NIMEMSALITI MUME WANGU BILA KUTAKA - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Saturday, May 25, 2019

NIMEMSALITI MUME WANGU BILA KUTAKA



Mimi nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa watoto 4. Ndoa yetu ilipofikisha miaka 4-5 mume wangu alicheat, nikamkamata through sms akapinga sana lakini baadae alikubali akakiri kosa na kuomba msamaha nikamsamehe
Tumeendelea kuishi na nilipopata mtoto wa tatu akanicheat tena, safari hii alikuwa nje ya nchi kimasomo, napo alikiri na kuomba msamaha, nikamsamehe
Wakati niko mjamzito mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi alinicheat na house girl wanga akampa ujauzito. kwa hivyo wakati mimi nina mimba na House girl naye mjamzito (japo sikujua kama house girl alikuwa mjamzito kwani aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtoto wa aliyekuwa house Girl wangu ni wa mume wangu
Kama kawaida yake akaomba msamaha safari hii hadi kupiga goti na kulia ili nimsamehe...na mimi kwa kuwa bado nampenda na nimemvumilia kwa mengi nikaamua kumsamehe tena..ila tulikubailana masharti mengi na akakubali masharti yote niliyompa..mwanzoni alibehave vizuri sana akawa muwazi kwangu hanifichi chochote kuhusu huyo mtoto.. na tuliishi maisha ya furaha kwani alinijali mno na alionekana kweli amerigrate.
sasa cha kushangaza siku za karibuni amebadilika sana, amekuwa msiri na hasemi chochote kuhusu huyo mtoto wa nje..siku hizi anatuma hela kwa siri na pia anawasiliana na huyo mama wa mtoto kwa siri haniambii chochote..
Nilipoona mabadiliko niliamua kumuuliza imekuwaje tena mbona siri tena wakati tulikubaliana kila kitu kiwe open? hakunijibu isipokuwa alikuwa mkali na kufoka na kusema hilo swala tumeshamalizana nalo sitaki kulisikiasikia tena..
Nikajaribu tena siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa kifupi hataki na anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa...sasa najiuliza kwa nini anafanya siri? kama hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini? ina maana kuna kitu zaidi ya mtoto.
Sasa jamani mimi nimeamua kama ifuatavyo:
1. Na mimi nimeamua kuwa na mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu nami pia nahitaji kuliwazwa na kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na mastress yasiyo kuwa na mwisho, sikuwahi kumcheat mume wangu katika maisha yote ya ndoa. ila sasa atanisamehe tu hata akijua wala sijali, nipo tayari kwa lolote..
2. Sina mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi hapa hapa kwani sipendi watoto wangu walelwe na mzazi mmoja..watoto hawajui kinachoendelea in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi sijawaambia na wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yangu..kwa nje tunaonekana familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio tunaojua ndani kukoje
3. Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu na marafiki nimeamua kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani kwani sometime naona kama nazidiwa mawazo vile

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa