DADA/MWANAMKE GOLI KIPA ULIYEKO KWENYE NDOA HII YAKO - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Wednesday, May 22, 2019

DADA/MWANAMKE GOLI KIPA ULIYEKO KWENYE NDOA HII YAKO



Sisi kama wana jamii tunapenda sana kujidanganya,,kawaida mtu fulani anapokuwa na hali flani nzuri,hali ya raha,,hali ya kutokufanya kitu fulani lakini akafaidi kila kitu,,anakuwa na tabia ya kujidanganya kila siku hali itakuwa ile ile na mambo hayatakuja kubadilika,,
Hata kama anajua kabisa yatakuja kubadilika lakini kutokana na raha anazopata za bure basi ni ngumu kuamini hali hiyo kuwa itaisha,,hiki ndicho kitu kilichopo katika ndoa nyingi na ndio kitu ambacho wanawake wengi tunacho,,
Ni ngumu sana kumuambia au kumuaminisha mwanamke ambae yupo kwenye ndoa ya raha,,mumewe anampa kila kitu,,anampenda na kumuonyesha kuwa yeye ndiyo kila kitu,,,
Ni ngumu mtu kuamini lakini ni kweli,,mwanaume hataishi na wewe milele,,narudia hataishi na wewe milele hata kama mlipendana vipi ipo siku mtatengana na kila kitu alichokupa kitaisha,,
Kuna kutengana kwa aina nyingi,,kwanza ni kwa yeye kukuacha na wewe kulazimika kuanza upya,lakini kuna kule kubaya ambapo Mungu anaweza kumchukua,,najua utasema vipi akianza kukuchukua wewe,,nikwambie tu hiyo ndiyo dua ambayo mwanamke kula kulala ambaye hujui kutafuta unatakiwa uiombe kila siku,,
Kwamba ili hizo starehe anazokupa ziwe za milele ni lazima uombe wewe utangulie kufa lakini akitangulia yeye utalazimika kusimama mwenyewe,,ni ukweli ambao hatuuongei lakini upo na unaendelea kuwepo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa