SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial) - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, December 7, 2019

SIMULIZI: EQUATORIAL FOREST (msitu wa Equatorial)




MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 01



UTANGULIZI: kwa Jina naitwa Najma, Nina umri wa miaka 22 na soma university mwaka wa pili sasa, wazazi wangu wote wapo hai ila baba yangu mzazi alifungwa jela sasa ni  mwaka mmoja kwa kesi ya uchochezi wa wana nchi ili waweze kuleta mgomo selekalini kuwa mshahara waliopewa ulikuwa mdogo,  nakumbuka siku hio baba na wafanyakazi wenzie (walikuwa ni wajenzi) hivo walipata tenda kutoka kwa mkuu wa mkoa ili waweze kujenga Ofisi za selekalini, baba na wenzie tenda hio waliichukuwa kwa mikono miwili Baada ya kukubaliana kipato kizuri, walipomaliza mkuu wa mkoa na ma supervisor waliokuwa wakiwasimamia takribani wa nne waliwapa pesa ndogo sana kama asilimia arobaini kwa ile waliokuwa wamekubaliana hali ya kuwa selekali ilitoa pesa ya kutosha, kitendo cha kupewa pesa ndogo kiliwafanya wachukie na kudai pesa yao, siku moja baba na wenzie ishirini Walikubaliana waende kwa viongozi wa Juu wakaombe msaada ikiwezekana wawawekee hata asilimia kumi Juu zingine wakaushie ila kila waliekuwa wakimlilia aliwapotezea kama vile wanamsumbua, waliamua wachukuwe uamzi wa kwenda kituoni kulipotia swala lile ajabu mkuu wa mkoa aliwazunguka wote wakawekwa Chini ya ulinzi kwa kesi ya kuleta vurugu nchini hivo Walikaa siku nne selo, supervisor mmoja akawafuata selo akawaambia wakaushia Ila baba akazidi kuwapa moyo wenzie waendelee kutetea haki yao Ipo siku mheshimiwa Raisi litamfikia Jambo hilo na atawachukulia hatua,  mwishowe baba alichezewa mchezo wenzie wakamzunguka Baada ya kupewa pesa ndogo wakampachika kesi kuwa Yeye ndie alikuwa anawachochea waje kuleta vurugu selekalini ili kuwachafulia Jina hali ya kuwa pesa walipewa zakutosha hivo kesi Ilikuwa kubwa tena kubwa Mara dufu,  kila Tukienda Mimi na mama yangu kuuliza tulikuwa tukiambiwa kesi imeshikiliwa mahakamani hivo tulipata wakati 
mgumu sana. 

*******************************************

Mama yangu Umu-kulsum toka baba aingie jela alipatwa na ugonjwa wa presha kutokana kutulea Mimi na mdogo wangu Latina ilikuwa kazi kubwa kwake ukija kuangalia sote tulikuwa Wa kubwa na tulikuwa sote tunasoma university Mimi mwaka wa pili mdogo wangu Latina mwaka wa kwanza na pesa yote ya Ada ya shule ulikuwa ni mkopo baba aliouchukuwa selekalini akiamini angelipa taratibu taratibu ila majanga ndo hayo mwaka sasa yupo jela hilo ndilo lilizidi kumchanganya mama licha kila siku tulikuwa tukimpa moyo asijali tupo kwa ajili yake tukimaliza chuo tukapata kazi nzuri tutamsaidia baba na tutalipa madeni yote tunayodaiwa. 


SONGA NAYO! 

Asubuhi mapema ya tarehe 2 may mwaka 2019 Mimi Latina Pamoja na mama yetu tulijiandaa tukaelekea mahakama iliopo dar es salam maeneo ya... Maana Sisi makazi yetu yalikuwa dar es salam maeneo ya kijitonyama, tulipofika mahakamani kesi za watu wengine zilisomewa mwishowe baba akaletwa kizimbani ili kusomewa hukumu aisee nilipomuona baba yangu anahofu nyingi na sio Kawaida yake machozi yaliyatawala macho yangu Nikajilazimisha kumpa moyo huku nikitabasamu, baba alipoiona familia yake imekuja kumpa moyo alifurahi moyoni,  kesi yake haikuwa na wakili hivo alikatiwa kifungo cha miaka mi tano au faini ya milioni tano, mama aliposkia hivo nguvu zilimuishia akalegea huku akipumua vibaya, Tulianza kumpepea huku tukilia Pamoja na wasamalia waliokuwa hapo, kitendo kile kilimfanya baba aanze kumwita mama kwa uchungu: Umu Umu Umu mke wangu !!!

Mapolisi walimchukuwa baba na kumrudisha jela,  Baada ya lisaa limoja kupita tulikuwa tupo njiani tunarudi nyumbani huku mama akionekana vizuri tofauti na Muda uliopita. 

Tulipofika nyumbani Nilimpa moyo mama asiwaze Sana milioni tano sio pesa nyingi atatoka jela muda sio mrefu. 

Siku hio ilipita kila mtu Hana raha,  siku moja Baadae niliporudi nyumbani Baada ya kutoka shule Latina kwa presha aliniambia: mama hali yake sio nzuri. 

Nikashangaa na kumuuliza: Kulikoni? 

Latina: ndio toka asubuhi anaongea maneno ya ajabu hata simwelewi. 

Nikamuuliza: anaongeaje? 

Latina: Njoo umwone mwenyewe. 

Tuliingia ndani nikamkuta mama amekaa sebuleni huku akivuta vuta uzi taratibu uliopo kwenye nguo aliokuwa amevaa,  nilikaa pembeni yake na kumuuliza: mama nini shida? 

Mama hata hakuniangalia aliendelea kufanya alichokuwa Anafanya ndipo Nikamuuliza tena: unafanya nini mama??? 

Mama alikurupuka na kunisukuma kisha akasema kwa sauti ya Juu: Mume wangu yupo wapi??? 

Mimi na Latina Tulimshangaa ndipo mama akatoka nje anakimbia huku akipiga kelele,  Tulitoka hapo tukamfuata haraka ila kwa mbio alizokuwa nazo Alituacha mbali,  siku nzima iliisha tukiwa tunamtafuta ila hatukuweza kumwona.

 Majira ya jioni tukiwa tupo njiani Mimi na Latina mwenye umri wa miaka 20 njia nzima tulikuwa tunalia bila kujuwa wapi tutamwona mama, tukiwa tunazidi kulanda Landa mtaani mdada jilani yetu alitusimamisha na kusema: mnisubiri Kidogo. 

Tulisimama ndipo akatufikia na kusema: mama yenu nimemwona kule Chini ya barabara kuelekea Ilala.

Tuliposkia hivo tulimuomba atusaidie atupeleke huko nae hakuwa mgumu kwetu alitupeleka huku tukikimbia Sana,  tulipofika maeneo aliotuambia alisema: ndo Yuleeee..

Tulimuona kwa mbali alikuwa ametupa mgongo huku akiwa amekaa Chini kama vile kuna kitu anachambua,  mwonekano wa mama ulinifanya niangushe kilio kikali ndipo mdada Yule akanipa moyo nisijali Allah yupo Pamoja na Sisi,  mdada Yule Alituacha hapo akaenda nyumbani maana muda ulikuwa umeenda,  tulimaliza kama dakika kumi tukiwa tunamtazama kwa mbali ndipo Latina akaniambia: tukimfuata akatuona wallah hatutampata tena Sasa sijui tunafanya nini. 

Nikamjibu: Kikubwa tunamuona, Ngoja mi niende kumwona Yule Doctor  Rafiki yake baba   nikamwambia ikiwezekana aje kutusaidia. 

Tulikubaliana hivo Mimi nikaenda kumtafuta mzee huyo,  Baada ya muda tulikuja nae akiwa ameongozana na Manesi wengine wanaohusika kuwalinda Wagonjwa wa hakili,  tulipofika walimsogelea taratibu ile kuwaona tu alishtuka Ila walikuwa tayari wamemchoma sindano ya kumpunguza nguvu mwilini.

Siku hio ilipita mama alihifadhiwa hospitalini nasi tukarudi nyumbani.

Baada ya siku nne sasa bila kwenda chuo kutokana na Matatizo ya familia, siku hio tulikuwa tumekaa sebuleni Mimi na mdogo wangu ndipo Latina akaniambia: dada pesa ni ndefu Sana sasa Kama sindano moja ni Elfu stini hio gharama tutaiweza kweli? 

Nikamjibu: kesho twende chuo mambo mengine tutayajuwa Baadae. 

Latina: tunaendaje shule na Hali ya familia Ipo hivi? 

Nikamjibu: shule tuliifanya mkombozi Wa familia yetu Acha tusome baba Ndo anavyotaka ikiwezekana nikamaliza mambo yote yatakuwa sawa Najuwa baba nikimtoa jela Halafu mama akamwona basi atapona na familia yetu itarudi kwenye furaha kama mwanzo. 

Latina: sawa. 

Siku iliofuata tulielekea chuo, kizuri sote tulikuwa tunasomea science hivo chuo kilikuwa kimoja tulipofika tulishangaa kukuta maandalizi sio ya Kawaida mpaka tukashindwa kuelewa ndipo mdada Rafiki yangu Jina lake Joyce alikuja tulipokuwa tumesimama na kusema: come on Najma mbona hivo? 

Nilitabasamu na kumjibu: Kwani nipoje?

Joyce: Jana nakupigia haupokei simu why?

Nikamjibu: mama yangu amechanganyikiwa Baada ya hukumu ya baba Ndo maana siku hizi sikufika chuo. 

Joyce: Oohh my God pole Sana my dear. 

Nikamuuliza: kuna nini mbona Mishe Mishe Sana? 

Joyce: my dear hapa tuna ugeni mkubwa Si unamjuwa Yule specialist mkubwa hapa Tanzania kwa maswala ya upasuwaji wa moyo! atakuja kutembelea chuo chetu Leo na atatoa somo kwa masaa ma wili Baada ya hapo anaenda England aisee Najma yaani sio Mimi ntaona Nimeiona sura yake naskia watu wanamsifia ni kijana mdogo mdogo tena handsome.

Nikamjibu: tatizo you talk to much. 

Joyce alicheka kisha akaondoka zake kwa maringo,  Latina aligeuka kuniuliza: mbona hukutaka kumsikiliza?

Nikamjibu: Nina raha gani? 

Latina: Ila huyo specialist kwa masuala ya upasuwaji wa moyo unamjuwa maana nahisi atakuwa peke yake hapa Tanzania nzima kama atakuwa mbongo.

Nikamjibu: Anaitwa Derick ni mwana science mkubwa alisomea wingereza anauwezo mkubwa Sana na nitegemezi nchi nyingi za Africa mpaka ma ulaya. 

Latina alishtuka na kuniuliza: ulijuwaje? 

Nilimpita huku nikimjibu: niliambiwa na teacher. 

Latina alitabasamu kisha akanifuata kwa nyuma. 

Baada ya muda tulijipanga freshi baadhi ya wanafunzi walisimama mokono wa kushoto Wengine mkono wa kulia katikati kuelekea ofisini kwa mwalimu mkuu walitandika red-carpet Chini ili ugeni Huo mkubwa tuuoneshe kuwa tunaujali sana,  nikiwa nimesimama mawazo yalienda mbali nikamkumbuka mama hali alionayo nikajikuta nakosa furaha kwa dakika mbili,  Latina akiwa amesimama upande wa pili aliponiona Nimeingia kwenye imotion mbaya alinipa moyo kwa kunionesha dole gumba ndipo nikatabasamu na kumrudishia dole gumba, muda Huo kwa mbali tuliona gari za kifahari kama tatu, watu macho yaliwatoka wakitamani kujuwa Nani anaekuja Ila Mimi sikuwa na habari nao. 

Gari Zile zilipakiwa sehemu maalumu kisha wakatoka vijana wawili na Wazee wa nne,  walipofika pale red-carpet inapoanzia walitabasamu kwa furaha kisha wakaanza kupiga hatua huku wakisalimia mwanafunzi kwa mwingine kupitia mikono,  wanafunzi walipomuona Derick walitamani Sana kumuuliza maswali mengi kuhusu science ila muda ulikuwa bado,  mdogo wangu Latina alipomuona Derick alijawa na tabasamu isio ya Kawaida ila Mimi hata kupoteza muda eti nipo nawatazama wala.

Derick kila mwanamke Aliekuwa akimpa mkono alionekana kushoboka Haina mfano, Derick alipofika mbele yangu na kuiona sura yangu alishtuka Ila  Mimi nilijifanya kumpotezea ndipo akanipa mkono, Nilimpa bila kujali ndipo akaushika mkono wangu kwa dakika mbili huku akinitazama Mpaka kila mtu hapo akashangaa kwa kile kinachoendelea, aibu ilinitawala nikaamua kujikohowesha ili aniachie, ndipo akaniachia na kuendelea bila hata kuwasalimia wanafunzi waliokuwa wamebaki maana alionekana kuchanganyikiwa baada ya kuniona,  Baada ya muda Wageni wakiwa wapo ofisini kwa mwalimu mkuu Latina alinifuata na kuniuliza: hivi ni wewe Wa Muda ule si? 

Muda Huo alifika Joyce na kuniuliza: Najma it's you? 

Niliwapotezea nikaamua kuondoka zangu.

 Baada ya muda somo ilianza na Aliekuwa akiendesha somo alikuwa ni Derick, wana science wote kuanzia mwaka wa kwanza kuendelea tulikuwa kwenye class moja,  nikiwa nimekaa na mdogo wangu Latina nilimwambia kwa sauti ya Chini: tukitoka hapa twende magereza kumuona baba ili tumpe taarifa kuhusu mama. 

Latina: Nikweli ila hujaniambia Derick Muda ule alikuwa anakwambia nini?

Nikamjibu: Potezea.

Latina: Mbona sasa anabaki anakutazama Muda wote? 

Nikamjibu: kama huwezi kusoma toka nje. 

Latina: sawa basi yaishe.

Derick alianza kuzunguka darasa taratibu, alipofika nilipo alisimama kama vile kuna jambo anataka kuniambia,  muda Huo watu wote waligeuka kumwangalia Derick huku kila mtu akijiuliza maswali bila kupata majibu,  Nami Muda Huo nilijikausha kama vile simuoni, Derick uzalendo ulimshinda akasogea kwenye dawati yangu akaweka mikono huku akinitazama usoni,  Latina alishtuka mpaka akabaki anashangaa ninavyompotezea,  wanafunzi hawakuamini haswaa Mabinti wenzangu, Derick alipomua kwa kasi kama mtu mwenye hasira vile, Nami wala sikumpa muda macho yangu pembeni tu ndipo Derick akaniuliza huku akiwa yupo serious: Kwanini unanifanyia hivi? 

Latina uzalendo ulimshinda Akajishika kwenye mdomo ishara ya mshangao, bila wasi wasi wala kuteteleka nikamjibu: Kwani wewe Nani? 

Wanafunzi waliokuwa nyuma hawakuamini, Latina alishindwa aseme nini akajibu pahali yangu: muelewe anamatatizo Muda huu. 

Latina alinigeukia na kusema: Ndo nini sasa mtu mkubwa Kama Huyu kumjibu utakavyo? 

Sikumjibu Niliendelea kufanya inshu zangu ndipo Derick akasema: unanipa wakati mgumu Sana, kila siku nafikiria Upo wapi Kumbe upo hapa hapa Tanzania why hukunitafuta?

Nikamjibu: Kwani Mimi nikuhusu tena?

Derick: somo ikiisha usiende bila kuonana na Mimi please. 

Alichukuwa kauntbook yangu ajabu akaandika namba, alipomaliza Akaniambia: this's my fone namba please ni call kabla ya kwenda nyumbani.

Derick aliondoka wala hakutoa somo tena alitoka moja kwa moja nje ndipo akaingia mzee waliekuja nae ili kuendeleza somo, wanafunzi walitamani Sana kuniuliza maswali kadhaa Ila kwa kuwa soma nyingine ilianza waliamua wakaushie, muda wote Latina macho kwangu Mpaka akashindwa aniweke kwenye Aina gani ya binadamu.

Simo ilipoisha tu wanafunzi waliniwahi kama wote maswali yalianza kutoka kila kona * Najma ulimjuwaje Derick *
*Najma ulikuwa unajuwana kabla na Derick *
*Najma mbona kakushobokea sana Kulikoni? *

Nilinyanyuka na kusema kwa sauti ya Juu: Simjui hanijui mniacheeee.

Niliwapita nikatoka zangu nje huku Joyce na Latina wakiwa wananikimbilia, waliponifikia Joyce alisema: Shostiii Mbona upo hivo? 

Nikamjibu: nipoje? 

Joyce: why hili swala unalikwepa sana Huyu mtu mnajuwana Eee??? 

Latina akadakia: dada sema ukweli bwana Mbona kama vile anakujuwa sana na wewe unamjuwa Sana Ila ukaamua kumpotezea na Kwanini Sisi watu wako wa karibu hutaki kutwambia? 

Joyce: wallah atuweke wazi Nipo nakwambia Derick mpaka walimu wametamani namba zake hawakuzipata ila wewe kirahisi rahisi hata Haujamuomba amekuandikia unajuwa hata Watoto wa maraisi wanatamani Sana kufanyiwa alivyokufanyia wallah siwezi kukuelewa. 

Nilipaza sauti kwa hasira huku nikiwajibu: niacheniiii! Eti Watoto waraisi wanaitamani nafasi ile hivi wewe unawajuwa Watoto waraisi vizuri sasa kwa taarifa yenu naondoka na sitampigia kwanza na namba nachana. 

Nilichana ile karatasi iliokuwa imeandikiwa namba kisha nikaichana Chana vipande vidogo vidogo kwa hasira na kutupa Chini,  Latina na Joyce walibaki wameachama kwa mshangao ndipo nikawapita na kuondoka zangu. 

Nikiwa nipo njiani naelekea magereza machozi yalianza kunitiririka ndipo nikasema:........!!!!!


   Unahisi nini kitatokea! 
Usikose mkasa huu!



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa