ENDELEA......
.......Nilishtuka mno baada ya kuona zile taarifa za kuonyesha kuwa mimi nina ugonjwa wa UKIMWI. Si peke yangu bali hata Salha ile taarifa iliweza kumpa mashaka sana kilichoweza kuendelea ni mshangao tu ndio ambao ulitawala kati yetu kujiuliza kwa nini hawa watu wameweza kunizushia vitu vya hatari. Ilipita kama wiki hivi mimi nikiwa ndani ya nyumba ya Salha Daktari mzuri sana, ukweli sikuwa nafahamu baadhi ya vitu vingi kwani akili yangu nilishapoteza kabisa kumbukumbu.
Siku moja nikiwa mezani nyakati za usiku mimi na Salha tunasubiri chakula kiweze kuiva ili tupate kula, chakula hiko kiliandaliwa na mfanya kazi wa ndani humo. Salha alikuwa ananitazama sana kiasi mpaka mimi nilishindwa hata kumuelewa kwa nini ananitazama kiasi kile.
"Mnali, samahani kama nitakuudhi nahitaji kukuuliza swali". Nilimkodolea macho wakati huo nimeacha kwa kile nilichokuwa nakifanya nimsikilize yeye, ila kwa muonekano nilimuona kuwa hakunielewa kwa kile alichosema ikambidi aweze kurejea ile kauli yake."Mnali, naongea na wewe mbona unanikodolea macho! Naweza kukuuliza swali?".
Hapo nilikohoa kisha nikaongea "Ukimya wangu una maanisha kuwa ongea nipate kukujibu" alicheka kwanza "Mh! Yani wewe una vituko sana, eti tukiachana na maswala ya matatizo uliyonayo je kwa upande wa maisha yako ya kawaida wewe ni nani zaidi". Nilivuta pumzi kwani swali ambalo alikuwa anauliza nililiona ni jepesi sana.
"Mimi hapa ni Mvuvi" niliweza kumjibu kwa kujiamini kuwa kazi yangu ni ya uvuvi. "Haya unafaidika na nini kupitia kazi hiyo unayoifanya?". Aliuliza kwa mara nyingine.
"Mh! Faida ninayoiona ni kuwa napata samaki pia naendesha maisha yangu kwa njia ya Uvuvi". Alifurahi sana kusikia hivyo. Muda mchache chakula kilikua tayari na sisi maongezi yalikuwa yameishia pale. Ghafla mwili wangu ulianza kuweweseka baada ya kuona nyama zilizopikwa zipo pale mezani, mate yalianza kunitoka mithli ya mbwa koko anaetamani mnofu lakini kupata hawezi.
Salha najua alinishangaa sana kutokana na ile hali na mimi nilijitahidi kuweza kuficha udhaifu wangu au matatizo yangu ili nisije gundulika mapema mbele za wale wenye kunipa msaada japo sikufahamu ile kauli ya wahenga kuwa ( Mficha Uchi Hazai ). Baridi lilianza kunishika kwa kasi sana alafu misuli yangu ya miguu ilianza kunishika sana huku ikivuta kwa kasi ya ajabu kama tu aliyekamatwa na ugonjwa wa Ngili. Mambo yalianza kubadilika pale mezani. Harufu ya ule wali ulianza kunichefua kisha nikatapika kabisa pale sakafuni.
Salha na yule dada mfanya kazi walihaha huku na kule ili kunisaidia binadamu mwenzao, Salha nilimsikia akiwa analia sana huku akilalamika kuwa nini kimenikuta, ndipo ghafla sikusikia sauti yake tena pale sebuleni zaidi ya yule mwenzake, punde Salha namuona akitokea chumba cha karibu na sebule akaja pale nilipo.
Nilisikia kitu kikiingia mkononi mwangu kichungu sana kumbe ni sindano. Nilipoteza kabisa nguvu na kulala palepale, kwa mbali nahisi kama nabebwa hivi alafu naachwa mahali kumbe nilikuwa napelekwa kitandani.
Majira ya usiku nilinyanyuka ilikuwa kiza totoro, nilipapasa kitandani nikahisi kama kuna mtu yupo, nilinyanyuka polepole kwa kuwa niko kawaida kabisa.
Nilinyanyuka kisha nikatua miguu yangu juu bila hata kumgusa yule aliyepo kitandani kwa kuwa sikuwa namfahamu hapo mwanzo. Nilipapasa ukuta ambao nilijua kuwa swichi niliyoelekezwa kuwa ndipo pa kuwashia nilibonyeza lakini umeme haukuwaka kabisa.
Hakika nilichoka sana nikabaki nimeduwaa pale natafakari 'hivi hii hali yangu wapi inaelekea ina maana kuwa nitabadilika moja kwa moja kama wale viumbe?, lakini tofauti na hilo kwa nini yule jamaa kule kisiwani aliniambia nisije kumueleza yeyote kuwa kile kisiwa kipo kule na kuna wale viumbe? Je? Nimueleze huyu dokta apate kunisaidia au nikae hivihivi nikiuficha ukweli wangu?'.
Wakati naendelea kutafakari ndipo umeme ukawa umerejea. Macho yangu ya kwanza ni kupeleka kule ambako yupo yule mtu pale kitandani. Ndipo naiona sura ya Salha.
Nilishtuka nikajiuliza kwa nini yeye alikuja kulala pale kitandani kwangu. Wakati huo akili yangu ilikuwa kama imepumbazwa hivi na yale matukio ya kila mara kwenye mwili wangu. Tumbo lilianza kudai chakula na wakati tangu usiku sikula kutokana na yale majanga niliyoyapata. Niliamua kuufungua mlango kwa upole sana. Nikazipiga hatua kadhaa kisha nikaelekea maeneo ya jikoni. Chumba hiko cha jiko kulikuwa na kila aina ya chakula vyakula vingi vilikuwa vimehifadhiwa kwenye Mafriji.
Niliwasha taa kisha nikaanza kufunua sufuria moja baada ya jingine. Ghafla pua zangu zilianza kuchezacheza, zikitanuka na kupata harufu ya nyama iliko, nilijilazimisha kutoitaka hiyo harufu lakini wapi ilizidi kunipanda kwenye akili yangu. Hatimae nilisonga kule ambako iliko moja kwa moja hadi kwenye Friji moja nilifungua nikakutana na nyama ambayo iliwekwa ili isioze ilikuwa bichi. Akili yangu ilibadilika kabisa na nikajihisi mtu tofauti maana mpaka mate yalianza kunitoka. Nilijifosi kutochukua lakini acha tu nilipata tabu sana, nikachukua kipande kimoja nikakitafuna na kingine na kingine mpaka kingine.
Hapo ndipo hali ilirejea kabisa. Lakini nilijiona mtu mwenye nguvu nyingi sana alafu hisia za mwili zilianza kunitawala. Kila kiungo changu kilikuwa na hamu ya kufanya kazi, mikono yangu ilitamani hata kuvurugavuruga vitu vilivyomo mule ndani, miguu yangu iliwasha ilitamani hata kukimbiakimbia. Pia sehemu zangu za siri nazo ndio usiseme nilijichafua kama mara mbili hivi.
Nguvu ya Uume wangu ulikuwa mara dufu na kawaida. Nilijilazimisha kutoka na kurudi kule chumbani lakini huku jikoni sikuweka sawa kama nilivyokuta mwanzo.
Nilichojua ni kujifuta tu ile harufu mdomoni. Kama nilivyokuambia kila kiungo kilihitaji kufanya kazi yake vile ipasavyo, nilimkuta bado Salha akiwa kalala huku kajifunika shuka akiacha kichwa tu. Salha nadhani alikuja lala kule kutokana na hali yangu kuwa mbaya wakati ule wa usiku. Mimi tayari akili yangu inanituma niweze kumuingilia kimwili Daktari huyu aliyejitolea kunipa msaada.
Niliweza kumfunua ile shuka na kumkuta akiwa kama alivyozaliwa na wakati huo taa ilishawashwa. Akiwa anajizungusha kama kujinyoosha ndipo na mimi akanifanya niwe chizi zaidi. Hapo nafahamu sikuwa na akili yangu mwenyewr ila kama nilikuwa naendeshwa tu. Nilivua nguo zote nikabaki kama nilivyozaliwa haki ya nani sehemu zangu nyeti zilisimama kama mchongoma.
Nilimshika mguu ndipo Salha akashtuka alipoamka anakutana na mimi niko kwenye hali ile.....
ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜
Jamani Inauma sana sifurahishi ila yasikukute...
TUKUTANE TOLEO LIJALO




No comments:
Post a Comment