SABABU YA KWELI AMBAYO INAKUFANYA USIMSAHAU MPENZI WAKO WA KWANZA - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Sunday, March 3, 2019

SABABU YA KWELI AMBAYO INAKUFANYA USIMSAHAU MPENZI WAKO WA KWANZA



Ilikuwa ni mwezi wa saba pale Debora na Samweli walipokuwa wanafanya sherehe ya kudumu kwa ndoa yao. Walikutana wakati wanasoma high school mwaka 1996.

lakini kabla hujaanza kupiga mahesabu yako , ya kuwa hawa watu wana miaka mingapi, nataka nikukatishe hapo. Ingawa walikutana high school wakawa wanapendana na kila moja ndio ilikuwa mara ya kwanza kumpenda mtu. walibaki kwenye ndoa kwa miaka minne tu.

Sawa tu na wapenzi wengi ambao mahusiano yao ya utoto hayakuweza kudumu, kila mtu alienda kivyake na kuolewa na kuoa na kuanzisha familia .Samweli alioa mara mbili , wakati Debora aliolewa mara moja, lakini hakuna alimsahau mwenzake.

Samweli na Debora hawako peke yao, kulikuwa na familia ya karibu kwangu ambao nao waliungana wakiwa high-shool na walikuwa wakitafuta kiwanja cha kujenga nyumba pamoja. ili wajenge nyumba yao, lakini baadae  kila mmoja alienda njia yake.

Zaidi na Zaidi imekuwa kwamba wale walikuwa wamependana  mwanzo hurudiana tena. Ni kwa nini?

Mtu mmoja alinisimulia kuwa, ukikutana na mtu kimwili, anakuachia alama fulani ambayo haisahauliki, na hio alama ni kumbukumbu . lakini tukiangalia Kisayansi zaidi, ni kwamba, mwili hutoa stress ya Homoni norepinephrine, Ambayo hukupa hisia za makosa ya kuvutiwa kwa mapenzi, mapigo ya moyo , kupumua kwa kasi na ule woga. lakini pia hufanya kitu kimoja zaidi.

Wachunguzi waligundua kuwa hii homoni inasababisha tukio kuwa kumbukumbu. Na pia ina njia ya kipekee ya kukufanya usisahau. ndio maana watu wanaweza kukuambia kitu walichokuwa wanafanya 9/11 lakini hawawezi kukuambia kitu kilichotokea siku moja kabla.

Lakini pia Homoni hio ya norepinephrine haikumbushi mabaya tu , inakumbusha hata siku za matukio ya furaha. hicho ndicho kinacholeta hali ya kushangaza kwenye matukio ya maisha kama kumpenda mtu kwa mara ya kwanza ni vigumu kumsahau.

Wachunguzi wanasema kumbukumbu hizi zinaweza kudumu- maishani . Na hio ndio sababu Debora na Samweli walikubali hilo kwamba mara zote hukumbukana.

Bila shaka, kutosahau ni kitu kimoja.  Sijawahi kumsahau rafiki yangu muhimu sana, lakini haina maana kwamba nataka kuolewa nae. wakati tunajaribu kuelewa tofauti, tuangalie kwa maneno mengine, wakati ukiwa karibu na huyo mtu tena, kuna vitu vinasababisha zile kumbukumbu za zamani na hisia kurudi upya. hio sio kwamba umesahau ; unapowaona tena, hisia lazima huwa zinarudi.

Turudi kwenye kesi ya Debora na Samweli, walipoteana miaka 30 hawakuonana. Siku moja kulikuwa na sherehe shuleni. na Hawa watu walialikwa kila mtu tofauti. huko ndiko walikokutana tena. Mara ya kwanza waliongea tu na kutembea tembea. Waliendelea kufanya hivyo kirafiki tu.

Lakini, Kadri Debora alivyokuwa anasimulia historia,” Usiku mmoja kilitokea kitu….. hata muhudumu alielewa kitu kilichokuwa kinaendelea” mambo hubadilika.

Norepinephrine iliingia mjengoni. walitumia muda wa kutosha pamoja na kukumbushana hisia zao za ujanani na mapenzi waliokuwa nayo.

Haikuchukua muda Samweli na Debora kutambua hisia zao. waliamua kuanza upya mahali walipoachia muda mrefu uliopita. kwa hio kitendo hicho sio cha Debora na Samweli peke yao, Kinaweza kutokea hata kwako.


umepanda hii makala ? shirikisha wengi wajifunze.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa