TIPWATIPWA TETEMA- 25 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, November 29, 2019

TIPWATIPWA TETEMA- 25


TIPWATIPWA TETEMA- 25
ILIPOISHIA:
Licha ya misukosuko hiyo iliyotokea, bado mipango yangu ya kwenda kuonana na Jack ilikuwa palepale, nilipofika kituoni, nilimpigia simu, akapokea na kuanza kulalamika eti kwa nini sijafika mpaka muda huo.
“Foleni mama, nipo jirani nakuja lakini kuna bonge la foleni, usijali nakuja!”
“Fanya haraka bwana,” alisema Jack kwa sauti ya kudeka flani hivi, nikakata simu na kushusha pumzi ndefu.
SASA ENDELEA...
Akili yangu haikuwa imetulia kabisa, muda mwingine nikawa natetemeka mwenyewe kwa hofu huku maneno ya baba mdogo yakijirudia ndani ya kichwa changu.
“Yaani mimi nahangaika kumlea mwanamke anapendeza halafu mtu mwingine aje kujilia kirahisirahisi tu, tena siku nikimkamata itabidi kwanza nimuoe ndiyo nimchinje!” kile alichokisema baba mdogo kilijirudia ndani ya kichwa changu, nikawa naitafakari kauli hiyo.
Mambo ya mwanaume kumuoa mwanaume mwenzake, kisha baada ya hapo amchinje na kutenganisha kichwa? Eti kisa cha yote hayo ni mwanamke tu? Niliona kama nikifanya mchezo kweli naweza kujikuta kwenye matatizo makubwa.
“Hapana! Hapana! Nimekoma,” nilisema huku nikiendelea kutetemeka kwelikweli, kijasho chembamba kikawa kinanitoka.
“Vipi, unaumwa kijana wangu?”
“Aah! Hapana, hapa...na! Najisikia vibaya.”
“Ooh! Maskini polee! Unaelekea wapi kwani?”
“Naenda Sinza Mori!”
Mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa abiria waliokuwa wakisubiri daladala pale kituoni, aliniuliza baada ya kuona hali yangu ikiwa si ya kawaida. Mara tu baada ya kumaliza kuzungumza na Jack na kumdanganya kwamba nipo kwenye foleni, nilianza kujisikia hali isiyo ya kawaida.
Mwili ulikuwa kama unachemka, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio, jasho linanitoka lakini wakati huohuo, nikitetemeka utafikiri nimewekwa kwenye friji. Ni sababu hiyo ndiyo iliyomshtua abiria huyo ambaye naye alikuwa akisubiri usafiri.
“Ooh! Maskini polee, jaribu kunywa maji yanaweza kukusaidia,” aliniambia kwa upole, nikamuona akienda kununua maji ya baridi kwa muuzaji aliyekuwa pale kituoni na kuniletea. Ujue wanawake wengi ni viumbe walioumbwa na huruma sana! Ni rahisi sana mwanamke kukupa msaada anapokukuta ukiwa kwenye hali ya uhitaji, kuliko mwanaume.
Basi niliyapokea yale maji na kuanza kuyagida mfululizo! Ndani ya muda mfupi tu, chupa nzima ilikuwa imeisha, nikashusha pumzi ndefu na kukaa vizuri kwenye kiti, yule abiria mama akawa amekaa pembeni yangu akiwa ananitazama kwa makini.
“Vipi unajisikiaje?”
“Aah! Najisikia ahueni kubwa sana, asante mama! Ahsante sana.”
“Maji ni dawa! Tena dawa nzuri kwelikweli!” aliniambia, basi nikamshukuru sana. Muda mfupi baadaye, daladala ilikuja, hata sijui yule mama alipotelea wapi maana nilitaka kumshukuru tena na kumuaga kabla sijaondoka kwa sababu huo ndiyo uungwana, niligeuka huku na kule nikimtafuta lakini sikumuona, basi nikamshukuru kimoyomoyo kisha nikapanda kwenye daladala.
“Njoo ukae! We dada mpishe huyo kijana anaumwa nimemuwekea siti,” alisema yule mama huku akinionesha ishara. Kumbe wakati mimi nikiwa nimezubaa pale kituoni, yeye aliwahi kupanda kwenye daladala na kwenda kunikabia siti!
Kiukweli nilifurahi sana ndani ya moyo wangu kwa upendo aliokuwa akiuonesha yule mama ambaye kiumri naweza kusema kwamba ni mwanamke wa makamo, akiwa na kati ya umri wa miaka thelathini na tano hadi arobaini.
Nilijisikia amani ndani ya moyo wangu, basi haikupita muda mrefu yale mawazo ndani ya kichwa changu ambayo ndiyo yaliyosababisha niwe kwenye hali ile yalianza kujirudia tena.
“Unaitwa nani kijana.”
“Naitwa Chande.”
“Unaonekana haupo sawa! Nini kinakusumbua, hebu nieleze labda naweza kukupa msaada, ujue wewe ni kama mwanangu!”
“Mh! Mama, kuna mambo yananichanganya sana kichwa hata sielewi cha kufanya,” nilisema huku nikimtazama machoni. Alionesha kuwa mwanamke mwenye moyo wa kipekee sana na japokuwa hakuwa amefikia ‘levo’ ya kulingana na mama, kwa heshima niliamua kumpa cheo hicho.
“Nimekuona kuanzia kule kituoni ndiyo maana nikakushauri unywe maji. Unasumbuliwa na nini kwani? Mchumba wako amekukataa?” aliniuliza swali ambalo sikulitegemea, nikajikuta nikitabasamu na kukwepesha macho kwa aibu.
Sikutaka kumueleza kila kitu ndani ya daladala kwa sababu ningewafaidisha watu wengine lakini kutoka ndani kabisa ya moyo wangu, nilikuwa nahitaji mtu wa kumshirikisha mambo yaliyokuwa yananisibu kwa sababu nilikuwa najihisi kuchanganyikiwa.
“Ni stori ndefu kidogo, siwezi kukuhadithia hapa kwenye gari,” nilisema, akiwa anataka kuzungumza kitu, kisimu changu kilianza kuita mfululizo, basi harakaharaka nikaingiza mkono mfukoni na kukichomoa lakini katika hali ambayo sikuitegemea, kiliniponyoka na kudondoka chini, basi betri ikaangukia upande wake, laini upande wake na mfuniko upande wake.
Lilikuwa ni tukio la aibu kwangu kwa sababu nilijitahidi kuvaa vizuri na kupendeza lakini simu niliyokuwa naitumia ilikuwa inaniangusha sana. Aliyekuwa akinipigia alikuwa ni Jack na nakumbuka siku ile aliponiona nayo kwa mara ya kwanza alinicheka sana na kuniambia kwamba atanipa simu yake ndogo anayotumia lakini kwa bahati mbaya tukapotezana mpaka siku hiyo.
Yule mama alinisaidia kwa kila kitu, akanipa simu yangu ikiwa imesharudishiwa jinsi ilivyokuwa mwanzo, nikajihisi aibu kubwa ndani ya moyo wangu.
“Makumbusho mwisho wa gari!” konda alisema kwa sauti ya juu, ni hapo ndipo nilipogundua kwamba kumbe tulishafika mwisho wa gari!
Kwa kuwa mimi nilikuwa nimekaa dirishani, ilibidi yule mama ambaye bado sikuwa najua anaitwa mama nani mpaka muda huo au anajishughulisha na kazi gani, alinyanyuka na kuchukua mkoba wake, akanishika mkono kama mama anavyomshika mkono mwanaye wanapovuka barabara ili asije akagongwa na magari.
“Tunaomba njia jamani, nipo na mwanangu mgonjwa,” alisema yule mama ambaye alikuwa na lafudhi fulani hivi ya kama Mzanzibari, basi tukashuka mpaka chini huku akiwa bado amenishika mkono, tukasogea pembeni ambako kidogo kulikuwa na utulivu.
“Kwa hiyo hapa Mori si unaweza kufika mwenyewe?”
“Ndiyo mama! Nashukuru sana.”
“Haya! Mimi naelekea Mikocheni! Hapa inabidi nichukue Bajaj, au nikufikishe unakoenda?”
“Aah! Hapana mama, nashukuru! Nashukuru sana.”
“Sawa mwanangu! Hebu andika jina lako na namba yako ya simu hapa, najua una mengi ya kuniambia lakini muda hautoshi,” alisema huku akitoa simu yake kubwa na nzuri ambayo ilinifanya niduwae kidogo nikiishangaa. Basi nikaandika namba yangu na jina.
“Mh! Kumbe unaitwa Chande?”
“Ndiyo mama!”
“Haya mwanangu, yangu ni hiyo inayoishia na kumi na mbili, nitakuflash ukiwasha simu,” alisema huku akianza kutembea kuelekea upande wa pili kulikokuwa na Bajaj, nikamsindikiza kwa macho mpaka alipopanda kwenye Bajaj na kuondoka! Nilifurahi sana kutokana na wema alionionesha ambao ulinisahaulisha kabisa msala uliotokea nyumbani.
Harakaharaka nikaelekea kwenye daladala za kuelekea Sinza, nikawasha kisimu changu na kumpigia tena Jack ili nimwambie kwamba nimeshakaribia.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.


     ðŸ”žWAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa