RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA TISA 09 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, January 23, 2020

RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA TISA 09





ENDELEA.......
.................Kauli ya bwana Manyota ilinishtua kiukweli eti Tunaharibiana siku kivipi labda. Basi nilibadilisha zile nguo ambazo zilikuwa zimelowa tayari kisha nikavaa nguo nyingine ambazo tuliletewa.
Lakini kitu ambacho kilikuwa kinanishangaza ni pindi tu nilipomuona dereva na jamaa mwengine mwenye Miraba Minne wakiwa wamekasirika sana. Aliangalia nyuma akatuona wote tumekaa ndipo akawasha gari na kuliondoa pale ufukweni. Safari hii tulifika hadi kule hotelini lakini ofisini kwa Mzee Paul. Tulishushwa nje huku tukisubiria nini kinaendelea.
Mimi kwa Wasiwasi Nilimfuata Manyota. " Oyaa! Leo vipi kwani?".
Walonichunia haya Musa na yeye akawa ananichunia nikaona isiwe kesi kubwa zaidi nikatulia pembeni.
Niliona sasa kazi inaanza kama kuota nyasi mapema sana. Walikuja vijana kadhaa ndipo wakafungua lile gari nyuma wakachukua wale samaki. Mmoja wao alihamaki kwa kuona wingi wa wale samaki huku akisifia kuwa ni wengi sana kuliko kawaida ambayo wao walikuwa wamezoea.
Ndipo kwanza akaitwa Musa Ofisini. Wengine tulibaki tukaona leo mambo yameiva. Wakati tunaendelea kusubiria Manyota akanigeukia "Mnali umetuuza sana leo". Nilikunja uso kwa mshangao mkubwa
"Nimewauza! Sijakuelewa bado"
"Ndio walipofika walifurahi na wale samaki tuliowapata ila walikuulizia tukasema umekwenda kuwachukua wengine ila daaah!.." hapo ndipo Jina la Manyota lilivyoitwa na Musa akatoka nje.
Muonekano wa Musa kweli ulionyesha ndani si pema mimi nilihisi patanishinda mapema tu. Muda mchache nikaitwa Mimi nikahisi kabisa kuwa haja zinataka kunitoka miguu yangu ilitetemeka ndipo nikavuta pumzi kwa nguvu kisha nikashusha pumzi kisha nikaingia ndani. Niliwakuta watu wanne mule ndani niliowafahamu ni yule dereva, yule jamaa mwenye Miraba minne pamoja na Mzee paul wakiwa wananisubiri.
Nilijihami kwa chochote kile ambacho kinataka kutokea kwangu. "Haya keti kwenye hiko kiti". Nilikaa kisha nikawatumbulia macho kuwasikiliza nini hicho walichoniitia pale na kama kunifukuza walinitaka wenyewe mimi sina shida kabisa nitaondoka.
"Unaitwa Mnali?"
"Ndio".
"Sawa ebu tueleze historia yako ya elimu kidogo ili tujie tunachotaka kukipata kutoka kwako".
Duu! Niliona sasa ubaguzi wa kielimu umeanza sasa.
"Mimi niliishia elimu ya msingi na sikupata cheti ila nilibahatika kupata kazi ya mikono yangu na nilipoachishwa hiyo kazi kwa kuwa sina elimu basi nikajiingiza kwenye mambo ya uvuvi hapo ndipo mliponiona".
Niliona dereva na baadhi wanacheka sana. "Daaah! Nilijua labda unacheti chochote sasa hapa sijui tunakusaidiaje ok! Utafanya kazi mwezi huu kisha mkataba wako tutaufikilia sawa?"
"Aaah! Sasa nitafanyaje ila mngeniuliza tangu nipo kulekule lakini si leo kuja kunidhalilisha hapa haina shida sijaanza kula ela yenu naomba bora niache nikapigane na maisha yangu mwenyewe".
"Kijana tulitaka kukusitili tu. Nimepata habari yako kuwa ni mvivu sana huko baharini unawaachia Manyota na Musa sasa utafika hapo mbele kwenye ule mlango mpatie hii karatasi kisha utaondoka kabisa hatukuitaji".
Huwezi kuamini kuwa nililia sana pale nilipokakaa.
Kwa hasira sikutaka kuchukua hata ile karatasi wakati nanyanyuka ndipo waliitwa wale wengine yaani Musa na Manyota. Walipoingia niliwaona kama wanacheka hivi.
Nilisimama huku nikitetemeka na kutoka kwenye kiti.
"Kijana chukua hii karatasi umpelekee yule dada atakupatia ela ya kuendelea na maisha yako na ya pole kwa usumbufu maana sisi tunataka vijana kama hawa wachapa kazi na si ndezi kama wewe."
Maneno ya bwana Paul yalikuwa yanauma sana moyoni mwangu
"Usijali Baba sina shida na iyo ela yako, kikubwa nina uzima nitaenda kupambana na hali yangu sisi tusiokuwa na elimu basi acha tukaishie huko".
Nilitoka mule mfukoni nikiwa na kama elfu ishirini tu.
Nilitafuta gari likanipeleka hadi nyumbani, nililala kupunguza mawazo nikijiuliza kwa madhambi yapi ninayoyafanya mpaka nakosa maisha hata ya kujidai kama wengine. Niliwaza kuwa uvuvi nao niuache.
Lakini niliwaza jambo moja kuwa nitafute kwa nguvu zangu. Niliona vyema niende kwa Mama mke wa Marehemu Kibona ili nikaongee nae jambo. Nilikwenda kweli nikamkuta akiwa amejiinamia hana hili wala lile.
Tuliongea mengi sana na mke wa Kibona jambo ambalo niliona ni la umuhimu kuongea nae ni kuhusina na mimi kutaka kuanzisha sehemu ya kuuzia samaki pale nyumbani.
"Sasa Shemeji nakuomba huyu mwanao Mihayo niende nae baharini anisaidie kisha wewe uwe unauza samaki ambao tutakuwa tunawapata".
"Shem kweli vipi huko ambako mlikuwa mnafanya kazi"
"Aaah! Achana nae huko bhana maana nahisi kama unanichoma moto vile sasa hivi ila Mwambie Mihayo jioni aje nyumbani pale natengeneza sehemu ya kuuzia hivyo mwambie aje".
"Haya kila la heri shemeji ila hata leo hatuna hata cha kula mpaka natamani nirudi kijijini maisha ya hapa yananishinda kabisa".
"Hapana Shemeji mimi niliahidi pale baharini kuwa kama Rafiki yangu Kibona Kafia mule basi nitahakikisha kuwa familia yake nailinda mimi mpaka mungu atakapotuchukua mmoja kati yetu."
Niliondoka kuelekea nyumbani kisha nikaanza kutengeneza kibanda kikubwa hivi cha kuwekea samaki wabichi ambao niliamini kuwa watu watajaa na watakuja kununua kabisa. Jioni kweli Mihayo alikuja nikamuelekeza na tukaanza kazi hadi pale tulipomaliza.
Majira ya usiku nilikwenda nae baharini tulifanya kazi kwelikweli mpaka tunafika majira yale kuondoka tuna samaki wa kutosha na asubuhi na mapema tunawakusanya ili kuondoka nao.
Akina mama wengi wakitaka kugombaniana hadi kutaka kupigana kabisa kwa kuhitaji wale samaki.
"Jamani kama mnawataka hawa samaki njooni nyumbani ndiko sasa ninakouzia". Walitufuata hadi nyumbani nikamkuta Mama Mihayo akisubiria mzigo tuliwapanga mpaka sehemu ikajaa na haikutosha.
Tuliwauza wakabaki kiasi ambacho baadhi tuligawa na wengine tukabaki nao kwa matumizi. Walikuja kununua kwangu kwa kuwa nilikuwa nauza bei nafuu tofauti na sehemu zingine.
Jioni yake Mzee yule ambae aliniunganisha na bwana paul alikuja nyumbani. Alinikuta nikifanya baadhi ya mahesabu na mipango ili nijue natoka vipi kutokana na wale samaki. "Sasa kijana umetoka kule kwa bosi kwa sababu gani?"
"Mzee nimeamua kutulia mwenyewe sasa hivi sihitaji usumbufu kabisa maisha yangu nataka kujitegemea mwenyewe, wale wasiotutaka sisi tusiosoma basi waendelee na hao wasomi". Mzee basi aliondoka.
Ndipo waliingia akina mama kuja kutaka oda ya samaki kwamba wakija tu basi wao wawe wa kwanza.
Nilijihisi kama Bosi masikini maana si kwa hali ile. Asubuhi na mapema kama kawaida nilikwenda kuangalia mazingira na kuandaa vifaa hukohuko baharini.
Kila mmoja aliniangalia sana huku wakinionyeshea vidole. Wakati narudi sasa akaja rafiki yangu mmoja na yeye Mvuvi. "Ndugu unajua wewe rafiki yangu sikufichi hata neno moja"
"Najua hilo"
"Wamepanga kukuua ndugu yangu siku hizi za karibuni maana wewe ni mgeni kwenye Uvuvi baada ya Kibona kukufundisha kwa muda mfupi sasa hivi umewapita wote kila mteja anakuja kwako wamekasirika ndio maana nikaona nikuambie wanataka kukuulia ndani ya bahari kama kibona".
Nilishtuka baada ya kusikia wataniua kama kibona.
"Ina maana Kibona Aliuliwa, je na ni nani huyo anaepanga hizo hatua?"
Nilimuuliza
"Mnali! Usijali tukutane leo jioni kabla ya kuja kufanya kazi pitia nyumbani".
Niliondoka pale nikiwa na wasiwasi...

TUKUTANE TOLEO LIJALO



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa