HUWA inatokea kuna neno mwanamke huwa anataka kusema ila anasita. Kuna jambo huwa anatamani kufanya, lakini anaishia kujishauri tu bila kulifanya. Wanawake wengi wanaumia bila hata kujulikana.
Wanateseka sana katika mahusiano bila jamii kuhisi wala kujua. Katika hili wanaume wanapaswa kubeba lawama kamili
Mbali na tofauti za kijinsia ila pia mwanamke na mwanaume wametofautiana sana katika aina ya vitu wanavyopenda, namna wanavyoamua na hata ufanyaji wao mambo. Mwanamke na mwanaume ni tofauti sana.
Dunia imemtengeneza mwanamke katika mazingira fulani ya kusubiri na ya kumuangalia zaidi mwanaume kwanza. Katika mapenzi kama ilivyo katika mambo mengine mengi, wanawake huwa wanasubiri sana mwanaume aanze jambo fulani.
Japo mwanamke husika huwa anapenda labda uogee jambo fulani hasa la faragha, ila huwa anaona itafaa zaidi kama neno litaanza kutoka kwa mwanaume.
Hali hiyo kwa wengine huwa inaanzia katika hatua za uanzishaji wa mahusiano husika. Japo Khadija anaweza kuwa na hisia za kweli juu yako ila anaweza asiongee kwanza akakungoja wewe.
Katika kukusukuma uanze kusema, hapo anaweza kukufanyia mambo mengi ya kukufanya ukajua namna anavyokuhitaji katika maisha yake.
Kwa kufanya hivi mwanamke huwa ni silaha yake ya kusema ‘nakupenda’ ila ni wa wachache sana wanaoweza kufikia hatua ya kufunua vinywa vyao na kuongea dhati za moyo wao.
Hutamaduni huu wengi wameendelea nao mpaka hata baada ya kuwa katika ndoa. Anaweza akawa anapenda jambo fulani ila akasita kukueleza na akasubiri mwanaume aanze kusema.
Japo kwa wapendanao haipaswi kuwapo kwa hali hii ya aibu ila ni vyema mwanaume akabeba majukumu yale yanaotegemewa na wanawake wengi.
Kwa kusema hivi, maana yake mara nyingi mwanaume anapaswa kuwa mwepesi wa kuhisi na kutambua mwenzake anapenda nini. Katika hili mwanaume anabidi awe mjanja katika kumuuliza anapenda nini au hapendi nini.
Pia yeye awe huru kumueleza mwenzake nini anapenda na kitu gani huwa si vyema kwake. Kuna wengi katika mahusiano yao wanawaangusha wenzao.
Unakuta mwanaume akiwa na mwenzake anakuwa kama kuna kitu anahofia au anasita kusema jambo. Unapokuwa katika hali kama hii mwanamke anazidi kuwa mnyonge.
Hawezi kujiachia ikiwa wewe kama kiongozi anayekutegemea unakuwa hujiamini. Anadhani akikwambia anapenda hivi utamchukulia tofauti.
Katika kumuweka huru mwenzako jaribu kusoma ni vitu gani wanawake wanapenda kisha jaribu kumfanyia au kumuuliza uone atajibu nini.
Najua wanawake wengi wanafanyiwa nusu ya wanayopenda kufanyiwa na wenzao, ila wanasita kuwaambia. Wanasita kwa sababu wanadhani wakisema watapata mtazamo tofauti.
Mwanaume akisema napenda kukufanyia hivi inaweza kuchukulika kawaida. Ila mwanamke akismea hivyo inaweza kutengenezwa maswali mengi kwa muhusika.
Si kwa sababu nyngine ila ni kwa vile mazingira yanamfanya mwanamke awe msikilizaji na wakati mwingine ajichukulie kama mwanafunzi wa mwanaume japo katika baadhi ya mambo hasa ya mapenzi kila mmoja anaweza kuwa mwalimu kwa mwenzake.
Ili kutengeneza mazingira ya kupata chote anachotaka kukupa mkeo inabidi uwe huru naye kuongea naye kila jambo zuri lihusulo upamoja wenu.
Kwa kufanya hivi mwenzako atakuchukulia kawaida na kufanya ajiweke huru sana kwako. Hapo atakueleza nini huwa anafurahia, nini hafurahii. Ni kitu gani unapaswa kupunguza ama ni kitu gani unapaswa kuongeza.
‘Ukiact’ kinyonge kwa mpenzi wako unamfanya kuwa mnyonge zaidi. Amua kumtendea yalio mema naya kumfurahisha ili naye ajihisi aji kufanya ama kusema anayotamani.
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments:
Post a Comment