RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA KUMI NA NE 14 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, January 23, 2020

RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA KUMI NA NE 14





ENDELEA......
........Nilimkodolea Macho huku akiifakamia ile nyama, Aiseee nilishindwa hata kuila nikaiacha chini ndipo ilipodondoka chini.
Jamaa alinyamaza hata kuongea kabisa hakutaka hata kusema neno lolote. Kwa kuwa nilikuwa naumwa sana na sikujua nini kimeniumiza kwenye moja ya kalio langu.
Bwana nikajilaza pale huku nikiwa simuamini kabisa pia natafakari juu ya maisha ya yule jamaa. Ilikuwa usiku sana niliposhtuka baada ya kusikia vile vibwengo vikiwa vinapiga kelele pale chini. Nyumba au kibanda cha huyu jamaa ilikuwa juu ya mti mkubwa sana ambao ulikuwa na matawi mengi sana. Jinsi alivyokuwa ameijenga alifahamu mwenyewe, basi wale viumbe walizidi kupiga kelele za ajabu, nilichungulia chini na kuwaona wakiwa na macho yenye rangi nyekundu yalikuwa yanang'aa sana, hakika niliogopa kiukweli.
Nilianza kuhaha pale lakini nilichoshangaa yule jamaa alikuwa kimya hana hata dalili ya kulala alikuwa anawasikiliza tu. Mpaka asubuhi naamka pale kidogo nilijihisi vizuri kiukweli maana maumivu yalipungua kiasi hata kusimamisha mguu niliweza kwa kweli. Nilipata kujiuliza maana akili yangu tayari ilishanijia kutaka kuondoka pale.
Sikumbuki kule kisiwani nilikaa kwa muda wa wiki au masiku mangapi ila nilichukua muda mrefu nilichojua ni jua kuzama na kutokeza giza kutoka na kuingia yani wengine wanasema ukawa usiku ukawa mchana. Katika hayo masiku ambayo niliweza kukaa mule msituni hadi pale nilipozoeana na yule jamaa. Historia fupi ya yule kijana iliweza kunisisimua mpaka nikaanza kunitoa machozi.
Ila mpaka anafika hatua ya kuhadithia kwanza nilifanya kazi kubwa ya kumfundisha lugha ya vitendo, kwa kuwa hakuweza hata kuongea kwa muda mrefu zaidi ya hapo hasira itamshika na kukaa kimya tu.
Aliniambia na yeye alikuwa anafanya biashara zake za kawaida kipindi cha zamani sana kwa upande mwingine tofauti na ule ambao mimi nilitokea, katika shughuli zake alijikuta anaingia kwenye hatari kubwa sana baada ya kushawishiwa na wakongwe wa mji yani vile vibosile kuwa kuna mali mahali fulani kwenye bahari.
Walimuomba huyo jamaa sana kwa kuwa kidogo ana ujuzi wa kuogelea waweze kwenda nae kisha wakifika eneo ambalo walisema kuna mali basi yeye aingie chini ya maji kisha achukue wagawane kwa pamoja. Ndipo siku ya siku ikafika na watu wakajiandaa ili kwenda kuchukua mzigo ndani ya bahari. Huyo jamaa alibebwa japo ni mara yake ya kwanza kufanya kazi na tajiri huyo ila aliona jambo la kheri kwake kufanya nae ili aweze kupata chochote kitu.
Safari ya boti ilianza pale hadi maeneo fulani hivi ndipo boti likasimamishwa kwa ajili ya kuifanya kazi yao. Jamaa huyu aliingia ndani ya maji hadi pale alipoelekezwa na kweli alikuta sanduku kuukuu la zamani sana lakini kulibeba alishindwa kutokana na uzito na kukamatiana na udongo wa chini pale. Aliibuka na kuwapa taarifa kuwa ameliona ila hana nguvu ya kulichukua, ndipo ilibidi itumike njia mbadala ambayo ni kuchukua ndoano kubwa kama nanga na yeye kwenda kuivalisha kisha wao kuivuta hadi juu.
Mafanikio yao yalizaa matunda sasa jambo la ajabu sana pale tu yule tajiri anavyobadilika kama kinyonga kwa kumbadilikia jamaa huyu huku akimuambia kuwa pale hana chake, alijitetea kwa kusema yeye ndie kaingia je? Angewapa taarifa kuwa halipo au angekataa kuja.
Japo kauli hiyo haikuwafanya wao kuacha kumcheka na kumtisha huku wakitaka kumdhuru. Jazba na hasira za kudharauliwa ilimfanya kutaka kulishika lile sanduku ili kulitupia mulemule, lakini walimshikilia huku wakimtundika makonde ya nguvu, jamaa hakutaka kuachia mpaka pale damu zinamvuja kwa wingi lakini alilishikilia kwa nguvu zake zote na kulisukuma mule ndani ya maji. Baadhi ya wale matajiri waliogopa kwa woga hawajui kuogelea pia kupoteza lile sanduku walioamini kuna mali, moja wa tajiri ambae alipigana sana kumpiga jamaa ni mzungu aliyefanya utaratibu wa kugundua kama yale maeneo yana mali zilizoachwa kwa kipindi kirefu sana. Lakini mpaka jamaa anapigwa ngumi ya koo alilegea kisha akadondoka na lile sanduku ndani ya maji, lakini pia alijitahidi kwa zile nguvu alizonazo mpaka kulifikisha mahali pengine kabisa na kuliachia.
Liliingia ndani chini kabisa ya bahari, na yeye akapoteza fahamu. Mpaka siku anajiona yuko hai yuko pembezoni mwa kisiwa wakati huo kang'atwa na wale viumbe ambao mimi wamenibana. Anashangaa lakini ilimbidi kuendana na masiha yale aliyonayo.
Kila siku anabadilika na kupenda kula nyama mbichi mpaka pale alipofikia.
Daah! Alikuwa ananihadithia lakini mimi pale chozi lilianza kunitoka kwa wingi.
Nilijua kuwa mwenye matatizo ni mimi Mnali peke yangu kumbe kuna watu wana matatizo zaidi yangu daah! Ama kweli Mtazame aliye chini yako ili umshukuru mungu kwa kichache ulicho nacho, ila usimtazame aliyejuu yako usije kumkufuru mungu kwa nini hajanipa.
Hapo ndipo nikapata nguvu sasa ya kujua naishi vipi pale. Ila nilimuuliza jambo moja.
"Ina maana baada ya wale viumbe kukung'ata ndio wamefanya sasa uwe unatafuna nyama mbichi?".
"Ndio..baada ya kuning'ata ndio nilianza kuzipenda sana nyama mbichi".
Daah! Nilijishtukia sana.
"Ehee! Kwa hiyo mimi hili jeraha nimelipata kwa kung'atwa au?"
"Ndio.."
"Tobaaaaaa!!, kwa hiyo na mimi nitaanza kutafuna nyama mbichi"
"Ndio..ila dawa niliyokupa itakuzuia kidogo hutotafuna kwa kiasi kikubwa kama mimi"
Jamanii ina maana nimeathilika na hali ya wale wanyama kweli.
"Sasa unaweza kunisaidia mimi kurudi nyumbani kwetu?"
"Ndio utarudi ila unisaidie kitu kimoja"
"Kitu gani?"
Nilimuuliza
"Nataka tukachukue lile sanduku, kisha ufike nyumbani baada ya kukupa maelekezo ndipo ukirudi utakwenda kwenu".
"Sasa kwa nini niende peke yangu? Bora twende sote".
Lakini mwisho wa muda tulikubaliana kuwa tukatafute lile sanduku kisha mimi nirejee nyumbani ndipo nipange safari ya kurudi hadi upande wa pili wa bahari kwao kufanya kile alichoniambia.
Ghafla anapita swala karibu yetu ndipo akaniziba mdomo, alitembea taratibu sana hadi akamrukia na kumkamata pale. Muda mchache alimrarua vibaya mno na kuanza kunyonya damu yake kisha akamleta pale kwangu.
Ukiangalia nina kiu ya maji haswaa na yeye ndio anasema kuwa damu ya wanyama ndio maji yake kule hakuna kitu chochote zaidi ya vile afanyavyo. Niliinama na mimi nikajikuta nina hamu ya ile damu maana kama nimeathirika hivi, mate yalinitoka huku nikitamani ile nyama.
Niliinama na kuanza kuchukua mnofu na kuuweka mdomoni daaah! Nilitafuna ila kumeza nilishindwa nilificha tu mdomoni na kutema. Nilipata wazo kuwa nitafute mwanzi mkavu mkubwa, nilipoupata nikauvunja kati kwa kati kisha nikaulaza chini, nikakata kijiti cha mwanzi uleule kisha nikanza kusugulia pale kwenye mwanzi mkubwa penye uwazi mkubwa uliopo.
Wakati huo nyasi nimezisogeza, jamaa alikuwa ananiangalia sana kile ninachokifanya. Hadi moto unatokea anashangaa kwani hakuwahi kufikilia kitu kama hiko ndipo wahenga wakasema "Ukijua hili, mwenzako anajua lile".
Niliweka kuni pale moto ukawa mkubwa ndipo ule mwanzi nikaufanya kama kisu maana nao unajitahidi kwa makali.
Nilikatakata nyma ambazo ziliwezekana, kisha nikazibanika sehemu kwenye mjiti mkubwa kisha nikawa naongeza kuni. Sikujua ilichukua masaa mangapi, zilikuwa tayari ndipo nikampa atafune kwanza.daah! Alifurahi sana ndio ikawa chanzo cha jamaa kuacha nyama mbichi.
Sikujua ni siku ngapi zilipita tena mpaka ile siku majira ya usiku ananipeleka sehemu ambayo kulikuwa na boti nzuri kidogo hivi ambayo iliwezekana kunitoa pale. Niliweza kutumia nguvu tu kuisukuma ile mashine maana hata mafuta haikuwa nayo.
Safari sasa ilianza mimi na jamaa kuelekea yale maeneo husika. Tulipofika ndipo akaniomba nitulie kwanza aliniambia kuwa anaenda na kamba akiifunga basi ataitikisa kisha mimi niivute tu.
Kweli muda tu aliingia humo kisha baada ya muda kidogo akaitikisa kuhashiria kuwa niivute sasa. Niliivuta ilikua ni nzito sana kupindukia. Nilivuta hadi inafika juu kweli ni sanduku dogo hivi la zamani. Nilibaki kumsubiri atokee lakini kimya. Nilisikitika sana baada ya kupita masaa mengi jamaa hajatokea, nikajua kuwa kajitoa maisha yake kwa ajili yangu pia nilimshukuru sana.
Nilitoka pale mdogomdogo kutafuta eneo ambalo nilitokea. Safari yangu ilikuwa ndefu sana mpaka njaa ikanikuta. Hali ya mwili wangu ilibadilika sana pale nilipokuwa natamani sana nyama mbichi, nilijilazimsha kukataa yale mazingira lakini yalinizidi, hadi sasa nikafanya mpango hata kuwakamata kwa kuwachoma na mjiti wale samaki waliokuwa wanafuata nyuma kama wanacheza.
Nilibahatisha mmoja na kuanza kumtafuna vilevile. Ilitulia kidogo. Mabadiliko ya mwili wangu sikujua yanaenda kufikia wapi. Nilitembea usiku na mchana hadi siku nabahatisha kuona ufukwe kwa mbali sana watu wakiwa wamefurika.
Sikufahamu nini kilikuwa kinaendelea pale, nilichohitaji mimi kufika nyumbani kwangu kwanza. Nilihisi kama nitajulikana kwani nilifahamu kuwa watu wengi wanajua kuwa nimekufa ndani ya maji kama Kibona. Nilisubiri ifike usiku ndipo niweze kuingia mjini kwangu.

Itaendelea........



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa