MAMBO MAKUU YANATOSABABISHA KUTENGANA KWA WAPENDANAO - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Friday, July 5, 2019

MAMBO MAKUU YANATOSABABISHA KUTENGANA KWA WAPENDANAO



















Kutofanya uchaguzi ulio sahii wa mke/mme au mchumba.
Vijana wengi siku hizi hujilaumu sana  juu ya chaguo la mwenza wake. Ukikosea mwanzo ujue utaoa na kuacha mke zaidi ya mmoja. Pakifikia mahali unaanza kutamani wanawake/mwanaume wa nje na kumsahau wako wa ndani ujue ni ishara kwamba hukufanya chaguo zuri ujana wako.
Wazazi kutopendezwa na mke/mme.
Hapa wazazi nawazungumzia wale wanaopenda kuingilia mambo ya ndani ya watoto wao. Kuna watu wanaitwa mawifi, hawa ndio chokochoko kubwa na mke na mme kutengana. Watatumia maneno ya uzushi na unafiki ili mradi mke au mme yule waachane. Mwisho ndoa au uchumba unavunjika.
Dini tofauti.
Hili ni suala la mdahalo karibu dunia mzima. Inapotokea mme na mke wameanzisha uchumba, na kila mtu ana dini yake, mwanzo wa penzi hakuna aneyekumbuka nini athali kwa hapo baadaye. Muda unasonga, na kila mmoja anahitaji afunge ndoa au wazazi wafahamu, hapa kila mmoja anaanza kukumbuka utofauti wao. Kutokana na imani kali au kutokuwa na uelewa mwanzo, wanaamua kutengana ili kulinda maslahi ya dini au dhehebu la kila mtu. Hii mara nyingi hutokea kama mmoja wao ni Mkristo au Muislam. Katika ndani ya ukristo kuna misingi inayoongoza kanisa la SABATO. Hapa pia hawaruhusu muumini kuoa au kuolewa nje ya dhehebu hili   vinginevyo anatengwa na kanisa.
kutofikia kilele wakati wa tendo la ndoa.
Hakuna ndoa inayoweza kudumu kama tendo la ndoa halifanyiki. Au kama linafanyika ni kwa kulidhika mmoja na mwingine asitosheke. Hii ni sahemu muhimu sana inayomfanya mke au mme aweze kuwa na mahusino na mtu mwingine ili aweze kujitosheleza. Kila mmoja hupenda atosheke, na inapotokea vinginevyo migogoro huanzia hapo na hatimae kuvunjika kwa penzi lao. Zao la hili ni kutoroka kwa mke/mme au mchumba na kuanzisha uhusiano na mtu mwingine.
Tabia ya uzinzi kupindukia.
Hapa nazungumzia tabia ya umalaya ya mwanamke au mwanaume nje ya mpenzi wake. Hawa ni watu ambao uzaliwa na genes za aina hiyo na wamerithi kutooka kwa wazazi. Hivyo kwa mtu aliyorithi inakuwa ni rahisi zaidi kutoka nje ya ndoa yake na kwenda kufuata wengine ili mradi atimize malengo yake.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa