ENDELEA.....
.......Nilibaki kuhemea ndani ya chombo changu huku nikisubiri muda wa kutoka pale, nilipanga kusubiri mpaka pale usiku utakapoingia ndipo na mimi niweze kuondoka zangu.
Kila dakika zilivyokuwa zinazidi kwenda na mimi hamu ya kula nyama mbichi ilizidi japo kuwa nilishakula kabla na sikutamani kabisa kula tena maana nilihisi na mimi tayari nitakuwa mmoja wa wale vibwengo kule kisiwani.
Pia nilipata kujiuliza maswali mengi ikiwemo na lile la kula nyama mbichi itakuwaje kule ambako naelekea kuishi na watu ambao mambo hayo ni tofauti kabisa. Pia swali hilo lilitoweka baada ya kujiuliza kuhusu lile sanduku lina nini ndani yake?.
Majira hayaongopi yalitembea na kufikisha majira husika yale ambayo niliyataka. Usiku ulipoingia ndipp nikaanza taratiibu kutoka, zile kelele ambazo nilikuwa naendelea kizisikia ziliendelea kuzidi na si kitu kingine ni Mziki.
Nilikwepesha kidogo na yale maeneo ambayo wao wapo pale, nilipofika karibu na ufukwe ndipo nikatoka ndani ya mtumbwi na kuanza kutembea taratiibu. Mwendo wangu ulikuwa mpole na wenye wasiwasi sana. Mwili wangu uliendelea kutetemeka meno yangu yalizidi kugonganagongana huku mate ya uchu wa nyama yakivuja.
Nilipofika sehemu zile zenye mchanga nilishangaa kuwaona wanawake na wanaume wengi sana, mambo yalikuwa tofauti na yale ambayo mwanzo niliyaacha. Kwanza nilikuta kama vijimba vimejengwajengwa hivi, na kama miamvuli mikubwa ipo na watu wa kila aina pale walikuwepo.
Nilitoka sasa nikaitafuta njia ya kwenda nyumbani kwa kuwa kumbukumbu nilikuwa nazo hapo awali. Nilifika hadi nyumbani nikakuta nyumba yangu ipo na kufuli mbili kubwa wakati huwa sina hata tabia ya kugunga kufuli kubwa tena mbili. Nilifanya jitihada hata kuvunja mlango lakini nilishindwa ndipo nikapitia dirishani.
Nafika hadi ndani hakika sikupaelewa kabisa kwani pamebadilika sana, vitu vilikuwa vimekaa shaghalabaghala. Nikiwa bado nimeathirika na ile hali ya uhitaji wa nyama sana nilijikuta najifosi kutafuta kokote kule iliko japo nilishindwa na kulala. Nilishtuka asubuhi baada ya kupatwa na usingizi wa ghafla.
Nje nilipata kusikia sauti za miziki ikiwa inaendelea kulia tena karibu na nyumbani kwangu pale nilipo, nilitoka taratiibu na kufungua mlango kwa kuugonga na nyundo ambayo ilikuwemo ndani humo. Nilifanikiwa kuvunja na kutoka nje.
Mtu wa kwanza kumuona machoni mwangu alikuwa mama mmoja ambae namfahamu vyema alikuwa mteja wangu sana wa samaki. Alivyoniona hakika alishtuka sana kwani sijajua kuwa alinifikilia kama mtu wa aina gani pale.
Ila mawazo yangu ya kwanza nilijishika kichwa nikihisi kuwa labda na mimi nimebadilika na kuwa kama wale viumbe ambao walikuwepo kule kisiwani, walikuwa na vichwa vidogo kweli hivyo nilijishika kuhakikisha kama na mimi nina kichwa kama chao ndio maana ananikimbia kumbe ni tofauti kabisa na mafikilio yangu.
"Jamaniiiii njooni! Njooni mumuone Mnali karudiiiiiii"
Alikuwa anaongea maneno mengi, nilibaki kushangaa kwa nini alafu alikuwa ananikimbia sasa. Nilivyoona kuwa wale watu wote wa pale kwenye sherehe walitoka kuja nyumbani kwangu ndipo nilipoingia ndani na kufunga mlango.
Nilipatwa na wasiwasi nikijiuliza mimi nimepatwa na nini mpaka wananishangaa?, sikuwa na majibu zaidi ya kubaki na kuwasikiliza wao wanaongea nini. Nilibaki kuwasikiliza kwa nje wakiwa wanaongea.
"Hivi, mnamjua yule Mvuvi mzuri aliyekuwa analeta samaki wengiii!!" Mtu mmoja aliuliza mwenye sauti ya kike.
"Ndio tunamjua"
"Ehee"
"Ndio hivo nimemuona kwa macho yangu haya mawili kwenye nyumba yake hii".
"Acha uongo Mnali umuone wewe si utani huu, tusimuone sisi ambae tumezunguka bahari umuone kwenye nyumba hii".
Mpaka pale nikajua kuwa kuna watu walikuwa wanafanya jitihada za mimi kunitafuta. Nikiwa bado nipo ndani ndipo nasikia kauli ambayo ilinivunja moyo kabisa.
"Lakini jamani si ilisemekana kuwa Mnali kafa huko baharini iweje leo museme mumemuona inakuaje tena hapo?"
"Ndio ebu lakini kama yumo ndani tufungue kwanza ili tujue kama ndie yeye au laah!"
Nikiwa ndani humo najisikia hali mbaya ya mwili natamani kutapika kutokana na kichefuchefu nilichonacho.
Muda mfupi niliona mlango ukisukumwa taratiibu na mwanga wa jua ukiingia mule ndani. Nilibaki kuduwaa pale ulipokuwa wazi na kuwaona watu wakinishangaa sana.
Nilinyanyuka ndipo watu wakaanza kunikimbia pale, nilipatwa mfadhaiko mkubwa lakini nilipata fahamu kuwa wengi wao wanajua kuwa mimi nimekufa baharini ndio sababu tosha kuwa wananikimbia. Haikupita dakika hata kumi na tatu gari la polisi linaingia palepale wanashuka na kuanza kuniangalia kwa umakini.
Nilimuendea askari mmoja lengo nipate kumuuliza kulikoni?, lakini na yeye alirudi nyuma na kunionyeshea silaha aina ya SMG kama mhalifu vile. "Usinyanyue mguu wako kusogea mbele yangu nitakumwaga ubongo"
Aliongea yule askari
"Afande mbona sielewi mimi nimefanya nini?" Baada ya kusema hivyo ndipo wengi wao walishangaa
"Eeeeh!! Anaongea kumbe"
Ghaa! Walijua kuwa mimi bubu. Walinichukua na kuniweka ndani ya gari. Mimi nikiwa na lile sanduku langu dogo. Safari hadi kituo cha polisi. Nilipifika kule wakaniweka chumba changu peke yangu. Niliendelea kuishi kule kwa masaa kadhaa niliyoyaona kama mwaka mzima.
Ndipo nikatolewa na kupelekwa hadi hospitali moja hivi maarufu sana. Walinipima huku nikiwa na ulinzi mkali.
"Haya, mgonjwa wetu anasumbuliwa na nini pia ni binadamu au mzuka huyu"
Askari mmoja aliuliza
"Kwa nini awe mzuka?"
Dakatari alihoji
"Ilisemekana kuwa alipotelea baharini kwa kipindi cha miezi minne na ilisemekana kuwa kafariki, alivyorejea tukapigiwa simu ndio maana tunakamleta kwanza tujue afya yake".
Hayo yote walikuwa wanaongea nayasikia maana nilijifanya kama nimelala.
"Msijali kabisa, ni binaadamu ila kaathirika hapa"
"Daaah!!! Pole yake sasa tunashukuru daktari ngoja tumpeleke nyumbani akapatiwe uangalifu zaidi."
"Mimi ningewaomba muacheni kwanza ili apate pumzi kidogo kisha nitawaruhusu afande tumuache apumzike kwanza".
Askari wote walitoka nje tukabaki wawili tu pale mimi mgonjwa mtuhumiwa na yule Dakatari.
Ndipo yule daktari wa kike alinifunua shuka yangu na kuniamsha kwanza, nilimuangalia kwanza ndipo nikaamka na kumsikiliza.
"Kaka, kwanza pole sana kwa yaliyokukuta ulifanya kosa gani huko mtaani".
"Dada ni stori ndefu sana ambayo hata hapa nashindwa kukuelezea nianze wapi maana we acha tu" nilikuwa natoa chozi kwa uchungu kutokana na watu wale wanavyonifikilia kuwa mimi nilikuwa nimekufa japo nia yao ndio ilikuwa mimi nife kabisa nisionekane.
Yule dada alinionea huruma akachukua leso kisha akaanza kunifuta chozi langu ambalo hata mama na baba yangu marehemu wangeliona wasingevumilia mtoto wao nateseka vile.
Japo mimi mwenyewe nina damu yangu lakini mpaka pale sijui yuko wapi mtoto wangu, sijui yuko wapi mwanangu na anaendeleaje.
"Kaka usilie nitakusaidia, ngoja kwanza nakuja ila lala wakija polisi usionyeshe dalili ya kuamka"
"Sawa dada"
Alitoka nje baada ya muda ndipo akaingia tena. Akaniamsha kwa kunigusagusa lakini sikuamka maana nilijua kuwa ni wale askari.
"Mimi hapa bwana amka kwanza"
Niliposikia sauti yake ndipo nikaamka. "Nimewaambia kuwa kutokana na maradhi yako mimi nitakaa na wewe kukulinda mpaka unakuwa salama na wameondoka kabisa".
Nilipumua pumzi kubwa kisha nikamshukuru. Ilipita siku ile nikiwa mule hospitalini ndipo nikatoroshwa na yule daktari hadi nyumbani kwake. Ndipo siku moja nikamuambia ukweli wangu na yale yote yanayonisibu kuanzia mwanzo hadi mwisho jambo ambalo lilimuacha hoi yule dada na kumtoa chozi kabisa.
"Pole sana Mnali yani sikudhani kama kweli kuna watu wanapata shida kama zako, imeniuma sana ila kuna swala nataka kujua"
Aliposema hivyo nikashtuka kwanza.
"Kitu gani"?
"Usishtuke tulia tu kwanza...wakati nakupima kwenye mwili wako nikakuta kidogo damu yako ina utofauti yani umeathirika"
"Imeathirika..sijajua una maana gani dada yangu"
"Usiniite dada bwana naitwa Salha"
"Sawa Nifafanulie salha"
"Yaani damu yako kuna vidudu vimeingia tofauti na binadamu anavyotakiwa kuwa navyo si UKIMWI hapana huo hauna ila una vinasaba tofauti na vya kibinadamu wa kawaida".
Nilishangaa nini hiki vinasaba maana kwa kutoelewa au kwa kutosoma huku ni shida.
"Salha, Vinasaba ndio nini?"
"Haaah! Haaah! Haaaaah!"
Alikuwa ananicheka sana nikajua ndio dharau ile ya kunidharau mimi nisiejua hata kusoma hakika sipendi na nilikasirika kwelikweli,"basi naomba usinune sina maana nakucheka mnali ila nafurahi tu kusikia sauti yako kama hivi ninachomaanisha kuwa tayari kuna vimelea ambavyo vimeingia ndani ya damu yako ambayo vinaendesha mwili tofauti na wewe je? Kuna jambo gani limekupata?"
Niliamua kumficha japo nilijua ipo siku ambayo atafahamu tu. Ilipita siku kama mbili ndipo waandishi wa habari wanakuja kwa daktari pale mimi nikiwa ndani nimelala.
Niliamshwa na wakaanza kunihoji maswali kadhaa ambayo niliwajibu vyema.
"Bwana mnali, ilikuwaje maana ilisemekana kuwa ulipotea kabisa kwenye uso wa dunia jambo gani lilikukuta?"
Aliuliza mmoja wa waandishi wa habari. "Ilo swala siwezi kulijibu kwa sasa mpaka pale nitakapojua ilikuwaje kwa sasa hakuna ninachofahamu".
"Sawa vipi kuhusu maisha ya huko uliko hadi hapa kurudi"
"Hata hilo mkuu sifahamu"
"Tumesikia kuwa umeathirika je? uliuapata kwa njia gani?"
"Niliapata kwa sababu nina vimelea tofauti na mimi kama binadamu vilivyoingia ndani ya mwili". Wakati wanaendelea kuniuliza Salha akaja kisha akanitoa maana nilikuwa naropokaropoka tu pale. Siku iliyofuata nasikia kwenye Televisheni na si kusikia tu na najiona kabisa wakisema mimi ni mmoja wa wale ambao wamejitokeza kujitangaza kuwa mwathirika wa UKIMWI daaah!! Walimwengu acha tu...
TUKUTANE TOLEO LIJALO




No comments:
Post a Comment