Sasa hivi ukitaka kupiga sound demu unatumia maneno haya yanayokwenda na wakati
- Vita ya kutazama uzuri wako haijawahi kuziacha hisia zangu salama.
- Nipe makinikia ya moyo wako.
- Naahidi kulipa mirahaba yako na kodi zote za mapenzi.
- Sitakudanganya kiwango cha madini kilichoko kwenye mchanga wa madini ya mapenzi kama acacia.
- Please usizuie contena la mchanga wa madini ya penzi langu kwenye bandari ya moyo wako.
- Usiniundie kamati za marafiki zako kufanya uchunguzi wa makanikia ya upendo wangu.
- usinitangaze kuwa naiba utajiri wa mgodi wa moyo wako hadharini mbele ya vyombo vya habari.
- Nitakufata hata kwa private jet kama rais wa Barick.
- Nitakuomba ukae kwenye meza ya mazungumzo ili uniruhusu kuchimba sukari ya moyo wako.
- Usiwahusishe viongozi wastaafu ma X wako katika katika ombi langu sababu wengine watakuwa walikusainisha mikataba mibovu ikakuumiza na wengine wamepumzika baada ya kazi kubwa ya kulijenga taifa la moyo wako
No comments:
Post a Comment