipande cha fimbo na kupigapiga chini kama vile anacheza.
“Mnh! mama Kibo bwana, kwani si hata hapa kuna maisha?”
“Kweli hata hapa kuna maisha, lakini mjini kuna maisha bora mwanangu. Kule hakuna kulima kama huku kijijini?” mama Kibo alizungumza maneno ambayo yaliniingia hasa pale alipogusia suala la kilimo. Nikameza funda la mate ya kutamani kuondoka pale kijijini.
“Sasa huko mjini mimi nitakwenda kwa nani?” nikahoji kwa hamasa.
“Wamfahamu yule dadaangu BI.FATUMA anayeishi Dar es salaam?”
“Ndio namfahamu”
“Si waona jinsi alivyo na maisha mazuri?”
“Ndio, nafahamu” nilijibu kwa upole huku nikisikiliza kwa makini maneno yake yaliyokuwa matamu kwenye masikio yangu. Kusema ukweli dada yake huyo aliyekuwa akimzungumzia alionekana kuwa na maisha mazuri. Alipokuwa akija pale kijijini kusalimia alikuwa anaonekana ni kijana kuliko hata mdogo wake mama Kibo kwa jinsi alivyokuwa anapendeza. Zawadi alizokuwa akiwaletea ndugu zake pale kijijini hazikuwa za kawaida. Kwa kigezo kile niliamini kwa asilimia tisini na tisa kuwa mjini kulikuwa na maisha mazuri. Na kwakuwa nilikuwa nachukia sana jembe basi ndio kabisaa nikazidi kuvutiwa na maisha ya mjini.
“Na mimi ningekuwa na ndugu Dar ningekwenda, maana kulima kushanichosha” Nilizungumza kwa sauti iliyokuwa imekata tamaa ya kuishi kijijini. 
Mama Kibo alitoa tabasamu baada ya kuniona nimevutiwa na mazungumzo yake.
“Yule dadaangu ahitaji mfanyakazi wa ndani” alisema mama Kibo.
“Kwahiyo mie naweza enda huko Dar?” nilihoji kwa hamasa huku nikiinuka kidogo kuonesha kuvutiwa na taarifa ile. Nilikuwa tayari kwa njia yoyote ile ambayo ingewezekana ilimradi niondoke kijijini.
“Ndiomaana nimekwambia weye kwasababu najua waweza kaa na dadaangu kwasababu unatabia nzuri na heshima” mama yule alizidi kunitia hamasa kwa maneno yake yale ya kunipamba.
“Basi njoo nyumbani uzungumze na baba” nilimwambia huku nikonekana wazi kuwa nilikuwa na furaha juu ya taarifa zile.
“Usiwe na wasiwasi mwanangu jioni naja” mama yule alizungumza huku akijiinua na kusiamama. Namimi nilisimama na kujinyoosha viungo vyangu kisha nikachukua khanga niliyokuwa nimeitandika chini na kujifunga kiunoni tayari kwa safari ya kuelekea nyumbani. Tuliinua majembe yetu kisha taratiibu tukaanza kuondoka tukiwa na nguvu mpya iliyokuja baada ya mapumziko.
****
Taarifa za mimi kwenda mjini kufanya kazi za ndani zilipowafikia wazazi wangu, hawakuniwekea pingamizi chochote. Waliniruhusu niende mjini kwa dada yake mama Kibo kwasababu walikuwa wakifahamiana sana na mama yule. Nilifurahi sana ndani ya moyo wangu na kujiona nilikuwa nimeshinda kuepukana na adha ya mpini wa jembe pale kijijini Tanganyika.
Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika jijini Dar es salaam tangu nilipokuwa nimezaliwa. Nilikuwa  nimesimama kwenye bango moja la Cocacola ambalo nilikuwa nimeelekezwa nilipokuwa nikiondoka kijijini kwetu Tanganyika. Niliambiwa nisiondoke sehemu ile hadi mwenyeji wangu atokee kunipokea. Nami nikafanya kama ambavyo nilikuwa nimeagizwa.
“T u m u !” nilisikia sauti ya mtu ikiniita kutokea upande wa kushoto. Nilipogeuka nilimkuta dada yake mama Kibo akitembea kuelekea pale nilipokuwa nimesimama. 
“Oooh mama!” nilihamaki kwa furaha. Sikupata taabu kumtambua kwasababu ni mara nyingi sana nilikuwa nikimuona alipokuwa anakuja kule kijijini kwetu Tanganyika kuwasalimia ndugu zake.
“Pole kwa safari mwanangu” alisema mama yule.
“Ahsante mama. Shikamoo”
“Marahaba, umesubiri sana enh?” 
“Hapana mama nimeshuka sasahivi”
“Wahuni hawaja kusumbua?”
“Wamenisumbua lakini nilijitahidi kuwakwepa”
“Haya twende nyumbani mwanangu” alizungumza mama yule na kunisaidia begi langu dogo lililokuwa na nguo. 
Tulipofika nje ya geti la Ubungo tuliingia kwenye Pajero moja kali sana ya rangi nyekundu ambayo ndiyo alikuwa amekuja nayo mama yule. Niliingia kwenye gari ile huku nikishangaa shangaa. “Ama kweli mjini raha” Nikajiambia ndani ya moyo wangu baada ya kuona msururu mrefu wa magari yaliyokuwa kwenye foleni pale kwenye mataa ya Ubungo. Majumba marefu na wingi wa watu vilinifanya nigundue utofauti uliokuwepo kati ya kijijini kwetu Tanganyika na pale jijini Dar es salaam.
 Mama yule aliendesha gari lake kwa kunyata na kulibembeleza. Jamani nyie mjini kutamu, kijijini kwetu havikuwepo vitu kama vile. Kama nisingekwenda mjini mambo yale ningeyaonea wapi? Unadhani ningepanda lini gari kama lile la Bi.Fatma? Siwaongopei jamani mjini kuzuri, sio kama kwetu kijijini ambako nilikuwa nimezoea kuona ngedere na ndege. Mjini ni magari, mataa ya barabarani, na majumba marefu marefu hadi mbinguni. “Ooh Mama Kibo ubarikiwe sana, bila ya wewe nisingefika huku Ulaya” nilizungumza mwenyewe kimoyomoyo huku nikizunguusha macho kutazama majumba marefu.
ITAENDELEA



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa