RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA KUMI 10 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, January 23, 2020

RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA KUMI 10





ENDELEA......
.................Nilipatwa na Mshangao sana maana si kwa hali ile. Kumbe kuna watu wananiandama hivihivi. Ila nilijipa Moyo kuwa nitashinda katika vita ya wanafiki na wale wasiopenda mafanikio ya wengine. Nilifika mapema nyumbani siku hiyo nikitafakari huku nikijitahidi kufikiri katika swala lile nyeti. Siku hiyo hata sikutaka kuandaa chochote kile kinachohusiana na mambo ya uvuvi nilisubiri jioni ifike niende kwa rafiki yangu akanieleze kisa na mkasa.
Kabla ya jioni nilifika kwa yule jamaa baada ya kwenda kutoa taarifa kwa Mke wa Kibona kuwa leo sitokwenda kabisa Baharini maana kuna jambo kama lile linanitatiza. Safari yangu iliendesha na hulka ya Moyo kupiga kwa kasi mapigo yake pamoja na nafsi kutamani kumjua na kujua mpango mzima wa hao watu wanaotaka kuniua.
"Haya, Mnali unafahamu kama hili swala ninalotaka kukuambia ni hatari sana japo linahusu kuhatarisha maisha yako?" Aliniuliza swali huyo rafiki.
"Aaah! Unajua ni kweli hatari ila naona hatari zaidi kwa mimi ninaetakiwa kudhuriwa". Nilimjibu huku nikimuangalia usoni.
"Ndio ila basi tuseme kuwa sisi sote ni hatari kwa wewe unaepangiwa kuuliwa pamoja na mimi".
"Mh! Kivipi yani".
Nilimuuliza
"Unajua kuwa mpango wa wewe kukuua ulianza muda sana kipindi upo na Kibona siku ambayo mulitakiwa kuuwawa wewe hukuwepo akawepo Kibona pekee. Nikisema ni hatari kwako ndio maana nakuambia ili ujihadhari kwa kuwa ni rafiki yangu na hatari kwangu kwa kuwa mimi ndio mtoa taarifa kwako ya haya mambo pindi wakifahamu nimetoboa siri hii".
Nilisikitika sana ila nilijikaza kiume nipate ukweli zaidi wa lile swala.
"Sasa kifo cha Kibona Kilikuwaje ".
"Daaah! Mnali kifo cha Kibona kiukweli kinasikitisha sana Mpango huo mimi nilishilikishwa kiulazima kwa kuwa niliwakuta wakiongea kuwa Kibona anapata samaki wengi sana kuliko kawaida, nilipowashtukia walinikamata na kutaka kuniua ila waliniomba kuwa niwe katika hilo kundi siku hiyo ilikuwa hivi..
Akiwa ana hadithia.
..Kibona alikuwa anasukasuka Nyavu yake huku akiwa anatumbuiza na nyimbo kadhaa. Ndipo akaingia Mzee Mmoja makamo ya Kibona kisha akakaa.
Waliongea machache ndipo yule mzee akamuuliza maswali kadhaa.
Kibona unajua siku hizi hali ni ngumu sana, ndio ni ngumu lakini hatuna jinsi ya kusema zaidi ya kujitahidi kupiga kazi kila siku., ndio ila kwa nini kwa upande wako baada ya kumpata kijana yule Mnali Mnapata Mavuno mengi sana kuliko sisi, khaa! Yani huwezi amini kabisa maana ananisaidia kila hatua, unajua kama huyu atakuja kukubadilikia, mh! Haiwezekani kabisa afanye hivyo namuamini. Ndipo yule mzee akasimama na kuondoka.
Mzee Kibona hakusita kabisa kuhusu yule Jamaa kuondoka kwa kutoridhika yale aliyojibiwa.
Muna roho mbaya sana nyinyi kama si binadamu maana kila siku nyinyi kuwangalia watu tu wanafanya nini.
Jioni yeye Kibona aliingia kazini huku akiwaangalia wengine hakuona watu kabisa. Naona leo watu wamechoka kabisa hakuna watu haya ngoja niingie, Kibona akiwa na Imani tosha anaingia ndani ya mtumbwi ndipo Mimi nikajitokeza nikiwa na hamu ya kutaka kumuambia kuwa anakokwenda siko kuzuri kwani wale vijana kadhaa wamejitega baadhi ya sehemu kule mbele.
Lakini nilimuacha aende maana niliogopa kabisa kuongea ili nisije kuuliwa na wale watu. Wakati Kibona akiwa anaelekea ndani kabisa baharini mimi nilirudi nyuma ambako baadhi ya vijana ambao walibaki kule nchi kavu.
Baada ya hapo ndipo muda baadae vijana walikuja ndipo wakaanza kuhadithia kuwa tayari wameshammaliza na wakamtumbukiza kwenye maji. Hapo ndipo habari ya Kibona iliishia na yote haya yalisababishwa na yule mzee ambae kakufanyia mpango wa kwenda kwa bwana Paul.
Alimaliza Kuhadithia.
Nilipatwa na kigugumizi huku chozi likinitoka baada ya kuhadithiwa kisa cha Kibona. Nilijikuta naondoka pale kisha nikapata na hasira kubwa sana baada ya kukipata kile kisa cha kuhudhunisha na sikutaka hata kumhadithia Mkewe.
Ilipita kama wiki hali yangu ilikuwa nzuri ya kimaisha nilifanya mpango wa kuanza kutengeneza nyumba mpya. Nilisimama kwa muda swala la uvuvi kwa kuogopa lile jambo na nilianza kuwa na hofu kubwa juu yao. Nikiwa usingizini niliota ndoto kuwa Kibona anakuja usiku na kuniambia maneno ambayo yalinifanya nishituke toka usingizini. "Mnali, usije kuogopa kuvua samaki kwa kuwahofia hao hapana wakijaribu kukufanyia chochote hakika kila mmoja lazima alipize". Nilishtuka kutoka usingizini majira kama saa nane.
Ile ndoto kwangu ilikuwa na maana gani na ilikuwa inanieleza jambo gani.
Sikupata hata lepe la usingizi nilikaa mpaka asubuhi.
Nilijihisi kama mtu mwenye hamu ya kwenda kuvua samaki. Nilifanya hivyo kwa kuwa nilikuwa na Mitumbwi kama sita mingine niliiweka ya kukodisha na mmoja nilitumia mwenyewe.
Mauzo ya samaki kwa upande wangu niliona kabisa yanafaida kubwa sana. Nikiwa baharini napita kuzunguka nione wapi naweza kutega kwani niliamua kubadili mazingira. Ndipo nikaliona boti likija kwa kasi kubwa pale nilipo niliogopa nikihisi labda majangili hawa wanakuja kunivamia.
Uwezo wa kuwakimbia sikuwa bao kwani mashine ya mtumbwi wangu haikuwa na uwezo mkibwa kama lile boti la kutengenezwa kutoka kiwandani.
Ndipo liliponikaribia na nikamuona Manyota na Musa wakipita na Nyavu zao, walisimama.
"Mnalii aaah! Afadhali sana tumekuona ndugu yetu"
Aliongea Musa.
"Unajua tangu utoke hatupati samaki wakubwa kama wale wa ile siku".
"Poleni"
"Ahsante sasa unaonaje tuvue na wewe alafu tunakulipa"
"Hapana mimi siku hizi nina wateja wangu ambao nawapelekea mizigo".
Nilishangaa wakiondoka kwa haraka huku wakisema Achana nae huyo atakufa masikini.
Narudi na samaki kadhaa ambao niliona wanafaa kwa siku hiyo maana bahari kidogo ilichafuka haikuwezekana kuwapata wengi.
Nilirudi hadi Nchi kavu na kuliona gari la kifahari likiwa limesimama na watu wengi hasa akina mama ambao walikuwa wanasubiri mzigo.
Niliwapatia kile ambacho walikuwa wakikisubiria lakini nilihisi kama mtu ananifuatilia kimyakimya pale nilipo. Nilipatwa na woga sasa. Baada ya kumaliza nilitaka kuondoka ndipo akanigusa begani yule niliyekuwa namhisi.
"Kijana Unahitajitajika na tajiri kwenye lile gari".
Nilishangaa maana nilidhani kibaka au wale waliopanga kuniua.
"Tajiri nani?"
Nilimuuliza
"Kijana unapata bahati unachezea twende utamuona".
Nilihisi kuwa hakuna salama unajua ndugu msomaji Nilifanyaje?.....

TUKUTANE TOLEO LIJALO



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa