RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA KUMI NA TATU 13 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, January 23, 2020

RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA KUMI NA TATU 13





ENDELEA...............
.......Ilinibidi nikae mule kwenye maji kwanza huku nikitafakari nimefika vipi mule na wale viumbe nawakwepa vipi.
Ilikuwa ni kasheshe sana pindi vile viumbe vya ajabu nilivyoviona kama vibwengo hivi vinanisubiria muda wote vikiwa vinatembea pembezoni mwa ukingo wa bahari.
Ilikuwa ni asubuhi hiyo maana jua lake lilikuwa tamu sana kwenye mwili wangu. Nilipiga hesabu nyingi sana lakini ziligoma. Ndipo nilipoamua kutafuta msaada kwa kuangalia kama kuna mtu yeyote ambae anaweza kujitokeza na kunisaidia. Baada ya muda kupita vile viumbe viliondoka mbali kabisa na pale nilipo ndipo na mimi nikaanza kujitoa kidogokidogo sasa kuelekea tena kule kwa mwanzo.
Mwendo wangu ulikuwa makini kwa kujua pindi likifumuka mimi nakimbilia kwenye maji, hatua ya kwanza, ya pili na ya tatu nikawa nimefika eneo husika la Kisiwa kutoka baharini.
Nilichungulia kwa umakini wote nikaanza kuingia sasa kutoa miti ambayo inanizuia mbele yangu. Jambo la kwanza nashukuru sikukutana tena na vile vibwengo mpaka nafika ndani ya kisiwa.
Mule ndani hakika ni pabaya sana. Miti imeshonana na kuweka kiza kizito. Sauti za ndege na wadudu pekee ndizo zilikuwa zinatawala pale. Wakati nashangaa kuangalia juu ndipo nikajikwaa na kudondoka chini, pale chini nilikutana na mizoga ya watu pamoja na wanyama kadhaa.
Mara yangu ya kwanza kumuona mtu aliyekufa ilikuwa siku hiyo, nilitetemeka sana kiasi kwamba nguvu pia ziliniishia nikashindwa hata nifanye nini. Nilijiziba mdomo baada ya kumuona kiumbe mmoja akikatisha mbali na pale.
Niliogopa sana na kujua sasa maisha yangu yamefikia mwisho kabisa na vile nilivyokuwa natarajia kabisa. Nilinyanyuka ili nitafute hata sehemu ya kujihifadhi na wakati huo tumbo langu sasa linadai chakula. Siku ya balaa ni balaa tu na siku ya bahati ni bahati tu ndivyo hivyo ilivyo.
Wakati natoka kwenye zile maiti nilikutana na mtumbwi upande mwingine wa kisiwa, daaah! Nilifurahi nikajikuta napiga yowee kubwaaa.
"Yerewiiiiiiiiiiiiiiiiii"
Nakuja kushtuka kumbe zile kelele zilisababisha mambo mengine baada ya ndege juu kuruka kwa wingi na sauti za wale viumbe nikivisikia kwa mbali kama wanakuja pale nilipo.
Nilipiga hatua kama za wanajeshi hivi wakipiga gwaride lile la guz-match kama hatua tatu nakutana na ule mtumbwi lakini.
Niliduwaa baada ya kuona ndani yake kuna mwili wa mtu.
"Daaah!!! Hawa viumbe washenzi wanaua watu hivi jamani yalaaa sasa nafanyaje".
Niliongea peke yangu mule msituni, mwanaume siku zote penye shida ndipo anajua anafanya nini. Niliukokota japo ulikuwa mzito nilijitahidi nikaona bado nafanya kazi ya bure.
Nilichukua miti kadhaa jambo la harakaharaka huku nikiwa na ujasiri wa hali ya juu sana niliipanga kwa chini yake kisha nikaisukuma na likatambaa juu ya miti ile ikawa kama kiterezeshi.
Nilifanikiwa kulitoa hadi nje na kuona bahari ilipo. Nilifurahi sana na nikajua sasa nyumbani napaona japo sijajua nyumbani ni upande gani. Nikaipanga tena nikatumia nguvu zangu zote likatereza hadi sehemu ya maji yalipoanzia.
Wakati nafika kwenye maji wale viumbe wanaingia maeneo ya ufukwe yale kutoka ndani ya kisiwa.
"Ooooh!! Jamanii mtumbwiii haraka kwendaaa!!"
Niliufosi mtumbwi kusonga kwenye maji kwa maneno nikiamini ndio njia ya pekee kwangu ya kuondoka pale.
Ndani ya mtumbwi au Dau lile bado ile maiti ilikuwepo iliendelea kutoa harufu kali lakini sikujali bola ya hayo kuliko mimi kubaki pale na kuuliwa na wale viumbe.
Nilishukuru kuufikisha kwenye maji, kwa sababu najua ujanja wa wale viumbe huwa hawawezi kugusa maji kabisa.
"Shenziiii!!! Mnadhani mtanipata marabuuku mimi ndio Mnali baba yake Asante sasa nyinyi viumbe mtakula kwa macho".
Nilijitapa sana pale kwa madaha bila hata kujua jambo la mbele baada ya kumtukana mamba kabla ya kuvuka mto.
Jamani haya mambo yaacheni nahadithia kama mazuri ya kufurahisha ila inahuzunisha kwani, nilitembea kama hatua tatu za mguu ndipo nikaona kwanza niondoe ile maiti imezidi kunitia woga, ile naondoa kumbe ndio ambayo ilisaidia kuzuia maji kupenya. Kutokana na ule mwili kukaa kwa muda mrefu uliozesha mpaka mtumbwi kwa chini lakini maji mwanzo hayakupita kwa kuwa ulikamatana na ule mwili.
Baada ya kuuondoa ndipo maji yakaanza kuingia kwa kasi, niliduwaa sana kama kifaranga asiekuwa na mama vile.
Ndipo ikanijia kumbukumbu kuwa nimefika pale baada ya watu wa Paul kutoboa Boti langu na kupitisha maji kama vile.
Chozi lilianza kunitoka 😭😭😭 moyo wangu ulipwita kwa hofu kubwa sana hivyo nikajua sasa sina jinsi inabidi nitoke kwenye mtumbwi na kuuacha ukizidi kujaa maji na kuzama taratiiibu.
Hiyo ndio inaitwa Usitukane mamba na mto hujavuka. Njaa ilinigonga sana kiasi hata nguvu zilinishia. Nilikaa kwenye maji yale huku nikiwaangalia vile viumbe vya ajabu.
Ningejua ningewakubalia wale jamaa kuwafanyia kazi zao naamini haya leo yasingetokea, lakini kwa nini wanionyeshe roho ya kutu kama hii lengo lao kuniua sasa jamani daaah!!! Uvuvi wangu mdogo tu unanipa shida kama hizi leo nakutana na viumbe hata siwajui je wangapi wanawafahamu hawa.
Ilipita kama majira kadhaa jua likiwa katikati, lilinifanya nioene mwili unachemka kwa joto kali sana.
Hatimae sijifahamu kabisa baada ya kuona naanguka kwenye yale maji kwa kukosa nguvu, macho yangu yalipoteza nuru na kiza kikitanda.
Sauti za wale viumbe zilitawala masikioni mwangu sikujua kama wanakuja kunichukua au nini. Ndipo nikapoteza fahamu na sikufahamu kipi kilifuata. Nakuja kushtuka ni baada ya kujiona nipo kwenye moja ya kajumba fulani cha miti nikiwa nimelazwa. Nilikurupuka na kukutana uso kwa uso na binadamu ambae kajichanjachanja kama wale wamakonde wenyewe wale.
Alininyooshea mkono usoni kwangu kama trafiki anaposimamisha gari kwa kuonyesha kiganja chake. Nilibaki kuduwaa nikiikodolea ile mikono. Basi nilirejea kuegemea lile tawi ambalo limejengewa kama nyumba fulani hivi.
Yani huwezi kuamini niliapa mimi mwenyewe huku chozi likiwa linanitoka "yani nikifanikiwa kutoka huku bwana Paulo atanieleza".
Ajabu zaidi ni pale nilipohisi maumivu makali sana maeneo ya tako langu la kushoto. Jamaa akanivua suruali nikagoma khaa!! Huyu vipi anivue suruali mimi mwanaume pumbavuuu unataka uni nini mimi nyooo!.
Nilimuangalia kwa jicho la kumtamani kumtafuna ila sikuwa na jinsi nipo kwenye himaya yake, alilazimisha kunivua suruali nikagoma daaah!!! Nilipokea kofi la shavu nikatulia tuliii,
Akanivua akanigeuza, nilipeleka mkono wangu na kupapasa pale nilipohisi maumivu kumbe kuna kidonda kama shimo hivi.
Akaniweka dawa gani aiseee nilipiga kelelee akanitwanga vidole vya shingo sehemu za mshipa uliokuwepo karibu na sikio nikakata moto.
Nakuja kushtuka maumivu yanazidi kuwa makali nilijigeuza na kuona kweli kulikuwa na jeraha ila sikufahamu limetokana na nini?.
Kingine huyu jamaa haongei kabisa na hapo ilikuwa kama saa za jioni.
Nilimuona mbali kidogo akifanya shughuli zake. "Ina maana huku wanaishi watu kweli?, au huyu jamaa ndio walewale maana ila kawa msaada wangu tosha". Ilipofika majira ya usiku ndipo naisikia sauti ya huyu jamaa.
"U..u..unaitwa..na..ni?"
Nilishangaa kuwa umbe anaongea ila kama kigugumizi hivi
"Khaaa! Unasemaje?"
Nilizidi kumuuliza mpaka akachukia sana na kumuona kakasirika.
"Oooh! Samahani mimi naitwa Mnali"
Alitikisa kichwa
"U..u...k..u...umel..etwa na.. nani?"
Daaah! Aisee hiki kisanga ilibidi nilazimishe kumuelewa hivyohivyo anavyotaka.
"Mimi sijui nani kanileta, nilipata ajali kule ng'ambo nikazama majini nikajikuta natokezea huku alafu nawakuta watu wapo huku wadogoooo wanakula nyama mbichii..."
Nilikuwa namuelekeza na huku najitahidi vitendo kumuambia.
"Po...le..nak..wenda...kula"
Aliposema hivyo kuwa pole alafu anakwenda kula aliruka kutoka pale juu ya mti hadi chini akatokomea. Daah!!! Sasa anaenda kula mimi nakula wapi na nitakula nini?.
Aliporejea alikuja na nyama mbichi pale. Akanikabidhi. kwa kuwa nilianza kumjua tatizo lake la kuongea nikamuuliza.
"Moto uko wapi tuchome ili tutafune?"
Nilimuuliza kama mara tatu hakunijibu ndipo alinionyesha kwa vitendo tu.
Akachukua kipande chake akaanza kutafuna jamaniii
"Tobaaaaaaaaa!!"
Yani na mimi nile nyama mbichi....

TUKUTANE TOLEO LIJALO.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa