SIMULIZI :RAHMA 04 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Monday, December 9, 2019

SIMULIZI :RAHMA 04





Hadithi ____ RAHMA
Mtunzi ____Ruvuly De finisher

👉NAMBA 04

Tunaendelea ......

Yule mama alikataa kwamba hajamuona mtoto yeyote kwa mbali ilisikika sauti ya mtoto akilia fatuma aligeuka kisha akafuata sauti ile alikwenda huku akiita mwanangu , mwanangu, wakati anakimbia aliangusha ile cheni tena pale pale katika eneo la yule mama fatuma akiwa anaifuata ile sauti alipofika sehemu sauti ilipokuwa inatoka alimkuta mama mmoja akiwa amembeba mtoto mgongoni kichwani akiwa amebeba kuni. Fatuma alifika akamvamia yule mama akamnyanganya mtoto alipomwangalia usoni aligundua mtoto yule sio rahma, Fatuma aliishiwa nguvu akapiga magoti huku akilia sana. Yule mama alisimama baada ya kuanguka chini akaja sehemu aliyokuwepo Fatuma akamchukua mtoto wake kisha akaondoka akiwa na wasiwasi mkubwa .

Yule mama mwenye nyumba alipoona fatuma kaondoka nyumbani kwake aligeuka ili aingie ndani kumtazama mtoto aliyemuokota yule mama kabla hajaingia ndani aliona cheni akaiyokota alafu akasema :-

   ""Hii cheni inanini mbona huyu binti alikuwa  analia sana baada ya kuona  hii cheni, au huyu mtoto aliye ndani ni mtoto wake kweli '' mmmmh hapana wengine huwa ni wezi wa watoto siwezi kumuamini mungu nisamehe kama nimefanya kosa kutosema kama nimeokota mtoto , Hata Mimi nahitaji mtoto pia kama ni mama wa kweli wa mtoto huyu alifikaje kwa mbwa wangu na damu zile zilitoka wapi duuh mbona hali hii inanitisha jamani .

Baada ya mama yule kujiuliza maswali mengi aliingia ndani akamkuta Mtoto ( rahma) akiwa amelala akasema .. :-

  ""Mtoto wangu nisamehe sana kama hiki nilichofanya leo nitakuwa nimekukosea sana au kama nitakuwa nimekulinda itakuwa vyema zaidi kwa sababu simjui mama yako mzazi na ndio maana sikumuamini aliyekuja leo , laiti kama ungekuwa unazungumza ungesema kama yule ni mama yako lakini nakuvisha cheni hii huenda itakuwa inamaana katika maisha yako.""
  
Baada ya maneno hayo mama aliingia ndani akawasha moto ili atengeneze chakula cha mtoto ,Fatuma alisikitika sana akasimama  akaondoka huku akiwa katika dimbwi zito la mawazo , Alitembea kwa muda mrefu sana akatokea katika barabara kubwa inayoenda mjini , alivuka barabara akiwa na mawazo Wakati anavuka barabara ghafla lilitokea gari likamgonga Fatuma. Dereva alishuka haraka haraka akamkuta fatuma yupo chini anahangaika damu nyingi zikimtoka ,Yule dereva alimnyanyua fatuma na kumuweka kwenye gari na kuondoka nae ili kumuwahisha hospitali kwa matibabu. Dereva aliendesha gari kwa mwendo mkali sana ili kujaribu kuokoa maisha ya msichana aliyemgonga. Fatuma akiwa kwenye gari muda wote alitamka "Mwanangu " Mwanangu" Mwanangu.

Dereva alikimbiza gari kwa uwezo wake wote hadi hospital japo palikuwa mbali sana lakini alijitahidi akafika mapema kwa sababu hospital hiyo ilikuwa mjini , alipofika aliomba msaada kwa wahudumu wa pale hospitalini , wahudumu walimsaidia na kumchukua mgonjwa haraka haraka ili kumpatia huduma kwa sababu Fatuma alikuwa ametapakaa damu wahudumu walitoa huduma ya haraka zaidi. Yule dereva akiwa nje anasubiri majibu, alikuja nesi akamwambia mgonjwa atakuwa vizuri  muda si mrefu kwakua hakuumia sana. Fatuma alipewa kitanda akalazwa katika hospital ile. Yule dereva alirudi nyumbani kwao alipofika nyumbani  alimsimulia kaka yake aliyekuwa  anaishi nae pale nyumbani , kaka yake akampa pesa kwa ajili ya matibabu kwa mgonjwa.

Baada ya muda kupita  Fatuma alipata fahamu akajishangaa yupo hospitali na amewekewa drip ya maji , alistajabu na kujiuliza  kimempata nini hadi yeye akawepo pale hospitalini , Wakati akijiuliza yupo wapi mlango ulifunguliwa akaingia yule dereva na kaka yake . Fatuma alipowangalia walioingia akastuka mno akasema #SULEYMAN !!!!!!!!!!!! . Fatuma akasimama akachomoa ile sindano  iliyokuwa  mkononi mwake kwa hasira kisha ...........
___________ITAENDELEA___________
#SHARE ili na mwingine ajifunze kitu kama wewe unavyojifunza ahsante.


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa