RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA KUMI NA NANE 18 - UHONDO KITANDANI

Hot

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa

Thursday, January 23, 2020

RIWAYA:: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA KUMI NA NANE 18





ENDELEA.........
.......Kwa kuwa bwana Mjumbe nilimuona akiwa mbishi kama pilipili yenye kuwasha mdomoni pindi inapoliwa. Niliondoka na kumuacha akiwa ananiangalia huku akinisindikiaza kwa kauli ileile ya awali ambayo nilipata kuisikia kwa umakini zaidi ya awali."Wewe kijana huu mtaa utakushinda kabisaa kwa hali hiyoo na kiburi hiko ndicho kilimfanya Kibona aweze kufa". Nilitamani kusimama lakini nikabakia kusikitika kwa nafsi yangu pamoja na mwili wangu kuusongesha mbele kwa kutohitaji swala lolote baya.
Nimeshafika hadi nyumbani nafanya nini hali ya kuwa hakuna chochote kilichomo ndani, nabaki kuduwaa na wakati nazidi kuduwaa ndipo nashtuka kushikwa na mtu akiwa nyuma yangu hakuwa mwingine bali ni yule mzee ambae aliniunganishia dili kwa bwana Paul, "khaaa! Mnali, achaa weeee haya mbona maajabu". Nilimuangalia sana huku nikimshangaa "maajabu kivipi?" Nilimuuliza swali. "Wewe huoni kama unazidi kuishangaza dunia haya umeponapona vipi huko baharini!" Swali la huyu mzee lilinipa picha kidogo kuwa dili la mimi kufa kule lilipangwa na huyu akiwemo sasa atanitambua. Nilipepesa macho kisha nikabadilisha sura ya mshangao na kuweka sura ya huzuni niliyoichanganya na busara za uongo kumbe nikiwa na lengo langu.
"Babu yangu huwezi kuamini kuwa walimwengu ni wabaya sana na mwenyezimungu ni mkubwa sana na hamtupi mja wake". Wakati huo nilikuwa namshika bega nahisi huu muda ningekuwa na ile ashki ya kuhitaji nyama mbichi na ukichanganya hasira nilizonazo hakika ningemtafuna hata bega nyambafu kama huyu. "Mh! Unasema kweli kijana haya ilikuwaje maana sisi kusikia tu kuwa umekufa huko baharini eti ulikuwa unafuata mwili wa rafiki yako kibona ni kweli?".
Nilicheka kidogo, "babu hapa kuongelea mada hizo hapana ebu tuingie ndani kisha nikuhadithie vyema". Basi tuliingia ndani hali ya kuwa hajui kuwa nina nia gani mimi kwake. Nilipohakikisha tumekaa mahali ambapo hawezi kupita mtu yeyote na kutuona ndipo niliposimama "hapa panatosha mzee" nilimuambia, "haya nihadithie". Nilijipanga kumvaa vyema mzee huyu kwa kumkaba shingo mpaka pale atakaposema kile ambacho nakihitaji.
"Babuu! Unawafahamu watu ambao walitumwa kuja kuniua kule baharini?". Nilibadilika kidogo kutokana  swali ambalo nilimuuliza na sauti ambayo niliitoa. "Aaah ah ah! Kijana hapana ndio nataka kujua akina nani hao". Nilimshika shingo barabara kisha nikamuangusha chini hakika alikosa hata nafasi ya kuongea vyema pamoja na kujitetea, niliyafanya hayo huku nikikumbuka yale mabaya yote ambayo niliyapata kule kisiwani.
"Babu nakuomba unieleze naamini dili la mimi kuja kuvamiwa unalifahamu, kwa sababu wewe ndio muhusika wa kila kitu ambacho kinafanywa kule baharini naomba uniambie haraka kabla hata sijabadilika nikakutafuna". Alipupapupa pale nikaona jicho linamvimba na kuja rangi nyekundu nilimuacha kidogo "Mnali unafanya nini unataka kuniua mimi hapana ihusiki na jambo lolote lile kabisa". Nilimbadilikia kwelikweli "mzee nakuomba sema ukweli wako nitakunyonya nyama sasa hivi" wakati huo tayari alishapokea kichapo mpaka suti zake zote zikachafuka vumbi, kilichonipa uhakika ni zile nguo kwani mtu wa pwani kama yule mzee ni nadra kuvaa suti za ela.
Suti zile sikuziona kwa huyu mzee peke yake bali hata kwa Musa pindi aliponikuta kule njiani akiwa na gari niliamini kabisa hata Manyota na yeye atakuwa nazo hizi na wamezipata wapi, itakuwa kulekule kwa Paul ina maana kuwa anafanya nao kazi hawa na ndio maana wamefikia hatua hii.
"Sawa siku hizi unafanya kazi gani?" Nilimuuliza baada ya kuona kuwa zile nguo zinanitatiza. "Hapana sifanyi kazi yeyote hata uvuvi nimeacha kabisa". Nikaona hapohapo "sawa unafanya kazi na bwana Paulo?" Hapo alisita kidogo. Mimi sikujali kama ni mzee wa umri gani nilimfyatua vya kutosha maana ni muuni na mzee asie na huruma anafanya kazi ya kuuza madili kwa vijana.
Kazi ilikuwa pevu mpaka pale alipoamua kusema ukweli kabisa kuwa Paulo ndie ambae katuma kikundi cha watu ili waje kuniua mimi. Hakika hasira nyingi zilinikamata na nilitamani hata kumuua mzee yule, lakini punde si punde mdomo wangu ulianza kuwa mchachu akili yangu kabisa niliiona kuwa inaniruka mbali na kufanya mambo ya ajabu, sasa ya leo ikawa kali zaidi ya zote wakati nazidi kuangaika mzee huyu alibaki kuduwaa akishangaa ile hali.
Mwili ulianza kutetemeka nguvu za miguu ilikuwa mara dufu hamu ya nyama mdomoni ikihitajika, "Babu nakuomba kaa mbali na mimi tafadhali kaa mbali na mimi tafadhaliiiiiiiii". Mzee huyo alishuku sana ile kauli alinijia karibu huku akisema "Kijana hata kama umeniadhibu kiasi nashindwa kufanya jambo ila siwezi kukuacha ukiwa peke yako umepatwa na nini?". Alihoji.
"Hapana nakuomba ondoka haraka nimeshakusamehe nendaaaaaa". Nilipiga ukelele ambao sauti nilihisi kabisa sio ya kibinadamu "Sawa ngoja nikaite gari ikupeleke hospitali haraka". Nilitamani kumuambia kuwa hapana ila nguvu ya maumbile tofauti yalinizidi ndipo niliachama mdomo na kutoa ulimi wangu aisee nikiwa bado kwa mbali najielewa niliona natoa ulimi usio wa kawaida wenye rangi nyeusiiii yule mzee alipoona vile alistaajabu na kujibamiza kwenye ukuta huku akitafuta nafasi ya kukimbia.
Hasira zangu zilipelekea kufika kwenye hali ambayo siwezi kuiongoza mwenyewe.
Ilichukua kama dakika kumi hivi kabla yeyote kugundua nini kilinitokea zaidi ya yule mzee. Nilimuona kwa mbali yule Mzee akija pamoja na mtu mwingine kwa haraka sikumfahamu. Mimi hali yangu ilirudi kama umeme unavyoshtua kwa yule ambae kakamatwa na umeme. Palepale nilizimia ila neno la mwisho nililosikia ni kuhusu mimi kunitoa na kunipandisha kwenye gari. Sikujua ananipeleka wapi huyu mzee.

TUKUTANE TOLEO LIJALO



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

https://play.google.com/store/apps/details?id=chumba.cha.wakubwa