RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA KUMI NA MOJA 11 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, January 23, 2020

RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA KUMI NA MOJA 11






ENDELEA.....
................Niliona wanalazimisha ikawa sio kesi acha mimi niende nikawasikilize. Nilitrmbea mdogomdogo kama wimbo ule wa Msanii wa Tanzania Diamond Platnum hadi pale kwenye gari nikiongozana na yule jamaa.
Niliishia nje ya gari sikutaka kuingia kwa kuwa nanuka shombo ya samaki pili sikuwa na uhakika na wale majamaa wanaojiita matajiri.

"Ndugu yangu, nimekufuatilia sana tangu kipindi kirefu ila nahitaji msaada wako"
Nilimshangaa kuniambia anahitaji msaada wangu yani mimi leo niwe mtu wa kumsaidia mwenzangu.
"Khaaa! Msaada gani ambao unahitaji kutoka kwa mtu kama mimi?"
Walicheka sana kisha wakatulia
"Kwa nini unajidharau sana"
"Lazima niwe nashangaa kwa sababu watu kama nyinyi wakubwa ndio wa kuwasaidia wengine kama sisi tena sisi tuwasaidie nyinyi hivyo vichekesho".
"Hapana haya tuongee biashara sasa"
"Biashara?"
"Ndio"
"Biashara ipi tena".
Ghafla niliona wakinizunguka kwa haraka vijana kadhaa kama watatu hivi.
Walinishika na kunisweka ndani ya gari, gari lile liliwashwa haraka na kuanza kuacha sehemu za bahari na kuelekea barabara kuu ya kuelekea mjini.
"Nyinyi vipi sasa mnanikamata?"
"Utajua huko mbele si hutaki kuelewa unaleta kiburi ngoja tufike mahali utuelewe vizuri zaidi tena kwa haraka".
"Ila kwa nini sisi mnatuonea hivi "
Hawakutaka kunisikia tulitembea umbali kidogo hadi kwenye shule moja ya watu binafsi kisha likasimama.
"Sikiliza, tumekuleta huku kwa maana. Mr Paul anahitaji mzigo mkubwa sana Hoteli yake inataka kufa kutokana hakuna upatikanaji wa samaki wa kutosha, vijana waliokuwepo hawawezi kukidhi mahitaji ya pale. Sasa tunataka wewe urudi tena pale".
Kila neno alilokuwa analiongea liliniingia masikioni vizuri sana na kunipandisha hasira.
"Yani kunitisha kote huko mnilazimishe kufanya kazi zenu?"
"Ndio utafanya au hufanyi"
"Sasa..."
Kauli yangu ilisitishwa na mlio wa gari uliokuja pale watu kadhaa wakatoka waliovalia suti ndipo namuona bwana Paul anaingia kwenye lile gari nililopo mimi akakaa mbele yangu huku nje baadhi ya vijana wakirandaranda.
"Mnali habari za siku"
"Safi"
"Karibu tena"
"Wapi?"
"Teh teh teh! Unanichekesha, ok! Manyota na Musa nataka niwafukuze hawafanyi kazi yeyote  ile na kilichonifanya hivyo ni baada ya kuona kuwa una mchango mkubwa sana na sitoangalia kigezo cha elimu wala nini kama elimu nitajitahidi utajua kingerez kuongea na wageni pamoja na hilo naongeza mshahara wako mara mbili ya pale".
Nafsi ilinisuta kutokana na umasikini nilionao. "Daaah! Ila hapana nipe nijifikilie".
Aliingia upande wa dereva kisha akatoka na boksi sikufahamu ni aina gani ya simu. Aliifungua na kuitoa simu nzuri sana hizi sijui wanaziita Smat poni sijui smatphone. Alinikabidhi.
"Hii ni simu chukua itakusaidia kufanya mawasiliano na mimi imesetiwa kila kitu".
Niliishika na kisha nikawa naiangalia sijui hata wanaitumiaje.
"Aaah! Mimi sijui hata jinsi ya kutumia". Walicheka kidogo.
"Hapana usijali wanafanya hivi..nimeitengeneza hii Whatsapp nitakuwa nakupigia huku tunaonana".
Alitumia kama nusu saa kunielekeza ile simu hadi nilipoikubali kuona dunia ilivyo. Walinisindikiza hadi karibu na nyumbani kisha wakaondoka kusubiri majibu yangu kama nimekubaliana nao.
Nilikaa sana pale kufikilia lile jambo kama kwenda kuwafanyia kazi au nitulie na shughuli zangu mwenyewe.
Nilipata majibu kuwa bora nifanye shughuli zangu binafsi sitaki kuwa chini yao kuwa mtumwa kila muda.
Nilipanga kabisa kuwa sitaki kwenda tena kule. Ilipita siku kama mbili nikawa nafanya shughuli zangu mwenyewe ndipo Mke wa Kibona alishindwa kuishi pale na ndipo akaondoka kabisa kwenda kijijini.
Nilibaki peke yangu huku nikiwa makini kila hatua ambayo naipitia. Siku moja nikiwa narudi nyumbani niliona nyayo za tairi la gari likikunjia pale nyumbani na kuondoka. Sikutaka kufikiria mengi sana.
Ile naingia ndani tu na gari hili linaingia, walishuka haraka sana vijana kama wawili. Waliniachia barua kisha wakaondoka zao. Nikiwa naendelea kuishika ile barua na sijui ni akina nani anakuja Manyota pale nyumbani. Manyota alionekana kuwa ana jazba sana kuliko kawaida.
"Mnali umeridhika si ndio"
Nilipigwa na butwa
"Umeridhika nilijua tu kuwa wewe ndio kila kitu na ni chanzo cha haya yote"
Alionekana ana hasira ndipo niliingia ndani kwanza nikachukua maji na kuja kumpatia anywe ili apunguze zile hasira.
Lakini kile kikombe alikitupilia mbali
"Manyota unaonekana hauko sawa tatizo nini lakini?"
Nilimuuliza
"Unajifanya hujui sasa hivi sisi tumefukuzwa kazi kule kwa bwana Paul"
"Mh! Mmefukuzwa kaziiiii!!!"
"Unajifanya kushangaaa sasa hivi wakati naliona gari la Mr paul hapa kwako kama mara ya pili inakuja na kuondoka na hapo umepewa ela nyingi na sisi tumetolewa ili wewe ukae pale sasa tunakuambiaje sisi ndio wazawa wa bahari tutakuharibia mulemule yani"
Aliondoka huku akiniacha na mkanganyiko wa mawazo.
Niliingia ndani kisha nikakaa kitandani na kuifunua ile barua ili nipate kuisoma. Nilipoifungua nikakutana na picha moja ya mwanafunzi nilipomuangalia vizuri alikuwa mwanangu Asante.
Niliifungua ile barua na kukuta maelezo kadhaa kuhusu ile picha.
""Mnali kama kweli damu ni nzito kuliko maji basi tunataka kuona jeuri yako. Mtoto wako muda wowote tunaweza kumchukua na kumpoteza ila angalia mwanao ana akili sana kumpoteza kiumbe kama hiki. Tunachotaka sasa ni amri tuletee mizigo kumi ya maana ya samaki laa sivyo nahakikisha anaangamia mwanao.
Fungua watsapp"".
Jasho jembamba lilinitoka pale huku mikono ikinitetemeka sijui hata nifanye nini.
Nilichukua simu kisha nikaangalia nakutana na video ambayo walikuwa wanaongea na mwanangu Asante.
"Unaitwa Nani?"
Naitwa Asante
"Ahaa baba yako unamuambia nini"
Baba Nampenda sana na nasoma vizuli na mtihani nimefaulu
Video ilikatwa hakika nililia sana sikujua kwa nini nafanyiwa hivi mpaka kwenye familia yangu inaingiliwa kwa kazi yangu ya kipuuzi ya Uvuvi daaah!.

TUKUTANE TOLEO LIJALO



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa